Uongozi wa SUZA, Chuo Kikuu cha Sultan Qaboos, serikali za Zanzibar na Oman.

Wananchi wa Zanzibar kupitia serikali yao wapata nafasi adhimu ya nafasi za masomo kutoka Serikali ya Oman chini ya Mfalme Qaboos iliyozinduliwa rasmi öleo na Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho, ambaye ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamo Mkuu wa SUZA, Pro. Idrisa A. Rai, amesema kuwa kuwa ana furaha kubwa sana kupata heshima ya kuitangaaza rasmi Sultan Qaboos Academy Fellowship Programme for SUZA kwa ajili ya Wazanzibari na yenye lengo la kuwajengea uwezo katika rasilimali watu ambapo programu hiyo itaweza kuleta wataalamu watakaoleta maendeleo nchini kwa ustawi bora wa uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo ambao umehudhuriwa pia na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar, Bwana Mansour Nasser Abouseed, uliofanyika katika majengo ya SUZA yaliyopo Tunguu, nje ya mji wa Zanzibar, Prof. Rai amesema kuwa programu hiyo ni kwa ajili ya wafanyakazi wa chuo hicho na wasiokuwa wafanyakazi wa chuo isipokuwa kila mtu mwenye sifa anaweza kuomba iwapo watakuwa na sifa zinazostahiki kupata nafasi hio. Pia amesema ni ukweli usiopingika kuwa ajenda hio itaweza kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kuyatimiza matarajio ya Sultan Qaboos wa Oman pamoja na Rais wa Zanzibar yenye lengo la kuona wazanzibar waliowengi wananufaika na hatua hii adhimu kwao.

Pia amesema kuwa SUZA ndio taasisi pekee yakizalendo hapa nchini ambayo ilikuwa na mtaala wa kuweza kuandaa rasilimali watu na maendeleo endelevu katika muktadha wa kuangalia kwa mapana maendeleo ya muda mrefu ya Zanzibar kama ni miongoni mwa kisiwa katika bahari ya hindi kilicho na mazingira ya kipekee ya kuvutia tofauti na nchi nyingi duniani, Kufuatia hatua hio makamo mkuu wa chuo hicho amebainisha aina tatu za wanafunzi wenye sifa ambazo wataweza kuomba nafasi katika Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA nazo ni

1.Waombaji ambao ni waajiriwa wa SUZA
2.Waombaji ambao si waajiriwa wa suza lakini watapatiwa ufadhili elimu wa Sultan Qaboos lakini wafanye kazi suza baada ya kumaliza masomo yao.
3.Waombaji makini kutoka katika taasisi nyengine ambao wanauwezo na utayari wa hali ya juu.

Aidha amesema kuwa Qaboos Academi Fellowship Program for SUZA itakuwa nautaratibu maalumu wa kuwafunza wasomeshaji katika fani elimu,afya,mazingira,miundo mbinu ujasiriamali katika ngazi ya cheti,shahada ya kwanza,uzamivu kutegemea mahitajio ya kistrajia ya muda mfupi,wakati na mrefu wa zanzibar.

Wakati akibainisha aina tatu za waombaji watakaofaidika na programa hii amesema kuwa miongoni mwa watakaopata nafasi hii wataweza kusoma katika nchi za ulaya zikiwemo marekani,Asia,na nchi nyengine zaidi duniani amesisitiza kuwa mfumo huu utakuwa endelevu kila mwaka na utaweza kupeleka wanafunzi hamsini kufuatia hatuwa hii chuo kikuu hicho kitashirikiana vyama taasisi hio pamoja na wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar kwa lengo la kuhakikisha kuwa program hii inafakiwa kama ilivopangwa

Aidha amesema kuwa maombi ya nafasi hizo yatakuwa bure na yatatumwa kupitia mtandao ambao utaonesha utaratibu wote utakao muwezesha mtu kujua ni vipi anaweza kuomba nafasi hizo na mtandao huo utaonesha taarifa zote kuhusu sifa zinazochaguliwa lakini amesisitiza kuwa usajili utakuwa na kikomo ila kwa sasa bado usajili huu haujaanza mara tu utakapokuwa tayari taarifa kupitia vyombo mbali mbali vya habari nchini vitawajuulisha wananchi kuhusiana na hatuo hio,mafunzo hayo yataanza rasmi kwa mwaka wa masomo 2013-2014.

Kwa upande wake waziri wa elimu na mafunzo ya amali zanzibar Mh Shamhuna amesema kuwa hatuwa hio ni faraja kwa wazanzibar na kuwataka wazanzibar waitumie vyema nafasi hio kwa wale watakaopata fursa hio pia amewahakikishia wananchi wa zanzibar kuwa hakutokuwepo kabisa na suala la upendeleo wa kupata nafasi hixzi badala yake atakaepata ni yule mwenyesifa tu ambae atateuliwa na tume iitakayoundwa na watu sita watatu Zanzibar na watatu kutoka Oman, pia mh waziri amewataka watu wenye ulemavu nao kuwomba nafasi hio ikiwa wana sifa zinazohitajika.

Stori na Picha kwa hisani ya Hamed Mazroui wa Mazrouy Media, Zanzibar

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.