Kiongozi wa upinzani wa Myanmar, Aung San Suu Kyi.

Wapigakura nchini Myanmar wamemiminika vituoni katika uchaguzi unaotarajiwa kuzishawishi nchi za Magharibi kuondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo ya Asia Kusini, baada ya Marekani na Umoja wa Ulaya kugusia uwezekano huo, endapo uchaguzi wa leo utakuwa huru na wa haki. Mataifa hayo yameahidi uwekezaji mkubwa katika nchi hiyo ambayo ni masikini lakini yenye utajiri mkubwa wa rasilimali ikipakana na mataifa yanayoinukia kiuchumi, China na India. Suu Kyi, ambaye ni mshindi wa Nishani ya Amani ya Nobel aliyewahi kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani kwa miaka 15 hadi mwaka 2010, amelalamika kuwepo kwa “matukio yasiyo ya kawaida”, lakini si makubwa mno kiasi ya kukizuia chama chake cha National League for Democracy (NLD), kutokushiriki uchaguzi huo. Bonyeza hapa kusoma habari kamili.

Chanzo: Deutsche Welle Kiswahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.