Zanzibar Yetu Sote

Published on :

Mimi nawapa hongera, tena hongereni sana Mumefanya ya busara, matendo ya kiungwana Tukisimama imara, mambo yetu yatafana Zanzibar ni yetu sote Zanzibar ni yetu sote, lazima kuitetea Tukiiacha itote, wenyewe tutaumia Tukisimama kidete, nani atatuchezea? Huu wajibu kwa wote

Dhalimu

Published on :

Mungu nakushitakia, mja wako madhulumu Sina pa kuelekea, ila kwako ya karimu Nguvu zishaniishia, taabani mahmumu Yarabi nisaidia, londoke hili dhalimu Yarabi nisaidia, londoke hili dhalimu Lipotee baidia, linisahau dawamu Likitaka nirudia, ulipofuwe uyunu Likome kunidamia, na kunyonya yangu damu

Sumu Yake Bado Kali

Published on :

Hata akivua gamba, sumu yake bado kali Nyoka huyu ndiye mwamba, kuteka zetu akili Ameshiba na kuvimba, kwa zetu rasilimali Kifo chake nakiimba, tayari kalala chali