Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar

Na Sujae Juma Mkiji

Ni ukweli usiopingika kwamba, since Wazanzibar kwa UOMJA wetu tufanye maamuzi ya kukubali na kuunga mkono UUNDWAJI wa Serikali ya UMOJA WA KITAIFA tumeshuhudia ukuaji mkubwa wa DEMOKRASIA ndani ya Baraza la Wawakilishi (BLW). Ila pamoja na hilo, bado tunashuhudia udhaifu mkubwa pia kwa baadhi ya Wawakilishi wetu katika kujenga HOJA.

Binafsi nashuhudia Wawakilishi wachache tu ambao wanauwezo na umakini katika kujenga HOJA juu ya masuala mbali mbali ya Kitaifa. Tumeshuhudia Serikali ikipata UPINZANI mkali kutoka “BACK BENCHER” ila pamoja na hilo siridhishwi na UWEZO wa baadhi ya Wawakilishi katika KUCHAMBUA na kujenga HOJA juu ya Masuala mbali mbali ya Kitaifa.

Sisi kama Wananchi wa kawaida, tunatamani sana kupata FURSA ya kuchanganyika na Wawakilishi wetu katika huo mlolongo wa Semina zao ili nasi tupate FURSA ya kujibu na kuwapa CHALLENGE juu ya HOJA zao DHAIFU.

Nina HOFU kuwa baadhi yao kwa sababu tu ya kushiriki katika Jumba lile la Chukwani, wanadhani kuwa wao ndio wanauelewa mkubwa juu ya kila kitu jambo ambalo wanajidanganya.

Tunawashuhudia baadhi yao wakiongozwa na Itikadi za KISIASA, wakiwa na fikra mgando huku wakifungika kimawazo juu ya HOJA ya kuwa na mabadiliko juu ya Taifa letu. Kwa wale Wawakilishi ambao bado wanang’ang’ania kuwepo kwa mfumo huu wa MUUNGANO, tunataka waelewe kuwa hawana nafasi ya KUTUDANGANYA kwa HOJA zao dhaifu.

Tumekuwa makini sana kusikiliza hizo wanazoamini kuwa ni HOJA, na wametuthibishia kuwa….UGONJWA unaowasumbua ni UBINAFSI na TAMAA.

Kutoka mtandao wa kijamii wa Facebook

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.