Na Eddy Riyamy

Vifungu vifuatavyo vya Katiba ya Zanzibar, ambavyo vinapatikana katika Sura ya Tatu isomekayo kama Kinga ya Haki za Lazima, Wajibu na Uhuru wa mtu Binafsi, katika Toleo la 2010, vinahusika kikamilifu:

18.(1) Bila ya kuathiri sheria za Nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote, bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

  1. (1) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi,ama moja kwa moja au kwa kupitia Wawakilishi waliochaguliwa kwa hiari.

(2) Kila Mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu yeye maisha yake au yanayolihusu Taifa.

Tarehe 15 Septemba 2010, Katiba ya Zanzibar ya Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ilianza rasmi kufanya kazi yake. Historia ya Katiba hii ni refu na kilele chake ni pale ilipoidhinishwa na Baraza letu la kutunga sheria la Wawakilishi na matunda yake leo tunayaona. Kutokana na mfumo na “ufinyanzi” wa katiba hii imebidi, na itabidi, Katiba ya Jamhuri ya Muungano nayo pia iende sambamba na marekebisho muhimu yaliomo ndani ya Katiba ya Zanzibar.

Majuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, aliueleza umma jinsi alivyoibariki azma ya kupata Katiba Mpya na akatoa mchanganuo na aina ya ushiriki wa mchakato wa kutufikisha huko.  Jambo ambalo kila mmoja wetu amelipokea kwa uono wake.

Wito wangu hapa ni kwamba, kila Mzanzibari, awe wa rika yoyote ile, itambidi naye atumie nafasi hii kwa kutoa mchango wake, ili kujihakikishia kuwa maamuzi yatayotolewa na pande zote mbili za Muungano, yatampa kaki yake kama raia. Hii ni fursa nzuri sana ya kuweza “kushiriki” kurekebisha na kuelewa kila haki msingi katika maendeleo ya nchi yetu.

Wakati mzuri wa kuweka sawa kwa kushiriki katika kukosoa au kuboresha kila liitwalo “kero za muungano” na pia kuitumia haki hii kikamilifu kama ilivyoanishwa na Katiba yetu. Wakati pekee wa kuchagua mfumo wa Serikali na aina ya uongozi ndio wakati huu. Kuisoma na kuifahamu katiba yetu na kuyadodosa mapungufu kama yapo ni kipindi hichi cha marekebisho ya Katiba!!

Ndugu zetu wa Bara tayari wameshajizatiti na hivi majuzi Wasomi wamejikita kuanzisha mijadala yenye format ya Town Hall Meetings ili Kudodosa na Kushadiisha Katiba waipendayo. Natoa Wito na Ombi kwa Wasomi Wetu na Bobea wote wa fani ya Katiba na Experience wa fani hii ndani na nje ya nchi kwa pamoja tuyawache yote tuliyonayo na tushiriki kikamilifu kwenye kadhia hii.

Natoa Ombi la Ndugu zetu Viongozi wa zanzinet haraka na halllaaan leo kwa kesho Ukumbi wa KIJIWE uazimwe na paruhusike “OpenTown Hall” CyberMeeting ili Usiku na Mchana tujadiliane na kubadilishana mawazo na kusaidiana kupanua wigo wa Kadhia hii adhiim na muhimu kwa Utaifa wetu na Nchi yetu kwetu na Vizazi vyetu!!

Mtandao na Mawasiliano yatumike kwa umuhimu na aina yake katika hili na uhuru wa maoni wenye natija na mbinu za kudumu na Kheri kwa nchi yetu na Taifa letu iwe ndio Kipamubele,umuhimu wa pekee kwenye kila lenye njia nzuri kwa mustaaqbaal wa Nchi yetu Zanzibar kwa taratibu tulizowekewa na kujiwekea kwa Natija yake iwe ndio chachu na Hatua nzuri za Busara ndio iwe kipaumbele na mijadala itumike kama vigezo kwa viongozi wetu.

Wito kwa waandishi wetu wa habari ambao wengi wamo humu na vyombo vyao ndivyo vitumiwavyo katika kutugawa na kutudanganya ni kutizama wapi watahitaji kutoa kipaumbele kwa nchi yao au utashi wao kwa Vyombo vyao vingi vikiwa haribifu kwa kupotosha ukweli. Tutapeleka ombi makhsusi kwa Serikali yetu SUK kuweka kiungo ili kila Maoni mazuri na yenye natija yapatiwe upembuzi yakinifu na yanfanyiwe kazi stahiki.

Kwa leo natoa chamgamoto nikisubiri kwa hamu mchango wa wenzangu kote mlipo duniani!!

Ningeomba wale wenye soft copy ya katiba zetu na Articles of The Union na Ammendments zake.

Calling Dr Harith Al Ghassany et al. ziwekeni humu zijadiliwe kwa kina. Wale wanaoona kadhia hii haiwahusu au haina maana kwao basi iwe hivyo lakini kwa wale wanaoujua umuhimu na busara zinazohitajika basi haraka tuwe mbele tena mbele san asana tu kadiri ya speed tutoweza ku take off!!

Imechukuliwa kutoka Ukumbi wa ZanziNet

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.