
Licha ya Sudan na Sudan ya Kusini kufanya mazungumzo ya kutatua mzozo baina yao, hali ya kutokuaminiana inaongezeka huku Sudan ya Kusini ikisema Sudan inavishambulia visima vyake vya mafuta ili kuwatisha wawekezaji. Kauli hiyo ilitolewa na msemaji wa serikali ya Sudan ya Kusini, Barnaba Marial Benjamin, hapo jana jijini Nairobi katika mkutano wake na waandishi wa habari. Endelea kusoma habari hii.
Habari na picha kwa hisani ya Deutsche Welle Kiswahili