
Katika kukusanya ya Maoni ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano, watu wa shehia ya Kinuni, wilaya ya Magharibi Unguja, wamesema wanataka kuiona Zanzibar ikiwa huru kwanza, halafu pawe na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika. Jumla ya watu 135 walitoa msimamo huo mbele ya wajumbe wa Tume ya Katiba juu ya katiba, huku 44 wakitaka mfumo wa sasa wa Muungano ubakie kama ulivyo.