1. ZANZIBAR NI NCHI NA TAIFA HURU ZANZIBAR DOLA,TAIFA NA NCHI HURU

1.1 Utangulizi

1.1.1 Zanzibar ya kale

Kiasi cha miaka millioni mia moja na khamsini (150 million) iliyopita Barahindi ilikuwa
ni sehemu ya Bara la Afrika na hatimae baada ya mgawanyiko wa pole pole wa ardhi,
Barahindi ikaelea elea hadi kujiegeza na ile milima leo ijulikanayo kama Milima ya Himalaya.
Ardhi na nafaka za Bara Hindi, miti na misitu yake, ufukwe wake wa pwani
uliyojaa minazi, viungo vyake (pili pili, mabizari, karafuu, mdalaasini, hiliki, achari tofauti
n.k.), matunda yake (shoki shoki, madoriani, matufaa, embe), ndege wake, vinyama
vyake (komba, manyani, makima na tumbili), wanyama wake (tembo na chui) vyote hivi
vimefanana mno na hali ya Zanzibar, ingawa tembo na chui, kama vile nyangumi, kasa,
kobe na mamba, wametoweka Zanzibar kutokana na usasi wa kibiashara wa vipusa.

Mifano ya ardhi, wanyama na kadhalika kama hao wanaonekana sehemu mbali mbali za
mashariki ya karibu na za mashariki ya mbali kama Sri Lanka, Singapore, Malaysia,
Indonesia n.k.; wakati Malagasy, Ngazija na Mroni, Shelisheli (Seychelles), Sokotra
n.k. zikiwa mashariki ya kando, zina mlingano kama huo na Zanzibar. Kuna baadhi ya
wataalam wananakili kwamba visiwa viwili vya Unguja na Pemba vinatokana na asili
tofauti, wataalamu hao inaonyesha wamesahau kwamba asili ya Barahindi inaambatana
na ufukwe wa Mashariki ya Afrika, vile vile wataalam hao, na wale wanaowakariri,
kwa sababu zao za kisiasa, wakijaribu kuuhalalisha Muungano, wanasahau tofauti ya
ardhi ya kusini Unguja yaani Makunduchi/Mtende/ Kibuteni/Kizimkazi, zikiwa na udongo
mwekundu na mawe na majabali, ikifananishwa na ardhi za Unguja ya kati na ya kaskazini
zikiwa na rutuba tofauti. Kwa mujib wa historia ya kale ya enzi zetu, kuambatana na maandishi ya “Perpulus of the Erythran Sea” na “Claudius Ptolemy”, Edris, Chronicles of Kilwa n.k.

Zanzibar (Menouthias Island) ikijulikana kama nchi iliyokuwa na biashara na nchi mbali mbali za Arabuni, Barahindi, Uchina na Japan tokea enzi za kale. Katika maandishi hayo ambayo ni katiya ya zamani kabisa kuhusu Afrika ya Mashariki hakujatajwa nchi au taifa lijulikanalo kama Tanganyika. Hadi April 28, katika mwaka wa 1885, sehemu ya Mrima ikijuli kana kama ni Mamlaka ya Bara ya Sultani wa Zanzibar. Tarehe hiyo yaani 28 April, mwaka 1885 ndiyo tarehe Serikali ya Kijarumani alipoamua kuzinyakuwa maili 60,000 za eneo la Mrima. Baada ya hapo ndipo makubaliano baina ya Mngereza na Mjarumani yakafikiwa, Muingereza ikachukuwa Hegoland, kama kiinuwa mgongo, na Mjerumani kuchukuwa Mrima. Unyakuwaji wa Wazungu wa ardhi ya Bara la Afrika, ulitokea baada ya Mfalme wa Belgium kuitisha mkutano wa nchi zilokuwa zikiongoza Ulaya katika mwaka 1876, huko Brussels, Ubelgiji. Muda mrefu sana kabla ya hapo Zanzibar ilikwisha julikana kama ni nchi, taifa na dola kamili, kinyume na Tanganyika.

2. DOLA LA ZANZIBAR

2.1 Dola la Zanzibar

Zanzibar ikiwa ni taifa kamili, lina haki kamili ya kuwa na vyama vyake huru vya kisiasa
bila ya kulazimishwa kuungana na chama chochote cha Taifa la Tanganyika, ambalo vile
vile ni taifa huru. Taifa, Dola au Nchi haziundwi kutokana na ndoto za mtu mmoja au
watu wachache. Ili taifa litambulike kama taifa, kunahitajika sifa maalum za lazima na
sio za kulazimishwa, kuzushwa au kubuniwa. Kwa mujib wa sifa za kimataifa Zanzibar
ni nchi na taifa kamili – bila ya kujali nani ana au wanabuni vyengine. Nchi ye nye
mipaka inayotambulika kimataifa, na kuwa na watu wenye sifa maalum za nchi hiyo, kwa
kusema lugha inayotambulika kuwa lugha ya au za nchi hiyo, yenye utamaduni na kabila
au makabila ya nchi hiyo, yenye jamii halisi na makhsusan, siasa inayoifuata na uchumi
wake wa kujitegemea wenyewe, inatambulika kama ni nchi, aidha ikiwa huru au ikiwa
imetawaliwa, yaani kama Zanzibar ilivyokuwa chini ya ukoloni wa Kiingereza (na hata
ukoloni wa sasa). Nchi kama hiyo ikiwa huru inatambulika na Umoja wa Mataifa kama ni
Nchi na Taifa huru.

Bila ya haja ya kukariri zaidi Zanzibar inazo sifa zote ambazo zina hitajika ili nchi itambulike kama taifa huru, pamoja na kuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa, ambacho kipo wazi tokea kuundwa Muungano katika mwaka 1964. Kabla ya kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa Tanzania, Zanzibar iliwekewa pingamizi na vikwazo vya
kutounda vyama vyake huru, na ilihitajika na kulazimika kwamba vile vyama vitakavyoundwa viwe na sifa za “Kitaifa” na visiwevya kijimbo, kidini n.k. kama alivyobuni Julius K. Nyerere. Kwa vile nchi ilikuwa chini ya utawala wa chama kimoja chenye kawli na amri ya mwisho, Wazanzibari na Watanganyika ikawabidi, shingo upande wafuate kauli na amri ya watawala wao, wananchi wa nchi mbili hizo wakisubiri kwa hamu kubwa, siku mambo yatakavyobadilika, na hatimae kuyabadilisha masharti hayo. Wengi zaidi ya Wazanzibari na Watanganyika, ambao pia ni wenye sifa za kuwa nchi na taifa huru,
hawakuamini kwamba Tanzania ni nchi au ni taifa, kama isemekanavyo. Tanzania ni nchi
na taifa la kubuni, kama taifa la ndotoni na sio nchi au taifa halisi kwa mujib wa tafsiri za
kimataifa zinavyotambulika.

Tanzania si nchi wala si dola, bali ni Muungano wa nchi/taifa mbili huru zote mbili zilikuwa na uwakilishaji kamili katika Jumuiya ya Madola.Muungano wa Tanzania ni sawa
na Muungano wa Misri na Syria,”United Arab Republic” ambao umeshavunjika kwa hivi
sasa na kubaki jina tupu, na kila nchi kuwa na mamlaka yake wenyewe.

Mfano mwengine ni Muungano au shirikisho la Kisovieti-ambalo limeshamungunyika na mfano mwengine ukiwa Muungano/shirikisho la iliyokuwa Yugoslavia;- tofauti na hali hiyo ni Vietnam ambayo ni nchi mmoja na imeshaungana, wakati Korea ikiwa na serikali mbili katika nchi moja zilizotengwa na ukoloni kwa maslahi ya kikoloni. Muungano wa Tanzania ni sawa na muungano wa Uingereza na Ireland ya kaskazini yaani baina ya mtawala na mtawaliwa, ingawa Ireland inaweza kuunda vyama vyenye sifa ya Kiireland tofauti na Zanzibar.

Mtu au Chama tawala kinaweza kulazimisha watu wafuate na kuitii fikra au sheria fulani,
lakini hawawezi kulazimisha watu kuamini fikra hiyo ya kubuni, kama vile mtu anaweza
kula zimishwa kuamini kuwa nyoka ana miguu, lakini kutoweza kumfanya mtu huyo
aamini hivyo. Mzanzibari ni rahisi kulazimishwa kukariri kuwa Zanzibar si nchi wala
dola bali si rahisi kumfanya aamini hivyo. Kulazimisha uundaji wa vyama viitwavyo vya kitaifa baina Tanganyika na Zanzibari ni kitendo kisichokuwa cha kihalali, kisichokuwa
na msingi na ni kitendo potofu. Hatua nyingi za kisiasa ni hatuwa za muda na za kupita,
sio hatua za kimaumbile; ni hatua zinazotungwa na kupitishwa na binaadam na kila kinachoundwa na binaadam kinaweza kubadilishwa yaani si cha milele au cha kudra na lazima kama roho.

Mwenye Enzi Mungu ndie anayeumba binaadam na kuwapa roho na maisha,
kuwapa uume na uke, na kuwapa makabila na sura ili wajuane. Vile vile kuwapa vitongoji,
vijiji, mashamba na miji, nchi na mataifa ili waishi pamoja, wajiongoze, kujitawala
na kuheshimiana. Ikiwa mtu au watu watachukuwa wadhifa wa Mwenye Enzi Mungu,
ata au watakuwa wanakosea na yale watakayo ya jaribu kuyabadilisha yatawashinda na
hatimae kuwarudi. Nchi, kiini cha taifa, haiundwi kama ilivyokuwa watu hawaundwi
bali huumbwa. Majaribio ya kutaka kuliumba taifa la Tanzania yamezidi kuwa katika
sarakati ’lmawti (likikata roho) tokea Watanganyika walipozidi kuvinjari na kulidai taifa
lao wenyewe na Bunge lao wenyewe. Khatua hii imedhihirisha zaidi kukuwepo kwa
mataifa mawili huru, kinyume na madai ya hapo kabla kwamba Taifa lilikuwa ni moja tu.
Sasa wimbo wa kuwasingizia Wazanzibari kutaka kujitenga umeanza kupunguwa kasi na
ukweli wa mataifa mawili huru yaliyoungana, kuzidi kujichomoza. Zaidi ya yote hayo
mara nyingi watu husahau kwamba Tanzania si nchi bali ni: “Jamhuri ya Muungano wa
TanZania, “iliyoundwa kwa makubaliano ya watu wawili tu, Nyerere na Karume.

2.2 Muungano – kisheria na kisiasa

Mijadala mirefu na mingi ya kisheri imekaririwa kuhusu Muungano wa Tanzania, karibu
yote ya mijadala hiyo ikipinga uhalali wa kisheria wa uundaji wa Muungano huo. Wengine
badala yake kuuita uharamia wa kisheria na wa kisiasa.

Uchambuzi huo wa kisheria umesaidia kufafanua mambo mengi ya maana, ingawa bado
tunasubiri kauli sahih za baadhi ya wanasiasa waliyoshuhudia namna ya utekelezaji wa
tukio hilo. Kwa sababu ya pungufu za uhuru wa kutoa maoni na demokrasia kwa jumla,
mjadala wa suala hili muhimu wa kisiasa umekuwa pungufu na dufu. Kuna mambo mengi
mno ambayo hayajagusiwa kabisa kuhusu misingi ya uundaji ya Muungano huu. Itakuwa
ni jambo la maana sana ikiwa kutatupwa mchanga wa moto ili kuzidi kushajiisha mjadala
wa suala hili muhimu sana. Njia moja wapo, ambayo sio lazima ya pekee, itakayosaidia
kutupia nuru suala hili ni kujaribu kulidadisi suala hili kwa historia ya kisiasa ya chama cha Afro Shirazi Party, uundaji wake, siasa na maisha yake, kushiriki kwake kwenye mapinduzi na katika Baraza la Mapinduzi na hatimae kuunganishwa na TANU.

2.3 Misingi ya vyama vya kisiasa Zanzibar

Ili kupata ufafanuzi kamili, madhubuti na wa kinaganaga kuhusu asili na misingi ya vyama
vya kisiasa Zanzibar, hapana budi kutafuta msaada kutokana na historia ya Zanzibar kwa
jumla na historia ya tawala zake makhsusan. Historia ya Zanzibar hasa ya kisiasa ina
upungufu mkubwa, na inahitaji uchunguzi na uchambuzi wa makini wa kisayansi na ulio
huru. Uchunguzi huu ni mgumu sana kwani mara nyingi utafiti wa historia unapambwa
kupendeza utawala uliyopo kama utakuwa unaandikwa wakati utawala wenyewe ukiwa
khatamuni, au kuambatana na aina ya siasa au idiologia ya muandishi au ya utawala unaohusika.

Kuna watu wengi wana nadharia ya kuweza kuandika au kushiriki katika uandikaji
wa historia ya punde ya Zanzibar, lakini ama wamekuwa wakiogopa kutokana na utawala
katili wa Zanzibar au utawala kandamizi wa Muungano, au kupungukwa na hamasa za
kisiasa waliyokuwa nazo watu hao kiasi cha miaka 30 na 40 iliyopita. Kuna wengine wanachelea kuandika kwa sababu ya mazoefu mabaya ya usiri au kungojea mabadiliko
ya serikali, mambo ambayo ama yanapotosha historia kutokana na upungufu wa kuweza
kukumbuka au kutokana na vifo ama vya kawaida au vya kuuwawa kutokana na sababu
za kisiasa. Vile vile usiri huo unasaidia serikali za kikandamizaji kuzidi kubaki katika
utawala kwa vile wananchi wanakuwa hawaujuwi ukweli sahih uliyopitika nchini.

Ni matumaini ya kijitabu hichi kwamba, wale wenye ujuzi wa kihistoria muhimu watajitokeza na kuchangia kumbukumbu muhimu kama hii na kwa hivyo kuwafichuwa wale wanaoandika historia ya uwongo na ya kupendeza watawala. Ni jambo la maana kwa
hivyo kudokeza kidogo juu ya mgawanyiko wa jamii ya Kizanzibari wa tokea enzi za kale
ili kufahamu mfumo wa matabaka yaliyosababishwa na mgawanyiko wa jamii hizo. Hichi
ni kijitabu kidogo ambacho hakiwezi kuieleza au kuifafanua historia ya Zanzibar ambayo
ni nyingi na ya kupepea. Kijitabu hichi hakidai kutoelemea upande fulani wa kiidiologia,
ingawaje kinajaribu kwa kadri inavyowezekana kuchambua hali halisi na ya kinaganaga
ili kutoa mwangaza katika mambo fulani ambayo ingawa wengi wanayajuwa, lakini bado
hawajaamuwa kuyaeleza.

2.4 Mzizi wa fitina

Mzizi wa fitina wa siasa ya Zanzibar uko katika historia, na kabla mzizi huu haujakatwa
hapatokuwa na maendeleo ya maana ya kuwanufaishaWazanzibari kwa jumla. Zanzibar ni
nchi yenye historia ndefu na nyingi, hasa kufananisha na eneo lake, ilitajirika kutokana na
maingiliano yake na kila aina ya watu wenye sifa mbali mbali bora na za kupigiwa mifano,
watu waliyotoka sehemu mbali mbali ulimwenguni. Kuingiliana kwa Wazanzibari na staarabu mbali mbali tokea nyakati kabla kuzaliwa Nabii Issa I‘bn Mariam, kumeifanya
Zanzibar iwe sehemu mojawapo yenye sifa njema na ustaarab wa kuwekewamfano. Katika
watu wa kale waliyotajika na waliyovuma kwa kiwango cha juu cha ustaarabu na elimu
ilikuwa ni Machina, Wahindi,Wamisri naWagirigi. Zanzibar ilifaidika kupata matunda ya
staarabu hizo tokea enzi za kale. Zanzibar ilitembelewa na wataalamu na wafanya biashara
na wavuvi kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni, na baadhi yao walipendezwa na
majira hayo na utu wa majira hayo na kuamuwa kugeuza Zanzibar makwao na kutotaka
kurudi tena walikozaliwa, hapo wakaowa na kuzaliana na kuchanganya damu. Wengi wa
hao walitoka sehemu za Arabuni, Uajemi, Barahindi, Uchina n.k. Wengi wao walikuwa ni
wafanya biashara, wavuvi, mafundi, maagenti, wataalam na wana ahli l kitaab. Misafara
hiyo na uhamiaji huo ulitokea zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita kabla ya utawala wa
Mashirazi, Wareno, Waomani au Wangereza; ingawa kuja kwa watawala hao baadae
nako kulichangia na kuhaibisha ustaarabu na utamaduni wa Zanzibar kwa kiwango fulani.
Wahamiaji kutoka Arabuni, Barahindi na Shiraz walihamia Zanzibar kwa sababu tofauti.
Wahamiaji wa Kishirazi wa mwanzo katika Afrika ya Mashariki wanasemekana waliwasili
Afrika ya Mashariki katika karne ya sita (The Arab Chronicles of Kilwa).

Wahamiaji ha wa walihama makwao ama kwa sababu za kisiasa, kidini au kibiashara. Katika karne ya 10 baada ya vita vya ukhalifa huko Uajemi, Sultan Hassan wa Shiraz pamoja na wanawe sita wa kiume na majahazi yao saba kwa jumla yalitweka kutoka Shirazi, huko Uajemi, leo kujilikanako kama Iran, yakaelekea Afrika ya Mashariki. Baada ya ku wasili pwani pwani mwa Afrika ya Mashariki Washirazi hawa wakaendeleza utawala wao wa kifalme katika Afrika ya Mashariki. Ishara na kumbukumbu zake bado ziko dhahiri pwani pwani mwa Afrika ya Mashariki yote. Ukumbusho madhubuti katika visiwa vya Unguja na Pemba ni ule wa Ufalme wa Mwinyi Mkuu, mfano mwema wa Mzanzibari aliyechanganya damu akiwa na asili ya Kishirazi na Kizanzibari.

Karne tano zilipita kabla Wazungu kuishitukia Afrika ya Mashariki na Kati na mapambano makubwa ya mwanzo aliyoyapata Mwinyi Mkuu yalikuwa alipopambana na mkoloni wa Kireno (Ruy Lourenco Ravasco 1503) katika Unguja Ukuu, ambako kwa wakati huo ulikuwa ndio mji mkuu wa Zanzibar na baada ya kushindwa na kusalim amri Wazanzibari hao na Mfalme wao walilazimishwa kulipa kodi ya kila mwaka kwa mfalme wa Ureno. Katika mwaka 1509, mkoloni wa kireno, Duarte deLemos, aliwasili Zanzibar kudai ushuru au kodi hiyo kuto ka kwa Wazanzibari, ambao waligoma kulipa kodi hiyo, na hapo pakapigwa vita dhidi ya majeshi ya Kireno yaliyokuwa na silaha bora zaidi za mabunduki na mizinga. Wazanzibari wakashindwa kwa mara ya pili, kukimbilia misituni, huku nyuma Wareno wakaendelea na kwiba, kunyang’anya, kuteketeza na kufisidi. Vita hivyo vilimfanya Mwinyi Mkuu akimbize watu wake na ufalme wake kutoka katika ufukwe wa bahari na kujifichia maporini na hatimae kujenga ngome yake huko Dunga.

Kwa mara ya mwanzo, Wareno walipowasili Afrika ya Mashariki walistaajabishwa sana
na kiwango cha juu cha ustaarab. Kukuta mavazi ya haiba, ya lasi na haririr ya tunu na
tamashana, ujenzi wa sifa na ustadi wa kifani, uliyopendeza na kupambika. Wakakuta
ustaarabu uliyozalika kutokana na maingiliano ya karne na karne baina ya Afrika ya
Mashariki na madola ya mashariki ya kati hadi mashariki ya mbali, kutoka Yemen hadi
Uchina na Japan. Wareno, kabla kufika Afrika ya Mashariki, walipitia Afrika ya Magharibi,
na walitarajia kuikuta Afrika ya Mashariki katika kiwango cha ustaarabu sawa na ule
waliyoukuta Afrika ya Magharibi, lakini walistaajabishwa mno na kupigwa na mshangao
kukuta majenzi na mavazi ya haiba na kupendeza kabisa, na Wanaafrika wa Mashariki
walidharau kwa kejeli thamani ya zawadi walizoletewa na Wareno hao. Zanzibar kwa
wakati wote kabla ya hapo, yaani kabla hata ya kuzaliwa kwa Nabii Issa, lilikuwa ni soko muhimu sana katika Afrika ya Mashariki na ya Kati, na kushughulika na biashara ya
vipusa, ngozi, nyangumi, miti, nafaka, mbao n.k.

