Jengo la Beit-el-Ajaib likiwa limeanza kuporomoka upande mmoja.
Jengo la Beit-el-Ajaib likiwa limeanza kuporomoka upande mmoja.

Jengo maarufu la kihistoria Zanzibar, Beit-el-Ajab (Nyumba ya Ajabu) limeporomoka usiku wa tarehe 1 Disemba 2012. Akizungumzia tukio hilo, mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe ambako ndiko liliko jengo hilo, Ismail Jussa, alikuwa na haya ya kusema kupitia mtandao wa Facebook: “Aibu iliyoje leo kufikia Beit-el-Ajaib kuanguka baada ya Serikali kupuuza hatua zote za kuwazindua kuwa jengo hilo liko katika hali mbaya. Katika kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi cha mwezi Juni/Julai 2011 na 2012 nilizungumzia suala la uwezekano wa majengo haya ya kihistoria kuanguka kutokana na kutotunzwa au kufanyiwa matengenezo.

“Nikaandika na swali maalum kuhoji matengenezo ya majengo hayo hasa baada ya mradi wa MACEMP unaofadhiliwa na nchi wahisani na mashirika ya kimataifa kuwa na fungu la matengenezo la majengo ya Kasri (Palace) na Beit-el-Ajaib. Kama kawaida ya majibu ya Serikali, tuliambiwa, ‘Tusiwe na wasiwasi’. Nikatahadharisha kuwa binafsi nimeyatembelea majengo hayo mawili kuona pamefanyika matengenezo gani kutokana na fedha zilizotengwa, na kuona hapana matengenezo ya maana. Nikajibiwa, ‘Tutafuatilia’. Sasa leo hii turathi ya kitaifa (national heritage) ambayo ni jengo la kwanza refu katika Afrika Mashariki, la kwanza kuwa na umeme na la kwanza kuwa na lifti kiasi cha kuitwa Jumba la Ajabu (House of Wonders) limeanguka kwa uzembe wa Serikali. Shame on them!”

Naye mwandishi wa habari wa siku nyingi visiwani Zanzibar, Ally Saleh alikuwa na haya ya kuandika kulilia jengo hilo ambalo limekuwa alama ya Zanzibar kwa karne na karne:

i cry when i hear
When with my eyes i see
part of me go into disrepair
but it touches my heart
and crushes my brain

when that part of me crumbles
oh…what happens to the symbol of zanzibar…
can this happen to eifel tower
or to the statute of liberty
but here it happens
where our past has nothing to bind us…
loose and loose and loose we have been
as scattered as we are
and no one is to care
for my building
the building that has made me to be me
cry the house of wonder.

One thought on “Beit el Ajab yaporomoka”

  1. wazanzibari wenzangu haya yote ni matokeo ya mfumo wetu wa maisha tulioundiwa ili tusisonge mbele na bado hatupendi kubadilika ,hebu fikiria kuingia beit el ajaib ni dola tano na people palace ni dila nane kwa mtalii lakini wapii zinaishia mifukoni kwa watu wachache na huku majengo yanaporomka dhulma juu ya dhulma ndani ya zanzibar imevuka mipaka haya sasa wala bado na kwa bundi huyo mlomueka hapo ni msiba tu .iko siku mungu ataleta hukumu yake hapa hapa duniani kwa yote haya tunofanyiwa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.