Matokeo ya mvua iliyonyesha leo (27 Nov. 2012) mjini Zanzibar. Hata hili serikali inashindwa?

Kuwepo kwa miundo mbinu mibovu ndani ya mji wa Zanzibar ndicho kitu kinachopelekea mji huo kupoteza ile hadhi yake ya zamani iliokuwa ikitambuliwa na mataifa mengi sana ulimwenguni yakuwa zanzibar ni mji uliokuwa bora na wenye vivutio kwa watalii wengi sana.

Lakini leo hii mji huu umekuwa ukitajika kwa sifa ya uchafu na harufu mbovu kabis,  zaidi katika maeneo ya Darajani – katikati ya mji.  Ni ukweli usioficha kuwa mji wa Unguja kwa sasa ni mchafu, na ikiwa serikali wanataka kuirudisha Zanzibar katika hadhi yake, basi ipo haja kwa jamii pamoja na serikali kushirikiana kikamilifu katika kuusafisha mji huu pamoja na kuhakikisha kuwa mitaro yote ilioziba inazibuliwa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.