Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, imeahidi kutekeleza agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, la kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa barabara ndani ya mwezi mmoja.

Afisa Habari wa Manispaa hiyo, Sebastiane Mhowera, alisema jana kuwa zoezi hilo litafanyika ndani ya mwezi mmoja baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa.

Zoezi hili tulikuwa tunasubiri tu Mkuu wa Mkoa aturuhusu, maana mwanzoni tulilianza, lakini baadae kabla ya kutimiza malengo Waziri Mkuu akawa ameruhusu biaashara za usiku ambazo ni chanzo cha jiji kuwa katika hali ya uchafu,alisema Mhowera.

Mhowera aliongeza kuwa Manispaa hiyo ipo katika mchakato wa kukamilisha masoko manne ambayo ni Mburahati, Magomeni, Mwenge na Bunju kwa kuyaboresha ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiasahara ya Wilaya ya Kinondoni.

Pia katika kuwaboreshea maeneo ya kafanyia kazi wafanyabiashara wa wa wilaya yetu sasa tunakamilisha masoko manne ambayo pia tutatoa mikopo kwa wafanyabiashara ambao watasajiliwa, hayo yote ni maboresho tu, alisema.

CHANZO: NIPASHE

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.