2.5 Utumwa

Utumwa ni mojawapo katika njia za kuzalisha mali iliyotumika sehemu zote ulimwenguni.
Wazungu mwanzo kuwafanya wazungu wenziwao watumwa, Machina kuwafanya
Machina wenzao, Wahindi kuwafanya wahindi wenzao watumwa na kadhalika. Chanzo
cha utumwa katika jamii zote ilikuwa ni kwa kawaida kushindwa vita, kudaiwa deni
na kutolipa, adhabu kufuatia uhalifu n.k. Wazungu baadae wakasahau kwamba wao
ndio waliyokuwa wahalifu wakubwa kabisa katika kuendeleza utumwa wa watu wao
wenyewe na hatimae wa Waafrika kwa niaba ya msalaba, baadae wakajaribu kuudanganya
ulimwengu kwamba wao ndio waliyoondosha utumwa, kutokana na wema wao.
Vile vile walisahau kusema kwamba walipopendekeza kuondoshwa kwa utumwa, ilikuwa
kwa sababu utumwa haukutia faida tena za kiuchumi na ulibidi ubadilishwe na uzalishaji
mali mpya wa “kibwanyenye” uliyoweza kukamuwa wanyonge faida kubwa zaidi bila ya
huruma. Jambo jengine wasilotuambia ni kwamba walikuja makwetu kwa madhumuni
ya kutukalia vichwani kwa kututawalia kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni, kututia
chemere na kutunyonya, na sio kutufanyia wema au kututowa utumwani. Kwa njia ya kudai
kukandamiza utumwa manuwari za Kiingereza ziliteketeza na kuchoma moto madau
na majahazi ya wafanya biashara yakiwa yalikuwa na watumwa au bila ya watumwa. Walidai
kwamba vile vyombo vilivyokuwa havina watumwa vilichomwa moto kwa sababu
eti vyombo hivyo havikufaa kusafiriwa. Wakati ukweli wenyewe ni kwamba Maafisa hao
walipata mapesa mengi kutoka serikalini walipoteketeza vyombo hivyo, wakati huo huo
11
maafisa hao waliiba na kunyanganya mali za watu kinyume na sheria. Madhumuni hasa ya
khatua hizi ilikuwa ni kukata mshipa wakitovu wa biashara baina ya Afrika ya Mashariki
na nchi za Mashariki ya Bahari ya hindi. Kwa njia kama hizo Mngereza akaweza kuwa
na uhodhi wa uchumi wa Afrika ya Mashariki na Kati, na kuiuwa biashara ya makarne na
makarne baina ya Afrika ya Mashariki na nchi za Bahari ya Hindi. Biashara alizoziwacha
Mngereza kuendelea zilikuwa ni za papa, nguru na n‘gonda, majamvi na mikeka. Wangereza
wakati wakidai kupiga vita usafirishaji wa Watumwa kutoka Afrika ya Mashariki,
wakati huo huo waliruhusu uuzaji na uzalishaji mali waWatumwa katika Bara la Afrika ya
Mashariki na kujinufaisha kisiasa na kiuchumikutokana na faida za utumwa. Ilidhihirika
mwishoni kwamba azma ya ukandamizajiwa utumwa ilikuwa ni kuitawalia Zanzibar, na
kwa vile Zanzibar ilikuwa kiini chautawala na biashara ya Afrika ya Mashariki na ya Kati,
alipiga ndege wawili kwajiwe moja, na kuweza kuuzitawalia nchi zote za sehemu hizo vile
vile.
Kama sehemu nyengine ulimwenguni, Afrika ya Mashariki na Kati ziliendeleza njia ya
kuzalisha mali na biashara ya Utumwa, na Zanzibar ikageuzwa bandari na sokomojawapo
muhimu la watumwa. Bandari, soko na vituo vyengine muhimu vya jiranivikiwa Bagamoyo,
kwengineko ni Tabora, Kilwa n.k. Wengi wa watumwa hawa amawalibaki Mrima,
kusafirishiwa Arabuni, Uajemi, Barahindi na Visiwa jirani kamavile Seychelles, Re’union,
Ngazija, Mauritius, wengine hadi Marekani, Brazil n.k. Baadhi yao kufanya kazi katika
mashamba ya karafuu, wengine kufanywawachukuzi, mahamali, watumishi wa majumbani
na kazi kama hizo ndogo ndogo.Ingawa Zanzibar ilikuwa bandari na soko muhimu
la watumwa, watumwa hawahawakutoka Zanzibar bali walitoka Mabara ama kutokana
na kusakwa na kuwindw ana wachuuzi wa watumwa wa Kiarabu na wa Kienyeji, au
kuwa mateka wa vita bainaya machifu, ufalme na makabila mbali mbali yaliyopigana vita,
12
kama vile Wahiyao,Wamakonde, Wamakua, Wandonde n.k., au kutokana na kushindwa
nguvu aukutegwa kwa ujanja wa wenzao. Inasemekana kwamba hakuna Mzanzibari asiliaaliyeuzwa
kama mtumwa, na ndio maanaWazanzibari asilia si watu wanaolimbikizachuki
za kitumwa, kirangi au za kikabila zenye misingi ya kitumwa. Katika mwaka wa kulipitishwa
sheria ya kukomesha biashara ya utumwa Zanzibar na watumwa wote kupewa au
kununua uhuru wao. Wengi wa watumwahawa hatimae walirudi mabara na wengi ya wale
waliyobaki walishiriki kikamilifu katika jamii ya Kizanzibari hata kabla ya kuondoshwa
utumwa na kuwa na hisiakamili za Kizanzibari. Ingawa Mngereza akidai kuukomesha
utumwa tokea wakatihuo lakini kwa kweli Wafaransa na Wareno waliendeleza biashara
ya watumwa baadaya hapo na Mngereza hakuinuwa hata ukucha kuwazuwiya wazungu
wenziwe katikabiashara hiyo ovu. Ingawa sheria ya kukomesha utumwa ilipitishwa katika
mwaka 1873, kuambatana na siasa ya ASYL, ya serikali ya Zanzibar na ya CCM, wataliihadi
leo wanazugwa kwamba ati Zanzibar kulikuwa na utumwa hadi 1964.
Utumwa ni aina mojawapo ya njia za uzalishaji mali, ambayo ni ya kashfa, na kwamujib
wa sifa za utukuzaji wa ubinaadam, waliyokashifika zaidi wakiwa wale wauzajina hata kuliko
watumwa wenyewe, kwani wao ndio waliokuwa wapungufu wa sifaza utut wa kibina
ada. Utumwa ulitumika ulimwenguni kote na kama historiainavyotukariria, nyenendo za
uzalishaji mali hubadilika wakati njia bora zaidi yauzalishaji mali inapozalika. Utumwa
haukuondoshwa na Uingereza au nchi za ulaya kwa jumla, kama nchi hizo zinavyodai
wanapojaribu kujipa sifa za utu bora. Nchiza Ulaya zilitumia njia za uzalishaji mali
za utumwa katika kunufaisha matabaka yajuu yaliyokuwa yaki tawala makwao. Mfano
dhahiri niWaafrika waKimarekani wahuko Marekani, waliyoujenga uchumi wa Marekani
kwa damu na jasho lao, wakatitabaka lao likiselelea nyuma. Wazungu, hata baadhi ya jamii
zao wenyewewalizigeuza watumwa vile vile. Wakati utumwa ulivyokuwa haunufaishi
13
tena uchumiwa matabaka hayo, kwa vile kwanza mmilikaji watumwa ilibidi anunuwe watumwa
n ahalafu awagharimie makaazi, chakula, nguo, matibabu na mapumziko wakiumwa
namahitaji yao mengineyo, njia yenye faida zaidi ya uchumi ilibidi ichukuwe pahalapa
uzalishaji mali wa utumwa. Maendeleo ya jamii kwa jumla hutokana na nyenendompya
za kupeleka njama mpya za kuendeleza maisha, njama mojawapo ikiwakuendeleza njia
bora za uzalishaji mali. Kwa hivyo tokea siku za “primitivecommunalism”, (yaani maisha
ya kijamii ya enzi za kale na kale, kama vile uwindajiwa pamoja wa jamii), mabadiliko
ya jamii yalitokana na uendelezaji wa njia zakuzalisha mali. Ustadi wa kazi kama vile
wengine kuwa wavuvi, wengine wasasi,wengine kuwa mafundi na wengi-ne wahunzi ni
kati ya maendeleo ya kijamiiyanayoleta upigaji khatuwa mbele wa kijamii.
Wanawake, kutokana na upungufu wao wa nguvu za kimusuli, kwa wale waliyoishi karibu
na mito, maziwa na bahari walitega samaki, lakini wengine walishughulika zaidi na kazi
za uvunaji wa nafaka mwitu na uchumaji na ukusanyaji wa matundamwitu. Hizi ni kati ya
khatuwa za mwanzo za uendelezaji wa njia za kuzalisha maliza ukulima. Kujishughulisha
na ukulima wa kale kulitokana na ushupavu nauangalifu wa wanawake, ambao zaidi ya
kwamba wakilea watoto, na kukusanyavyakula mwitu, walitanabahi kwamba zile kokwa
za matunda nafaka na walizokulaambayo wakitupa tupa sehemu walizo piga kambi au
kuishi, hatimae zilitowa michena kutoa matunda na nafaka. Wanawake kwa ujasiri wao
ndio waliyokuwa watu wamwanzo, kutambua umuhimu wambegu na kuanzisha kilimo,
maana baada ya hapandio walipoanza kupanda mbegu na miche na hatimae kukuza uchumi
wa kilimo,kuanzisha kuhodhi, rasilmali na kuzidisha uwezekano wa ustadiwa kazi mbali
mbalizilowezekana kwa sababu ya maendeleo hayo. Zile sehemu zilizokuwa na wanyama
wengi wa kusaka na samaki wengi wa kuvua, ziliwafanya wasasi na wavuvi wa siku hizo
kuacha au kupunguza tabia ya kuranda randa kutafuta chakula. Baada yakwamba kupiga
14
kambi kulisaidia kilimo, kuliwezesha vile vile, kama tulivyoona hapo juu, ukuzaji wa aina
ya makazi mbali mbali kama vile mafundi wa kutengenezasilaha, kutengeneza mitumbwi,
mitego hatimae wahunzi na mafundi mbali mbaliwakazalika. Utengenezaji wa vifaa mbali
mbali uliendeleza ulimaji, usasi, uvuvi,ujenzi n.k.
Haya ndio aina ya mabadiliko katika jumuiya yanayoleta maendeleo katika jamii
nahatimae kuleta mabadiliko ya uzalishaji mali wa aina mpya. Haya ndio aina yamabadiliko
ya uzalishaji mali ambayo hufanya mtindo wa uzalishaji mali fulani kamavile
wa utawala kubadilika. Njama mpya hizi huwa kwa desturi ni alama yamaendeleo ikifananishwa
na nyenendo zilizo kwisha pita. Utumwa kwa vile ulikuwa uzalishaji mali
kongwe na zorota ulibidi ubadilike napahala pake kuchukuliwa na uzalishaji mali wa
“Kibwanyenye/Kimwinyi”. Uzalishaji huu wa mali ulimfanya mtumwa kuwa huru kwa
kiwili wili, lakini si kiuchumi walakifikra, kwani uhuru aliyoupata ulikuwa uhuru wenye
vigezo na vikwazo fulani.Mtumwa hapo akawa mtumishi wa rasilmali na mfumo mpya wa
kisiasa, akiwa nakiwili wili chake tu huru wakati nguvu zake na akili yake zikiwa si mali
yake,yaani akiweza kuchagua tajiri/bwanyenye /bwana gani atamtumikia kwa malipoasiyooweza
kuyakatia uamuzi, na mara nyengine hata kutoweza kuchagua muajiriwake. Mtu
huyu baada ya kupata uhuru wake ilimbidi ijipatie makaazi, chakula,nguo, matibabu,
ulinzi n.k. yeye mwenyewe, wakati mambo hayo huko nyumayakihudumiwa na yule
aliye mmiliki. Kwa mara nyingi kiwanja chakujengea nyumba yenyewe au upangishaji
wake, ulitokana na muajiri wake, mara nyingiakiwa yule yule aliye mmiliki kabla na
maingiliano yao yakiwa hayana tofauti sana,kwa vile muajiri mpya alikuwa akimkamuwa
na kumnyonya kwa kumkodishakiwanja, nyumba, kumkopesha kwa matumizi ya chakula
na mengineyo nakumlipisha riba ya kiwango atakacho bwanyenye. Ingawaje sio waajiri
15
wotewaliyokuwa na mtindo huo , na inasemekana, hadhi ya watumwa Zanzibar ilikuwabora
zaidi kuliko kwingi kwengineko, kwa sababu ya imani ya kiislam. Ubwanyenye
ulikuwa njia ya uzalishaji mali bora zaidi ya uzalishaji mali wakiutumwa kwa vile ulipiga
khatua kubwa zaidi katika kuendeleza uchumi hasa wakilimo, kuruhusu na kushajiisha
kuweko kwa muuzaji wa bidhaa kama ni kiungobaina mali fulani na mali nyengine na
hatimae mchuuzi huyu kuweza kuhodhi nakutajirika kwa kutosha na kuweza kutanua njia
za usafiri na kuanzisha utumizi wa vifaa na mashine katika uzalishaji mali, kama vile meli
za stima. Hatimae kuletauwezekano wa maendeleo ya mafundi, wahunzi na wengineo.
Kufuatia njia yauzalishaji mali wa Kibwanyenye, pakazaliwa daraja jingine la uzalishaji
malilijulikanavyo kama uzalishaji mali wa Kibepari, kama litavy okaririwa baadae, hiini
njia muhimu ya uzalishaji mali ya wakoloni.
2.6 Utumwa na Uislaam
Wakoloni wote pamoja na wa kiingereza walifanya/na wamo wakifanya njama za siri za
kujifanya wao wazuri na kuja kwao Bara la Afrika kulikuwa na madhumuni yakuleta
kheri na fanaka pasi na kuwa na lengo jengine lolote, la siri au la dhahiri.Njia yao moja
wapo muhimu waliyoitumia ilikuwa ni Makanisa na Mapadri. Kupigavita “ushenzi”,
“utamaduni uliyoselelea wa Kiafrika” na kuleta ustaarabu waKizungu lilikuwa ni jambo
mojawapo waliyodai na kuliweka mbele. Tukifuata utamaduni wao tutakuwa kama wao
kuvaa nguo zao, kula kama wao, kutumia vituvyao na kuuwauzia vitu kwa bei zao na
kununua kutoka kwao, tukifanywa kuwana thamani kama zao. Wao, peke yao na wazungu
wenzao, walidai kuwa walistaarabika, wengineo wote ni wakiwa hawajastaarabika na
16
wakiwa washenzi,kwa mujib wa propaganda zao. Watu au tawala zozote zilizowaunga
mkono Wangereza katika njama zao za kuwatawalia watu wengine walipewa heshima,
ulwana ulinzi maalum.
Kwa Zanzibar, wakoloni wa Kiingereza, baada ya kuwanyanganya khatamu zenyewe, ndio
waliyoulinda na kuuhifadhi ufalme wa Kibunsaidi, lakini baadala yakuuita utawala huo
kwa jina lililostahiki, yaani wa Kibunsaidi, walitunga mbinu zakuupa jina ambalo lili kuwa
na azma ya kuwapa faida waoWangereza zaidi. Kwahivyo wakaamuwa kuuita utawala huo
ni waWaarabu, na hata sio wa Kiomani auWakimanga, maana kwa kweli, sioWaarabu wa
kila aina waliyotawala Zanzibar.Lengo la kuuita utawala huo ni wa Kiarabu, lilikusudia na
shabaha nyenginekabisa, nalo ni kwambaWaarabu niWaislaam. Kuuita utawala wa Zanzibar
waKiarabu kulikuwa na shabaha mbili, moja wapo ni kuufanya Uislaama uonekanembaya
na ukikandamiza Mwafrika na Uzungu na Ukiristo ukiwa ni mwema. Utumwa uli
kuwepo Afrika ya Mashariki hata kabla ya kuzaliwa Nabii Issa, kwa hivyo kabla ya ufuasi
wa Kiislaam wa Nabii Mohammad, salallah alayhi wasalaam. Lakini Mkolonikaufanya
Utumwa umeletwa na Mwaarabu, wakati huo huo, kwa kweli, akikusidiakuchochea chini
kwa chini na kusema ni Uislaaam ndio sababu ya Utumwa. Wakati ambapo utumwa
ulipigwa marufuku Zanzibar, wakati huo huo, Wareno na Wafaransa walishughulika na
biashara ya utumwa Afrika ya Mashariki, na kazihiyo waliifanya bila ya kuingiliwa kati
na manuwari za Kiingereza zilizowekwamaalum kulinda usafirishaji wa watumwa. Mngereza,
na vibaraka wake wakikiristo, hawasemi hayo wala hawasemi kwamba kulikuwa
na Wangereza hapo hapo Zanzibar wakifaidika kutokana na jasho la Watumwa, na ndio
maana mwanzoni kilekilichopigwa marufuku kilikuwa ni usafirishaji wa wa tumwa na sio
kumilikiwatumwa. Walisahau vile vile kusema kwamba huko kwao hapo zamani kulikuwa
nautumwa, ingawa huko makwao kulikuwa hakuna Uislaam. Wangereza walikuwahawat-
17
wambii juu ya maafa ya Waafrika wa Afrika ya Magharibi waliyopelekwa Marekani ya
kaskazini kusini na Caribbean ambako hakukuwa na Uislaam. Wazunguwalipo kwenda
Marekani walikwenda kwa niaba ya jina takatifu la Ukiristo, na kwa niaba ya jina la Msalaba,
wakateteketeza wenyeji wa huko na kuwatawalia.
Njama za kuufanya Uislaam uonekane mbaya Afrika, ilikuwa kama kufanyakiini macho.
Kuleta chuki za kugonganisha vichwa baina ya Wazanzibari kwa Wazanzibari,
Watanganyika na Watanganyika, ili kuweza kuwatawala kwa urahisi na kuweza kutambaza
dini ya ukiristo, hilo ndilo lilokuwa lengo muhimu la kampenihiyo, ingawa wengi
wa wazungu hao walikuwa hata hawaamini Mungu, balikuutumilia ukiristo kuwatawalia
na kuwanyonya Waafrika. Mkoloni alisahau kwambakwa niaba ya ukiristo Christofer
Columbus aliwateketeza Wahindi Wekundu, nakazi hiyo ovu ikaja baadae ikaendelezwa
na wenye asili ya Kiingereza na kufikahadi kwamba leo Wahindi Wekundu baada ya
kuteketezwa wamekuwa wachache”minority” makwao wenyewe. Mkoloni hajatwambia
kwamba huko Australia na NewZealand aliwateketeza wenyeji wa huko,”ma aborigens”
kwa kutumia mbinu ovu mbali mbali, moja wapo ikiwa kuwagawiya watu wa huko
mablangeti yaliyokuwa na magonjwa mbali mabli, kama vile tetekuwanga, kifua kikuu,
ndui, magonjwa ambayo watu hao kwa wakati huo walikuwa hawana kinga viwili wilini
mwao kuwezakujikinga na magonjwa hayo. Kwa vile watu hao siku hizo walikuwa
hawakuchanjwawala kuwa na ulinzi wa kuzaliwa nao, walipukutika na kufiana kama
nzige nahatimae Wangereza wakaweza kumiliki makoloni na kufanya sehemu hizo ni
nchizao. Mitindo kama hiyo walikuwa wanataka kuifanya huko Afrika ya Kusini naZimbabwe,
lakini wakaula na chuwa. Na sisiWazanzibari, baadala ya kuamka nakuzitambuwa
mbinu za Mkoloni za kutugonganisha vichwa, Waislaam kwa Waislaam,na Waafrika kwa
18
Waafrika, tukabaki tunauwana wenyewe kwa wenyewe, baadalaya kukaa kitako na kujaribu
kutatuwa tofauti zetu kwa njia za kisiasa na kidugu.Mkoloni alisahau kuwambia
wananchi kwamba katika biashara ya utumwa Zanzibar ,kuwa Waislaam hawakufanywa
watumwa na waliyosilim kutolewa utumwani.Lakusikitisha zaidi ni kuona hata wale waandishi
na wataalam wanaosifika kuwawameendelea, wametekwa nyara na tafsiri ya ukoloni
ya utumwa, na badala yakuukariri utawala huo kama ni wa kitabaka, mara nyingi na
wao wan ajiingiza katikamtego wa kibaguzi. Hadi hii leo Uislaam unapigwa vita sana
sehemu mbali mbaliulimwenguni, ingawa leo hazitumiwi sababu za utumwa bali sababu
nyenginezo,kama vile kuvunja Katiba ya Muungano wakati Zanzibar ilipojiunga na Umoja
wa Nchi za Kiislaam, na badala ya serikali ya Zanzibar kusimama kidete, kutetea utu, nchi
na imani zao, ikakubali kamsujudia Nyerere.
Kwa kutumia mbinu kama hizo, za kutumia Uislaam na Ukabila badala ya tafsiri yakitabaka,
Mngereza alifanikiwa kuleta chuki na uhasama baina yaWazanzibari,wakati yeye
akishirikiana na kuuhifadhi utawala huo huo aliyouita wa Kiaarabu.Kwa njia kama hiyo
Mngereza akafaulu kutufanya tukabane roho wenyewe kwawenyewe na kusahau kumpiga
vita yule adui wa kweli, yaani Mkoloni wa Kiingereza. Hivi sasa Mngereza kesha ondoka
hadharani, wamebaki vibaraka wakehasa huko Bara wanaoimba wimbo huo huo, ilhali
babu zao (machifu) ndiowaliyokuwa wakikamata watumwa hao na kuwauza.
2.7 Ubepari
Ubepari nao ukifananishwa na Ubwanyenye, na Utumwa n.k. ni njia iliyoendelea bora
zaidi katika kuleta maendeleo kwa jumla. Binaadam ni kiumbe anaeendelea kila usiku
19
ukicha na siku zote atataka kuona anaendelea zaidi, kwa hivyo njiafulani ya maendeleo
ikisha zorota inawekwa kando na kubadilishwa na njianyengine iliyo bora zaidi. Mngereza
anadai kwamba aliuondosha utumwa Afrika ya Mashariki, lakini alisahau kusema,
kama ilivyokaririwa hapo juu, kwamba kwao wenyewe waliendeleza uzalishaji mali wa
utumwa na jamaa zao wa Marekani walijenga na kuendeleza njiaza uzalishaji mali wao
kwa kupitia utumwa na hadi hii leo Waafrika wa Kimarekanibado wako katika daraja
la chini kabisa katika jamii zote za huko Marekani.Kukomeshwa kwa utumwa Ulaya na
Marekani kulipitishwa kwa sababu ya kwambaaina ya uzali shaji mali huo kwa wakati huo
ulikuwa umesha zorota na haukuletafaida za kiuchumi tena. Mbali ya Mngereza kusahau
kusema kwamba uchumi wasiku hizo ulikuwa haufaidiki tena kwa kutumia njia ya utumwa
kwa vile amilikaewatumwa ilimbidi awalipie gharama zote za kila siku, gharama ambazo
apata e uhuruwake ilimbidi ajihudumie mwenyewe. Vile vile amesau kusema kwamba
vita vyakedhidi ya utumwa viliambatana na uenezaji wa utawala wake wa kikoloni na
kusahaukusema kwamba uchumi wake ulifaidika kutokana na jasho la Watumwa.
Maendeleo ya uzalishaji mali ulimwenguni hayakwenda sambamba, kwa vile kuna
nchi mbali mbali katika uliwengu wa tatu ambamo maendeleo ya uzalishaji malihayakufuata
vidaraja kama vile vya nchi zilizoendelea, yaani kutoka utumwa, kwenda ubwanyenye
halafu kwendea ubepari. Kutokana na upungufu wamaendeleo ya kisayansi na kiteknologia
karibu nchi zote za ulimwengu wa tatu hadihivi leo hazijafikia kiwango cha uzalishaji
mali wa kibepari. Mabepari wamehakikisha kwamba nchi hizi zinabaki nyuma na kuwa ni
masoko ya bidhaa zamabepari ambao walikuwa ni wakoloni wao, na ardhi yao kuigeuza
bustani za mauana mashamba ya chai, kahawa na viungo walivyovihitaji wao, wakati huo
huo kuwani bidhaa zisoweza kushibisha walimao au kutoweza kuwahatarishiya uchumi
20
wawakoloni. Ni hivi karibuni tu ambapo nchi chache za huko mashariki ya mbali ndizo
zilizoruhusiwa kutumia uzalishaji mali wa kibepari. Hali hiyo imemkinika kwasababu
