Inna lilahi Wainna Illaihi Raajuni Zanzibardaima imepokea taarifa ya kifo cha Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania anaejuulikana kwa jina Juma Kilowoka maarufu kama (Sajuki )msanii huyo amefariki duni alfajiri ya kuamkia leo katika hospitali ya Taifa muhimbili jijini Daresalam.

Ineleweka  kwamba  msanii huyo alikuwa anauguwa na maradhi yaliosababisha uvimbe ndani ya Tumbo lake lakini kwa msaada wawasamaria wema waliweza kumchangia na kumfanya apate matibabu nchini India ambapo hali yake iliendelea kuimarika na kuwa nzuri kwa afya yake badae na baadae kurudi Nchini Tanzania.

Baada ya kurudi nchini Tanzania msanii huyo aliona ni busara kwenda kuwashukuru baadhi ya watu waliosabaisha kufika kwake India kwa matibabu na baadhi ya mashabiki wake ndipo alipoamua kuenda Mkoani Arusha takribani wiki moja iliopita kwa lengo la kutoa shukrani kwa wakaazi wa jiji hilo kutokana na ushirikiano wao waliouwonesha kwake  wakati akiugua,Jijini Arusha alipokelewa na Umma mkubwa wawatu uliofika hapo kwa ajili ya kumuona msanii huyo lakini kutoka na watu kuwa wengi sana waliofika kumuona kukampelekea Sajuki  kupata mshituko wa Moyo ghafla na kuanguka chini na badala yake kukimbizwa hosptil kwa ajili ya matibabu zaidi lakini kwa kudra ya Mwenyezimungu ameweza kumchukua kiumbe wake alfajiri ya kuamkia leo.

 

Kwa hisani ya Abdalla Abeid

36 thoughts on “Mkasa mzima kifo cha Sajuki huu hapa”

  1. Poleni wapenzi wote wa Sajuki ambaye ni msanii wa filamu za kitanzania. Je hajawahi kuona umati wa watu kama hao? Labda Mola alikuwa anamuhitaji na muda wake umefika.

    L.W.K.

  2. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,na ampe moyo wa ujasiri wastara kwani hiyo yote ni matihani ya mwenyezi mungu.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.