Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khatib Mwinyichande, akikabidhi ripoti ya tume yake kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Joto la Uchaguzi miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa sambamba na wanachama pamoja na wapenzi wa vyama vya siasa litapungua au kuondoka kabisa endapo Tume ya Uchaguzi itaendelea kuwa karibu na washirika wake.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar { ZEC } Ndugu Khatibu Mwinchande alisema hayo wakati yeye na wajumbe wa Tume hiyo walipokuwa wakimuaga rasmi  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakikaribia kumaliza muda wao wa utumishi wa miaka mitano unaomalizika  Januari Mosi 2013.

Ndugu Khatib Mwinchande ambae katika mazungumzo hayo akimkabidhi Balozi Seif  Ripoti kamili ya Utumishi wao wa Miaka Mitano alisema ukaribu wa Tume ya Uchaguzi kwa washirika wake ndio njia pekee ya kuondosha malalamiko au dhana potovu ya wadau hao dhidi ya Tume hiyo.

“Ni mara ya kwanza katika Historia ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kutoa fursa  kwa Vyama vya Siasa kulikaguwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hii ni ishara kwa Tume hii kuwa karibu na wadau wake ili kupunguza  joto la Uchaguzi”. Alifafanua Ndugu Khatib Mwinchande.

Mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Mwinchande alifahamisha kwamba daftari  la wapiga kura litaendelea kuwa la kudumu katika dhana ya kuimarisha Demokrasia licha ya changamoto zilizopo za ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo.

Alisema harakati za kimaisha zinazoendelea kukuwa kila siku zinachangia kulifanya daftari hilo kuwa la kudumu kutokana na ongezeko la idadi ya watu sambamba na baadhi ya wananchi kuhama sehemu moja kwenda nyengine.

Akizungumzia uhusiano wa Kitaifa na Kimataifa Ndugu Mwinchande alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar imefanikiwa kuoneza ushirikiano wa karibu kati yake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania { NEC } sambamba na Tume za Kimataifa za Nchi za Sadc na zile za Umoja wa Afrika { AU }.

Alisema hatua hiyo imeijengea uwezo zaidi Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kufikia kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Bara la Afrika { Sadc }.

“ Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } imefikia daraja ya kuwa sehemu ya Tume ya Uchaguzi ya Umoja wa Afrika { AU }”. Alifafanua Mwenyekiti huto wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Mwinchande.

Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuijengea uwezo Tume hiyo uliosaidia kufanikisha majukumu waliyopangiwa baada ya kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa watendaji wa wizara tofauti  za Serikalini.

Akitoa pongezi zake kwa kazi kubwa iliyotekelezwa na Wajumbe wa Tume hiyo ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar  imefanya  kura ya maoni iliyopelekea  uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010  kuingia katika  historia mpya ya amani na utulivu.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Uongozi makini wa Tume hiyo kwa kiasi kikubwa  umesaidia kusimamia kupunguza joto la kisiasa ndani ya visiwa vya Zanzibar lililodumu kwa kipindi kirefu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wajumbe wa Tume hiyo inayomaliza muda wake kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kuona Tume mpya itakayochaguliwa itapatiwa  vitendea kazi pamoja na fedha kwa lengo la kufanikisha kazi za zake.

“  Tutahakikisha changamoto zilizojichomoza ndani ya kipindi cha  utumishi wenu wa miaka mitano, Serikali inazipatia ufumbuzi wa kudumu”. Alisisitiza Balozi Seif.

Joto la Uchaguzi miongoni mwa Viongozi wa vyama vya siasa sambamba na wanachama pamoja na wapenzi wa vyama vya siasa litapungua au kuondoka kabisa endapo Tume ya Uchaguzi itaendelea kuwa karibu na washirika wake.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar { ZEC } Ndugu Khatibu Mwinchande alisema hayo wakati yeye na wajumbe wa Tume hiyo walipokuwa wakimuaga rasmi  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakikaribia kumaliza muda wao wa utumishi wa miaka mitano unaomalizika  Januari Mosi 2013.

Ndugu Khatib Mwinchande ambae katika mazungumzo hayo akimkabidhi Balozi Seif  Ripoti kamili ya Utumishi wao wa Miaka Mitano alisema ukaribu wa Tume ya Uchaguzi kwa washirika wake ndio njia pekee ya kuondosha malalamiko au dhana potovu ya wadau hao dhidi ya Tume hiyo.

“ Ni mara ya kwanza katika Historia ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kutoa fursa  kwa Vyama vya Siasa kupatiwa fursa ya kulikaguwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hii ni ishara kwa Tume hii kuwa karibu na wadau wake ili kupunguza  joto la Uchaguzi”. Alifafanua Ndugu Khatib Mwinchande.

Mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Mwinchande alifahamisha kwamba daftari  la wapiga kura litaendelea kuwa la kudumu katika dhana ya kuimarisha Demokrasia licha ya changamoto zilizopo za ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo.

Alisema harakati za kimaisha zinazoendelea kukuwa kila siku zinachangia kulifanya daftari hilo kuwa la kudumu kutokana na ongezeko la idadi ya watu sambamba na baadhi ya wananchi kuhama sehemu moja kwenda nyengine.

Akizungumzia uhusiano wa Kitaifa na Kimataifa Ndugu Mwinchande alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar imefanikiwa kuoneza ushirikiano wa karibu kati yake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania { NEC } sambamba na Tume za Kimataifa za Nchi za Sadc na zile za Umoja wa Afrika { AU }.

Alisema hatua hiyo imeijengea uwezo zaidi Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kufikia kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Bara la Afrika { Sadc }.

“ Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } imefikia daraja ya kuwa sehemu ya Tume ya Uchaguzi ya Umoja wa Afrika { AU }”. Alifafanua Mwenyekiti huto wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Mwinchande.

Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuijengea uwezo Tume hiyo uliosaidia kufanikisha majukumu waliyopangiwa baada ya kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa watendaji wa wizara tofauti  za Serikalini.

Akitoa pongezi zake kwa kazi kubwa iliyotekelezwa na Wajumbe wa Tume hiyo ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar  imefanya  kura ya maoni iliyopelekea  uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010  kuingia katika  historia mpya ya amani na utulivu.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Uongozi makini wa Tume hiyo kwa kiasi kikubwa  umesaidia kusimamia kupunguza joto la kisiasa ndani ya visiwa vya Zanzibar lililodumu kwa kipindi kirefu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wajumbe wa Tume hiyo inayomaliza muda wake kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kuona Tume mpya itakayochaguliwa itapatiwa  vitendea kazi pamoja na fedha kwa lengo la kufanikisha kazi za zake.

“  Tutahakikisha changamoto zilizojichomoza ndani ya kipindi cha  utumishi wenu wa miaka mitano, Serikali inazipatia ufumbuzi wa kudumu”. Alisisitiza Balozi Seif.

Na Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.