KATIBU MKUU WA JUMUIA YA WASIOONA ZANZIBAR (ZANAB) BW, ADIL MOHAMMED ALLY
KATIBU MKUU WA JUMUIA YA WASIOONA ZANZIBAR (ZANAB) BW, ADIL MOHAMMED ALLY

KUMALIZIKA KWA AWAMU YA KWANZA YA MCHAKATO UKUSANYWJI MAONI YA WANANCHI KATIKA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA UPANDE WA ZANZIBAR HAUJASHIRIKISHA IPASAVYO WATU WENYE ULEMAVU KUTOKANA TAARIFA ZILIZOTOLEWA HAZIKUWAFIKIA KWA WAKATI JAMBO AMBALO LINAWEZA KUSABABISHA KUPATIKANA KWA KATIBA ISIYOZINGATIA FURSA, HAKI NA MAHITAJI MAALUM YA WATU HAO.

HAYO YAMEELEZWA NA KATIBU MKUU WA JUMUIA YA WASIOONA ZANZIBAR (ZANAB) BW, ADIL MOHAMMED ALLY WAKATI AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI HUKO OFISINI KWAKE WELES MJINI ZANZIBAR.

AMESEMA ILI IPATIKANE KATIBA YENYE KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA KATIKA KUJALI HAKI NA FURSA KWA KILA MWANACHI LAZIMA IZINGATIE MATAKWA YA WATU WENYE ULEMAVU KWA LENGO LA KUUNDA JAMII MJUMUISHO.

BW, ADIL AMEFAHAMISHA KUWA KATIKA MCHAKATO HUO HATA WALE WATU WENYE ULEMAVU WALIOPATA FURSA YA KUTOA MAONI YAO HAWKUSHIRIKI KIKAMILIFU KWANI HAWAKUWA NA UELEWA MZURI JUU YA UUNDWAJI WA KATIBA HIYO.

AMESEMA KUWA KUTOKANA NA BAADHI YA MAENEO KATIKA MIKUTANO YA UTOAJI MAONI YA UUNDWAJI WA KATIBA HIYO KULIJITOKEZA VURUGU NA MACHAFUKO JAMBO AMBALO LILIPELEKEA WATU WENYE ULEMAVU KUSHINDWA KUFIKA KATIKA MAENEO HAYO KWA KUHOFIA USALAMA WA MAISHA YAO.

AIDHA AMESEMA KUWA SUALA LA KUUNDWA KWA KATIBA MPYA LINATKIWA KUCHUKULIWA KWA UZITO MKUBWA KWA MASLAHI YA NCHI NA WANANCHI KWANI KATIBA NDIYO MUONGOZO NA DIRA YA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA UTAWALA BORA WA KISHERIA KWA FAIDA YA WANANCHI.

HATA HIVYO AMEWASHUKURU WASHIRIKA WA MAENDELEO FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY KWA MCHANGO WAO WA KUTOA MAFUNZO NA RUZUKU KWA KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU ILI WAWE NA UELEWA KATIKA UTOAJI WA MAONI YA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA.

BW, ADIL AMEIPONGEZA TUME YA UKUSANYAJI WA MAONI YA KATIBA MPYA KWA KUTOA AHADI YA KUWAPATIA NAFASI YA PEKEE YA WATU WENYE ULEMAVU KUTOA MAONI YAO ILI YAINGIZWE KATIKA MCHAKATO HUO ILI YAFANYIWE KAZI KWA VITENDO NA WAHUSIKA.

AIDHA AMEISHAURI SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUCHUKUA JUHUDI ZA MAKUSUDI KATIKA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA NAMBA 9 YA WATU WENYE ULEMAVU YA MWKA 2006 KWANI IMETUNGWA BILA YA KUWEKEWA KANUNI ZA UTEKELEZAJI WA SHERIA HIYO JAMBO LINALOKWAMISHA HARAKATI ZA KUJIKOMBOA KWA WATU HAO.

PIA AMEWATAKA WAZANZIBARI KUBADILIKA KIFIKRA KWA KUJIEPUSHA NA MIGOGORO PAMOJA NA VURUGU ZISIZOKUWA NA ULAZIMA KATIKA JAMII ILI KUEPUSHA MAAFA YANAYOWEZA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA ULEMAVU KWANI NCHI NYINGI BARANI AFRIKA ZILIZO SHINDWA KUKEMEA HALI HIYO ZIMEKUWA NA HALI MBAYA KIUCHUMI NA KIJAMII PAMOJA NA KUPELEKEA KUONGEZEKA IDADI KUBWA YA WATU WENYE ULEMAVU.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.