
“Tunatangaza rasmi uhuru wa Azawad kuanzia leo,” alisema Mussa Ag Attaher, ambaye aliongeza kwamba waasi hao wataheshimu “mipaka ya mataifa mengine.” MNLA imesema kwamba kutokana na mafanikio yao ya kuliteka eneo wanaloliita Azawad, wanasimamisha mara moja operesheni za kijeshi kuanzia usiku wa jana. Katika tangazo hilo “la uhuru”, Ag Attaher alisema: “Tunakubali dhamana na dhima kamili inayotuwajibikia kuilinda ardhi yetu. Tumekamilisha jukumu muhimu la ukombozi…sasa kazi kubwa zaidi iko mbele yetu.” Endelea kusoma habari hii.
Chanzo: Deutsche Welle Kiswahili, 6 Aprili 2012