ya gharama za uzalishaji mali huko Ulaya na Marekani zimekuw- a juu sanakutokana na
kupigania haki za wafanya kazi huko nchi zilioendelea. Hali hii ikawafanya Mabepari wa
nchi za magharibi kukimbilia zile nchi ambazo gharamahizo ziko chini na kujihakikishia
na kuweza kuhakikisha faida kubwa zaidi. Kinyume na ilivyo dai la baadhi ya wataalamu
fulani wa kisiasa na kihistoria, Zanzibar haikuwa na njia ya uzalishaji mali wa kibepari.
Katika nchi zilizoendelea hasa zile za kibepari, uzalishaji mali wa utumwa kwa desturi
hufuatiliwa na uzalishaji mali wa Kibwanyenye/Kimwinyi na hatimae ubepari kufuatia.
Baada yakuondoshwa utumwa Zanzibar hapajatokea maendeleo yoyote ya maana ya uzalishajimali,
bali msingi wa uchumi wa Zanzibar uliselelea pale pale na kuwa wa kale ukiwa
wa Kibwanyenye na ukitegemea vuno la karafuu, nazi na pilipili hoho, napakitumika njia
zile zile za kulimia za enzi za mababu na mababu. Ukulima wa vifaavya kisasa ulikuwa ni
jambo duni, na viwanda vya aina yoyote, zaidi ya viwanda vya lazima vya ukamuaji wa
mafuta ya karafuu na ya nazi, kiwanda cha sukari,kilicho-anzishwa na Barghash, vilikuwa
duni. Uendelezaji wa uzalishaji maliulikuwa ni dufu, Zanzibar ikiwa shamba la kuchumiya
ubepari wa kikoloni nakuselelea kuwa katika uzalishaji mali wa ki- bwanyenye na wakati
huo huo, kupitia tabaka la Wafanya biashara, kuwa soko la bidhaa za kibepari kutoka kwa
Wakoloni na kituo muhimu cha usambazaji wa bidhaa hizo katika sehemu nyengine za
Afrikaya Mashariki na ya kati.
Ubwanyenye au Umwinyi ndio uliyokuwa mwenendo wa kitawala na wa kuzalisha
mali Zanzibar na hadi leo hakuna mabadiliko makubwa katika fani hizi. Maingiliano .
ya “kimwinyi na kiskwatta (squatter)” ndio maingiliano yaliyojenga msingi wakisiasa wa
21
hivi sasa Zanzibar. Msingi huo ulionekana kama ni mfano wa kujengeamfumo wa uongozi
wa vyama vya kisiasa viwili muhimu vya Zanzibar yaani ASP naZNP. Umwinyi au
ubwanyenye vile vile ndio uliyokuwa msingi mmojawapo muhimuwa chuki za kikabila,
hasa kwa vile ya mamwinyi au mabwanyenye wa Kizanzibariwalikuwa waliyokuwa na
asili ama ya Kiarabu au ya Kishirazi na maskwatta wakiwawenye asili za Mrima/Bara.
Misingi miwili mingine muhimu iliyoleta chuki baina yajamii ya Kizanzibari ilikuwa ni
utawala wa Kisultan na utawala wa Kiingereza.Ingawaje, kabla ya kuja tawala mbili hizo
Zanzibar, tawala za wajukuu wa Hassan,Sultan wa Shiraz, hasa ya utawala wa Mwinyi
Mkuu, ilikuwa ni tawala iliyotumiautumwa kama ni njia ya uzalishaji mali – wa hapo
kale. Zanzibar ilipokuja chini ya mamlaka ya Seyyid Said bin Sultan (1832) palikuwa na
makubaliano baina ya Sultan huyo na Sultan Mwinyi Mkuu kwamba, kila mmoja atawale
na kuwa na mamlaka ya sehemu yake, hatimae pakatokea mfarakano mkubwa kwa vile
Seyyid Said alichukuwa utawala wote hata kutia ndani aukuhamisha nchi tawala za Kishirazi.
Inasemekana kwamba, kabla ya utawala wa Mabusaidi kutawala Zanzibar,Wazanzibari
walipeleka Ujumbe kwa Sultani wa Omani, wakiwaona kama Waislaam wenzao, waende
Zanzibar kuwasaidia kuondowa utawala wa makafiri wa Kireno. Usultani huo hatimae
ukaifanya Zanzibar mamlaka yake, pekee. Mabwanyenyewenye asili ya Kiomani wakawa
hatimae ndio wenye kumiliki ardhi kwa wingi zaidi na kunufaika zaidi kiuchumi na hali
hii ikawafanya kuwa tabaka la juu kabisa Zanzibar na wenyeji wao, Mabwanyenye wa
Kishirazi, wakashushwa hadhi na kuwatabaka dhaifu zaidi. Ingawaje, hili ni tabaka lililojiwe
za zaidi kuliko Waswahili wengine waliyokuwa hawana asili ya Kizanzibari halisi.
Karibu wote hawa wa kundila mwisho walikuwa katika tabaka la chini.
Utawala wa kisultani Zanzibar haukuwa wa Kiislaam, au wa Kiarabu kama Wangereza
22
walivyotufanya tuamini, kwani watawala hao hawakutawala kwa mujib sheria za kiislaam
na hawakutoka Arabuni kote bali walitoka Omani na hata huko Omani walikuwa ni watu
wa ukoo mmoja tu, nao ni Mabusaidi na sio aina zote zaMabusaidi. Na hata wale mabwabyenye
wengine wa Kiomani waliyokuwa matajiri,kuwa na mashamba na nguvu nyingi
hawakuwa watu ambao wakiwakilisha maslahiya utawala wa Kibusaidi tu. Baadhi yao,
kama vile ilivyo desturi katika baadhi yawatawala au mabwanyenye tofauti, kulikuwa na
migongano, michuano na mivutanoya kujinufaisha binafsi. Katika Zanzibar, kwa mfano,
wengi wa Mabarwani hadi siku za mwisho za Usultani walisemekana kuwa wakipinga
Ufalme na msimamo huo walikuwa nao tokea siku za Juma Barwani alipochukuwa silaha
kupambana na Seyyid Said bin Sultan.
23
Chapter 3
USULTANI NA UKOLONI
3.1 Usultani wa jana na Utawala (Usultani) wa leo
Tabia ya kutawala au ya kunyanganyana utawala au mali, si sifa za Waarabu tu,Waomani
au Mabusaidi peke yao. Ulimwenguni kuna tawala tofauti, na tawala hizizinaweza kugawika
katika makundi mawili makubwa, moja likiwa na maslahi natabaka la utawala, na
kundi la pili likiwa na maslahi halali ya umma mzima nakuwapa watu haki sawa. Sifa
ya kuhifadhi maslahi ya takaba la utawala haitegemeiutawala huo una rangi gani, kwani
tumeona mifano ya utawala wa Sultan na utawalawa Karume. Utawala usio na maslahi ya
umma kwa desturi unakuwa ni wakutumiamabavu na kutowashirikisha wananchi katika
uamuzi wa mambo yao wenyewe.Utawala kama huo huchaguwa vibaraka wake kuwatumilia
katika kuendelezautawala au mtawala aliyehusika. Serikali nyingi za Kiafrika
zilisahau maagizo na ahadi walizozitowa wakati walipokuwa wakipigania uhuru, na kusahau
kwamba walichokipigania kilikuwa niserikali ya watu, iliyochaguliwa na watu kwa
maslahi ya watu. Karibu serikali zoteza Kiafrika baada ya kupata uhuru zilifuata mtindo
wa utawala wa Kidikteta nakusahau ahadi zote walizozitowa kabla ya hapo. Wengine
walitumia siasa dhidi yautumwa na kupinga Usultani kama ndio kampeni yao, lakini hatimae,
walipopata khatamu za utawala wakaonyesha kuwa ni tawala akhasi za Usultani
na ukoloni.Baadhi yao walidai uhuru wa Mwafrika lakini walipopata khatamu za utawala
walizidi kumkandamiza Mwafrika, na waliendeleza siasa ya udikteta, utawala wamabavu
na kutaka kumtawalia huyo huyo Mwafrika kwa kujigeuza Mabwana/Wakoloni wepya,
24
kama Tanganyika na Zanzibar. Watawala wa Kiafrika wakipata khatamu za utawala wana
mtindo wa kutakakuselelea katika utawala milele na hata watakapo kwisha ondoka au
kulazimishwa kuondoka bado huwa wanataka kuingilia kati mambo ya utawala, kama vile
Nyerere, kupinga aumuzi wa Bunge la Tanganyika la kutaka Bunge na Serikali ya Tanganyika
na kuwalazimisha Wazanzibari bila ya khiari zao kubaki katika Muungano kwa
kulazimisha serikali moja. Tumemuona Karume, aliyedai siku zanyuma kumpimgania
Mwafrika na hatimae tukaona ukatili aliyomfanyia Mwafrika mwenziwe, mtu yule yule
ambaye aliyempa yeye nguvu hizo, ndiye hatimaealiyemgeuza adui na kumteketeza. Kwa
hivyo suala la kuliangalia kwa makini na kulidurusu kwa kituo ni aina yautawala unohusika,
na kama utawala fulani una maslahi na wananchi au la , na siotu kwamba utawala
huo una jinsiya gani, ya kutoka Butiama au kwengineko. Kwanihata utawala usio wa
kikoloni unaweza kuwa mkatili hata kupitia ukoloni. Suala lakulizingatia ni kama utawala
huo ukiwa wa kienyeji unatekeleza maslahi ya umma au maslahi ya watawala na jamaa
zao, na hata ukiwa ni utawala wa kienyeji, mradi unakandamiza wananchi lazima up igwe
vita mpaka utokomee, na utawala halaliwenye misingi ya kidemokrasia uwekwe badala
yake.
3.2 Kumiliki Ardhi Zanzibar
Katika historia ya leo kuna madai mawili muhimu kuhusu umilikaji wa ardhi Zanzibar. Dai
moja ni la wale wanaodai wamenyangnywa ardhi baada ya Mapinduzi ya 1964, wakidai
warejeshewe ardhi zao walizo nyang’anywa, hizo zikiwa ni malizao za kihalali; wanadai .
Kwa upande wa pili kuna waleWazanzibari wanaodaikwamba mababu zao walihamishwa
25
kwa nguvu kutoka zile sehemu zenye ardhi yarutba na kuhamishiwa kwenye sehemu za
ardhi duni (Kuna kikundi chengineambacho hakitajwi sana, nacho ni cha wale Wazanzibari
ambao ni vitukuu navirembwe wa watumwa waliyotoa jasho lao katika mashamba
hayo, bila ya kupatamalipo.) Suala muhimu, katika madai mawili haya, ni jinsi gani kupitisha
haki bainaya Wazanzibari bila upendelevu wowote, lakini kabla ya kuweza kufanya
hivyo itabidi ijulikane nani MNYANG’ANYA NA NANI MNYANG’NYWA. Hili sio suala
rahisi kwa sababu kwa uchache vitendo hivi vya uhodhi wa ardhi vilitokea kamamiaka
160 iliyopita yaani baada ya Seyyid Said kuhamia na kuhamishia mji mkuu wa utawala
wake kutoka Oman kuja Zanzibar. Seyyid Said mwenyewe alijigawiya ardhibora kabisa
yenye nafaka, na haifikiriki kwamba alimuomba Mhadimu, Mtumbatu,Mshirazi rukhsa ya
kuchukuwa ardhi hiyo au kujulikana kwamba ilikuwa ni ardhiisiyotumika kabla ya hapo.
Hatujui kwamba Mwiny i Mkuu nae alipochukuwa ardhialiomba au kununua ardhi kwa
nani au kwamba ardhi hiyo ilitumika kabla ya hapoau sivyo.
Baada ya “Harameli bin Ali” kuleta miche ya karafuu kutoka R’union katika mwakawa
1929 na Seyyid Said kutilia mkazo na kushajiisha upandishaji wa zao hilo muhimu, mfalme
huyo aligawa ardhi kwa zile koo za Kiomani zilizotukuzwa na ufalme huo, pamoja na
kuwa aila hizo zilikuwa na rasilmali ya kutosha ya kuwezakukuza zao hilo. Ingawaje huko
Pemba kati ya makabila muhimu yaliyotia mizizi kabla ya utawala wa Omani kudhibiti
Zanzibar, ilikuwa Mazrui na Mauli, namakabila haya yalikuwa yameshajizatit kuoleyan a,
kuchanganya damu na kumilikiardhi muda mrefu kabla ya vitendo hivyo kupitika Zanzibar.
Itakumbukwa kwambatokea kutolewa kwa Mreno kwa mara ya pili katika 1728
huko Mombasa, mara yakwanza ikiwa mwaka 1660, kabila la Mazrui lilikwisha tia mizizi
Momba sa na Pemba pia. Ingawaje hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba watu hawa
ambao na wao piawaliyokuwa na asili za Kiomani walinunua ardhi hiyo kutoka kwa mtu
26
yeyote katikahizo siku za mwanzo au walizipata kwa sababu za kuingia ndoa. Lakini, vile
vile, hakuna ushahidi uliyotolewa unaoonyesha kwamba kulikuwa na watu waliyomiliki
ardhi hiyo hapo zamani, waliondoshwa mashambani ama kwa sababu wakiishi sehemu hizi
au kuzimiliki. Zanzibar ya kale haikuwa nchi ya ukulima na uchumi wake kutotegemea
uuzaji wa mazao ya ukulima na kwa hivyo si suala dhahirikwamba ardhi hiyo ilimilikiwa
kwa madhumuni ya ukulima wa biashara. Jambo wazini kwamba ardhi hiyo ilitumika
kwa madhumuni ya kujilisha wenyewe, jambo ambalohalikuhitaji sehemu kubwa ya ardhi
kutosheleza mahitaji hayo. Zaidi ya hayo idadiya Wazanzibari kwa wakati huo ilikuwa ni
ndogo sana hata kutoweza kutumia ardhiyote ama kwa makaazi au kwa ukulima au kwa
yote mawili, na ndio maana wakati wautumwa na wa baadae ilibidi kuleta watumwa na
vibarua kutoka Bara ku ja kutumikamashambani. Kabla kwa kuja kwa karafuu, uchumi wa
Zanzibar ulitegemea zaidibiashara baina ya nchi za Bahari ya Hindi na Afrika ya Mashariki
na ya Kati, naZanzibar ndio ikiwa kitovu au kiini cha biashara hiyo, yaani kuwa soko na
bandari muhimu, huu ndio uliokuwa msingi wa uchumi wa Zanzibar.
Suala muhimu ni, jee ni halali kwa mtu kutoka nchi nyengine na kuja kuikuta ardhi
haikaliwi, kuichukwa, kuilimiya na kudai ni yake. Ardhi ya nchi kwa ufupi nirasilmali ya
dola kwa jumla na atakayeitumia kwa maslahi ya maisha yake, ya ukoowake na ya nchi
kwa jumla atakuwa na haki ya kuitumia akijuwa wazi kwamba hiyoni mali ya umma. Kwa
desturi, vizazi vilivyozaliwa katika sehemu fulani kwa karne na karne, ndiwo wanaotambuliwa
kuwa wamiliki wa sehemu fulani ya ardhi kwa vilewaliitolea jasho kwa kuifanyi
ya kazi sehemu hiyo. Ingawaje kuna wananchi wenginewa Zanzibar ambao hawakuishi
sehemu hizo za mashamba, bali waliishi mijini, nakwa desturi huwa hawamiliki ardhi
ingawa wana haki sawa ya kumiliki ardhi yanchi yao kwa jumla. Wale wanaosemekana
wamenunu wa ardhi, nao siku za mbelehuenda wakawa matatani, ikiwa kutakuwa na up-
27
ungufu wa ushahidi kutoka kwawale waliyowauzia ardhi hizo. Watumwa walifanyishwa
kazi katika mashamba tofautiZanzibar bila ya kulipwa, ingawa watumwa wengi walirudi
makwao mabara baadaya kupata uhuru wao, wale waliyobaki na kuigeuza Zanzibar nchi
yao kihalaliwanatakiwa kwa desturi wawe na haki ya kumiliki ardhi katika zile sehemu
walizolazimishwa kufanya kazi. Zanzibar ya leo ni Zanzibar yenye raiya (300/Km) kuwa
na wakaazi wengi hata ardhi kutotosha kwa wananchi wote kama itagawiwakihalali baina
ya wazalendo wote, ikitafsiriwa kwamba ardhi ni rasil mali ya umma. Wabara waliyowasil
Zanzibar kwa kazi za vibaruwa mashambani nao wanadai kuwana haki ya kumiliki ardhi
kupita wale wazalia wenye asili za Kiomani, wanadai hakihiyo si kwa sababu nyengine
zaidi, isipokuwa kuwa wao ni Waafrika na walikuwavibaruwa/maskwatta sehemu hizo.
Itaonekana kwamba watu hawa, tofauti nawatumwa, walilipwa kwa jasho lao walilolitowa
baada ya kukubaliana kufanya kazi kwa mikataba. Mtumishi karakhanani hamiliki
karakhana, ingawa naye hunyonywa.Yupi mwenye haki zaidi ya ardhi ya Zanzibar, yule
mwenye uzalia wa Kizanzibaritokea 1660-1728 (kutolewa kwa Mreno) na 1832 au yule
jirani aliyekuja kwamkataba wa kibarua makhsusan katika karne ya ishirini. Vijukuu,
virembwe navitukuu vya Kizanzibari ambao mabibi na mababu zao walikuwa watumwa
waliyofanyishwa kazi katika ardhi fulani ni kati ya watu ambao madai yao ya ardhilazima
yatiliwe maanani, suala hili litakapojadiliwa siku za mbele.
Katika kujaribu kuleta usawa baina ya Wazanzibari, Serikali ya Mapinduzi ilitaifisha
ardhi na baadae kugawa “eka” tatu tatu kwa wananchi, ingawa nia yalengo hilo ilikuwa ni
nzuri lakini ugawaji wenyewe haukuwa wa kihalali. KwanzasiWazanzibari tu waliyo pewa
ardhi hiyo, pili ugawaji huo haukuwa wa usawa kwaniwale waliyojiweza walizidishiwa,
na kupewa (kuchukuwa) mashamba zaidi ya mojana yale yaliyokuwa na rutba zaidi, mfano
28
mzuri ni wa Memba wa Baraza laMapinduzi wenyewe ambao tayari walikuwa na mishahara
miwili, wa Baraza laMapinduzi na Bunge la Tanzania. Uhalali wa kitendo hicho
umeingia dowa nakupotosha lengo na madhumuni ya ugawaji ardhi kihalali. Zaidi ya
hivyo, ardhihiyo iliyogawiwa umekuwa ikiuzwa ovyo ovyo, hivi karibuni hata serikali
ya Zanzibar imekuwa inagawa ardhi kwa madhumuni tofauti kwa njia za ama mapendeleo
au kwa kilanguzi, kuzidi kuwapa walonacho na kuwanyima wasonacho. Serikali
vile vile inasemekana kuwagawiya au kuwakodisha kwa bei za bure wataliana na wageni
wengine ardhi ya Wazanzibari, wakati wageni hao wakifanya kejeli, ufudhuli wa kuwafukuza
wenyeji sehemu hizo na kuwazuwiya hata kuvua. Wataliana hao waliosabiliwa
ardhi hizo, inasemekana wanatumia sehemu hizo kwa uendelezaji wa biashara za madawa
ya kulevya. Chau chau gani wanoipata serikali hiyo haijulikani. Kuna watu wengine
wanasemekana wamerejeshewa ardhi zao, mali zao na majumba yao, bila ya kutolewa
kielezo chochote, wakati wengine bado hawajarejeshewa mali zao. Kutokana na hayo
machache kuhusu ardhi, Zanzibar itakapojipatia uhuru wake, kutoka Bara, pata kuwa na
haja ya kuunda Mahkama au Tume maalum ya kisheria kulijadili suala la ardhi ya Zanzibar
kihalali na kikamili.
3.3 Wahindi kudhibiti uchumi
Baada ya kuja kwa utawala wa Kiingereza Zanzibar, Seyyid Said akaonjeshwa shubiri
aliyowapa kina Mwinyi Mkuu. Kwanza kwa kukaliwa juu ya kichwa na Mngereza, pili
kwa Mngereza kuondosha njia ya uzalishaji mali ya Utumwa ambaoUfalme huo ukiutegemea
katika zao lake la karafuu na tatu kwa kutiliwa mkazo kwanjia nyengine ya
29
uzalishaji mali yaani ya kibwanyenye ambayo hatimae ilishajiishakukuwa kwa mfanya
biashara, ambae alikuwa Mhindi, wengi wao kuselelea kuwaraiya wa Kiingereza. Hatimae
kugeuzwa karibu Mabwanyenye wote waliyokuwa naasili ya Kiomani kuwa kama ni
waangalizi tu wa mashamba ambayo kabla waliyamiliki, kwa vile karibu mashamba yote
yalikuwa yamewekwa rahhani, baadaya muflis uliyotokana na uuzaji wa watumwa, baada
ya hapo Wahindi wakapata satwa ya kuweza kuudhibiti uchumi wa Zanzibar. Kwa hivyo
khatamu za utawala na nguvu za uchumi hazijawa tena katika ukoo wa Kibunsaidi naWale
Wazanzibari waliyokuwa na asili ya Kiomani, bali utawala ulikuwa chini ya Mngereza
na uchumiwa ndani ya nchi kuwa mikononi mwa Mhindi, wakipeana wadhifa, Mngerezakukamata
serikali na uchumi wa nje na Mhindi kukamata uchumi wa ndani, akiwamjumbe
wa ubepari bila ya kuwa na njia za uzalishaji mali za kibepari.
3.4 Mngereza na mfumo wa matabaka
Kutawalia Zanzibar rasmi na Mngereza (1890), ambaye alikuwa na mgawanyiko wa
matabaka ya bayana zaidi kuliko yaliyokuweko Zanzibar wakati huo, kwa hivy oulizidi
kuyapanga matabaka Zanzibar kwa utulivu nabayana zaidi. Kwanza kwakuwapaWaarabu,
hasa wenye asili ya kiomani, na Wahindi ubora katika matabakaya jamii. Ingawaje
katika tabaka la wenye asili ya kiarabu na kihindi kulikuwa na mgawanyiko wa matabaka
mbali mbali, yakiwemo matabaka ya chini kabisa katikajamii. Baina ya tabaka la Mabwanyenye/
Wafanya biashara wa juu, na matabaka yachini kabisa kulikuwa na tabaka la
kati na kati, ambalo lilikuwa na wafanyabiashara wadogo wadogo, maafisa wa serikalini,
mafundi waliyojimudu, wakulimana wavuvi waliyomiliki ardhi na vyombo vya kuvulia,
30
na wengine waliyojimudu kwanjia nyenginezo. Katika tabaka hili kulikuwa na makabila
ya mchanganyiko.Tabaka la chini likiwa ni vibarua, maskwata na maproletariati “walolala
hoi” wengiwa hawa walikuwa ni walalahoi waliyotoka nchi za jirani ambao walivutiwa na
hali bora ya kiuchumi ya Zanzibar au walikuwa wakikimbia ulipaji wa “kodi ya kichwa
” makwao. Wale waliyokuwa wakijiweza mabara walibaki huko. Mngereza alipojizatit
Zanzibar alihakikisha kwamba ugawaji wa matabaka ulizidi kutia mizizi na katika njama
zake za kawaida za “kugawa watu ili aweze kuwatawala” kwa urahisi zaidi,alihakikisha
matabaka haya yamejengeka kwa msingi wa elimu, kipato, rangi nakikabila .Tabaka la Mngereza
mwenyewe bila ya shaka kuwa ni bora kushindayote, na kuwa tabaka la juu kabisa
katika jamii hata kushinda la mfalme, na wakatihuo huo kuwatumilia wale waliyokuwa
katika matabaka ya juu kuendeleza utawalawa kikoloni. Sababu zinazotokana na mfumo
wa utumwa kwa jumla; sababu za kuondoshwa na kupunguzwa hadhi kwa utawala na
ubwanyenye wa kishirazi uliyofanywa na SeyyidSaid, na sababu za ujenzi wa matabaka
kwa msingi wa kikabila uliyonufaisha ukoloni ambao ulifumwa na Mngereza na kuzaliwa
kwa tabaka la walalahoi lilokuwana sehemu kubwa zaidi kutoka bara; zimeleta sio
mfumo maalum tu na chuki zakikabila visiwani, bali muhimu ya yote zimeleta Mapinduzi,
Muungano na CCM.
3.5 Vyama vya kisiasa kabla ya Mapinduzi
Chanzo cha Mapinduzi kinatokana na misingi ya kisiasa na ya kijamii ya Zanzibar.Ili
kuweza kufahamu kwa urahisi zaidi matatanisho ya siku za nyuma kwa vijana waleo
wa Kizanzibari na baadhi ya Wabara; pana haja yakunakili uundaji, misingi,mifumo na
31
