Siku Maalim Seif alipoinusuru Zanzibar na umwagikaji damu uliokuwa karibuni kutokea, alipoyabeba Maridhiano kifuani pake na kukubali matokeo ya uchaguzi wa 2010, kwenye ukumbi wa Bwanani. Na katika picha hii ya kihistoria akimpongeza Dkt. Ali Mohammed Shein kwa 'ushindi wa Wazanzibari.' Je, Dkt. Shein ameyageuka Maridhiano?

Zanzibar Daima inakuomba usome habari hii hapa chini, kisha tujadiliane ikiwa kweli ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUKZ) kuna umoja linapohusika suala la hatima ya Zanzibar, hasa kwenye kipindi hiki muhimu sana kwa historia ya nchi yetu, ambapo mchakato wa Katiba Mpya, utaishia kwa kura ya maoni juu ya hatima ya Muungano (au angalau mfumo wa Muungano huo)? Kama una shaka kama ilizonazo Zanzibar Daima, basi kwa pamoja tusaidiane kuchukuwa jukumu letu kama umma. Vyenginevyo, hata miaka 50 ijayo haitatosha kutuvuusha kwenye bahari hii chafu. Soma habari yenyewe hapa.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.