Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar wakizungumza na Mzee Nassor Moyo.

Na Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar

Vijana wa Umoja wa Kitaifa- Zanzibar watoa tamko rasmi la kuwataka wanachama wake wote wakiwemo wanafunzi wa Vyuo vikuu, Wanafunzi wa Masekondari na Wazanzibar wote kwa ujumla wao bila ya kujali tofauti zao za kisiasa, kidini- kujiandaa kikamilifu kushiriki kutoa maoni kwenye tume ya Katiba, VUK- Zanzibar inaunga mkono Kauli ya Rais, Makamu wake wote, Mawaziri na Wawakilishi ya kwenda kutoa hoja madhubuti kwenye Tume ya Katiba.

Aidha, VUK- Zanzibar inasimamia hoja ya kuwa na Mashirikiano mema ya kimkataba badala ya Muungano wa Kikatiba uliokwisha pitwa na wakati usioweza kabisa kuhimili mageuzi ya kikanda na ya kimaitaifa.

VUK- Zanzibar wanataka mamlaka kamili ya Zanzibar ndani na nje na kuendeleza Mahusiano mema ya kijamii na Tanganyika pamoja na kwengineko duniani.
Uzuri wa Mashirikiano ya kimkataba ni kuwa unatoa fursa za nchi zinazoshirikiana kuweza kuangalia kila inapobidi ule mkataba wao bila ya vikwazo vya Kikatiba na hivyo kusukama mbele maslahi ya kila upande na kupata haki zake. Mfano mzuri EAC na EU.

Pamoja na Yote, Uzanzibari Utuunganishe!!
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA!!

3 thoughts on “Vijana wa Umoja wa Kitaifa waamua kwenda kwenye Maoni”

  1. Pamoja na Yote, Uzanzibari Utuunganishe!!
    JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA!
    Naam bila ya shaka hatutaki visirani kwetu

  2. hivi zanzibar kuna umoja wa wasomi wa elimu ya juu? na kama wapo wanafanya nini? mbona kimyaaaaaa????????

  3. Nawapongeza Vijana wa Umoja wa Kitaifa kwa uamzi wa kwenda kwenye maoni. Lakini Swala la msingi la kuzingatiwa ni hili: “Kwa kuwa Tume ya Jaji Warioba inakusanya maoni ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kutoka pande zote mbili za Muungano yaani Zanzibar na Tanganyika, na kwa kuwa Wazanzibar ni wachache kwa idadi ukilinganisha na Watanganyika, Je utatumika mchakato gani kuwezesha hoja ya Kupitiwa Upya Muungano kufanyiwa kazi ikiwa Wasiolitakia taifa mema waliopo pande zote wakaamua kujipanga kupiga kura na kutoa maoni yanayolenga kulazimisha hoja ya kuendelea na muundo uliopo?

Leave a Reply to Hatutaki Visirani Kwetu Cancel reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.