TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI 12 Disemba, 2009

‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’, kitabu kipya kuzinduliwa rasmi

Wapendwa Wanahabari,

Ufunuo mpya juu ya uhalisia wa Mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar mwaka 1964 sasa umo kwenye maandishi. Matukio na uchambuzi wa matukio hayo, ambayo yamekuja kuubadilisha kabisa mstatili wa mambo katika dola ya Zanzibar na majirani zake unawekwa wazi katika kitabu hiki kipya na cha aina yake, ambacho hakijawahi kuandikwa mfano wake kwa takriban nusu karne nzima iliyopita.

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru ni matokeo ya utafiti na ufuatiliaji wa kina wa Dkt. Harith Ghassany ambao ameufanya kwa zaidi ya muongo mmoja. Sasa kitabu kiko tayari na ndani yake muna maelezo ya kinagaubaga juu ya nini kilitokea, vipi kilitokea, wapi kilitokea, kwa nini kilitokea na, juu ya yote, nani hasa aliyekifanya kitokee na kwa malengo gani. Kinailezea upya historia ya Zanzibar, hasa ya tukio lile la Mapinduzi ya 1964, kwa kutumia mwanga na maneno ya wahusika wenyewe.

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru kimeandikwa kwa lengo moja kuu: udadisi mpya wa mambo. Kwa kutumia maneno ya mwanafalsafa wa Kiyunani, Socrates, “Maisha yasiyoathminiwa, hayana maana kuyaishi.” Mtazamo wa wananchi wengi wa kawaida, wanasiasa, wasomi na watafiti wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hata walioko nje, umekuwa wa aina moja panapohusika udhati wa Mapinduzi ya 1964 na, hivyo, historia nzima ya Zanzibar na Tanzania. Kitabu hiki sasa kinakuja na upande mwengine wa hadithi, na kwa hakika, upande halisi wa hadithi ya historia ya Zanzibar.

Hiki ni kitabu kinachopaswa kusomwa na kila anayeutaka na kuujali ukweli. Ni kitabu kinachostahiki kuwa sehemu ya marejeo ya wasomi na watafiti wengine walioko vyuoni na kwenye taasisi mbalimbali za kitaaluma. Lakini zaidi, kwa wepesi wa lugha yake na mtiririko wa hoja zake, ni sehemu ya fasihi inayopaswa kuwa hazina kwa kila familia.

Kuagizia kitabu hiki na au kupata taarifa zake zaidi, jiunge na mtandao wa Facebook kwa kubonyeza hapa.

Mnakaribishwa nyote.

6 thoughts on “‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’, kitabu kipya kuzinduliwa rasmi”

  1. Nimekisoma kitabu chote kwa muda wa siku mbili mfululuzo.Mwandishi wa kitabu inavyoelekea ni jamaa ya sultan alieondolewa madarakani baada ya wazanzibar wazawa kuchoka kunyanyaswa na waarabu.

    Kuna mahali anatukuza uarabu as if mzanzibar mmakonde hakuwa na sifa ya kuitwa mzanzibar.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.