`

WAKULIMA WA KILIMO CHA MPUNGA MICHEWENI PEMBA
WAKULIMA WA KILIMO CHA MPUNGA MICHEWENI PEMBA

WAKULIMA wa mpunga wa bonde la ‘Kinyakuzi’ shehia ya Kinowe, wamekumbwa na wasiwasi mkubwa wa kukosa mavuno mazuri, baada ya mbegu aina ya ‘bikensupa’ waliopewa kutofumua (kuchanua) viuzri.

Wakizungumza na Shirika la Utangaazaji Zanzibar, huko Kinowe wakulima hao wamesema, mbegu hiyo kwenye bonde lao ambayo ni mpya, kwa baadhi ya shamba haikuchanua vyema jambo ambalo linawapa mashaka ya kukosa mavuno.

Katibu wa wakulimua hao nd; Shaibu Nassor Tumu amesema, pamoja na kwamba mbegu hiyo ilikumbwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja ukosefu wa maji, lakini bado wakulima wanawasiwasi wa mavuno.

Katibu huyo alieleza kuwa, tayari hali hiyo wameshairipoti kwa wataalamu wa kilimo na Idara ya uazalishaji mbegu, lakini hawajapata jawabu rasmi.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Uzalishaji mbegu kutoka Idara ya Umwagiliaji maji Pemba, nd :Said Ali Salim, amesema hilo hata wao limewapa msahaka, kwani mbegu hiyo imepandwa katika mabonde kadhaa bila ya kuleta tabu.

Aliyataja mabonde ya Mangwena, Weni, Kimbuni, Dobi, Tibirinzi kuwa mbegu hiyo imepandwa na kufua vyema na wakulima kuifurahia isipokuwa bonde hilo la Kinyakuzi pekee.

Hata hivyo ameeleza kuwa, huwenda hiyo imesababishwa na wakulima wenyewe kwa kuchanganya mbegu hiyo na nyengine, hivyo kuzidiwa nguvu na kuchewelewa kufumbua.

Hata hivyo alisema tayari kitengo hicho kimeshatoa timu ya wataalamu kwa ajili kuchunguza hilo , na baadae watatoa taarifa sahihi kwa wakulima na kuwataka wawe wastahamilivu.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.