
Ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo umeanza rasmi mjini Unguja. Makandarasi wa ujenzi huo wameamua kuvunja pembea zote zilizopo hapo ili waweze kufanya kazi zao kiumakini zaidi na kuhakikisha kuwa wanakirudishia hadhi yake ya zamani kiwanja hicho. Ujenzi wa kiwanja hicho unashughulikiwa na kampuni ya CRJE kutoka China. Ujenzi huo unatarajiwa kuchukua miezi 15 hadi kukamilika kwake.