Ubantu na Uarabu wa Vivumishi

Published on :

Kivumishi ni aina ya maneno inayoliezea jina. Kuna vivumishi vya aina nyingi, ikiwa tunakusudia kuvigawa kwa makundi. Lakini muda mchache nilionao leo, nitautumia kuzungumzia aina mbili kati ya hizo – vivumishi vya idadi na vya sifa.

Herufi na Sauti za Kiswahili

Published on :

Kiswahili kilipoanza kurikodiwa kimaandishi hakikuwa kikiandikwa kwa herufi hizi zinazoitwa za Kilatini, bali kwa zile za Kiarabu. Kwa mtazamo wangu, miongoni mwa misiba mikuu iliyokikumba Kiswahili ni huu wa kubadilishwa herufi zake mwanzoni mwa karne ya 19 baada ya upwa wa Afrika Mashariki kuvamiwa na Wazungu wakoloni.

Vitenzi Vitatu: Kuwa, Kuwako na Kuwa na

Published on :

Kiswahili kina vitenzi hivi vitatu, ambavyo licha ya kuwa na maumbile yanayokaribiana, vina maana tafauti. Vitenzi hivyo ni kuwa, kuwako na kuwa na. Hiki kitenzi kuwako kinaweza pia kuandikwa kuwapo au kuwamo kwa mujibu wa muktadha unaohusika; lakini hiyo si mada kwa leo. Mada ni kuangalia mgusano na muachano wa […]

Majina yenye wingi na au kundi zaidi ya moja

Published on :

Kuna idadi isiyo ndogo ya majina kwenye Kiswahili ambayo huchukua maumbile na makundi tafauti. Miongoni mwa sababu ni kuwa aidha majina hayo yanawakilisha maana tafauti licha ya kuwa na umbile moja, ama ni majina yanayofanana kwa herufi zake lakini tafauti kwenye matamshi na hivyo makundi na, au, ni majina yanayowakilisha […]

Yaliyomo kwenye kundi la YU-A-WA

Published on :

Sadfa imeyaweka majina yanayonasibishwa na roho (nafsi) kwenye kundi la YU-A-WA, vikiwemo viumbe tunavyoviona – watu, wanyama, ndege na samaki – hadi tunavyoamini kuwapo kwake bila kuviona kama malaika, majini, mashetani au pepo. Wote hao wanaingia kwenye kundi hili. Sadfa pia imefanya hili liwe kundi pekee ambalo hayakutikani majina yasiyo […]