Nikuwinde Hadi Lini?

Published on :

Nikuwinde hadi lini, niipate salamuyo Wanikimbiya kwa nini, kunifanyia uchoyo Wajua nimapenzini, utosi hadi unyayo Ndio ukatenda hayo Ningojee hadi lini, kuuona wajihiwo Wajikimbiza gizani, waruka huna kituo Hikuuliza kwa nini, wanamba nitabiayo Wanijua taumiya