Macho angazeni, na muyafunue
Na masikioni, taka muzitoe
Midomo kosheni, musukutue
Sitaghafiruni, kwa Mola mwenyewe

Haitoki ufu, nazi ya makoma
Afadhali dafu, lingawa koroma
Ni kweli dhaifu, hana mwisho mwema
Musijikalifu, ya bui si ngoma!

Seyph Njugu
03.05.2011
Zanzibar

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.