Uongozi wa kanisa katoliki jimbo la Zanzibar umekanusha uvumi ulionea kuwa Padre Peter Minja amefariki kutokana na kupanda presha iliyosababishwa na tukio la kupigwa risasi kwa Padre Amrose Mkenda wa kanisa katolikiwa parokia ya Mpendae lililotokea usiku wa kuamkia juzi.

 

Hayo yalielezwa na Msemaji wa Kanisa hilo ambae pia ni Katibu ,kuu wa Kanisa katoliki jimbo la Zanzibar Padre Cosmas Shayo wakati akizungumza na Mwandishi wa habari hizi  huko ofisini kwake kaika kanisa la Minara Miwili Shangani Mjini Zanzibar.

 

Alisema Padre Minja alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupooza yaliyosababishwa na kuganda kwa damu katika ubongo kutokana na presha ya muda mrefu.

 

Aidha Padre Shayo Alifahamisha kuwa Uongozi wa kanisa hilo unathamini mchango mkubwa uliotolewa na marehemu kipindi cha uhai wake katika kuliendeleza kanisa kwenye huduma za kiimani na kiroho kwa waumini wa kanisa hilo.

 

Akizungumzia  kuhusu wasifu wa Marehemu huyo ,Padre Shayo alisema  kuwa Padre Minja amezaliwa mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Moshi na amepata wadhifa wa kuwa Padre mnamo mwaka 1982 na amefanya kazi zake za upadre katika visiwa vya Unguja na Pemba.

 

Pia alisema kuwa padre Minja amepata elimu yake ya shahada ya pili ya masomo ya dini ya kikiriso ambapo alikuwa akiendelea na kazi ya ualimu katika vyuo mbalimbali vya mafunzo ya hoteli.

 

Ibada ya misa ya mazishi ya marehemu itafanyika siku ya Jumamosi wiki hii katika kanisa katoliki Parokia ya Mpendae majira ya saa nne za asubuhi na mazishi yatafanyika katika kijiji cha kitope nje kidogo ya mji wa mji wa Zanzibar

Kutokana na matukio yanayoendelea kujitokeza Zanzibar padre Shayo aliitaka Serikali kuchukua juhudi za makusudi katika  kulinda Amani ya nchi kwani waumini wa dini ya kikiristo Zanzibar wamekuwa wakiishi katika hali ya weasi wasi kutokana na matukio yanayoendelea kujitokeza dhidi yao.

Na Nassor Khamis

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.