Kufuga kunguru kazi, hawezipo mazoea
Vya halali haviwezi, mizoga ang’ang’ania
Kwako kuwa makaazi, hiyo tabu nakwambia
Kunguru ndege kichaka!

Huwacha chakula ndani, alohalalisha Mola
Hukimbilia jaani, mizoga kwenda kuila
Humuwezi asilani, kumfuga ni madhila
Kunguru hasarifiki!

Yeye huwa akutega, angojea uzubae
Hapo mbawa atapiga, kwako wewe akimbie
Hukimbilia mizoga, jalalani machumoye
’Simfuge hafugiki!

Seif Njugu,
4 Disemba 2011,
Zanzibar

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.