Innalillahi wainna ilayhir raajiun! Zanzibar Daima imepokea taarifa ya kusikitisha kwamba wasichana wawili wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 19 wamefariki dunia jioni ya leo huko katika kijiji cha Shengejuu,  mkoa wa Kaskazi Pemba, wakiwa kwenye harakati za kuokoa zao la karafuu maeneo ya Kilimani. Mpasha habari wetu anatueleza kuwa wasichana hao walianguka na kuumia vibaya sehemu za vichwa na kusababisha vifo vyao ambavyo vilitokea hapo hapo. Allah awapokee ndugu zetu hawa akiwa ameshawasamehe makosa yao na awape moyo wa subira ndugu na jamaa zao. Tunaendelea kuifuatilia habari hii kwa undani na tutawaletea kwa ukamilifu wake, mara tu tutakapokamilisha kuwasiliana na vyanzo vyote ikiwemo hospitali, polisi na mashahidi.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.