Sheikh Suleiman Soraga mara baada ya kufikishwa hospitali kutokana na mashambulizi mwezi mmoja uliopita.
Sheikh Suleiman Soraga mara baada ya kufikishwa hospitali kutokana na mashambulizi mwezi mmoja uliopita.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad leo amefanya ziara ya kumtembelea Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga, na kumuombea apone haraka ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.

Amesema mtihani uliompata Sheikh Soraga mwezi uliopita wa kumwagiwa maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali haukutarajiwa, na kumtaka kuendelea kuwa na subra wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Sheikh Soroga anaendelea kupatiwa matibabu nyumbani kwake Mwanakwerekwe baada ya kurejea nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya awali baada ya kupatwa na mkasa huo wa kumwagiwa tindikali.

Sheikh Soraga ambaye anaweza kuzungumza vizuri, amemwambia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa kwa sasa anaendelea vizuri licha ya kupata majeraha mabaya hasa katika sehemu za usoni na kifuani.

Amewashukuru madaktari wa hospitali ya Miotnchini India kutokana na huduma bora walizokuwa wakimpatia katika kipindi chote alichukuwa hospitalini hapo, na kuelezea matumaini yake ya kupona na kuweza kuendelea na majukumu yake.

Sheikh Soraga alirejea nchini tarehe 16 mwezi huu akitokea nchini India, alikokuwa akipatiwa matibabu ya awali baada ya kumwagiwa maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali, wakati akifanya mazoezi ya viungo katika eneo la Magogoni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Na Hassan Hamad, OMKR

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.