Waziri wa Elimu wa Zanzibar, Ramadhan Abdullah Shaaban

Makala ya Sujae Sijauma Mkiji kwenye ukurasa wa Facebook, 20 Oktoba 2011

Nadhani mmesoma na kusikia kuwa Zanzibar imeingia tafrani juu ya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu. Suala hasa ni kuwa mikopo imetolewa kwa ‘aila za kifalme’ za Kizanzibari tu, — tuseme kama vile Uingereza akina Earl Spencer, akina Princess Diana hao na aila zao. Waliopewa mikopo ni watoto wa wenyewe kwa wenyewe, hakuna mtoto wa maskini humo. Hilo liko wazi, halitaki tochi wala kandili  kuliona. Wametengwa akina watoto wetu wa wanyonge, na wamepewa watoto wa wakubwa ambao wanao uwezo wa kujisomesha popote wanapotaka hata kwa miaka 10 mfululizo.

Ukweli hasa ubaguzi wa hali ya juu umepita. Rushwa na hasada dhidi ya watu wengine ndiyo iliyofanyika.

Zanzibar limezuka tabaka, tena tabaka kubwa sana bila wengi wetu kuliona hilo. Kupata ajira serikalini lazima uwe mwana wa fulani — akina Earl Spencer hao – kusoma lazima uwe akina Earl Spencer…. aila ya kifalme ya Zanzibar. Ukitaka kupewa mkopo wa benki au hizo SACOSS, pia lazima uwe mwana wa mwana wa kweli kweli ndio ufanikiwe — lazima uwe Royals, akina Earl Spencer au Queen Elizabeth na wenzake. Kama mwenzangu mshamba..huna jamaa, huna chama tena CCM, huna huyu wala yule utasota tu.

Mfano juzi tu nimekutana na kijana mmmoja amemaliza B.Sc katika IT (hana kazi, hana hana hana) amehangaika sana sana. Mimi nimemfanyia maarifa fulani hivi, na nashukuru Allah imefanya kazi….it works! sasa anasomesha pahala angalau kwa kujishikiza. Yeye kama mimi, hataki kuhama Zanzibar kwenda Tanganyika wala popote, anaumia ki-ofisa…..ndio maana anahangaishwa, anahangaika n.k. Akitaka afurahi, lazima aenda Tanganyika, atapata kazi nzuri…lakini hataki hataki hataki. Nashukuru nimemshikiza pahala…sadaka yangu kwake, na kwa nchi yangu, na kwetu sote. Allah ndiye atayelipa. Sio GNU wala SMZ, wala CUF au CCM.

Sasa, tatizo la mikopo ni kubwa sana, na anayepalilia mambo haya ni Mr.Kombo Hassan, mwenyekiti wa bodi ya mikopo na timu yake..akiwemo Dr……..fulani bina fulani (sitaki kumtaja maana mnamjua).

Kombo toke ahapo awali ni mtu complex, na ana khulka za kibaguzi, kuliko akina De Clerk (hawa ndio Boer weuzi, boers wa Zanzibar).

Maalim Kombo aliletwa Pemba kama afisa mdhamini wa wizara ya elimu Pemba…ohooooo…jamaa zetu huko wlaishika adabu, aliweza kuwasulubu sana Wapemba, na ni kipindi kile wengi walifelishwa, walimu wengi waliacha kazi, na elimu ilikufa kabisa kabisa Pemba mpaka leo. Kuna kipindi alifanya mambo sio mazuri, maana alimpekua mtoto wa kike hadharani eti anamtuhumu kuwa anaingia na ‘mabomu’ kukopia!. ilikuwa aibu na fedheha kubwa. Hawa akina Kombo, ndio hao akina De Klerk, akina Netanyahu, na at the same time, wanajifanya wao kama ndio ROYALS, wa Zanzibar na akina Earl Spencer wa Uingereza……wenyewe waingereza wanawaita ‘blue blood’ au watu waliozaliwa na vijiko mdomoni (born with silver spoon…in/into their mouth): inatumika kama ndio slang tu.
Sasa, wananchi, wanyonge wenzangu — hiyo ndio hali, vijana wetu wanalalamika , wananyimwa mikopo, na haki zao za msingi – kundi dogo sana ndilo linaloiadhibu Zanzibar kwa kila upande – kwenye siasa, kwenye uchumi, kwenywe sekta ya jamii — elimu, afya nk.

Wallah sina zaidi ila masikitiko tu, na inaniuma sana kuona akina Royals wanapewa mikopo, wanapewa mikopo na akina Netanyahu, na akina De Klerk!

_________________________________________________________________________________________________________

Makala ya Sujae Sijauma Mkiji kwenye ukurasa wa Facebook, 20 Oktoba 2011

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.