uendeshaji wa vyama vya kisiasa vya zamani hasa Afro Shirazi Party(ASP) na Zanzibar
Nationalist Party (ZNP) au Hizbu. Chama cha ASP kiliundwa katika mwaka 1957 kutokana
na muunganisho wa chama kile kilichojulikana kama African Association (AA) (ambacho
asili yake ilikuwa nikama tawi la TANUna kuwa na uongozi na wafuasi wa Bara) na Shirazi
Association(SA) chama chenye uasili wa Kizanzibari. Vyama hivi viwili vilikuwa na sura
zakikabila kutokana na misingi iliyowekwa na Mngereza kama ilivyokaririwa hapo juu.
Chini ya Uingereza watu waligawiwa kwa makundi ya kikabila na kwa kupitia njiakama
hizo ndipo makundi hayo yalipoweza kuwakilisha maslahi ya makundi yaoyaliyohusika.
Vikundi viwili hivi, yaani AAna SA, ni vikundi vilivyokuwa namaslahi tofauti yaliyokuwa
yakigongana. Shirazi Association ilikuwa ikiwakilishaWaafrika wenye asili ya Kishirazi,
waliyokuwa wazalia wa Kizanzibari kwa mababu na mababu. Wakati African Association
iliwakilisha Waafrika waliyozaliwa sehemembali mbali za Afrika ya Mashariki na
Kati, hasa bara la Nyika/Mrima, kati yaowalikuwemo waliyoishi Zanzibar kwa muda
mfupi ilhali wengine walikulia Zanzibarama bado wakiwa na uzi wao wa kitovu Bara
au wengine waliyokwisha kuukata uzihuo na kundi jengine likiwa wazalia wa Zanzibar
wenye asili ya Bara au kuwa naujamaa na Bara. Suala muhimu la pili liloyagawa makundi
hayo lilikuwa ni suala laki tabaka, Washirazi wengi walikuwa Mamwinyi wenye uwezo
bora wa kiuchumi, hatawafuasi wao wa chini ni waliyojiweza zaidi. African Association
iliwakilisha zaidi watu wa tabaka la chini zaidi, yaani wale waliyokuja Zanzibar
kwa kutafuta kaziza muda mfupi kama vile za vibarua, wachukuzi, makuli na wafanya
kazi wamashambani (maskwata). Uongozi wa SA vile vile ulikuwa umeelimika zaidi na
kwahivyo kuwa tabaka la juu zaidi. Kwa hivyo kulikuwa na mambo mawili muhimuambayo
yalivitenganisha vikundi viwili hivi. Vikundi hivi, mwanzoni vilipoundwa,havikuwa
na misingi ya kisiasa kama vyama vya kisiasa vya kawaida vinavyojulikana, bali kila
32
kimoja kikijaribu kutetetea uongozi wa kuwakilisha-0Bmaslahi ya jamii yake. Chanzo
cha uundaji wa AA, kwa kweli, haikuwa siasa au maslahi ya jamii yote kwa jumla, bali
kilianza kama ni chama cha riadha (mpira,ndondi) na hatimae kuanza kujishughulisha na
masuala ya kijamii, wakati baadaekikawa tawi la TANU. Ndani ya kila kikundi, kulikuwa
na mvutano, na baina yavikundi viwili hivyo kulikuwa na mchuano mkubwa wa kuweza
kuingia katika Majlis’ltashrih (LEGCO Legislative council). Muundo wa Legco siku hizo
ulikuwa nawawakilishi kwa misingi ya kikabila, kipato na kisomo. Hali hii ilipangwa na
Mngereza ili inufaisha mataba fulani na kunyima haki matabaka ya chini. Yalematabaka
yaliyonufaishwa kwa kuambatana na uteteaji wa maslahi yao walilindamaslahi yao kwa
kuzidi kumt-etea Mngereza na utawala wake. Siasa za kupigania uhuru zilipoanza, Nyerere
alijaribu sana kuunganisha AA na SA, hasa kwa vile AA ilikuwa kama ni tawi la
Tanganyika African Association,historia hatimae imetushuhudushia lengo la Nyerere la
kusisitiza hivyo. Historiaimedhihirisha kwamba Nyerere kwa siku zote alikuwa na lengo
la kuimeza Zanzibar na hatimae kuigeuza jimbo. Baada ya jitihada kubwa ya Nyerere
AA na SA zikaungana- katika mwaka wa 1957 na kuwa Afro Shirazi Union, yaani umoja
wa Waafrika na Washirazi. Ingawaje sio SA yote iliyojiunga na kuwa Afro Shirazi kwani
viongozi wa SA wa Pemba waliamua kubaki huru na katika uchaguzi wa mwanzo wa Zanzibar
wa 1957, Washirazi wa Pemba, Mohammed Shamte na Ali Sharif Mussa,waligombea
uchaguzi huo kama watetezi huru na kushinda kwa kiwango kikubwasana na kuonyesha
kwamba tokea siku hizo chama mama cha ASP, ambacho kwawakati huo kikijulikana
kama Afro Shirazi Union (ASU), hakikuungwa mkono Pemba. Ndio maana leo serikali ya
CCM inawalipizia kisasiWapemba kwa kuwanyimangazi zote za maendeleo na kuyafanya
maisha ya Pemba kuwa ya ufukara wa mwisho. Afro Shirazi Union ikashinda Unguja na
kupata viti vitatu kati ya vinnekimoja kuchukuliwa na mjumbe wa Muslim Association na
33
Shirazi Association kushinda viti vyote viwili vya Pemba, Hizbu kutopata hata kiti kimoja.
Kina Shamte hatimae wakajiunga na ASP iliyoongozwa na Abeid Amani Karume lakini
migongano mikali ilitokea kati ya uwongozi wa chama hicho.
3.6 Muamko wa kudai uhuru
Kumalizika kwa vita vya pili vya ulimwengu, kulileta muamko mpya katika makoloni
mbali mbali, kwanza kwa kushindwa kwa Mafashisti wa Kijerumani, Kijapani naKitaliana,
pili makoloni yaliyokuwa chini yaWakoloni kama vile wa Kiingereza walianza kuwa
na muamko mpya. Nchi kama za India na Uchina kujinyakulia Uhuruwao katika miaka ya
1947 na 1949. Baadae hamasa za upiganiaji uhuru na zakimapinduzi za nchi za Arabuni
ambazo zilikuwa za kiislaam, pamoja na kwamba Mngereza (1949) aliwapa Majahudi nchi
ya Mapalastina ambao wengi wao walikuwani waislaam, zilifanya muamko wa Wazanzibari
dhidi ya Mngereza kuzidi kutia fora.Mapinduzi ya Jamal Abdil Nasser (1952) na vita
vya Mchirizi wa Suez vya Misri (1954) dhidi ya Mngereza, Mfaransa na Jahudi vilifanya
jazba na damu yaWazanzibari kuzidi kuchemka na kuleta muamko wa kupigania uhuru
na kujitegemea. Mapambano ya Nkurumah, ya Ben Bella, ya Mau Mau na wengineo
yalizidi kurekibisha gurudumu la mapambano ya Wazanzibari. Mchemko wavuguvugu la
Misri uliwafanya wale wanafunzi wa Kizanzibari waliyokuwa wakisomahuko na wataalam
wengine wa Kizanzibari kuchukuwa msimamo madhubuti dhidi yaUtawala wa Kiingereza.
Kati ya wale waliyokumbwa na muamko huo ilikuwa ni Arab Association ya Zanzibar
na kufika hadi katika mwaka wa 1954 kugomea kwendamajlisi ’l tasrih, mmoja kati ya
viongozi wake washupavu alikuwa Ali Muhsin. Jinsihamasa za uhuru na azma ya ku-
34
jitawala zilivyokuwa ziko hali ya juu na hamu yakutaka kumuondoa Mngereza ilivyokuwa
kubwa, mmoja wa wanachama wa ZA, Inspector Sultan Ahmed Mugheri, alipovunja
mgomo huo na kuhudhuria kikao cha Legco, alipigwa visu na kuuwawa. Mtu aliyejitolea
kumuuwa Sultan Ahmed alikuwasi mwengine, bali ni baba yake Lt. Humud Mohammed,
yaani Mohammed Humud. Katika mwaka 1951 Wangereza walitaka kuanzisha kuchanjwa
n’gombe Zanzibar,lakini jinsi ya hamasa zilivyokuwa ziko juu dhidi ya Mngereza kati
ya wazalia wa Zanzibar, jambo lolote lile alilolitaka Mngereza kulifanya lilitiliwa shaka,
hasa kwavile tokea 1940 Mngereza alianza kuchukuwa ardhi ya wakulima wa Kiembe
Samakikujengea uwanja wa ndege. Hali hii ilizidi kutia fora baina 1949 na 1951 wakati-
Wangereza walipochukuwa ardhi iliyokuwa na Msikiti kwa madhumuni ya ujenzi.Kwa
hivyo watu walivyoambiwa n’gombe wao wachanjwe, waligoma na kuonakwamba Wangereza
walitaka kuwaulia n’gombe wao, kama ng’ombe wao walivyokufakufa Zanzibar
baada ya kukogeshwa katika madawa siku za kabla ya hapo, kwahivyo wakakataa. Badala
ya kutumia siasa, Mngereza akatumia kibri chake chakikoloni na kutumia nguvu na mabavu
kwa kuanza kutia viongozi wa wafugajin’gombe hao ndani na kuwapandisha Mahkamani.
Jambo hilo liliwakasirisha sanawazalia na kusababisha mgomo na mhadhara uliyoelekea
gerezani “kiinuwa miguu”na kuwatowa viongozi wao kwa nguvu. Mngereza kwa mara
nyengine tenaakaonyesha kibri chake cha kutumia nguvu na kupiga watu risasi, hapo
ndipovi kazuka “Vita vya N’gombe”. Tukio hilo ni tukio muhimu sana katika sera za kisiasa
za Zanzibar, kwani hapo ndipo gurudumu la kihistoria la kuleta mabadiliko na vuguvugu
la kuleta uhuru lilipozidi kupata nguvu. Vita hivyo vya N’gombeviliwaunganishaWazanzibari
wa matabaka mbali mbali na kuondosha yale mabomaya Mngereza ya kubaguwa watu
kwa makabila. Chanzo cha mgomo wa kupingauchanjwaji wa n’gombe ulianza Kiembe
Samaki, na watu wa huko wakiungwa mkonona mashamba mbali mbali wakaunda chama
35
na kukiita Hizbu ’l Watan Raiyat Sultani,na baadhi ya viongozi wao walikuwa ni Vuai
kiteweo, Miraaj Shaalab, Maalim Zaid,Haji Hussein n.k. Mngereza kwa kutumia nguvu
za kisilaha, nguvu za gereza nanguvu za mahkama zao waliukandamiza mdhahara huo
na viongozi hao. Hatimae Mngereza alishinda kijeshi lakini hakutanabahi kwamba alijichimbia
kaburi lakisiasa na kupigwa pigo lisotibika. Kumbukumbu hilo likawafanya
viongozi waHizbu, ambao chanzo chao kilikuwa Kiembe Samaki, na waliyokuwa hawana
asili yakiarabu, kuchukuwa khatuwa muhimu katika historia ya Zanzibar. Kwa vileviongozi
hawa walikuwa hawana elimu ya kizungu waliuendea uongozi wa ArabAssociation
uwasaidie katika mapambano yao na Mngereza. Matekeo yake yakawavyama hivyo viwili
kuungana na kufanya chama kimoja kilichojulikana kama Hizbu’l Watan au kilojulikana
kwa jina la kiingereza Zanzibar Nationalist Party (ZNP).Wakati vuguvugu la kusonga
mbele na kudai uhuru katika bara la Afrika lilikuwakatika kiwango cha hali ya juu kabisa.
Majina na mifano ya viongozi kama kinaKwame Nkurumah, Patrice Lumumba, Sokou
Toure, Jamal Abdel Nasser, ModiboKeita, Ben Bella, Didan Kimathi, Jomo Kenyatta n.k.
yalikuwa ni majina yakusisimua, ya kimapinduzi na ya kujivunia kwa kila Mzanzibari
na kwa Bara zimala Afrika. Viongo zi hawa waliichemuwa Afrika nzima na kuwaamsha
Waafrika wotekupigania Uhuru wao.
3.7 Upiganiaji Uhuru
Kama ilivyotajwa hapo juu ZNP ilishindwa na ASU (ASP) katika uchaguzi wa 1957,
lakini baadae mabadiliko makubwa ya kisiasa yalitokea. Viongozi vijana waKizanzibari
waliyokuwa Uingereza walishauriwa na uongozi wa ZNP kurudi nyumbani kwa madhu-
36
muni ya kushiriki katika kuanzisha upangaji wa mikakati wakuongoza mapambano ya
kisiasa na vuguvugu la uhuru. Viongozi hawa walikuwana umoja wao huko Uingereza na
kati yao walikuwa A. M. Babu, Khamis AbdullaAmeir, Ali Sultan Issa n.k. Viongozi hawa
waliamuwa kumpeleka Babu Zanzibar kutoka Uingereza kwa madhumuni ya kuchunguza
hali ya mambo na alitakiwaaepuke kujiunga na kundi lolote baina ya ASP na ZNP. Ingawaje,
Babu alipofika Zanzibar hatimae akajiunga na ZNP.Wenzake walipomsaili kuhusu
kisa cha kuamuakujiunga na upande mmoja, akawajibu kwamba kwa wakati huo ZNP ndio
iliyokuwa ikifuata siasa ya kimaendeleo na kwamba ASP ilikuwa bado inapinga uhuru na
kudai kwamba Mngereza asiondoke mpakaWaafrika wa Zanzibar wasome (“It is quite true
that the African Association of Zanzibar and Pemba does not favourthe proposed Round Table
Conference. As we are the backward community in theseislands, we shall ever beg our
needs and claim our rights for the benefit of Africans in this Protectorate for it is the adopted
policy of AfricanAssociation to achieve advancement and endeavour to win rights for our
selvesso long as we are sons and dauhgters of the soil. So our immigrant friendsshould not
forget that our aim is African self government,….not Zanzibari self-government – May 5,
1955 – Rankie Constitutional proposals). Hicho ndichokilikuwa kiini cha msingi wa chama
hicho baadae. Sumu hiyo ya kutodai uhuru kwa ASP ilitiwa na vibaraka wakiingereza
waliyopenyeza katika uongozi wa ASP. Inagawa ASP ilidai kuchelewesha uhuru hadi
Waafrika wasome, baada ya Mapinduzi kati ya watu wa mwanzo kuuliwa na serikali ya
Mapinduzi walikuwa wale wale viongozi wa Kiafrika waliosoma na serikali kuendeshwa
na wale wasiosoma. Hatimae viongozi wengine wa Kizanzibari wakawasili Zanzibar kutoka
Uingereza na shamra shamra na muamko wa kuendesha kampeni ukazidi kutia fora
na kabla ya miaka mitatu kupita vizuri, ZNP ikaweza kuchuwana na ASP katika uchaguzi
nakuweza kwenda karibu sare na ASP katika chaguzi za 1961. Kwa wakati huo ZNP
37
ndio iliyokuwa chem chem ya hamasa za upiganiaji uhuru wakati ASP ilitumia siasa ya
“Ugozi na Zuwiya”, yaani Ugozi wa rangi nyeusi nazuwiya Uhuru mpaka gozi asome.
Kwa upande mmoja chama cha ASP kiliaibisha Zanzibar, hasa wakati kulipokuwa na
mikutano mikubwa ya nchi za Kiafrika, kama vile PAFMEC kwani msimamo wa ASP
katika mikutano hiyo ulikuwa ule ule waUgozi na Zuwiya uhuru hadi Waafrika wasome
na ndio maana walikataa kuwaungamkono Hizbu katika kudai Uhuru. Suala hili lilileta
aibu hata kufanya viongozikama kina Nkurumah na Kanyama Chiume kuingilia kati na
kuwalazimisha ASPkujiunga katika mapambano ya kudai uhuru, na hatimae kusababishwa
kuundwa “kamati ya uhuru” ya ASP na Hizbu katika mwaka 1958. Katika mikutanoiliofanyika
PAFMECA, Mwanza 1958 na All African People’s Conference, 1959 Accra na
Zanzibar, ujumbe wa ASP, ulikuwa na wahka kwa sababu katika uongozi wake tokea hapo
nyuma kulikuwa na mgawanyiko baina ya Wa shirazi na Waafro, na katiya Wa Afro kulikuwa
wale wazalia hasa wa mashamba na “malumpa” “walala hoi” na ambao wengi wao
walikuwa si wenye asili ya Kizanzibari, na kulikuwa na kikundicha wasomi. ASP mwanzoni
walikataa kubadilisha siasa yao ya kuchelewesha uhuruna kukataa kutotumia ubaguzi
wa rangi kama ni msingi wa siasa yake, ingawajebaada ya kulazimishwa na PAFMECA
walikubali kufanya hivyo. ASP waliogopakusimama katika jukwaa la kudai uhuru pamoja
na ZNP kwa sababu waliogopakwamba suala hili lingeliondosha msingi wa siasa na kampeni
yao ya kudai kwamba Hizbu ni chama cha Waraabu, ingawa Hizbu walikuwa wote ni
Wakizanzibari kwa auzalia. Nyerere kwa kisiri siri akazidi kupalilia moto kwa kutia sumu
ya kusema kwamba maingiliano ya Wazanzibari bado yalikuwa kama baina ya ” Mabwana
nawengine Watumwa”. Ingawaje ASP ikadai katika PAFMECA kwamba, iko tayari
kuiunga mkono Hizbu katika kupigania uhuru na kuwacha ukabila mradi Hizbu nayo ingeli
ahidi kwamba pindi likitoka pande na kujigawa katoka ASP, hawataliunga mkono wala
38
kuungana nalo. Hizbu nao wakakubali masharti hayo kwamba hakuna upande wowote
ule utaounga mkono kundi lolote litalojitenga kutoka katika chama kimoja wapo. Kwa
kipindi fulani vyama vyote hivyo viwili vikawa vianapigania uhuru bega kwa bega kwa
hamasa za pamoja na kitaifa, hata kupanda majukwaa ya mikutano kwapamoja. Kutokana
na mvutano ambao kwa kimsingi ni wakitabaka na vile vile wenyemuelekeo wa uasilia
katika mwisho wa mwaka wa 1959, mvutano huo ulisababishakugawika kwa ASP na
kundi lenye mrengo wa kibwanyenye na kujitambua kamaWashirazi walitoka chama cha
ASP na kuunda chama cha Zanzibar and PembaPeople’s Party (ZPPP). Kwa upande wa
Hibzu nako kulikuwa na mirengo mitatu,mrengo wa kushoto ambao ulikuwa kina A. M.
Babu, Ahmed Badawi Qullatein, Ali Sultani, Abdulrazak Mussa Sima, Miraji Mpatani,
Abdulaziz Ali, Mzee wa Tarekh Muhsin Abeid, Amar Salim Kuku, Salim Ahnmed Salim
n.k.; mrengo wa kulia wa kina Juma Alley na wafadhila wa Wangereza waliyowacha kazi
za serikali dakika zamwisho na kuingia katika siasa, uhuru ulipokuwa unakaribia, kama
vile MohammedSalum Jinja, wengine wa mrengo wa kulia ambao ndio waliyopalilia siasa
ya chuki katika ZNP na kufuata mrengo wa kulia na kuzidi kuleta mifarakano ya kisiasa
baadala ya majadiliano na hatimae kutoka kwa Umma Party, ni Ahmed Lemky,Amani
Thani na Suleiman Malik. Kundi la kati na kati la ZNP lilikuwa ni akina Dk. Baalawi,
Maulidi Mshangama, Amour Zahor, Haji Hussein, Rashid Hamadi, Miraaj Shaalab, Vuai
Kiteweo, maalim Zaid na maalim Mandoa. Itaonekana kwamba hatakatika Kamati Kuu
ya Hizbu nako kulikuwa na mvutano mkubwa sana lakinimvutano huu ulikuwa zaidi baina
ya waliyoendelea wa mrengo wa kushoto na waselelea wa mrengo wa kulia. Kiongozi
wa Hizbu alikuwa Ali Muhsin na kwa sikuza mwanzo alikuwa ni kiongozi mshupavu wa
kujitolea kupigania uhuru wa Zanzibar. Vuai Kitoweo alikuwa Rais wa Hizbu na Katibu
Mkuu kuwa A. M. Babu. Kiongozi wa ASP alikuwa ni Abeid Amani Karume, ambae
39
alikulia Zanzibar, lak- ini Othman Sharif, msomi mmoja wapo katika ASP pamoja na
Abdulla Kassim Hanga, Hasnu Makame, Aboud Jumbe, Abdulaziz Twala walitarajiwa
hatimae kuchukwa uongozi kutoka kwa Karume, na Karume aliwaona hawa kama ni
wasaliti waliyojitayarisha kumpokonya n ofu lake la uongozi. Fungu lililomuunga mkono
Karume dhidi ya wasomi wa ASP walikuwa ni Afro Shirazi Youth League. ZPPP ilipoundwa
mrengo wa kulia wa Hizbu haukusita kunyakuwa nafasi yakuwaunga mkono na
kutarajia kupunguwa nguvu kwa ASP kinyume na ahadi walizozitowa katika PAFMECA,
Accra, ya kutoliunga mkono pande lolote litakalojigawa. Wakati huo, Hizbu ilipoungana
na ZPPP, Babu alikuwa safarini na aliporudi akakabiliwa na Karume na kusutwa
kwa maneno kama haya, “jee unaona tulisemaje sisi, unaona si wamewaunga mkono?”
Babu anadai kwamba alijaribu kusema na uongozi wa Hizbu, kwamba wamevunja ahadi
za Mkutano wa Accra bila ya kusikilizwa. Zaidi ya hayo kwa upande wa Hizbu wa
mrengo wa kulia walipata turufu mpya ya kuwapiga vita kina Babu kwa kupata msaada
wa mrengo wa kulia wa ZPPP. Kuundwa kwa ZPPP na kuongezwa katika uongozi wa
Hizbu kwa baadhiya vibaraka kama kina Amani Thani kwa bahati mbaya kulimbadilisha
msimamo na muelekeo wa Ali Muhsin na kumfanya kuelemea zaidi mrengo wa kulia
hata hatimae akishirikiana na Mngereza kumtia Katibu Mkuu wa ZNP A. M. Babu ndani,
akiwa kiongozi pekee chini ya ukoloni wakati wa serikali ya ndani, kuhukumiwa na kufungwa
kwa sababu za kisiasa. Njama za makusudi za kumfunga Babu zilipunguza kasi
ya mrengo wa kushoto na wakati katika uongozi wa Hizbu, namara tu alipofunguliwa
Babu mrengo wa kushoto ukadai watoke katika chamahicho. Babu akajaribu kuwazuia
wenzake kudai kwamba lazima wapambane navibaraka hao wakiwa ndani ya chama, na
hapo tu ndipo wangeliweza kuleta makubaliano ya kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibari
wote bila ya kujali ufuasi wa chama. Upinzani ulikuwa mkubwa na katika mkutano wa
40
kupendekeza na kupanga watetezi wa uchaguzi wa 1963 kundi la mrengo wa kushoto la
ZNP likadai kwamba chama cha ZNP lazima kichukuwe msimamo wa kitaifa na kuwacha
mtindo zorota wakusimamisha watetezi wa uchaguzi kwa mujib wa rangi au kabila. Yaani
Babu alidai, Ali Muhsin si lazima asimamishwe jimbo la Malindi na Abdulrasul Alarakiya
jimbo la Shangani. Babu alipendekeza Abdulrazak Mussa Simai asimamishwe jimbola
Malindi (Forodhani) na Ali Muhsin asimamishwe jimbo jengine lolote la uhakika, ili
kuwathibitishiaWazanzibari kwamba msingi wa siasa ya Hizbu haukuwa wa kikabila. Na
kuweka wazi kwamba kile ilichotaka Hizbu ni kuleta usawa kwa Wazanzibari wote kwa
jumla. Wale waliyokuwa na kasumba za mrengo wa kulia wakapinga mapendekezo hayo
na hatimae mrengo wa kushoto ukaamuwa kutokubali kufuata siasa hiyo ya kibaguzi na
kujitowa katika Hizbu na Julai, mwaka 1963, kikaundwa chama cha Umma Party na Babu
akawa ni Rais wake. Kufuatilia uchaguzi wa 1957 palifanyika uchaguzi mara ya tatu,
katika mwaka 1961,mwezi wa Januari, matokeo yalikuwa ASP ilipata viti 10, ZNP viti 9
na ZPPP viti 3. Katika mwaka 1961, mwezi wa Juni ASP ilipata viti 10 na ZNP kupata viti
10 na ZPPP viti 3. Katika uchaguzi huu kulitokea ghasiya na maisha ya watu kupotezwa
