Shoka la kuuchanga Muungano ndiyo dawa pekee kwa sasa

Miaka 47, maraisi sita kutoka Zanzibar wameshindwa kuipapatuwa Zanzibar. Hivi Rais Dkt Ali Mohammed Shein ataweza vipi kuikomboa Zanzibar? Hivi sasa Tanzania Bara imekuja na suluhisho moja tu la kulitatuwa jinamizi la Muungano. Kuifanya Zanzibar igeuke iwe kama Mombasa ndani ya Kenya kwa kupitia Muswada wa Katiba na kwa ridhaa za Wazanzibari.

Hakuna njia mbadala isipokuwa Zanzibar kujitenga na kujitangaza jamhuri. Tatizo kubwa ni kuwa kuna baadhi ya Wazanzibari wana khofu mishahara italipwa na nani na nafasi zao za baadaye zitakuwaje. Hawa ndio wa kutolewa khofu. Kama inavyosema Quran, shetani anamtia binaadamu khofu ya umaskini.

Bila ya kuinusuru Zanzibar hapa ilipofika, hakutokuwa na fursa nyengine ya kuikomboa ndani ya uhai wetu au hata wa wajukuu zetu. Zanzibar ina utajiri wake wa mali asili na watu wake ambao wametapakaa dunia Zanzibar.

Kama hatukufanya hivyo, basi tujitayarishe na mikakati ambayo tayari inayafanyiwa kazi na wapangaji kutuvurugia yote tulioyafikia mpaka hivi sasa ili tushindwe kuendelea na Agenda ya Zanzibar ili wao waweze kuendelea na Agenda ya kuulinda Muungano.

Bara wanataka lazima Muungano uhifadhiwe mpaka ifikapo 2015, na mpaka itakapofika 2020, na mpaka itakapofika 2025, na mpaka itakapofika 2030….


Na Ghassany, Aretas

5 thoughts on “Zanzibar na Muungano, dawa ni shoka la kuukata”

 1. Shoka linatisha.
  Kazi kubwa watu kuungana na kujua khasa nini kinachohitajika. GNU ina nafasi njema yakusema hili linalozungumzwa ni la Wa-Zanzibari wote wala sio la chama kimoja.
  Inaonyesha bado hatujafahamu hii KATIBA hasa ni kitu gani na nini athari ya katiba. Jee 1 au 2 au 3 ni athari ya kubakia na 2 na kwanini sio 1 au 3 sasa hapa ndipo watu kama mie Pangu bin Pakavu tunahitajia kuelimishwa.
  Nimeona wanaotufahamisha wanachukulia kuwa kila mmoja ana ufahamu, laa kuna haja ya kujifunza na iwe kwa kina na watu kupata fursa kubwa ya kufahamishwa na kujieleza.

 2. Ukiniuliza mimi nitakwambia iwe serikali moja, lakini kwa maana ya kila upande uwe na serikali yake moja na muungano huu usiwepo. Serikali mbili, tatu au hata zaidi ndani ya Muungano, si suluhisho tena kwa pande zote mbili. Wazanzibari haikuwasaidia kwa miaka karibuni 50 sasa, na Watanganyika wamepoteza utaifa wao. Suluhisho ni kutoka nje ya Muungano, kisha tukaanza mazungumzo ya ujirani mwema, kibiashara, kijamii na labda kiulinzi.

  1. ndio nakubaliana na mawazo yako lakini yakupasa ujenge hoja kwanini unataka muungano uvunjwe!
   Toa hoja pia bishana kwa hoja ili maamuzi yatakavyotolewa na wazanzabar kuhusu hatma ya Zanzibar wawe tayari kupokea matokeo yake na pia kukabiliana na matokeo yoyote yawe mazuri au mabaya kuhusu kuvunjika kwa muungano! Nakuunga san mkono lakini mwenzangu jaribu kujenga hoja nzito!

 3. mimi ni mtanzania asili yangu ni Tanganyika, nawapongeza sana wazanzibar kwa mtazamo wao wa kufikiria taifa walitakalo kwa manufaa ya watoto na wajuku wao! Ila ninachowaomba wazanzibar ni kutengeneza hoja nzito katika muungano. Ni kwanini Tanzania bara zamani Tanganyika wanapeperusha bendera ya Muungano kwenye mambo ambayo sio ya muungano mfano football, mashindano ya umiss Tanzania, IOC, WBF? KATIBA ya Zanzibar haitambuliki kama katiba ya wazanzibar pia Tanzania bara haiitambui Zanzibar kama nchi kama katiba ya Zanzibar inavyoeleza, je huu muswada wa katiba mpya umezingatiaje/umeheshimuje katiba ya zanzibar? Je kwa muswada ule uliopitishwa leo kua sheria utatoa katiba itakayoitambua zanzibar kama nchi?
  Wazanzibar nawashauri mfikirie juu ya mawazo yenu kama yataheshimiwa au laa juu ya katiba yenu mliyoibadilisha 2011!
  Kwa kweli itakua kituko kama zanzibar mmekubali kushiriki katika mchakato wa katiba mpya ile hali Zanzibar inajitambua kama nchi kamili kama katiba ya zanzibar inavyoeleza!
  Ama kweli itajulikana kama wazanzibar wana uchungu na nchi yao kama katiba yao inavyoeleza au laa?
  Je mnajua tanzania kama jamhuri ya muungano ingepaswa kua na ligi moja ya mpira wa miguu je kuna ligi ya jamhuri ya muungano?
  Madini ya jamhuri ya muungano je nyie wazanzibar mnafaidikaje ya hayo madini?
  Uchumi wa jamhuri ya muungano unaangaliwa kwa vigezo kutoka Tanganyika yaani Tanzania bara je Zanzibar inahusikaje katika hili?
  Nami kwa maoni yangu naitambua zanzibar kama nchi kwa mujibu wa katiba ya zanzibar, sasa iweje zanzibar ni nchi halafu mshiriki kwenye mchakato wa kupata katiba ya jamhuri kivuli ya muungano(Tanganyika).
  Chukueni hatua wazanzibar katika hili.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.