Baadhi ya Viongozi wa Uamsho (meza kuu) wakiwa kwenye mihadhara kabla ya kukamatwa kwao.
Baadhi ya Viongozi wa Uamsho (meza kuu) wakiwa kwenye mihadhara kabla ya kukamatwa kwao.

Amiri wa Muda wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar  amekanusha madai kwamba Waislamu wameiomba serikali iwatoe viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kabla ya sikukuu ya Krismasi, ambao wapo rumande kwa muda wa takriban miezi  miwili kwa sasa.

Amiri huyo  amewaomba Waislamu na wananchi kuwa wastahmilivu katika kipindi hiki ambacho maoni ya ukusanyaji wa maoni yamekamilika kwa upande wa Zanzibar na wasubiri utekelezwaji wa matakwa yao.

Akizungumzia vipeperushi vilivyosambazwa hivi  karibuni vya kutoa onyo ikiwa maamiri hawaataachiwa huru ikifika siku ya Krismas na mwaka mpya watachukua hatua, amesema vipeperushi hivyo havikutolewa na viongozi wa jumuiya hiyo na amewataka Waislamu kuwa makini dhidi ya maadui wasioitakia mema Zanzibar.

Amesema vipeperushi hivyo vilivyodaiwa vimetoka Masjid Jibril Mkunazini havihusiani na msikiti huo wala taasisi yoyote ya kiislamu Zanzibar.

Aidha amebainisha ya kwamba vipeperushi hivyo vina lengo la kuwashawishi wananchi kuchochea vurugu ambazo hazina faida kwa maendeleo ya Zanzibar.  Amewafahamisha wananchi na Waislamu kwamba suala la kuingilia mahakama ni kosa kisheria  hivyo amewataka Wazanzibari kutoshabikia masuala hayo wakati huu ambapo  kuna mambo muhimu yanayolikabili taifa.

Na baadhi ya waislamu ambao huswali msikiti huo wamewaomba wale wote amabo wanauchezea Uislamu waache tabia hizo kwani misikiti ni nyumba tukufu kwa ajili ya ibada na sio kwa ajili ya kuwagawa wananchi.

Chanzo: MzalendoNet

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.