
Naibu waziri wa biashara viwanda na masoko Mh Thuwaiba Anton Kisasi amewataka Kinamama kujishughulisha na kazi ujasiriamali ilikujiletea maendeleo na kujikwa mua na hali ngumu ya kimaisha
Hayo ameyasema wakati alipo fanya ziara ya kutembelea kikundi cha Ukweli ni njia safi cha Bweleo huko Wilaya ya kati Unguja.
Amesema kila mtu anajukumu la kuleta maendeleo ya Nchi hivyo ni vyema kwa wanajamii kujiajiri na kuacha kuteegemea ajira kutoka serikalini
Mh:Thuaiba amesema lengo la ziara hiyo kwa Wizara yao ni kuwainua Wajasiriamali na kuwapa Elimu ya kivitendo hao ili bidhaa wanazo zalisha kuwa imara na ubora ili kukuza soko la ndani na nje ya nchi
Nae Mjasiriamali Bi Safia Hashim Makame ambae pia ni Katibu wa kikundi hicho amesema wamekuwa wakizalisha mapambo zikiwemo herini za lulu mikufu mafuta ya mchai chai sabuni za mwani pamoja na keki za mwani
Sambamba na hayo wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitendea kazi pamoja na kukosekana kwa soko la uhakika kwa bidhaa zao
Hivyo ameitaka wizara kuwasaidia kukikuza kikundi hicho ili kuweza kuajiri watoto wasiokuwa na ajira pamoja na waliokatisha masomo.