Siutaki kwa khiyari, siutaki kwa lazima
Naupinga kwa viriri, kwa matendo na kusema
Hauna ila ya shari, mavunoye nnovuna
Kwa huu ni afadhali, kukosa nikawa sina

Siupendi kwa suraye, ilivyo ya kidhuluma
Hakuna autakaye, hausongi ushakwama
Wanikovyosha hadhiye, nakovyokwa usimama
Kwa huu ni kheri ugwe, ugwe shi usiwe tena

Siwebu na ugeleke, kwa miye hauna mana
Bure ghali bei yake, si kitu cha kujivuna
Bure musihangaike, mukadhani ‘taungama
Mungu ‘taja wapa wage, mushindwe n’kujikuna

Hamad Hamad
17 November 2011
Copenhagen

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.