Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiweka mchanga katika kaburi la marehemu bibi Kisa Mohd, mke wa Mbunge wa Wawi, Mhe. Hamad Rashid Mohd aliyezikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
kaburi
Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali wameshiriki katika mazishi ya bibi Kisa Mohd ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Wawi, Mhe. Hamad Rashid Mohd.

Mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya kisutu, yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa ADC bw. Said Miraji na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda.

Mwili wa marehemu huyo ulisaliwa katika msikiti Maamur ulioko maeneo ya Upanga na baadaye kupelekwa katika makaburi ya Kisutu kwa ajili ya mazishi.

Marehemu bibi Kisa Mohd alifariki Jumanne iliyopita baada ya kusumbuliwa na matatizo ya Presha kwa muda mrefu, na kuzikwa Alkhamis tarehe 29/11/2012.

Akizungumza katika mazishi hayo, msemaji wa familia hiyo amewashukuru viongozi na wananchi waliojitokeza kushirikiana nao katika msiba huo, na kwamba familia imepoteza mtu muhimu ambaye pengo lake haliwezi kuzibika kwa kipindi kifupi.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.