Gazeti moja la nchini Ufaransa linalojuulikana kwa jina la  Charlie Hebdo  leo limechapisha tena katuni za kiongozi wa Waislamu, Mtume Muhammad (S.A.W), hivi leo, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kitendo kama hicho kuzusha ghasia ulimwenguni. Msemaji wa serikali ya Ufaransa, Najat Vallaud-Belkacem, amesema kwamba ingawa huo ni uhuru wa kutoa maoni, lakini lazima athari za utulivu wa kijamii zipimwe. Najat amekiambia kituo cha habari cha France24, kwamba hakukuwa na haja ya kuongeza mafuta kwenye moto. Hapo jana, Iran ililaani kuchapishwa kwa katuni hizo, ikitaka hatua za kisheria zichukuliwe. Wakati katuni hizo zilipochapishwa kwa mara ya kwanza, hapo mwezi Septemba, maandamano na ghasia zilitanda kwenye ulimwengu wa Kiislamu, kulikolazimisha kufungwa kwa muda kwa taasisi na skuli nyingi za Ufaransa kwenye mataifa hayo. Waislamu wanachukulia kuwa ni haramu kuchora picha yoyote ya kiongozi wao.

SOURCE DW SWAHILI.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.