Mtunze Vyema Mkeo

Published on :

Mke mithili ya shamba, anahitaji matunzo Msiishi kama samba, mwisho hata hapa mwanzo Muijenge yenu nyumba, kwa kuyafata mafunzo Ndoa Mola twamuomba, iwe ni cha kheri chanzo Akikosa mwanamke, ‘simshikie upanga Si magumi na mateke, mke hupigwa kwa kanga Mwanamke mbavu zake, kila siku bado changa Ukizinyosha kwa nguvu, ni […]

Ya Bui Si Ngoma!

Published on :

Macho angazeni, na muyafunue Na masikioni, taka muzitoe Midomo kosheni, musukutue Sitaghafiruni, kwa Mola mwenyewe Haitoki ufu, nazi ya makoma Afadhali dafu, lingawa koroma Ni kweli dhaifu, hana mwisho mwema Musijikalifu, ya bui si ngoma! Seyph Njugu 03.05.2011 Zanzibar

Huu Kale Ushakwisha!

Published on :

Vipi wajipaparisha, umoja ‘meukhalifu Zama zake zimekwisha, upo kundini mwa wafu Sasa ni kubahatisha, shuruti pazuke tifu Kwa nini mwalazimisha? Muungano umekwisha Watu mlibabaisha, mkajipa uzoefu Watu mkawatingisha, nyoyo ziwajae khofu Nishani mkajivisha, kujifanya watukufu Kumbe mkitugeresha, Muungano ni dhaifu! Seyph Njugu, 03.05.2011 Zanzibar