bure na wengi katika hao waliyoshiriki katika ghasia hizi walikuwa ni watu waliyokuwa na
asili ya Bara. Katika uchaguzi huo mbinu mbali mbali za kuwezesha kushinda zilitumika
sehemu zote mbili. Njia mojawapo ZNP iliyotumia ilikuwa ni kutumia kura za ZPPP
pale ambapo wasingelishinda, kuhamisha wapigaji kura kutoka zile sehemu waliyokuwa
na uhakika watashinda na kupeleka zile sehemu waliyokuwa na wasi wasi wa kushinda.
Utafiti na uchunguzi wa makini na wautulivu ulifanywa na ZNP na kuweza kujua hesabu
ya kila mpigaji kura hadikuweza kujua tofauti ya kura moja. Katika uchaguzi wa mwaka
1963, mwezi wa Julai ASP ilipata viti 13, ZNP viti 12 na ZPPP viti 6 na kwa hivyo ZNP na
ZPPP wakaunda serikali. ASP nao walitumia mbinu zao katika kujitayarisha na uchaguzi
41
lakini mipango na njama zao zilikuwa koroma kwa vile wao walipigania wingi waidadi ya
kura na sio wingi wa ustadi wa upigaji kura.
Ahmed Hassan Diria (mmoja kati ya waliyowauza na kina Hanga na kuwanyanganya
maliWapemba) na Ali Mwinyi Tambwe, huyu akiwa wa Tanganyika, walishughulika sana
katika siku za uchaguzi kuleta Watanganyika kutoka Bara na kuja kupiga kura Zanzibar.
Tatizo lao katika njama zao ilikuwa kwanza wametumia wageni na kwa vile hawa ilikuwa
ni wageni walipelekwa zile sehemu ambazo zikiunga mkono ASP na kwa hivyo watu
wa sehemu hizo hawakulalamika kwa vile hawa wageni walikuja kuwasaidia wao. Kwa
njia hiyo ASP ilizidisha idadi ya watu katika zile sehemu ambazo walikuwa tokea hapo
lazima washinde. Vile vile ghasia za Juni (ati leo tunaambiwa zilikuwa majaribio ya
mapinduzi, yaani kumpindua mgereza kwa magongo) zilikuwa na madhumuni yakuleta
vurugu ili watu wasishughulishwe na kuangalia wageni waliyokuja kupiga kura na vile
vile kutisha watu wasiende kupiga kura hasa zile sehemu ambazo ASP ilikuwa na wafuasi
wengi. Kitu kilicho wafaidisha ASP ni baada ya kuhisabiwa kura hizo kudai kwamba wao
ingawa walikuwa na kura nyingi zaidi na hata hivyo walishindwa. Dai hili halikuwa na
tija yoyote, kwani mbinu walizozitumia zilikuwa mbaya. Ushindi ulitegemea idadi ya viti
na sio idadi ya voti; pindi ASP ingelitumia maarifa mengine labda ingelifanikiwa zaidi, na
leo tungelikuwa tunasoma historia nyengine kabisa.
Umma Party haikushiriki katika uchaguzi wa 1963, na mara tu baada ya kujitoa katika
ZNP ilianzisha maingiliano ya kitaifa ya waandishi wa magazeti mbali mbali, vyama vya
wafanya kazi na kuungana na wale viongozi waliyoendelea wa ASP. Wakati huo Hizbu
ilishajiisha chuki kubwa sana dhidi ya Umma Party na hata kuwalazimisha viongozi hao
kuzihama zile sehemu walizoishi Mahizbu wengi, kwakuwafanyia kila kashfa na chuki
42
za kipuuzi viongozi hao wakalazimishwa kuhamia Miti Ulaya. Hii ilikuwa si siasa bali
ni upuuzi wa kisiasa. Kushirikiana kwa Umma Party na vikundi tofauti vya kipinzani
kuliwafanya viongozi washupavu, waliyoendelea na wa mrengo wa kushoto wa ASP kama
vile Hanga, Khamis Masoud, Twala, Saleh Sadalla n.k. kupata nguvu zaidi ndani ya ASP.
Kuundwa na kushiriki kwa ZPPP katika makubaliano ya mbinu za uchaguzi katika
uchaguzi wa 1963 kulirahisisha kushinda uchaguzi huo kwa urahisi zaidi, na hatimae ZNP
na ZPPP kuunda serikali. Serikali hiyo ambayo ilikuwa na Waziri Mkuu Mohammed
Shamte na Kiongozi wa serikali Ali Muhsin mara ilisahau wapi ilitoka nakuanza kutumia
mbinu mbaya za kisiasa za kutumia mabavu ambayo hata Mngereza hakuyatumia. Kitendo
chao cha mwanzo cha kidikteta kilikuwa ni kupitisha sheria ya kufungia chama cha Umma
Party, khatua iliyo kwenda kinyume na misingi ya demokrasia. Umma Party, kwa wakati
huo, kilikuwa kikijaribu kuunganisha Wazanzibari wote kwa jumla. Kwa bahati mbaya
Serikali ya Hizbu iliingiwa na wasiwasi mkubwa na vuguvugu la kitaifa lililokuwa likizidi
kupata nguvu, na serikali hiyo ikafikiria zaidi maslahi ya serikali yake kuliko ya nchi
nzima. Kama ilivyofichuliwa baadae serikali hiyo ilikwisha tayarisha nyaraka za kutiwa
ndani kwa viongozi mbali mbali wa Umma Party na ASP, lakini kwa bahati watu hao walipata
fununu na kukimbia nchi, Babu kukimbilia Dar es salaam. Serikali hiyo, ikapitisha
sheria nyengine kinyume na demokrasia, nayo ilikuwa kulifungia ruhu- sa yauchapishaji
gazeti mashuhuri la ZANEWS ambalo ndilo lililokuwa gazeti la maendeleo la kifani lisilo
kuwa na upuuzi wa chuki za kikabila na siasa ya kupendelea matabaka ya kikandamizaji.
Vitabu vingi vilikamatwa na kuchukuliwa na serikali, kuzuilia watu haki ya kidemokrasia
ya kuwa na uhuru wa kusoma. Mambo yote hayo yalikuwa yakiruhusiwa hata chini ya
utawala wa Ukoloni wa Kiingereza. ZNP ilikiogopa chama cha Umma Party kwa sababu,
chama hicho kilikuwa kikiungwa mkono zaidi na vijana wengi sana na wale waliyokuwa
43
na siasa ya kishupavu.
3.8 Umma Party
Chama cha Umma Party kama ilivyonakiliwa hapo juu kiliundwa kutokana na mchuano wa
kujaribu kuhifadhi misingi ya kijananchi ya usawa na umoja baina yaWazanzibari, kupigania
uhuru wa kweli na sio kivuli cha uhuru kilichomficha mwenye khatamu za kweli za
utawala, yaani uhuru wa bandia. Mwanzoni suala lakupigania uhuru wa kweli lilikuwa ni
lengo halisi la kuundwa kwa Hizbu, chama ambacho kilizalika na vuguvugu la kihamasa la
Ujananchi wa kugomea Majlis ‘ltashrih na “vita vya n’gombe” vilivyo ongozwa na akina
Vuai Kiteweo. Historia ya Hizbu inadhihirisha wazi kwamba chanzo cha mapambano
ya chama hicho kilikuwani ya kimaendeleo, kama “vita vya n’gombe” vilivyothibitisha,
msimamo wa chama hicho ukaendelea kuwa na nidhamu ya kupigiwa mfano wa kupinga
kutawaliwa,kudai uhuru bila masharti yoyote, kupigania utawala uliyowekwa na watu
wenyewe, kuendeshwa na watu wenyewe na kwa maslahi ya watu wenyewe, na kuunga
mkono upiganiaji uhuru na ukombozi wa nchi zote zilizokandamizwa nakuwa dhidi ya
ukoloni na ubeberu. Kutokana na siasa shupavu chama hicho kikaweza kwa muda mfupi
tu kugeuza kushindwa kabisa katika uchaguzi wa 1957na kuwa na nguvu za kupata viti
karibu sawa na chama cha ASP katika uchaguziwa Januari na Juni 1961. Siku hizo Hizbu
ililitukuzisha jina la Zanzibar katika vikao na mikutano mbali mbali ya kupigania haki
za waliyoonewa ulimwenguni kote. Kuunga mkono vuguvugu la kugombania uhuru wa
bara la Afrika na kupinga vikali udhalimu waliyofanyiwaWaafrika mbali mbali kama vile
kukamatwa, kuteswa nahatimae kuuwawa kwa mpiganiaji uhuru mashuhuri na mshupavu
44
Patrice Lumumba. Baadhi ya viongozi wa Hizbu walipoanza kuona uwezekano wa kupata
khatamu ukokaribu wakaanza kubadilika na wengine nyuso zao za kikweli zikaanza
kudhihiri.Wale viongozi washupavu waliyompinga Mngereza kinaga ubaga na kupinga
siasaya kibaguzi wakaanza kupikiwa majungu na kuwekewa vikwazo vya aina mbalimbali.
Kutokana na mbinu kama hizo ndipo Katibu Mkuu wa ZNP, Babu, akabuniwa kesi
na kufungwa na serikali ya ndani ya chama ambacho alikuwa ni katibu wake. Hii ilikuwa
ni mbinu ya kumuondosha njiani ili kurahisisha kupitishwa kwa mamboambayo yeye angeliyapinga.
Wakati huo ndipo vitimba kwiri waliyokuwa hawana ujuzi au uwezo wa
kisiasa navibaraka wa kiiengereza walipozidi kupenyezwa katika uongozi wa ZNP hasa
wale waliyokuwa wakifanya kazi serikalini chini ya Mngereza. Walipoingiya katikauongozi
vitimba kwiri na vibaraka hivyo vikapewa nyadhifa za juu na kutapakaza kasumba
zao na kutia sumu na ubaguzi katika chama ambacho sifa zake zilikuwa ni za kifani kabla
ya hapo.
Wakati bahari ilipokuwa chafu na mawimbi kuwa makali, waungwana hao walificha
kucha zao na kungoja ufukweni, lakini kazi ngumu ilipomalizika na bahari kuwashuwari
wakaanza kujipenyeza katika uongozi, wengine kupewa nyadhifa wasizozimudu na kumtumikia
Mkoloni ama kwa kujua au kwa kutotambua. Hali hii iliaibisha sana kwa kuitia
ZNP doa na baka pale ambapo nuru ikin’gara. Nguvu za mrengo wa kushoto na wa kati wa
ZNP zikazidi kupunguwa na kufifia na vitimbakwiri na vibaraka wakazidi kukaza kamba
huku wakiiangamiza Zanzibar. Wakati A. M. Babu alipomaliza kifungo chake na kutoka
gerezani dosari lilikuwa ni kubwa mno bila ya kuweza kutengezeka. Ingawa walijaribu
kuirejesha ZNP katika mkondo wake wa kijananchi, wa kimaendeleo na wakimapinduzi,
haikuwezekana tena kwa vile athari iliyofanywa na kina Amani Thani ilikwisha tendeka
na kupitia mpaka.Waliyotoka serikalini kwa Mngereza walitoka pamoja na kasumba zao
45
bila ya kuweza kujirekibisha na kuwa na fikra zile zile za kitabaka na kibaguzi kama
walivyotiwasumu, vipi wafikiri. Ingawa hawa walikuwa ni Wazanzibari wa kizalia, lakini
kwa vile walikuwa karne za nyuma na asili ya kiarabu na kuwa wasomi, wakatafsiriwa na
wale waliyokuwa na upungufu na upeo wa kisiasa, wakafanywa kama ni kisingizio cha
kuwadanganya makabwela kuwa ni watu waliyotaka kuleta utawala wa kiarabu na wa wasomi.
Wanasiasa waliyokuwa wenye fikra za kikasumba walikuwa ndani ya vyama vyote,
hata na wale waliyojiitaWaafrika. Ubovu wao ulitokana na fikra zao na sio namna ya sura,
rangi au makabila yao au kwamba walikuwa wasomi au pangu pakavu. Kwa wakati huo
Bara la Afrika zima pamoja naZanzibar lilikuwa na wataalam wa hali ya juu bila ya kuwa
na asili ya Uarabu, naingawa Waafrika wa asili na jadi walikuwa na elimu ya juu kabisa
haikuwafanya wote kuwa na fikra za kisiasa madhubuti na za kimaendeleo, kwani kati yao
kulikuwa na waliyokuwa na kasumba ya hali ya juu kabisa. Ujuzi wa kisiasa una miko yake
nasio kila mtu anaweza kuwanayo. ZNP kuegemea viongozi waliyokuwa na upungufuwa
sifa za kisiasa na kuwa na sifa nyengine tofauti za kibwanyenye ilikuwa nimakosa ambayo
yaliirejesha Zanzibar nyuma sana. Wale waliyotumia siasa yaukabila walifanya hivyo
kwa sababu ya ukosefu wa mfumo wa siasa maalum yaku tatua matatizo ya nchi kisiasa.
Wakati wa kabla ya uhuru kupatikana, ulikuwa ni wakati muhimu sana katika historia ya
Zanzibar, kwani ilikuwa ni wakati huo ambapo hali ya juu kabisa yakisiasa ilikuwa itumike
kwa manufaa ya watu wote. Huo ulikuwa sio wakati ambapovyama vya kisiasa vili kuwa
vipapatikie ullwa na khatam za serikali. Huo ulikuwani wakati wa vyama tofauti vya
kisiasa kuungana na kuyalinda na kuyachungamaslahi ya Zanzibar na sio vuta n’kuvute.
Wale wenye akili za mchwa za kuila nyumba wakayo walitumilia hali hiyo ya ubina fsi
na kuzidi kutia chuki baina yaWazanzibari, chuki ambazo kwa desturi ni fikra za wale
watu ambao hawana kinaau upeo wa ufahamivu wa kisiasa, watu wa aina hii walikuwako
46
katika vyama vyoteviwili vikubwa vya kisiasa . Mwenye ujuzi wa kisiasa hutumia ho ja
za kisiasa na sioza kikabila, kwani siku zote kiini bora cha kisiasa huwa kinaambatana na
sababuza kimsingi nazo ni kukomesha sababu ambazo hujengeka kwa ubaguzi wakitabaka.
3.9 Zanzibar kama tausi
Kabla kuundwa kwa Umma Party, wale viongozi wa ZNP waliyokuwa na mrengo wa
kimaendeleo walijaribu kuunganisha Wazanzibari wa vyama mbali mbali, kuondosha
ubaguzi wa aina mbali mbali katika ZNP. Mapambano ndani ya ZNP yalikuwa nimagumu
na kama ilivyoelezwa huko nyuma wengi wa mrengo wa kushoto walitakakujitoa katika
chama hicho lakini A.M.Babu alisisitiza wapambane wakiwa ndani yachama na kwa njia
kama hiyo ndio wangeliweza kuubadilisha mfumo wa chama hichokuwa bora zaidi. Ingawaje
hatimae hata yeye nae, yaani Babu, alipungukiwa nasubra wakati Kamati Kuu
ya ZNP alipokuwa akiteuwa wagombeaji uchaguzi wamwaka 1963. Katika kikao hicho
Babu alisisitiza kwamba ili ZNP ionekane kwambani chama cha Kizanzibari kisichokuwa
na ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa vile ZNP ilikuwa ni chama chenye mchanganyiko
wa watu wenye asili mbali mbali basi,ilibidi uwekwe mfano dhahiri kwa kila mtu kuona
kwa macho yake mwenyewe. Kwahivyo katika mkutano huo Babu, kama ilivyotajwa
hapo juu, akapendekezaAbdulrazak Mussa Simai, msemaji mashuhuri katika mikutano ya
hadhara ya Hizbuambae alikuwa hana asili ya kiarabu, awe mtetezi wa jimbo la uchaguzi
la Malindi.Hili lingekuwa pigo kubwa kwa siasa ya Mngereza ya kutaka kugawa watu
kwamafungu ya kikabila na ingelikuwa ushindi mkubwa kwa siasa ya ZNP ya kukomesha
ukabila na kuweka Wazanzibari w-ote sawa. Mrengo wa kulia waHalmashauri Kuu
47
ya ZNP ikapinga pendekezo hilo na hapo ndipo maji yalipomwagika na kina Babu, Abdulrazak
Mussa Simai, Muhsin Abeid, AbdulazizAli, Miraji Mpatani, Ali Sultani, Amar
Salim Kuku, Ahmed Badawi Qulllatein, Salim Ahmed Salim, Dr. Ahmed Rashid, Tahir
Adnan na wengineo kutoka chama nakuunda Umma Party iliyokuwa na siasa ya Wazanzibari
wote kuwa sawa. Dr. Idarus Baalawi na Maulid Mshangama walikuwa ni viongozi
wawili wa ZNP waliyokuwawakitia na kutoa kujiunga na Umma Party na kwa kweli mkutano
wa mwanzo wawaandishi wa magazeti wa Umma Party ulifanywa katika nyumba ya
MaulidiMshangama, huko Mbuyuni. ZNP ilisahau kusisitiza uendelezaji wa sura ya Zanzibar
yakuwa nchi iliyokuwa na mchanganyikowa damu,makabila, mila, jamiina utamaduni
tofauti, nchi yenye rangi kama za tausi, tofauti ya rangi zake zikiwandio sifa na pambo lake.
3.10 Vugu vugu jipya la Upinzani
Chama cha Umma Party kilikuwa hakina kasumba za ugozi au ukabila, lengo lake lilikuwa
kuwakombowa Wazanzibari kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Lengola Umma
Party halikuwa kuimba wimbo wa kupigania uhuru tu bali ilileta mfumo mpya wa kisiasa
ambao uliwavutia Wazanzibari tofauti kutoka matabaka tofauti.Umma Party ilipendeza
kwa Wazanzibari kwa sababu haikuwa tu inadai uhuru bali ilikuwa imeshatayarisha program/
sera iliyohitajika ya kufanya maisha ya Mzanzibari bora. Ilikwisha tayarisha jinsi ya
haki za mfanyakazi zilindwe, kuhakikisha kwamba mtuanapata kipato kwa mujib wa mahitaji
yake, yaani yule mwenye ukoo mkubwaalikuwa apatiwe kipato cha kutosheleza ukoo
wake wote. Kuwahakikishia wafanyakazi kazi bora, sheria za kuwalinda na kuwaepusha
na ukosaji kazi.Kuwahakikishia wafanya kazi mapumziko ya likizo marefu na malipo yake
48
yakutosha. Kuwahakikishia malipo ya kujitizama wakikosa kazi. Kuwajengea makaazibora
na ya siha njema ili wawe watu wenye siha nzuri za kuweza kuitumikia jamii yao
vyema. Wakulima walikuwa wahakikishiwe uuzajiwabidhaa zao kwa bei muwafaka na kupatiwa
misaada wanayohitaji katika jukumu lao la uzalishaji mali bora. Walikuwa wapewe
vifaa vya lazima vilivyoendelea, kupewa mikopo ya kuendeleza kilimo bora,kusaidiwa
kwa ujuzi wa kisasa na kujengwa kwa sehemu za mashamba ili kuwezakujitegemea na
kuwekewa Benki ya maendelo ya ukulima na uvuvi. Mashambakuweza kuwa na huduma
zote zilizopatikana mjini bila ya haja ya kusafiri safiri.Kuwahaki kishia watu wa mashamba
umeme, maji safi ya mfereji, makaro, usafi namaskuli ya madarasa ya juu yaliyokuwa na
sifa sawa na mijini. Kuwajengea watuwa mashamba vituo vya siha vilivyoweza kuhudumia
magonjwa yote ya kawaida namagonjwa makubwa sana tu kupelekwa Spitali Kuu. Ujenzi
wa mashamba ulikuwauwe na vituo mbali mbali ambavyo vitu vyote vilikuwa viweze kupatikana
katika”centa” maalumm bila ya kulazimika kwenda mijini. Kulipangwa ujenzi wa
viwandambali mbali katika sehemu hizo za mashamba. Wavuvi walipangiwa uvuvi bora
wakutumia vifaa, mitambo na vyombo bora. Kuhakikishiwa usalama wao wakiwabaharini
kwa kuweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama wangelipata matatizo.Walikuwa wahakikishiwe
vyumba vya barafu vya samaki wao na kuhakikishiwaviwanda vidogo vidogo
vya kutia samaki katika vibati. Wavuvi kwa vile wengi waoni watu wa mashamba wangelipata
huduma kama zile wakulima waliyozipata kwa vilewote wakiishi katika mazingara
ya aina moja.
Maisha ya Wanawake yalikuwa yaendelezwe kwa kila fani, sehemu za wazazi maspitalini
zilikuwa ziendelezwe ili kumtukuza mzazi na kumfanya ajivunie kuzaana kutambuwa
kwamba kuzaa kwake kulikuwa ni kutekeleza wajib mtukufu katikajamii. Wazazi walikuwa
wapewe mapumziko maalum baada ya uzazi, wale waliyofanyakazi kuhakikishiwa
49
mishahara yao kamili kwa muda wa kutosha na wale waliyokuwawakifanya kazi za kutunza
ukoo kuhakikishiwa kipato sawa na mahitaji yao. Siha za watoto wao zilikuwa zitunzwe,
kuangaliwa na kufuatilizwa tokea wakiwa wachanga. Kuhakikishiwa kupata chakula bora,
kuchanjwa, kupimwa kwa majira kuhakikishiwa malezi bora ikiwa kwa kusaidiwa mabibi
zao waliyowaleya au kuwajengea sehemu maalum za kutunzwa wakati wazazi wao wakiwa
wameshughulikana kazi. Ilipangwa kuwahakikishia mabibi kazi na majira bora ya kazi
na kuwahakikishia kipato bora na haki sawa katika jamii. Elimu ya mabibi ilikuwaitiliwe
mkazo mkubwa zaidi.
Wazee wote waliyokuwa na jamaa au bila ya jamaa walikuwa wahakikishiwe maisha
bora bila ya kupata taabu zozote. Walikuwa watizamwe katika vituo maalum vyawazee,
pale ambapo pangelihitajika. Wagonjwa, wasiyojiweza na vilema walikuwa wapewe
haki saha na wananchi wengine na walikuwa watizamwe na kutunzwa bila ya ubaguzi
au dharau yoyote.Ilipangwa wapewe huduma zote za lazima bila malipo au mapendeleo
yoyote,kuhakikishiwa elimu na siha bora wakiwa chini ya uangalizi wa watu waliyojifunzakazi
hizo. Vijana walikuwa wahakikishiwe maisha bora majumbani mwao ambako
wazee wao walikuwa wahakikishiwe maisha bora na jamii kwa jumla ilikuwa iwahakikishie
kipato cha kutosha na kwa hivyo jamii kuweza kuwatizama vijana na kuwahakikisha
maisha bora. Kama vijana wangelihakikishiwa maisha bora majumbani mwao wangeliweza
kushiriki kikamilifu katika masomo tofauti ya kujiendeleza. Masomo ya aina mbali
mbali ya kutosheleza matakwa ya kijana wa Kizanzibari yalikwishapangwa ambayo yalisisitiza
umuhimu wa masomo mbali mbali kuambatanana mazingara yetu. Skuli za
kawaida zilikuwa ziende sambamba na maskuli mbalimbali ya ufundi kwa madhumuni
ya kutajirisha siasa+ na uchumi wa Zanzibar.Maskulini elimu ya kilimo ilikuwa itiliwe
mkazo kuambatana na mazao tuliyokuwanayo na yale ambayo yangewezekana kupan-
50
dishwa baada ya uchunguzi nautaratibu makini na maaluum. Mfano mwengine maskuli
hayo yangelifundisha zaidikuhusu bahari ya Zanzibar na hazina yake na kujuwa jinsi ya
kuitumia, kuitunza na kuihifadhi bahari hiyo. Masomo kama haya na mengi mengineyo
kama ya siha,uchumi, n.k. yalikuwa yaendelezwe tokea skuli za msingi na hatimae vijana
kuwana uzoefu bora wa kuchaguwa na kujua walichotaka kufanya baadae katika
maishayao yakiambatana na majingara ya nchi. Vijana walikuwa walindwe na uhuni
nakuzurura ovyo na baadala yake walikuwa wapewe nafasi tofauti za kuwawezesha kutumikia
jamii na kujifurahisha wenyewe kama vile katika riadha na michezo mbalimbali.
Vijana ndio walitizamiwa hatimae kulijenga taifa la Kizanzibari na kwa hivyo mipaka ya
kujiendeleza walikuwa wawe nayo wenyewe. Wazanzibari wote walipangiwa wawe na
haki sawa sawa na haki hizo kulindwa nakuhifadhiwa na Mahkama huru, zenye msingi wa
Katiba na Sheria halali.
Wafanyakazi serikalini walikuwa na haki ya kufuata siasa yoyote waliyoitaka,lakini walipokuwa
