Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika. Amefariki dunia leo hii.

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, amefariki dunia mjini Lilongwe, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mwanzoni redio ya taifa ilikuwa imetangaza kwamba Mutharika, mwenye miaka 78, angelipelekwa Afrika Kusini kwa matibbabu zaidi, lakini inaonekana kwamba alishafariki dunia wakati alipofikishwa hospitali. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, Makamu wa Rais Joyce Banda, ndiye anayechukuwa nafasi ya kiongozi wa nchi, ingawa kuondolewa kwa Banda kutoka chama tawala hapo mwaka 2010 kunaweza kutatiza kipindi cha mpito. Endelea kusoma habari hii.

Chanzo: Deutsche Wellle Kiswahili, 6 Aprili 2012

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.