Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikiliwa watu wawili kwa tuhuma zakumshambulia kwa  risasi Padri Paroko Amrosi mkenda mwenye umri wa miaka (52)mwishoni mwa wiki iliopita huko nyumbani kwake Tomondo.

Naibu mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar ASP,Yussuf Ilembo alisema jana kuwa  watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana kwa ushirikiano wa jeshi la Polisi na makachero waliotoka makao makuu Daresalam.

Hata hivyo ASP,Ilembo alikataa kuwataja majina ya watuhumiwa hao waliokamatwa kwa kuhofia kuingilia suala zima la upelelzi linaoendelea ambapo hwenda ikawa ndio sababu ya kuwakosa washukiwa wengine waliohusika.

Amefahamisha kuwa  watuhumiwa hao kwa sasa bado wanaendelea kuhojiwa ili kuwapata washiriki wenzao waliopanga kwa pamoja na kumvamia pamoja na   kumjeruhi kwa risasi padri huyo huko nyumbani kwake.

Aidha ASP Ilembo alisistiza kuwa Jeshi la Polisi litahakikisha wale wote waliohusika na shambulio hilo wanatiwa nguvuni na kuacha sheria ichukue mkondo wake dhidi yao.

Kwa hisani ya Habari leo

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.