Mwakilishi wa kuteuliwa na rais kupitia nafasi za walemavu, Mheshimiwa Raya Suleiman Hamad (kushoto), akimkabidhi Katibu wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Wilaya ya Wete Pemba, Salim Hamad Sharif, nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vipeperushi kadhaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu wilayani humo ili kijiweka tayari kwa kutoa maoni ya uundwaji wa Katiba Mpya. Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi itaanza hivi punde awamu ya pili ya ukusanyaji wa maoni, ambapo sasa itakuwa ni kwa makundi maalum. (Picha na Haji Nassor).


Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.