makazini mwao walikuwa wawe na wajib wa kuutumikia umma wa Kizanzibari bila
ya kujali imani na vyama vyao. Na serikali yoyote ambayoingelitawala isingelitakiwa
iwabadilishe wale wafanyakazi wa serikali ambao imanizao zisingeliambatana na siasa ya
serikali. Wafanya kazi hao walikuwa wahakikishiwe ulinzi wa haki zao zote za kifanya
kazi, kupewa haki zote zilizostahiki. Wale ambao wangelikosa kazi wangelifanyi wa mipango
ya kulipwa hadi kupata kazi upya. Wazanzibari walikuwa wahakikishiwe kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa dolalao na kupewa uhuru wa kuchaguwa viongozi ambao
wangeli wawakilisha katika Bunge halali na kuhifadhiwa haki zao zote za Kidemokrasia,
kama vile uhuru wakusema, wa kusoma na kuandika, wa kujikusanya na wa kufanya
mikutano,kugoma na kuuandamana, haki za kibinaadam kwa jumla n.k. Mipango iliwekwa
kuhakikisha kwamba hakutakuwa na tofauti yoyote baina ya Pemba na Unguja.
51
Umma Party ilikataa kujishughulisha na siasa za kipuuzi za Ugozi na Ukabila kwa sababu
ilikuwa na program maalum ya kuihifadhi na kuinusuru Zanzibar. Umma Party ilikuwa
na mpango maalum wa Uchumi wa kuinusuru Zanzibar. Mpango wa uchumi huo ulikuwa
ni usambazaji wa vituo tafauti katika sehemu maalum mbalimbali za Unguja na Pemba.
Vituo hivyo vilikuwa viwe kama chem chem, kiini chahuduma tafauti, zenye michirizi ya
kiuchumi, michirizi hiyo ilikuwa iizunguka chemchem hizo kutoka kila pembe. Michirizi
hiyo ilikuwa iwe kama mishipa ya damu,ikiwa na sifa zote za kijamii zikinufaisha maisha
ya mwananchi, kwa mfano mchirizi mmoja ungelikuwa unawakilisha tu seme ukulima au
uvuvi. Kwanza mchirizi huu ungelijengwa kwa mujib ya uwezo na mazingara maalum
ya sehemu inayohusika naungelipangiwa mipango ya hali ya juu kabisa kuambatana na
uchunguzi wakisayansi ili kuwezesha kuzalisha mazao bora kabisa. Mchirizi huo ungelihakikishiwa
usafiri bora kabisa na sio mabarabara mabovu yenye mashimo matupu, bara
bara zilikuwa ziwe za kuweza kusafirishia bidhaa kwa haraka na kwa usalama. Bara bara
hizo wakati huo huo zingelifaidisha maendeleo ya jumla yasehemu inayohusika na nchi
nzima kwa jumla na kuwezesha uuzaji na usambazajiwa vifaa na bidhaa tofauti. Michirizi
mingine ungelihusika na vitu kama vile ujenzi wa viwanda vidogo vidogo mbali mbali,
ujenzi wa majumba bora, ujenzi wa maspitalina maskuli, usambazaji wa umeme, soko na
vituo vya biashara, siha bora: vituobora vya siha, maji safi , makaro n.k. Upangaji makini
wa mambo hayo ungelizaamakazi mbali mbali katika sehemu hizo na kukuza hali bora
ya maisha ya wananchi sehemu zote. Vituo kama hivyo vingelisambazwa sehemu tafauti,
kila kimojakujishughulisha na mambo maalum yaliyohitajika nchini na yaliyoambatana
namazingara yao na vingeliingiliana kwa madhumuni ya kusaidiana na kushirikiana.Fedha
za ujenzi huo zingelitokana na uchumi wa nchi kwa jumla, uchumi ambao hatimae ungelinufaika
kutokana na maendeleo hayo. Kwa wakati huo uchumi wa Zanzibar ulikuwa
52
umenona. Wananchi wa sehemu hizo mbali mbali wenyewe walitarajiwa kupatiwa ujuzi
uliyohusika na hatimae wenyewe kuendesha miradi hiyotofauti ikipewa muongozo na
marekibisho tu na Serikali Kuu.
Siasa ya miaka ya mwanzo ya 1960 na kuendelea ilikuwa ni siasa iliyonuka mizoga ya
kikabila na ugozi, tofauti kabisa na siasa ya leo, wakati ambapo Wazanzibari karibu wote
wanapigania Uzanzibari na kukataa kumezwa na Bara. Ingawa leo wanaotumia siasa ya
ukabila ni wachache na wasiyokuwa na maana, juu ya hivyo bado pana haja kubwa sana ya
kukariri ubaguzi wa kikabila ili kufaham historia nasababu za kutumia njama hizo. Suala
hili litakaririwa zaidi wakati tukio la Mapinduzi na siasa ya CCM zitakapochambuliwa.
Umma Party ilibahatika kuwa na viongozi na wafuasi wengi waliyosoma, kushir- ikikatika
kuijenga ZNP na kwa kupitia njia hiyo kuweza kukielewa chama h- icho vizurizaidi jambo
lililokuwa na umuhimu mkubwa mno baadae. Baadae U- mma Party kwakupitia “United
Front” iliweza kusaidia kurekibisha mfumo wa wale viongozi waASP waliyokuwa mrengo
wa kushoto. Siasa ya Umma Party ilikuwa kuwapiganiawanyonge na ilibahatika kuwa na
mizizi katika tabaka la wafanyakazi na wakulima vile vile, hali hii ilizidi kupata nguvu
kwa kuungwa mkono na Umoja wa Wafanyakazi wa FPTU (Federation of Progressive
Trade Unions) ambao ulikuaUmoja wenye msimamo madhubuti, imara na wa kimaendeleo.
Kuungwa mkono kwaUmma Party na FPTU kulikuwa na umuhimu mkubwa sana
kwa vile Umoja huuulikuwa umeshatia mizizi katika umma wa wafanyakazi na wakulima
na Umoja ambao ulikuwa unaaminika na kuwa na maingiliano mazuri na ZPFL (Zanzibar
and Pemba Federation of Labour) Umoja wa Wafanyakazi uliyofanyakazi pamoja na
ASP. Maingiliano haya hatimae yakazalisha Zanzibar Revolutionary Trade Unions. Kwa
muda mfupi wa maisha ya Umma Party, kabla ya chama hicho kupigwa marufuku nana
serikali ya ZNP, kiliweza kuunganisha wanasiasa na vijana wote wa mrengo wakati na wa
53
kushoto. Wakati wa kuundwa Chama cha Ummanyoyo za watu wengizilifurahika na kuwa
na tamaa kubwa ya chama hicho kuleta mabadiliko yakimaendeleo Zanzibar. Pindi ingelikuwa
chama hicho hakikufungiwa na Hizbu miezisita tu baada ya kuundwa, basi Zanzibar
leo ingelikuwa inajitawala wenyewe, ikiwana wataalam wake wote na utajiri wake wote
mikononi mwake wenyewe kwa manufaaya kila Mzanzibari. Na maingiliano ye- tu na
Tanganyika yangelikuwa ya kidugubaina ya nchi mbili huru zinazohishimiana, kutukuzana
na kusaidiana kimaendeleo,na sio kutawaliana. Siasa ya chama cha Umma ilipendeza kwa
haraka sana hasa katika jamii ya vijana na baina ya watu wa matabaka ya chini wa vyama
vyote viwili vikubwa. Lengomojawapo muhimu ilikuwa ni kujaribu kuleta masikilizano
mema hasa na mrengo wakushoto wa ASP na haikuchukuwa muda mrefu vyama vyote
hivi viwili vikubwavikaanza kuingiwa na wasi wasi walipoona vijana na wafanya kazi wa
sehemu zotembili wakikaribiana katika mfumo mpya wa uhuru na umoja. Kushirikiana
huku na ASP, vyama vya wafanya kazi na vyama vya waandishi magazeti na wengineo
vilileta imani na muamko mpya visiwani. Hapo pakaundwa United Front “muunganisho
wa vyama na fikra tofauti ” na muelekeo wa mapambano ukaanza kutia sura mpya. Huu
ni wakati mmoja wapo muhimu sana katika historia yaZanzibar kwa ni kipindi hichi cha
muda wa miezi sita, kutoka Juni, 1963 hadiJanuari 64, nchi nzima ulipambwa na jazba
za kinajananchi zilizofanya damu zawana nchi kuchemka na kuwa na matumainio ya hali
ya juu kabisa. Jambo muhimu lililofanya hamasa za kijananchi wa Kizanzibari ilikuwa
ni uundaji wa Umma Party,kwani baada ya kuundwa chama hicho, mfumo wa upinzani
ulichukuwa sura mpyakabisa. Hali hii ya kujitolea ilitokana na program ya Umma Party
katika kuipangiaZanzibar mikakati ya kimapambano ya siku za usoni. Kuunganisha kwa
vikosi mbalimbali vya utayarishaji mabadiliko yakuleta neema nchini uliwafanya viongozi
mbalimbali wa vyama vilivyounga mkono ASP, kungana kwa dhati na Umma Party
54
katikakuijenga Zanzibar mpya. ASP kwa wakati huo ilikwisha shindwa katika uchaguziwa
1963 na viongozi wake waliparaganyika na kutokuwa na msimao madhubuti, nakutokuwa
na siasa na sera mkakati ya kupambana na serikali ya Hizbu. Kwa hivyokuchomoza kwa
chama cha Umma Party na kuchukuwa dhamana ya kujengaupinzani mpya kwa kuunga
nisha waandishi wa upinzani, vyama vya wafanyakazina wakulima, vijana na wanawake
na viongozi “militant” wa ASP na Umma Party,ulifanya muamko wa Zanzibar kupata
hamasa mpya. Wadhifa wa mwanzo wa umojahuu mpya ulikuwa kukuza elimu ya kisiasa
na kupanga mbinu za kupambana,kuweka misingi mipya ya kufanya kazi za kichama na
aina mpya ya mfumo wamapambano. Hali hii iliwezekana kutokana na ukakamavu na
uzoefu wa mipango yakisiasa wa uongozi na wafuasi wa Umma Party. Upinzani mpya
ukazalika na tamaaya kujikombowa ikazidi kutia nuru.
3.11 Serikali ya taifa
Muda ulikuwa mfupi kwa chama cha Umma kuweza kushiriki katika kampeni za kujiandaa
kichama, kwa hivyo chama hicho hakikupata wakati wa kukuwa nakujisambaza zaidi.
Nguvu za wana Umma hao zilikwishatumika kujenga siasa ya msingi ya kupigania uhuru.
Umma kwa sababu hizo iliamuwa kutoshiriki katika uchaguzi wa 1963 na badala yake ilijipalilia
kutowa elimu ya siasa ya kimsingi katika jukumu la kujaribu kuwaletaWazanzibari
wote pamoja. Kwa mara ya mwanzo tokea kuanza kwa siasa za kupigania uhuru palikuwa
na tamaa ya Wazanzibari wote kuungana, hasa katika mambo fulani ya kimsingi.
Wakati huo muungano wa ZNP na ZPPP ndio uliyokuwa ukiendesha serikali ya ndani
na kufuatia uchaguzi wa 1963 vyama viwili hivyo vikaishinda ASP na kuendelea kuende-
55
sha serikali peke yao, hadi kupatikana kwa uhuru Disemba 10, ingawa ASP ilipendekeza
kuundwa kwa serikali ya kitaifa yaani ASP nayo kuwemo serikalini. ASP ilivunjika moyo
sana kwa kutoshirikishwa katika uongozi wa nchi hasa kwa vile uhuru ulipiganiwa na
vyama vyote, na mada ya uongozi wa nchi ni wadhifa wawananchi wote kwa jumla, bila
kujali ufuasi wa chama fulani. Pindi pangelikuwa na serikali ya Kitaifa basi Zanzibar
leo ingelikuwa nyengine na kuweza kupiga khatuwa kubwa sana, kwani kusingelikuwa
na Muungano na nchi ingelitononeka. Katika serikali hiyo ya 1963, ni ZNP kwa kweli
ndiyo hasa iliyokuwa ikiendesha serikali na Mohammed Shamte alikuwa kawekwa kama
kilemba tu.
Serikali ya ZNP, badala ya kujishughulisha na uongozi wa taifa kwa njia ya kiusawa na
kihalali, kwa kweli ilishughulishwa zaidi na kuipiga vita Umma Party hata kuvisahau
vyama vya ASP na ZPPP. Ilifanya hivyo kwa sababu ilihisi kwamba Umma Party ilikuwa
na uwezo na ujuzi wa kuweza kupambana na ZNP na hatimae kuweza hata kuwachukuwa
wafuasi wa ZNP, hasa kwa vile ni makada wa Umma ndio waliyoijenga ZNP na wakizijuwa
mbinu na mipango yote. Kwa vile ZNP ilitambua ukweli huo. Chini kwa chini,
kwa siri kabisa, ikaanza kupika majungu ya siri kwa kugawa silaha baina ya wafuasi
wake chini ya uongozi wa wale vijana waliyofunzwa mambo ya kijeshi huko Misri, kati
ya vijana hao walikuwemo baadhiya wana ZNP wa mwanzo waliyofariki katika mapinduzi
ya 1964. Silaha hizo hazikutolewa kwa maksudi ya kupigia paredi. Moja kati ya
njama zilizopangwa naserikali ya Hizbu ilikuwa ni kumkamata Babu, pamoja na viongozi
fulani wa ASP, lakini Babu alizipata fununu hizo na kutoroka Unguja na kwenda Dar
es salaam. Ilidhihirishwa baadae kwamba kulikuwa na listi ya watu 120 serikali hiyo
ya ZNP alitaka kuwatia mbaroni, listi hiyo ilikamatwa baada ya Mapinduzi. Baada ya
uhuru serikali hiyo ikapitisha sheria za kikandamizaji ambazo hata mkoloni Mngereza
56
hakuzipitisha wakati wa ukoloni, nazo sheria hizo zilikuwa kinyume na dhidi ya haki za
kibinaadam na demokrasia kwa jumla. Hapo ndipo haki na uhuru wa kutoa maoni kuanza
kukandamizwa, uhuru wa kukutana na kuchapisha ukanyimwa, uhuru wa mtu kujiunga na
chama atakacho ukaingiliwa kati, uhuru wa kusafiri ukapunguzwa na uhuru wa mahkama
huru ukaingiliwa katikwa kuwa na kupalilia sheria ya kumweka watu vizuizini. Hatua
zote hizi za kuvunja haki za kibinaadam zilikuwa zimepangiwa Umma Party, chama ambacho
kilipigwa marufuku, kama ilivyotajwa hapo juu. Gazeti lake la Sauti ya Umma
na ZANEWS kufungiwa na kupanga mipango ya kuwakamata viongozi wote wa Umma
pamoja na viongozi wengine wa Upinzani, yaani wa ASP, FPTU na ZPFL. Mipango hii
ndio kwa upande mmoja iliyosababisha na kuharakisha kufanyika kwa Mapinduzi(Hizbu
wasimlaumu mtu kuhusu Mapinduzi kwani wame yapaliliya wenyewe). Hatuwa hizi za
kikandamizaji zilizidi kuwaleta pamoja viongozi wa Umma na wamrengo wa kushoto
wa ASP pamoja na vyama vyao vya wafanyakazi na waandishiwa magazeti pamoja na
vijana. Kwa upande mwengine kuungana kwa Umma na mrengo wa kushoto wa ASP
ambao ulikuwa na karibu wataalam wote wa ASP na wakati huo huo wakiwa ni Wazanzibari
asilia, ulileta mgogoro katika uongozi wa ASP. Uongozi wa ASP nao ulikuwa na
migogoro yake wenyewe hata kabla ya kuundwa kwa Umma Party. Itakumbukwa huko
nyuma, kwamba tokea kuundwa kwa ASP katika mwaka 1957 kulikuwa na matatizo baina
ya Washirazi na wale waliyokuwa na asili ya Bara na hapo ikabidi Nyerere aingie kati
na kufudikiza fudikiza. Matatizo hayo hayakutatuka nahatimae kina Shamte wakaunda
chama chao baada yakiongozi mmoja mashuhuri wa Shirazi Association, Sh. Ameir Tajo,
kuadhiriwa katika mkutano wa hadhara wa ASP na kufukuzwa chama. Ingawaje mgogoro
huu baina ya wenye asili ya kibara na ya Kizanzibari haukumalizika hapo kama tutavyoona
huko mbele. Mvutano mwengine ulitokana na waliyosoma na wasiyosoma, mfano
57
huu ulikuwa zaidi baina ya Karume, Othman Sharif na Abdulla Kassim Hanga. Waasis
wa ASP waliyotoka tokea African Association walijiona kuwa na haki zaidi ya uongozi
wa ASP. ASP ilikuwa na Umoja wa vijana wa aina mbili mmoja ukiwa wa YASU, yaani
Young African Social Union, Umoja ambao ulijitambulisha kama chama cha “kijamii na
kitamaduni” lakini kwa kweli kilikuwa chama cha vijana wa Kiafrika wenye muelekeo
wao wenyewe nyeti wa kisiasa. Wanachama wake wote walikuwa ni waliyosoma na wazalia
wa Kizanzibari. Kiongozwao alikuwa Othman Sharif, lakini Aboud Jumbe, Hasnu
Makame na Mdungi Usi nikati ya waliyoshiriki katika Uongozi wa vijana hao. Chama
hichi hakikujitambulisha wazi kuwa ni chama cha vijana wa ASP ingawa wote wao ama
walikuwa ni wafuasi au waunga mkono wa Chama hicho. Sh. Ameir Tajo ndiye aliyowapatia
msaada wakujenga jumba lao la YASU, huko Miembeni, baada ya Mapinduzi chama
hicho kilipigwa marufuku, ingawa chama hicho kilikuwa kikitowa huduma kwa watoto
wakiswahili ambao wengi leo wana elimu ya juu kabisa. Chama hasa cha vijana wa ASP
kilijulikana kama Afro shirazi Youth League, ASYL. Viongozi wa chama hichi walikuwa
ni wale waliyokosa elimu na wengi wao wakiwa na asili ya bara, ingawaje wafuasi wa
chama hichi hawakuwa vijana wa kweli kama vile vijana wa YASU bali walikuwa ni watu
wazima karibu wote wakiwa watabaka la chini kabisa, malumpa, walala hoi wakiwa wengi
wao wasiyokuwa wazalia wa Zanzibar. Hawa walimuunga mkono Karume kwa sababu
yeye mwenyewe hakuwa msomi kama wao, akiwa mtu wa tabaka la chini, asiyekuwa
mzalia wa Zanzibar bali alikuja Zanzibar akiwa ni mtoto. Na Karume nae kwa upande
wake akiwaamini ASYL kwa sababu hizo hizo, na siasa yao ilikuwa ni kutumia ugozi bila
ya kuwa na mfumo, muelekeo au sera zozote maalum za kisiasa za kuinusuru Zainzibar.
Zaidi ya mgawanyo huo, kulikuwa na chama cha wafanya kazi cha ZPFL ambacho ingawa
kilikuwa na baadhi ya wazalia wa Bara katika uongozi wake, kilikuwa na mfumo afad-
58
hali wa kimaendeleo ukifananisha na mfumo wa ubaraka , ingawa viongozi wachache wa
chama hichi ndio waliowauza kina Twala na Hanga. Kwa hivyo ndani ya uongozi wa ASP
kulikuwa na migawanyo ya migongano ambayo imeathiri sana hali bora ya Visiwa vyetu.
3.12 Malumpa wa Zanzibar
Malumpa, “walalahoi” au watu walio tabaka la chini kabisa la jamii ni kwa desturi ni watu
wenye malalamiko mengi zaidi katika jamii za kila aina. Tabaka hili, siku zote liko tayari
kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kijamii kwa sababu kama inavyosemekana ni tabaka
ambalo katika mapambano ya ana kwa ana, halijali, kutoogopa wala kuwa na wasi wasi,
kwa sababu huwa hawaogopi kupoteza maslahi yoyote , kwani wakipotezacho si zaidi bali
ni minyororo yao ya kisiasa na kiuchumi . Hili kwa desturi ni tabaka linyonywalo zaidi,
linalokandamizwa kuliko tabaka lolote na linaloteseka kikomo cha juu kabisa ukifananisha
na matabaka mengine ya jamii. Tabaka hili likipata uongozi mzuri ndilo tabaka linaloleta
mabadiliko ya kuendeleza maisha bora ya kila mwananchi. Ingawaje tabaka hili likikosa
viongozia u uongozi bora linaweza kuleta athari kubwa mno katika jamii. Zanzibar karne
za karibuni imekuwa ni nchi iliyofaidika na kunufaika kiuchumi.Watu wake walikuwa na
kipato cha kutosha na kuwafanya kutokubali kutumwa. Kwa kawaida ijapokua Mzanzibari
asilia alikuwa hali ya chini, aliweza kuwa na kipato cha kutosha cha kujiepusha
kuingia katika tabaka la “ulumpa”. Siku za uvunaji karafuu ilieleweka kwamba idadi ya
Wazanzibari wote kwa jumla ilikuwa ndogo zaidi kushinda ile iliyohitajika katika vuno la
karafuu, kwa hivyo Zanzibar ilibidi kuagiza wafanyakazi wa majira kutoka Bara la Afrika
ya Mashariki na Kati, wengi wao kutoka Mrima/Tanganyika. Jambo lililowavutia majirani
59
hawakuja kufanya kazi Zanzibar ilikuwa ni utajiri Zanzibar uliyokuwa nao kwa wakati
huo, na kuweza kulipa mishahara mikubwa zaidi kuliko nchi jirani na wakati huo huo
watu hao walikua hawatozwi kodi ya kichwa Zanzibar tofauti na kule walikotoka. Kwa
mfano mishahara ya vibarua wa Zanzibar katika miaka 1930 nakuendelea ilikuwa ni sh.
30/ kwa mwezi, wakati mishahara ya kibarua au skwatawa Kenya haukufikia hata sh. 15/
seuze ile ya Tanganyika ambayo ilikuwa chini zaidi. Mishahara ikaendelea kupanda hadi
1948 wakati kibarua akipata sh. 3/30 kwa siku. Kutokana na kuagiza vibarua kutoka
nchi za jirani idadi ya wakaaazi wa Zanzibar ilikuwa kama ifuatavyo: Kutokea mwaka
1923 hadi 1931 wafanyakazi wote waliyoingia Zanzibar walikuwa 21,852 na waliyoondoka
katika muda huo huo 14,055, katika miaka ya 1927 na 1928 jeduweli za wahamiaji
hazikuchapishwa. Baada ya hapo inakisiwa kwamba kiasi chawatu 2000 waliingia Zanzibar
kwa mwaka, wengine wengi waliingia kwa magendo bila ya kujulikana na kuhisabiwa.
Sensa zifuatazo zinaonyesha idadi ya wabara waliyokuwa Zanzibar. Katika mwaka 1924
kulikuwa na Wabara 64,828 Wazanzibari wenyewe wakiwa 119,360 (yaani Wabara kuwa
z aidi ya thuluthi moja ya wakaazi wa Zanzibar ) sensa ya mwaka 1931 ilionyesha idadi
ya kiasi cha Wabara 74,492 wakati sensa ya mwaka 1948 ilionyesha Wabara waliyoishi
Unguja na Pemba kuwa watu 51,227 wakatiWazanzibari wenyewe wakiwa 148,480 yaani
zaidi ya robo ya wakaazi wote kwa jumla na zaidi ya thuluthi moja ya Wazanzibari wote.
Baada ya mgomo wa Wafanya kazi wa 1948 wahamiaji kutoka Bara hawakuwa wakija
kwa wingi hasa kwa vile hata mishahara ilikuwa imepunguwa.
60
3.13 Mgomo wa 1948
Mgomo huo uliyotajwa hapo juu wa agosti-septemba 1948 ulikuwa ni wa wafanya kazi wa
chini kabisa hasa wale wa bandarini, makuli, wachukuzi, vibarua, wafanyakazi wa P.W.D,
hospitali na kadhalika. Kwa vile Zanzibar ikiagiza vibarua kutoka mabara, mgomo huu
ulikuwa umefanywa zaidi na Wabara kwani wao ndio waliyokuwa sehemu kubwa kabisa
ya tabaka hilo. Mgomo huo ulishajiishwa zaidi na mgomo wa Mombasa wa 1939 na
wa Dar es salaam wa 1947. Kutokana na mgomo huo ukakamavu na msimamo imara
wa wafanyakazi ukajichomoza na hatimae wengi wao walipokosa au kuachishwa kazi,
wakaingizwa katika tabaka jipya, na kupata sura mpya ya kilumpa, maprolitari wasokuwa
