Mkakati wa kuirejesha Zanzibar kwenye neema

Published on :

KUTELEZA si kuanguka na hivyo ingawa Zanzibar imekuwa ikiteleza kwa muda wa karibu nusu karne bado inaweza kuwa na nguvu za kusimama wima tena. Nguvu hizo itaweza kuzipata endapo tu itaubadili mfumo wa mahusiano yake ya kibiashara na mataifa mingine. Nadhani sikosei nisemapo kwamba maelezo ya mwanzo ya kina yanayoihusisha […]

Ya Pwani Mchangani ni matokeo tu – 1

Published on :

WATANZANIA kadhaa wanaotoka Bara wamepoteza makazi na biashara. Makazi na biashara zimeteketezwa moto na waharibifu. Wamerudishwa nyuma hatua nyingi. Wanahitaji kusaidiwa. Hakuna anayepata maumivu makubwa kama wao. Wapo wanaofurahia kilichowakumba. Naapa wapo. Tena wengi wakiwemo wenyeji wa maeneo yale. Wapo watu wamechukia mwisho wa kuchukia. Kwa bahati mbaya, baadhi yao […]

Nacha

Published on :

Nayacha macho ya wachwa, pale zama yachunzapo Nayacha kucha na kuchwa, yachecheapo nilipo Nayo yakijua yachwa, ndo uchunzi uzidipo Nacha sitachapo kucha, yachwayo nami nayacha Hamad Hamad 26 Mei 2011 Copenhagen Kutoka Kurasa Mpya

Nazingwa

Published on :

Nazingwa ni ndugu zangu, wasonijua nilipo Waumia kwa uchungu, kila wanikumbukapo Waniombea kwa Mungu, mafanikio na pepo Numonumo ndilo langu, tenda, tarudia kuko.

Hunifai

Published on :

Wanitaka niwe wako, ati wa ubani Niwe wako mali yako, niwewo mwandani Siliwezi penzi lako, sebu abadani Bora kaa peke yako, uwe mbali nami