Takusifu tangu leo

Published on :

Sitazikusanya sifa, mabindoni haziweka Hangoja siku ukifa, ndipo haja zitamka Sifa hazitena sifa, msifiwa ‘kisha uka ‘Takusifu tangu leo, upate kujitambua Wengi huwa wasifiwa, mauti kisha wakuta Ukaona wapambiwa, sifa ziso mlahaka “Marehemu alikuwa, mtu asokasoreka” ‘Tasaidiani sifa, kwa asiye zisikia?

Kiti

Published on :

Kiti kye miliki yangu, yukaja dhalimu Yukaniondosha Yukaiba hadhi yangu, na pya majukumu Yukanivulisha Kwa nguvu za walimwengu, na sauti ya kalamu Yukajikalisha Yukitumilia

Tupendanao ni Siye

Published on :

Wao… Msimu wao ni leo, wao wao kupendana Kuvaa nyekundu nguo, na maua kupeana Iishapo leo yao, mapenzi hayapo tena ‘Kangoja mwaka ujao, wakaja pendana tena Wewe… Nimekupenda zamani, bila mwenyewe kujua Hakuweka qalbini, ja yungi ukatuliya Ikapita mitihani, ya penzi kutahiniwa Yote tukaibaini, na shahada tukapewa

Upweke

Published on :

Upweke waadhabisha, pekeyo unapokuwa Maisha huwa yachosha, la raha karaha lawa ‘Kiona watu wacheka, utasema wazomewa Upweke nao maradhi Upweke watunyofowa, ndani kwa ndani watula Wakondefu tushakuwa, kukosa zetu aila Tuyafanyayo hayawa, twadhalilika madhila Upweke nao ni nduli

Udugu na Mwananyika

Published on :

Udugu tulionao, si wa damu si nasabu Si wa ndewe si sikio, si jamaa si karabu Udugu masingizio, kuzidiana hesabu Udugu na Mwananyika, siwezi ushanishinda Mwananyika eniona, ‘mekaa nimetulia Bukheri mwana mwanana, usoni naendelea Akajifanya yu mwema, “ati” anisaidia Udugu na Mwananyika, siwezi ushanishinda