na kazi. Wagomaji hao, ingawaje walipokuwa wakigoma, waliungwa mkono na jamii
nzima ya Kizanzibari katika madai yao halali na kupata misaada tofauti na hata mashamba,
waliwaletea vyakula, na watu wengine wa jamii kama vile Watumbatu kukataa kuvunja
mgomo huo kwa kufanya kazi baadala ya wagomaji hao, na akina mama wa Kizanzibari
kuwapikia vyakula wagomaji hao.
Malumpa hawa wakiwa wengi wao ni Wabara, kutokana na mgomo huu wakaanzisha
kikundi kilichokuwa na upungufu wa mfumo,upungufu wa siasa, sera au mipango maalum,
lakini watu hawa walikuwa ni watu wenye maslahi ya aina moja na waliyokuwa hawana
uongozi madhubuti. Lengo lao kubwa lilikuwa si la kitaifa bali la kuongezewa mshahara
tu, bila ya kuwa na mfumo wa kisiasa ya kitaifa. Baadae vyama vya wafanyakazi
vilipoanzishwa watu hawa wakawa katika mstari wa mbele na washabiki wakubwa. Kutokana
na hali ya tabaka lao la hali ya kuonewa kwa kunyonywa na kudhulumiwa, walipata
maarifa na elimu fulani ya kisiasa kutoka katika mgomo huo. Na kama desturi, malumpa
ni watu waliyokuwa tayari kuchukuwa khatuwa za kimapinduzi wakati wowote, ingawaje
61
wakipata uongozi mbaya matokeo yake huwani balaa kubwa mno.
62
Chapter 4
MAPINDUZI
4.1 Siri ya Mapinduzi ya 1964
Kama ilivyokaririwa hapo juu njama za serikali ya ZNP ya kuwakamata viongozi waupinzani
iliharakisha na kusisimua haja ya kufanya mapinduzi kwa haraka, hata kabla matayarisho
ya mapinduzi hayo kuwiva vizuri. Vile vile ile hali ya kwamba ASP ilipata
idadi ya voti nyingi zaidi kupita ZNP na ZPPP kwa jumla, iliwafanya ASP kuingiwa na
uchungu mkubwa na kwa hivyo wakaamuwa kulipiza kisasi kwa kufanya ghasia kama zile
za mwezi wa juni 1961. Lakini mwaka huo, wa 1964, walikusudia kuchoma moto sehemu
zote za mjini, yaani stone town, pamoja na vituo vya kuuzia mafuta ya petroli. Wapangaji
halisi wa mpango huo hawakuwa Afro-shirazi yenyewe bali ilikuwa Afro Shirazi Youth
League, wale waliyokuwa wanachama wa Chama cha Haki za Binaadam na askari polisi
wa bara waliyofukuzwa kazi na serkali ya Hizbu pamoja na baadhi ya wafuasi wa Bahai.
Mipango yao waliiweka siri sana hata karibu wote viongozi wa juu kabisa wa ASP walifichwa
nakutokujulishwa kiini cha mipango yenyewe mpaka dakika za mwisho. Kwani
wakati huo uongozi wa ASP ulikuwa umeparaganyika na mchuano mkubwa wa kudai
nakupigania uongozi ulifukuta chini kwa chini. Baadhi ya viongozi wa ASP walijihisi
wao wakiwa ni Wazanzibari halisi walikuwa na haki zaidi ya uongozi kuliko wale wenye
asili ya Kibara ambao vile vile walikuwa hawana elimu. Migongano mikali ilitokana
baina ya Wazanzibari kutaka uongozi. Othman Sharif, Hasnu Makame, Saleh Sadalla
na Idris Abdul Wakil iliwabidi wajiuzulu tarehe 2 januari, 1964 na kutoka katika ASP.
63
Katika mvutano huo kwenye dakika za mwisho kabla ya Mapinduzi, tarehe 10, 11 januari,
Othman Sharif kwa siri kabisa alimuendea Waziri Mkuu Mohammed Shamte na kumpendekezea
waunde serikali ya pamoja ya ASP na ZPPP. Wakati huo Othman Sharif alikuwa
amekwishapata fununu za Mapinduzi ambayo alikuwa hayataki kwa sababu yalikuwa si
ya ASP wala ya Wazanzibari khalisi. Shamte akawakatalia viongozi hao na kuwambia
kama walitaka kushiriki serikalini basi iliwabidi watoke katika ASP na waunganishe viti
vyao vya Bunge kwenye ZPPP, kina Othman Sharif wakashindwa na masharti hayo. Migogoro
hii jinsi ilivyokuwa ya hali ya juu, hata jina la Abdulla Kassim Hanga hatimae
lilionekana kukuwemo katika ile listi ya John Okello ya wale Viongozi waliyotakiwa na
ASYL kuuwawa mara baada ya Mapinduzi. Kwa hivyo kuuliwa kwa kina Hanga na ASYL
baadae sijambo la kustaajabisha. Ushahidi wa kupindukia ulionyesha kwamba Mapinduzi
ya 1964 hayakupangwa, kutayarishwa, kuandaliwa au kuongozwa na ASP. Na inaonyesha
wazi kwamba viongozi waliyotajwa hapo juu, waliyopendekeza kuu ngana kwa ASP na
ZPPP, yaani kina Othman Sharif, walifanya hivyo kutokana na upinzani wao wa kukataa
kuendeshwa na Wabara na hiyo ndio sababu wakawa wamekwisha hukumiwa kuuwawa
hata kabla ya ghasia hizo kufanyika. Wale waliyoanza suala la kutaka kuleta ghasia, kuchoma
moto, kuuwa na kuleta fujo kwa jumla walikuwa ni Afro shirazi Youth league na
kiini kilikuwa ni Kamati yawatu 14 yaani:
Committee of “14”
John Okello*
Abdulla Mfarinyaki*
Seif Bakari*
Abdulla Said Natepe*
Yusuf Himid
64
Ramadhan Haji
Hafidh Suleiman
Khamis Darwesh*
Pili Khamis
Said Bavuai
Said wa Shoto*
Mohammed Abdulla*
Hamid Ameir
Khamis Hemedi
Wageni wengine ambao walishiriki mstari wa mbele wa viongozi katika Mapinduzi
walikuwa ni Absolom Amoi Ingen, Matias Simba, Mzee Kenyatta n.k.
Nusu ya wanakamati ya “Committee of 14” hao wakiwa wasio na uzalia wa Kizanzibari
yaani hao wenye alama ya *. Itaonekana kwamba viongozi wanne wa- juu kabisa
hawakuwa ni Wazanzibari na hata Karume alikuwa hayumo katika Kamati hiyo ya watu
14. Karume alitiwa katika kamati hiyo baada ya Mapinduzi na baada ya kuondoshwa kwa
Okello na kushika pahala pa Okello. Katika mipango yao ASYL waliandaa Fete usiku
wa tarehe 11 kuamkia tarehe 12 januari 1964. Kama ilivyotajwa hapo juu ASYL haikupanga
kufanya Mapinduzi bali ilikuwa imepanga kufanya ghasia, fujo na kuchoma moto
mjini, Stone Town. Kutokana na hali ya kisiasa ya wakati huo, vyama vyote vya upinzani
vilikuwa vimeungana katika United Front. Kutokana na hali hiyo kiongozi mmoja wa
Umoja wa Wafanyakazi wa FPTU ambaye vile vile alikuwa ni kiongozi wa Umma Party
akadokezewa kwamba kulitaka kufanywa hizo fujo, ghasia na uchomaji moto sehemu za
mjini na wale makomred wenye jamaa zao huko sehemu za mjini wawaondoshe. Kiongozi
65
huyo, Ahmed Badawi Qulatein, kutokana na muamko wake wa kinadharia na msimamo
wa kimaendeleo akawaonya na kuwashauri viongozi hao wa ASYL kutofanya kitendo
hicho, kwani kufanya hivyo kungelikuwa ni sawa na kuwauwa watu wasio na hatia yoyote,
ambao karibu wote wakiwa ni wafuasi tu. Kati ya wale ambao wangeliuwawa bure
wangelikuwemo watoto, wanawake na wazee, kwa ufupi kungelikuwa kuuwa wananchi
ambao hawana hatia yoyote. Zaidi ya hivyo kitendo kama hicho kingeliwafanya wananchi
wakauwana ovyo na hatimae wale ambao wangelizianza ghasia hizo wangelikamatwa
kufugwa na kuuwawa pamoja na uongozi wote wa upinzani bila ya kuweza kuleta mabadiliko
yoyote ya kimaendeelo. Ndipo Qullatein akawaasa kwamba kama wanataka kufanya
jambo la maana basi bora wangelifanya “MAPINDUZI” na hatimae wachukuwe serikali
na ndipo watapoweza kuleta mabadiliko katika jamii. Kwa njia hiyo kuuwawa kwa watu
bure bure kutaepukika na wakati huo huo serikali itapopatikana mfumo wa jamii ulio bora
ungeliweza kuzalishwa. Sababu hizo zikawatwanga viongozi hao wa ASYL hasa kwa
vile kulikuwa na uwezekano wa wao wenyewe kuuwawa katika ghasia hizo. Ingawaje,
wakati huo fununu za ghasia zilikuwa zimeshaifikia idara ya usalama wa serikali ya Hizbu,
Karume mwenyewe akiwa mtoaji siri mmoja wapo, kwani alimuendea Ofisa mmoja wa
Polisi wa Kiingereza, na kumwambia kwamba amesikia fununu kwamba kulitaka kufanywa
ghasia, baina ya tarehe 11 12 Januari, lakini yeye alijikosha kutoka na ghasia
hizo kwani alisema kwamba alikuwa hayumo katika mipango hi yo. Kamishna wa polisi
akazidharau khabari hizo. Hasa kwa vile serikali ya Hizbu na Polisi wakishughulishwa
na kuwaandama Wana Umma, kuwadharau ASYL, na kutoona harakati zozote za Wana
Umma, habari hizo wakazidi kuzidharau. Ingawaje mchana kutwa wa tarehe 11 januari
1964, hadi masaa ya usiku kuliwekwa vizinga njia na askari wa PMF kuranda kutwa.
Tarehe 11 hiyo magariya PMF (Police Mobile Force) yakiwa yamejaa maaskari yalikuwa
66
yakiranda mchana kutwa sehemu zote za mjini silaha zao walizopewa zikiwa marungu
matupu. Usiku ulipoingia askari wa vikosi hivyo vilipoona Umma Party wameingia kulala
bila yaishara ya harakati zozote na hao askari wa polisi na wa PMF wakadharau habari hizo
na kwenda kulala Mtoni, ambako mara mbili pamema usiku huo kulipigwa matarumbeta
ya hadhari. Wale polisi wa Ziwani nao wakajiendea kulala, wakuu wao wa polisi na wa
PMF kuchukuwa nyum bani funguo za ghala za silaha. Kosa mojawapo kubwa serikali
ya Hizbu ililolifanya ilikuwa kuwafukuza na kuwapa notice ya kuwaachisha kazi polisi
waliyokuwa wana asili ya Kibara, baadala yakuwapa watu hao uraiya na kutukuza ujuzi
na uwezo wao. Baada ya- kuwawachisha kazi watu hao, serikali hiyo haikuwapa wote
wao nauli na kuwa-tayarishiya safariza kurudi makwao, kati yao hatimae, walisaidia katika
Mapinduzi kwa ujuzi waliyokuwa nao.
Saa sita za usiku wa tarehe 11 Januari, malumpa wa Youth League wakazishambulia kambi
ya polisi ya Ziwani na ya Mtoni wakiwa na mapanga, mishare, magongo, mawe, visu na
kadhalika. Baada ya kuiteka Mtoni, chini ya uongozi wa Ramadhan Haji, walinyakuwa
bunduki za aina ya rifle 200 , sub machineguns 25, Brengun nyepesi 2, bastola nyingi, magrenedi,
mabomu ya moshi na risasi. Wakati huo simu baina ya vituo vya polisi zilikatwa,
na mfano kituo cha polisi cha Malindi kilipojaribu kuwasiliana na kambi ya Ziwani na
Mtoni kilishindwa na hatimae kupeleka gari la polisi la 999 huko Mtoni kwenda kuchunguza.
Gari hilo lilipofika huko likakuta Mtoni imekwisha tekwa na askari hao ikabidi
wasalimishe roho zao kwa kukimbia na wengine kuogelea baharini kutoka Mtoni hadi
mjini.
Baada ya ushindi wa ghafla kikosi kutoka Ziwani chini ya Okello, wengi wakiwa na
mabunduki bila hata kujuwa namna ya kuyatumia wakaelekea Raha Leo ambako ndiko
kulikokuwa Makao Makuu. Baada ya hapo ndipo jina la John Okello likaanz kusikika
67
na vitisho vikaanza kuzagaa visiwani. Kwa kutumia Sauti ya Unguja,Okello aliwatia
terra sio wananchi tu kwa jumla, bali hata viongozi wote wa ASP hasa kwa vile walikuwa
hawamjui Okello ni nani. Okello alifanikiwa na kuwadanganya walalahoi wenzake
kwamba ati alishiriki katika vita vya Mau Mau, na hao kwa upungufu wa maarifa na
ujuzi wao kuhusu mapinduzi wakaamini nakumfuata kama vipofu. Sababu ya kutoroka
Okello kutoka sehemu mbali mbali za Uganda, Kenya na Pemba na Unguja, inasemekana
kwamba alikuwa jambazi, na ndio maana akawa na mwenendo wake wa kikatili. Wana
ASYL wakiwa wenyewe wakiongoza na kutekeleza maazimio yao bila ya kushirikisha
uongozi wa ASP waliteka Ziwani na Mtoni kwa usiku huo. Baadae huko Makao Makuu
Raha Leo ukakuweko uongozi uliyokuwa si wa ASYL. Bahati ni kwamba Aboud Jumbe,
Badawi Qullatein, Abdulaziz Twala, na Khamis Abdulla Ameir wakafika hapo na muongozo
wa kisiasa ukawa unatolewa, ingawa Jumbe kwa uwoga wake akajiweka chini ya
Okello. Ingawaje Jumbe alisaidia katika kupunguza upotovu fulani. Makomred wengine
wakashiriki katika ulinzi wa Makao Makuu, Raha Leo, wakiwemo Abdulla Juma, Salim
Saleh, Haji Othmani n.k. Hata kabla ya Mapinduzi kuanza Karume alikwisha penya na
kukimbilia Dar es salaam, kunusurisha roho yake, katika safari hiyo alimuomba Hanga
amshindikize. Babu kwa wakati huo alikuwa akiishi Dar es salaam tokea kukimbia
kukamatwa, kama ilivyotajwa huko nyuma. Wakiwa Dar es salaam, Nyerere hatimae
akawaita viongozi wote hao watatu, yaani Babu, Hanga na Karume na kuwashauri warudi
Zanzibar kwenda kuzuwia watu kuto uwana ovyo . Hapo ndipo Babu, Hanga na Karume
wakachukuwa boti la wayahudi Feinsilber na Abramovich tarehe 14 Januari 1964, kuelekea
Zanzibar na kushukia Fumba kwa madhumuni ya kuzuiya umwagaji wadamu. Ingawa sehemu
mbili muhimu za kiusalama zilikwisha tiwa mikononi, usiku wa baina ya tarehe
11 na 12 ya 1964, bado kulibaki sehemu fulani muhimu za kiusalama ambazo zilishinda
68
kuziteka. Kati ya sehemu hizo ilikuwa ni kituo cha polisi cha Malindi, ambacho Seif
Bakari alipewa wadhifa wa kukiteka lakini akashindwa na Gereza la Kiinua Miguu ambalo
lilikataa kusalim amri na sehemu hizo kupigana vikali na kusabababisha kuuwawa
kwa watu wengi sana waliyoshiriki katika kupindua . Hapo ndipo walipohitajika wenye
ujuzi na uwezo wa kupambana katika vita vya kimapinduzi mchana kumekucha kweupe,
kwani ASYL walipokwenda Ziwani na Mtoni walikuta askari wamelala na hawana silaha.
Lakini baada ya mchana kuingia vituo vyengine havikusalim amri bali vilikamata bunduki
na kupigana. Kituo cha polisi cha malindi kilikuwa na askari 70 waliokuwa na silaha
kamili na risasi zakutosha, chini ya uongozi wa Inspekta Salim Hakim Khasibi. Askari
hawa wakilindwa na makuta ya jumba hilo na kwa kutumilia urefu wa ghorofa, na kituo
hicho kuwa njia panda, waliweza kuteketeza watu wengi sana waliyojaribu kukaribia
na kutaka kukiteka kituo hicho. Wengi wa wale waliyokwenda kushambulia mwanzoni
walikuwa wamakonde ambao walikuwa mara ya kwanza kushika bunduki na walipewa
mafunzo ya kutumia silaha na makomred, wengine kati yao walijitwangana risasi wenyewe
kwa wenyewe walipo jaribu kumlenga adui. Wengine kama kina Seif Bakari walikamatwa
hapo na kuachiliwa na kugeuz wamjumbe wa kupeleka salamu kwa wakubwa zake, kutotambuwa
kwamba Seif alikuwa mmoja kati ya viongozi wa juu wa mapinduzi yenyewe.
Washambuliaji wengi sana walifariki hapo Malindi na wengine huko gereza la Kiinuwa
Miguu. Malumpa- walipoona mambo yanawazidi wakawaomba Makombred wa Umma
Party kwenda kuwasaidia kuviteka vituo vilivyobaki. Hapo ndipo kwa mara ya mwanzo
kwa Makomred walishiriki katika Mapinduzi kisilaha. Baada ya mashambulizi makali
yaliongozwa na komred Amour Doughesh, askari wa kituo cha Malindi wakakimbiana
gereza la Kiinuwa Miguu liliposikia makomred, wakiongozwa na Hemed Hilal walikuwa
wakijiandaa kuchukuwa dhamana ya utekaji wa ngome hiyo, gereza hilo likasalim amri.
69
Na baada ya hapo makada wa kikomred wakaendelea kuchukuwana kulinda vituo mbali
mbali kama kituo cha simu ya upepo. Kituo hicho kilichukuliwa chini ya uongozi wa
Hashil Seif na Kadiria Mnyeji. Aboud Jumbe akiwa ndiye aliyetowa amri ya kukiteka
kituo hicho. Ali Muhsin na Mawaziri wake, hatimae, walikwenda kwenye kituo hicho cha
simu ya upepo na kusalim amri kwa makomred, Kadiria Mnyeji na Hashil Seif, waliwapatia
usafiri na ulinzi wakupelekwa Raha Leo, kwa usalama na amani. Uwanja wa ndege na
kituo cha simu vilichukuliwa baaadae na makomred. Hizbu kabla ya mapinduzi, itakumbukwa
huko nyuma, kwamba ilikuwa imeshaanza kujitayarisha kutaka kukamata viongozi
wa upinzani na kujuwa kwamba vitendo hivyo vingekasirisha wafuasi wa viongozi hao.
Kwa hivyo Hizbu inasemekana ilikwisha jitayarisha na mapambano hayo kwa kugawa
silaha kwa wafuasi wake.Zaidi ya kugawa silaha waliwatayarisha baadhi ya wafuasi wao
washupavu katika mbinu mbali mbali za mapigano. Hizbu ilikuwa na wataalam fulani
waliyojifunza mbinu za kijeshi za kigorilla, wakiwa huko Misri na Dhofar. Kati ya askari
hao wasiri wa Hizbu walishiriki katika kujaribu kuikowa serikali ya hizbu isiangushwe siku
za Mapinduzi na walikuwa wakifanya mazinga ombo yao sehemu za Bubu, Bumbwini na
Kianga. Kati ya askari hao kuna waliyowahi kukamatwa mara tatu wakifanya operation
hizo siku zile za mapinduzi. Sehemu hizo zilizotajwa hapo juuzi liteketeza washambulizi
wengi mno hasa kwa vile Hizbu wa sehemu hizo walikuwa wametayarishwa vizuri na kuwa
na silaha madhubuti, kinyume na washambulizi waliokuwa na mapanga, magongo n.k. Ilibidi
vikosi kutoka mjini kwenda mashambani huko na kuwateka, baada ya kusalim amri
kwao. Serikali ya Hizbu iliwatomeza wafuasi wake waliyokuwa mashamba kutoa roho zao
kuhami serikali ya Hizbu, lakini wao viongozi wenyewe walisalim amri na kusalimisha
roho zao, kutoroka nchi na kusaliti, wakati wananchi wakiuwana wenyewe kwa wenyewe.
Katika mapinduzi watu wengi waliuwawa, na kutoka sehemu zote mbili, wengine wal-
70
iuwawa bure na wengine waliuwawa katika mapigano au kwa sababu walishiriki katika
mapigano. Kati ya wale waliyouliwa bure ni wa huko Bambi ambako makatili waliyokuwa
na msimamo wa kigozi waliwakamata wanawake, watoto kwa wazee, wakawatumbukiza
katika visima, kuwatilia makozi, makarare, na madufu, kuwaminia mafuta ya taa na
kuwatia moto, watu hao wakiunguwa hali watu wakiwa wazima wazima. Unyamana
ukatili huo hauitwi mapinduzi bali ni, ukafiri wa kikatili na wa kinyama kabisa,unaotokana
na chuki za kijinga walizotiwa na mwishowe kusahau kama hao waliowauwa ama walikuwa
ni ndugu zao, majirani zao au mara nyingine wema waona kuwa waislaam wenzao.
Baadala ya kuulani unyama waliyofanyiwa watu wa Bambi, Karume akawatunukia watu
hao kwa kuwajengea kati ya nyumba nzuri na bora kabisa baada ya mapinduzi. Mapinduzi
yasiyotayarishwa na wanamapinduzi washupavu wenye intidham na muamko wa
kisiasa uliyokomaa na wa hali ya juu lazima utakuwa na matokeo ya uovu wa kuvunja
sheria, kufanya mambo maovu na machafu. Kwa vile mapinduzi ya 1964 hayakupangwa
vilivyo, wahuni wengi na malumpa kadhaa walichukulia nafasi hiyo na kufanya mambo
maovu kama vile kuuwa ovyo, kuwaingilia wanawake na wanawari kwa nguvu, kuiba na
kuchukuwa ngawira, kuvunja na kupiga watuovyo. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuona
kwamba katika watu waliyoiba walikuwemo viongozi ambao hatimae wakawa mawaziri
na mabalozi, wengine sasa kuwa mawaziri wa serikali ya Muungano na kuna ushahidi
kwamba walishiriki kuiba dhahabu na mali nyingi za watu wa Pemba na zaidi ya hayo
kushirikiana na Okello kupiga viboko watu wazima wenye heshima zao. Wengi wa hawa
watu waliyoonewa walikuwa ni raiya wa kawaida wasiyokuwa na uongozi au uhasama
wowote. Bahati nzuri kulikuwa na Makomred ambao vile vile walisaidia kupunguza
uuwaji na ukashifishaji wa wanawake, wizi na maovu mengi mengineyo kwa sababu ya
elimu bora waliyopewa ya kisiasa. Kushiriki mwishoni katika Mapinduzi kwa makomred
71
kulipunguza balaa jingi kwa sehemu zote mbili za ASP na ZNP.
4.2 Haja ya Mfumo halali
Mfumo wa kijamii wa Zanzibar kwa wakati huo ulikuwa unahitaji mabadiliko makubwa,
kwani ulikuwa si mfumo wa kihalali wa kuwapa wananchi wote haki sawa. Ulikuwa ni
mfumo ambao uliwaweka wengi kwenye unyonge na umasikini wa kusononesha, ilhali
wakati huo huo wengine walikuwa wakiogelea katika utajiri. Kutokana na utajiri, ulwa na
ubwanyenye, wale watu wa matabaka ya juu walikuwa na kibri kikubwa na kuwadharau
wananchi wenzao, kuzidi kuwanyonya na kutumia utawala kulinda maslahi yao dhidi ya
haki ya waliyokuwa chini, na wakati huo huo kujidai kuwa ni waislaam wema. Kwa
hivyo Zanzibar kwa wakati huo palihitajika mabadiliko ya mfumo wa jamii na mabadiliko
yenyewe yaliyohitajika ni kuubadilisha mfumo uliyokuwepo wakati huo, kwa kutumia njia
ya kimapinduzi, kwa vile kulikuwa hakuna njia nyengine ya kuleta mabadiliko. Mapinduzi
yaliyo hitajika yalikuwa yale yaliyopangwa kwa makini na kuwa na wanamapinduzi
wenye siasa ya kimapinduzi makini, waliyopevuka kisiasa, wakiwa na sera za kuleta maendeleo
na waliyokuwa wakijuwa nini wakifanya. ASYL walikuwa ni watu wasiosoma na
kutowaamini wote waliyokuwa na elimu, kwa hivyo ndio maana hawakutaka kuwashirikisha
