TASAF

MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA, JUMA KASSIM TINDWA, AMEVITAKA VIKUNDI VYA UFUGAJI WALIOKABIDHIWA NG’OMBE NA MRADI WA TASAF KUHAKIKISHA WANAIENDELEZA MIFUGO HIYO, ILI IWEZE KULETA TIJA KWAO NA TAIFA KWA UJUMLA.

MKUU HUYO WA MKOA AMEELEZA HAYO LEO, HUKO MWAMBE KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI NG’OMBE WA ASILI 63, WENYE TAHAMANI YA SHILINGI MILION 86, KWA WANAJAMII WA KIJIJI HICHO, WALIOAMUA KUACHA UKATAJI WA MATOFALI

AMESEMA, MIFUGO HIYO INATARAJIWA KUWA IWANUFAISHE WAO NA KIZAZI KIJACHO, HIVYO HILO LITAFIKIWA IWAPO MIFUGO HIYO WATAITUNZA, KWA LENGO LA KUJINASUA NA UMASKINI

KWA UPANDE WAKE MRATIBU WA TASAF PEMBA BW: ISSA JUMA ALI, AMESEMA, KATIKA SHEHIA HIYO KULIKUWA NA JUMLA YA VIKUNDI 17 AMBAVYO WANANCHI WAKE NI WALE WALIOAMUA KUACHANA NA KAZI YA UKATAJI MATOFALI NA KUOMBA MRADI MBADALA WA UFUGAJI .

AMESEMA VIKUNDI VYENGINE VILIBAKIA, TASAF ITAANGALIA UWEZEKANO KWA AWAMU IJAYO YA TASAF, ILI NAVYO KUPATIWA MIFUNGO YA AINA HIYO PAMOJA NA MBUZI

MKUU WA WILAYA YA MKOANI JABU KHAMIS MBWANA , AMEUPONGEZA MRADI WA TASAF, KW AKUTIMIZA AHADI YAKE HIYO, HASA KW AVILE BAADHI YA VIKUNDI HAVIKUAMINI HAPO AWALI

AFISA MDHAMINI AFISI YA MAKAMU WA PILI PEMBA ND:AMRAN MASSOUD AMRAN AMESEMA HATUA HIYO WATAKAYOANZA NAYO NI KUBWA IWAPO MIFUGO HIYO WATAISHUGHULIKIA IPASAVYO.

WAKATI HUO HUO MKUU HUYO WA MKOA WA KUSINI PEMBA AMEKABIDHI SHILINGI LAKI SITA, KWA UONGOZI WA TAWIL LA CCM KENGEJA, IKIWA NI AHADI YA WAZIRI WA KAZI , UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI MH; HAROUN ALI SULEIMAN NA MWAKILISHI WA JIMBO LA RAHA LEO WALIOITOA HIVI KARIBUNI.

AKIKABIDHI FEDHA HIZO, MKUU HUYO WA MKOA AMEUTAKA UONGOZI WA TAWI HILO, KUHAKIKISHA FEDHA HIZO WANAZITUMIA KWA KAZI ILIOKUSUDIWA.

NA HAJI NASSOR, PEMBA

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.