Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka watendaji wakuu wa bodi ya mikopo kwa elimu ya juu Zanzibar kucha kabisa kuwa na muhali katika utendaji wa kazi zao.

Pia ameitaka bodi hio kucha kuwakopesha pesa za masomo wanafunzi ambao ni watoto wa viongozi ukizingatia wazazi wao wanauwezo wa kuwasomesha badala yake pesa hizo wakopeshwe watoto wa maskini wasiokuwa na uwezo wakulipiwa na wazazi wao.

Maalim Seif amayesema hayo huko katika ofisi ya bodi ya mikopo iliopo  mnazi mmoja mjini unguja kufuatia ziara yake katika taasisi mbali mbali za secta ya elimu ziliopo Zanzibar

Na kwaupande wake Mkurugenzi wa bodi hio ndugu Khamis Iddy amesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili bodi hio ni kuwepo kwa wanafunzi wengi sana wanaomba mikopo wakati wao hawana uwezo wa kuwapatia huduma wanafunzi wote wanaomba mikopo kupitia bodi ya mikopo ya Zanzibar,hivo basi ameiomba serikali kulifikiria suali hili ili kuweza kuwatatulia changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kizanziba.

Kufuatia ziara hio pia alipata nafasi ya kukitembelea chuo kikuu cha kiislamu kilichopo chukwani nje kidogo ya mji wazanzibar na kujionea shughuli mbali mbali ziopo chuoni hapo lakini pia amekipongeza chuo hicho kwa kuweze kuwa na kiwanda cha uchapishaji wakati hata serikali mara nyengine hutumia kiwanda hicho kufanya kazi zake.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.