Mwachekesha!

Published on :

Mwapenda mafanikio, kazi kwenu ni laana Mwaweka matumanio, ndoto zenu za mchana Utajiri kujiotea: “Kesho ‘tawa milionea” Mwajidanganya! Mwatakangia Peponi, ela kifo mwakikana! Mwachekesha!!

Ni Mpweke!

Published on :

Ni mpweke maishani, sina wa kuniokoa Ni mpweke ni tabuni, hakuna anayenijua Ni mpweke nikizani, hapana wa kunondoa Ni mpweke nidhikini, ndugu wananihadaa Ni mpweke mashakani, hekuna wa kunitoa Ni mpweke ni ndiani, siji kwa kuelekea Ni mpweke adhabuni, sina wa kusaidia Ni mpweke Athumani, baba ameshajifia Ni mpweke hadi […]