viongozi wa ASP waliyokuwa na elimu katika mipango ya Mapinduzi yao. Karume
mwenyewe alikuwa hakusoma, aliwaamini waliyokuwa hawana asili za Kizanzibari, na
kuwaogopa wana ASP waliyosoma, kwa hivyo alielemea zaidi kwa ASYL na ASYL
wakamuamini Karume kwa maslahi kwa sababu kama hizo. Youth League katika uongozi
wa ASP ikamuarifu Karume pekeyake baadhi ya siri kuhusu mipango yao, ingawa hata
naye hawaku mwambia siri zote. Hiyo ndiyo sababu mojawapo, wakati ghasia zilipokuwa
72
zikipangwa wiki mbili kabla ya Mapinduzi, viongozi fulani wa ASP wakajiuzulu kutoka
kwenye ASP tarehe 2 Januari, 1964, na hiyo ndio- sababu moja wapo mnamo tarehe 10, 11
Januari1964, viongozi fulani wa ASP, katika dakika za mwisho, wakamuendea Mohammed
Shamte kwa madhumuni ya kuunda serikali pamoja ili kuepuka Mapinduzi. Aboud Jumbe
alifanya kazi kubwa ya kuwaunganisha viongozi wa ASP na kuwahakikishia kwamba wao
ndio watakaondesha hiyo serikali baada ya mapinduzi kwani ASYL walikuwa hawana
uwezo huo. Kina Othman Sharif wakakubali hatimae kushiriki katika serikali hiyo, bila
ya kujuwa hatari gani iliyowangoja huko mbele. Kuambatana na orodha ya Gazeti Kuu
la Serikali la tarehe 24 januari, 1964 orodha ya Baraza la Memba wa Mapinduzi ni kama
ifuatavyo:
1. Rais Abeid Karume
2. Makamo wa Rais Abdulla Kasim Hanga **
3. Mhe. Abdulrahman Mohammed Babu*
4. Mhe. Hasnu Makame*
5. Mhe. Aboud Jumbe
6. Mhe. Saleh Sadalla**
7. Mhe. Idris Abdul Wakil*
8. Mhe. Othman Shariff**
9. Mhe. Abdul Aziz Twala**
10. Mhe. Hassan Nassor Moyo
11. Kamishna wa Polisi – Edington Kisassi
12. Field Marshal John Okello
13. Mhe. Yusuf Himid
14. Mhe. Seif Bakari
73
15. Mhe. Ramadhan Haji
16. Mhe. A.S. Natepe
17. Mhe. Pili Khamis
18. Mhe. Khamis Hemedi
19. Mhe. Hamid Ameir Ali
20. Mhe. Said Iddi Bavuai
21. Mhe. Siad wa Shoto
22. Mhe. Mohammed Abdulla
23. Mhe. Abdulla Mfarinyaki
24. Mhe. Hafidh Suleiman
25. Mhe. Khamis Darwesh
26. Mhe. Khamis Abdulla Ameir
27. Mhe. Muhammed Mfaume Omar
28. Mhe. Muhsin bin Ali
29. Mhe. Muhammed Juma
30. Mhe. Daud Mahmoud
Viongozi halisi wa ASP wenye alama za ** wameuliwa na wengine wenye alama za
* kuhamishwa nchi kama itavyokaririwa wakati suala la Muungano litapojadiliwa katika
kurasa za mbele. Kwa siku za mwanzo mara tu baada ya Mapinduzi, Karume pamoja na
Viongozi wengi wa ASYL, kutokana na hamasa za Mapinduzi, walionyesha kuwa ni watu
wenye fikra za kimaendeleo, baadae kwa sababu za njama za kuunda Muungano viongozi
hao wakatiwa fitina na chuki, na kutekwa akili na Nyerere. Katika majadiliano ya siri ya
Muungano ilionekana kwamba ikiwa Umma Party pamoja na viongozi waloendelea katika
74
ASP watashiriki katika serikali ya Mapinduzi kikamilifu, basi Muungano wa Nyerere wa
aina hii ya leo wa kututawalia usingewezekana. Na kwa kuwaondosha Umma Party na
viongozi hao wa juu kabisa wa ASP njiani Muungano ukawezekana kundwa haraka haraka,
kama- itakavyakaririwa huko mbele.
4.3 Mapinduzi yalitekwa nyara
Madhumuni ya mapinduzi ilikuwa ni kuleta usawa baina ya Wazanzibari, kuondosha
dhulma, mapendeleo, ubaguzi, umasini, kuoneyana, kuleta usawa, haki, elimu bora, siha
bora, uchumi bora, sheria halali, heshma ya kila Mzanzibari n.k. Mara tu baada ya mapi
duzi kulichomoza ishara mbaya dhidi ya matumaini hayo. Kati ya ishara hizo ilikuwa ni
uvunjaji sheria kwa baadhi ya viongozi na kuchukuwa sheria mikononi mwao. Sababu
moja wapo ya kufanya mapinduzi na kuondosha serikali ya Hizbu ilikuwa, Hizbu ilipitisha
sheria zilizo kuwa dhidi ya demokrasia, za kunyima haki huru ya mtu, ya kuunda
na kujiunga na chama atakacho mwenyewe, kama vile kufungia chama cha siasa, kama
vile kupiga marufuku chama cha Umma Party. Kwa hivyo kunyima haki ya chama cha
upinzani, kunyima haki za kuchapisha khabari/fikra huru au mtu kusoma na kuandika fikra
huru na azitakazo, kama vile kufungia ZANEWS na Sauti ya Umma, kuzuiliya haki za
kusafiri huru kwa watu wenye fikra tafauti na mengineyo, haikuwa mwendo halali na wa
kidemokrasia. Hatua hizo za serikali ya Hizbu zilikuwa ni ishara za mwanzo za udikteta,
udikteta ambao leo tunaupiga vita.
Kwa mshangao mkubwa, mara tu baada ya Mapinduzi, ikaonekana kwamba na ile serikali
ya Mapinduzi nayo ilikuwa na njama za kuto heshimu misingi ya demokrasia. Serikali hiyo
75
baada tu ya kushika khatamu, ilianza kwa ishara mbaya, kama vile kuwahukumu vifo viongozi
wa serikali iliyopita, adhabu ambayo haifanani na makosa yao na wala wakuwa peleka
mahakamani. Kama isingeli kuwa kutetewa kwa vikali sana na A. M. Babu katika Baraza
la Mapinduzi basi viongozi hao wa Hizbu leo wangelikuwa marehemu, kwani walikwisha
hukumiwa hukumu za vifo. Walipoponea hukumu za kifo ikaamuliwa viongozi hao watiwe
vizuizini, na wakawekwa ndani bila ya kupandishwa Mahkamani, hadi miaka 10, baada ya
vyama vyao kufungiwa. Ingelikuwa jambo la busara kama serikali ya mapinduzi ingeliwapeleka
watu hao Mahkamani, na kupata adhabu kuambatana na makosa yao wakipewa
fursa ya utetezi. Kufutwa kwa vile vyama vilivyokuwa vya serikali iliyopita pamoja na
kufutwa tena kwa chama cha Umma Party chini ya serikali ya Mapinduzi kilikuwa si
kitendo cha kimaendeleo; lingekuwa jambo la maana zaidi pindi serikali ya Mapinduzi
ingeliruhusu vyama vya upinzani. Na inakisiwa kwamba kama vyama hivyo vingeliendelea
kuweko, kwanza ingelikuwa mfano mwema wakuheshimu haki za kibinaadam na
za kidemokrasia na hapana shaka sheria halali zingeheshimiwa, na vifo vya akina Hanga,
Othman Sharif, Salum Jinja, Mohammed Humud, Saghir, Ali Othman, Mdungi Ussi,
Khamis Masoud, Abdulaziz Twala, Mikidad, Humud, Ahmada, Chwaya, Shindano, Said
Nassor na wengi wengineo, vingeepukika pindi watu hao wangelipandishwa Mahkamani
na Wazanzibari leo wangeliujuwa ukweli wa dhahiri. Hali hiyo ingeliendeleza uzoefu
wa kidemokrasia wa watu kushambuliana majukwaani na katika vikao maaluum na kuwa
ndugu wanao sikilizana na kushirikiana kujenga taifa kwa pamoja katika maisha ya desturi,
bilaya kujali nani ana fikra gani.
76
4.4 Afro-shirazi
Kama ilivyokaririwa huko nyuma, vyama vyote vya zamani vya Zanzibar vilikuwana
migongano ndani ya vyama vyao, Hizbu ilikuwa na kundi la Babu na la Ali Muhsin, ZPPP
kuwa na kundi la Mohammed Shamte na Ali Sharif, Umma Party kuwana kundi la Haki na
la Wasaliti wakati ASP kulikuwa na kundi la wale waliyoendelea ambalo limeteketezwa,
kundi la waliyopigania ukubwa, kundi la waliyokuwa na asiliya Kizanzibari na kundi la
waliyokuwa na asili ya Bara. Kundi hili la mwisholilikuwa limetia mizizi katika ASYL
chama ambacho ndicho hasa kilichopanga nakuyatekeleza Mapinduzi na ndio maana matokeo
ya Mapinduzi yakenda kamayalivyo kwenda. ASP kwa hivyo ikameguka meguka
na hatimae kusababisha uuwaji wa kikatili wa viongozi wa ASP uliyopitishwa na ASYL.
Kwa vile viongozi wakuu karibu wote wa ASP waliuwawa na wale waliyobakishwa zaidi
ya Karume na Thabit Kombo, walikuwa ni viongozi wazee au wa chini kama kina Sh.
Daud Mahmoud, Ibrahim Sadalla, Ali Shariff ambao walikuwa ni kama watu waliyotekwa
nyara, kwa vile ndugu zao walikuwa wameshauwawa na kwa hivyo wao kuogopea roho zao
pindi wangeliteleza. Saa zote walikaa na wasiwasi kama mtu aliyewekewa kisu cha roho.
ASP/ASYL iliwadanganya wafuasi wao, kwamba ukabila na utumwa ndizo sababu ya
maafa yao yote, lakini viongozi hao hao walivyopata khatamu za utawala baadaya Mapinduzi,
walisahau madai hayo na kuwatia wananchi wote kwa jumla, pamoja na wanachama
wa ASP, katika maafa makubwa ya kimaisha. Pindi viongozi hao wa ASYL(ASP) wangelichukuwa
msimamo wa kijananchi wa kufanya mazungumzo yamasikilizano baina ya
wananchi mapema, badala ya kuendeleza siasa ya kikatili, ya chuki na ya kipinga maendeleo,
uhasama ugelikuwa ndoto. Kwa njia kama hiyo maovu mengi tungeliyaepuka
kutokana na makosa hayo na wapenda maendeleo wasingeliuwawa bure na nchi yetu leo
77
ingelikuwa imeendelea kiwango bora zaidi.
4.5 Aboud Jumbe
Ndani ya chama cha ASP na hatimae ASYL, kulitokea maafa mengi, kama vile kuteketeza
viongozi wa chama hicho na chama chenyewe tu, bali hata kuwapatisha taabu wafuasi
wa kawaida wa chama hicho bila ya kiasi. Wafuasi wa ASP wengi walivunjika moyo
sana kuona chama chao wenyewe kikiwatesa. Wafuasi hao vile vile walishangazwa sana
kwa kutoshirikishwa katika ujenzi wa nchi yao, katika uongozi wa chama na serikali yao,
kutojulishwa au kushauriwa katika jambo lolote lilohusu chama au serikali yao. Wana-
ASP na Wazanzibari wote kwa jumla wana haki yakujuwa nini kilichotendeka katika
nchi yao. Wazanzibari wanastahili ukweli kutoka kwa kiongozi mkweli kuhusu mambo
mengi ambayo yaliwakuta Wazanzibari. Jumbe kwa vile alikuwa msomi na asiyekuwa
kati ya viongozi wa ASYL iliwashangaza wengi kuweza kuepuka haku uwawa kinyume
na viongozi wengine wa ASP, kuna fikra tatu kuhusu jambo hilo; moja ni kwamba Jumbe
alikuwa myenyekevu sana kwa Karume ambae akitumia manufaa ya kisomo cha Jumbe.
Vile vile wakati Hassan Nassor Moyo na Diria walivyowauza kina Hanga kwa Karume
walimtaja Jumbe kwamba alihudhiria mikutano hiyo. Karume alipomuuliza Jumbe kwa
nini haku ripoti, Jumbe akasema aliliona jambo hilo ni la upuuzi ndio maana haku liripoti
kwa Karume. Tafsiri ya tatu inasemekana kwamba Jumbe hakuuwawa kwa sababu yeye
kinyume na viongozi wa juu waliyouwawa alikuwa kazaliwa Bara. Pana haja muhimu
sana kwa mtu kama Jumbe kujitokeza na kuandika historia ya ukweli ya ASP na serkali ya
mapinduzi kama anavyoikumbuka yeye, kabla wauwaji hawajamteketeza. Jumbe alishiriki
katika mitihani mbali mbali, kuiona na kuwezakupitia mitihani tofauti, kuishuhudia mi-
78
gogoro ya ndani ya ASP. Jumbe akiwa ni msomi, lakini wakati huo huo aliyezaliwa Bara,
kuwa na marafiki na wahisani wasio maafro kama kina marehemu Maalim Zubeir, ni mtu
aliyeziona nyuso zote mbili zasarafu. Jumbe anasemekana alipinga msingi wa ghasia za
uchaguzi mwaka 1961. Kabla ya uhuru alikuwa na sifa za uongozi wa kitaifa, kushiriki
katika mijadala hadhara ya kisiasa na kijamii akichuana na watu waliyokuwa na siasa
tofauti na zake. Kama vile majadiliano ya hadhara na A.M.Babu. Jumbe tokea mapema
januri 12, 1964 alikuwa pamoja na Umma Party na kuweza kujuwa mchango wao katika
mapinduzi. Anajuwa kuhusu vifo vya kina Hanga .Alikuwa kalamu na tupa ya Karume.
Baada ya kuuwawa Karume, Jumbe ndiye aliyechukuwa jukumu la kutangaza kifo cha
Karume katika radio na kujuwa vilivyo hali ya Viongozi wenzake wakati huo. Baada ya
kifo hicho alipambana na kuwa na migogoro mingi na Seif Bakari katika kuwaniya kanda
za khatamu za utawala. Jumbe ndiye aliyejaribu kuifufuwa ASP kwa kuitisha Kongres ya
mwanzo baada yamapinduzi huko Pemba, lakini jaribio hilo kutofaulu, kwani khatamu za
chama zikashikwa na wale wale ASYL. Hatimae Jumbe alifanikiwa kwa kiwango fulani
kuwapunguzia Wazanzibari maafa kwa kupunguza nguvu za Baraza la Mapinduzi kwa
kuwa sambaza sambaza na kuwaleta vijana wepya serikalini, vijana ambao wengine wao
walikuwa wana YASU na wengine kutokuwa wanasiasa hapo kabla, hatimae vijana hao
walikuwa ndio shina la utawala wa Jumbe. Jumbe alifanikiwa kwa kiwango fulani kuwarejeshea
watu haki zao za kuweza kutoa maoni. Kosa kubwa mojawapo alilolifanya Jumbe
lilikuwa ni kufuta Chama cha kisiasa Zanzibar na kuifanya Zanzibar izidi kumezwa, alifanya
hivyo kwa kutarajia kupewa Urais wa Tanzania, hatimae. Kutokana na kuzidi
kujitambulisha na dini ya kiislaam na kutambuwa mbinu za Nyerere za kutaka kuifanya
Zanzibar jimbo, Jumbe, alitanabahi na kuzindukana, na kuchukuwa khatuwa za kuitoa
Zanzibar katika Muungano na kwa hivyo akaporopolewa na Nyerere. Haya ni baadhi tu
79
ya mambo ulimwengu unayoyangoja kutoka katika kauli ya kweli ya Jumbe. Historia ya
Zanzibar haitokamilika bila ya Jumbe kuichangia kwa ukweli anaoujuwa.
4.6 Makosa ya Umma Party
Chama chochote cha kisiasa hakina budi na kufanya makosa ya kisiasa, mara nyengine
makosa hayo huwa madogo na mara nyingine huwa makubwa mno. Makosa kama hayo
yalifanywa na vyama vyote pamoja na Umma Party na hatimae kusababisha athara kubwa
visiwani Unguja na Pemba. Moja katika makosa ya Umma ilikuwa kujiweka nyuma na
kuonyesha kwamba wao ni watu wenye roho safi na wasiopapatikia khatamu za utawala,
kusahau kwamba wao wakiwa hawatakuwa na uroho wa utawala, kutakuwa na wengine
wengi ambao hawatopapatikia utawala tu bali watautumilia dhidi ya maslahi ya umma.
Kuogopa kwa Umma Party kushika khatamu za utawala kulitokana na uwoga wa kuhutumiwa
kwamba walikuwa na njaa ya utawala, na kwamba badala ya kupigania wanyonge,
lile walilolitaka lilikuwa ni ulwa wa kuwatawalia wengine. Mawasiliano mazuri ya Umma
Party na baadhi ya viongozi wa ASP pamoja na vyama vilivyoshirikiana na ASP iliwafanya
Umma Party kuwa na imani kwamba ASP badaya kupata khatamu za utawala
itatawala kihalali na kupitisha haki. Umma Party ilisahau kwamba si viongozi wote wa
ASP waliyokuwa na ujuzi au nia safi, na kwamba wengine walishughulishwa zaidi na
maslahi yao binafsi. Umma Party haikutarajia kwamba viongozi wa ASP Youth League
watawageukia wengi wa viongozi wa ASP, viongozi ambao walikuwa na fikra za maendeleo.
Umma Party vile vile, katika jazba na hamasa za kimapinduzi ilisahau kwamba,
viongozi wa ASYL ingawa walijitolea kufanya mapinduzi, walikuwa kwanza ni watu
80
wasiyoelewa mambo ya kiserikali na kwa hivyo ilikuwa ni rahisi kubabaika na kulevywa
na khatamu za utawala. Umma ilisahau kwamba hawa watu walikuwa wanaupungufu wa
ujuzi wa kuendesha serikali. Badala ya kwamba Umma ilikuwa iwahakikishie viongozi
hawa wa ASYL kipato na satwa ya kudumu kwa mchango wao katika mapinduzi, waliwawachia
kuendesha serikali kama rikwama, wakitarajia kwamba yale mapendekezo ya
kimaendeleo waliyoyatowaUmma Party yatatumika katika kuendeleza nchi. Viongozi wa
chache wa Umma Party, waliyokuwa na sifa za ubinafsi, walisaliti na kujichukulia jukumu
la kuzidi kuwapeleka mbele baadhi ya viongozi wa ASYL, wakijuwa wazi kwamba watu
hawa walikuwa hawawezi kuziendesha nyadhifa hizo kama ilivyotakiwa. Badala yake
viongozi hao waASYL kutokana na upungufu wa ujuzi wao wakawa wana wahka na kuona
adui katika kila pembe, na badala ya kuinuwa maslahi ya wanyonge wakazidi kuwakandamiza
wanyonge hao hao ambao walidai kuwatetea. Pindi Umma Party ingelihakikisha
udhibiti mshupavu wa khatamu za utawala katika mikono halali na madhubuti, basi nchi
ingeliendelea kwa haraka na kwa amani. Um- ma wa Kizanzibari usingeliteseka, mauwaji
yangeliepukwa, vifungo na kutiwa watu vizuizini kwa miaka hadi kumi kungeliepukika.
Utawala wa mashirikiano ya Umma na viongozi wa ASYL na viongozi waliyoendelea wa
ASP ungeweza kuondosha uhasama na chuki za kisiasa na hatimae kuleta masikilizano hata
na ZNP na ZPPP, pindi ASYL wangeliwahiwa kupewa elimu ya siasa ya mapema na ya
kutosha. Wazanzibari wangeliweza kuwa kitu kimoja na pasingekuwa na haja ya Karume
kuwa na wasi wasi na kujiingiza katika Muungano bila ya kupenda. Khatuwa za kurekibisha
dira ya muelekeo wa nchi zingelifaa kutendeka mapema, yaani muda tu baada ya
mapinduzi au hata kabla ya ufanyajiwa mapinduzi yenyewe na hatimae kungeliepusha nchi
leo kutawaliwa na kuselelea nyuma. Ingawaje, wakati tu baada ya Mapinduzi palikuwa na
migogoro na mifarakano fulani hasa kwa vile baadhi ya watu, kwa jina la Mapinduzi, wal-
81
ifanya kila aina ya uovu. Haya mambo hayakuwafurahisha wana Umma, na ikafika hadi
baadhi ya wana Umma fulani waka mkabil John Okello na kumwambia awache kuadhibu
raiya wasiyokuwana makosa. Wakamueleza Okello kwamba akishindwa na kuzuwiya
vitisho nakufanya ukatili huo basi ingelimbidi akabiliane na wana Umma kisilaha ana kwa
ana. Okello wakati huo alikuwa akitakabar sana na nchi ilikuwa kama ikiendeshwa na
Marais wawili, upande mmoja Karume na wa pili Okello. Wakati huo viongozi wengi,
akiwemo na Karume, wakimuogopa sana Okello. Okello inasemekana mara kwa mara
akisafiri kwenda Kenya na Uganda kupeleka mali ya ngawira. Safari moja, mwanzoni
mwa march 1964, Okello aliporudi kutoka Dar es salaam, akalikuta Baraza la Mapinduzi
likimsubiri uwanja wa ndege kwa madhumuni ya kumfukuza nchi. Okello, wakati huo,
alikuwa akiogopwa sana kwa hivyo ilibidi waagizwe Makada wa Umma Party wakiwa na
silaha kamili. Baada ya Okello kusomewa madhambi yake na Karume, mbele ya memba
wa Baraza la Mapinduzi, huko uwanjawa ndege. Makada wa Umma Party waliyokakamaa
na silaha mkononi wakamshindikiza Okello hadi ndani ya ndege iliyokuwa ikimsubiri na
kumsafirisha kwendea Dar es Salaam na hatimae kurejeshwa kwao Uganda.
Absolom Ingen,aliyekuwa makamu wa Field Marshal Okello na kuwa kati ya waliyoogopwa
sana na waliyofanya fujo nyingi, utesaji mkubwa na kashfa nyingi baada ya
Mapinduzi nae alipotaka kuoondoshwa alitiwa mbaroni na makada wa Umma silaha
mkononi na baadae akarejeshwa kwao Kenya. Kama makada wa Umma tokea mwanzoni
wangelipewa nyadhifa kama hizo basi wale watesaji na wauwaji wasingelipata nafasi
hizo na nchi isingelikwenda mramba. Watu wawili hao, yaani Okello na Ingen, ni kwa
wakati huo viongozi wa juu kabisa katika mapinduzi, na ambao wakiogopwa Zanzibar
nzima, lakini ilipohitajika makada wa Umma Party waliwatia mbaroni kama mchezo wa
mdako. Hayo ni makosa ya Umma Party ambayo yanafaa kujadiliwa ili yaepukwe siku za
82
mbele.
83
Chapter 5
MUUNGANO
5.1 Umma Party na Muungano
Muda fulani baada ya Mapinduzi, fununu zilianza kuhusu kuundwa kwa Muungano , kwa
wakati huo Memba wengi wa Baraza la Mapinduzi hawakujua hatari ya Muungano, hata
Karume alo uunda Muungano pamoja na Nyerere, hakuelewa uzito wa khatuwa kama
hiyo. Umma Party mara tu kusikia fununu hizo za Muungano ikaanza kuupinga, na
ilikuwa kwa sababu ilitanabahi kwamba Zanzibar ingelipoteza uhuru wake pindi khatua
hiyo ingelitekelezwa. Umma Party ilitambua umuhimu wakuwa na umoja baina ya nchi
za Kiafrika, lakini umoja huo haukuwa lazima uwe wa Muungano wa nchi mbili huru.
Wakati huo kiongozi wa Umma Party, Babu, alikuwa safarini Indonesia, kungojewa amekwisha
ondoka na kutoshauriwa kwa makusudi, kuhusu uundaji wa Muungano huo. Huku
nyuma makada walivyo kuwa wakipinga Muungano, tarehe 23, mwezi wa marchi 1964,
wakaitwa Ikulu, Zanzibar na huko Karume akawaambiya kwamba kama hawakuwacha
upinzani wao wa Muungano, basi wangeliletewaWamakonde kufyeka fyeka na kuwapiga
mishare na Wamakonde hao. Karume alisahau Okello na Ingen walivyofirigiswa na
makada hao. Makada hao hawakushitushwa na vitisho hivyo vitupu, kwani waliujuwa
uwezo wa Wamakonde katika medani ya mapambano, wakitumia mishare kupambana
na vyombo vya automatic (Karume hatimae akawafukuza nchi wamakonde hao hao ).
Zanzibar wakati huo kukawa na vikundi viwili vikubwa, vya Umma, kimoja kikitaka
kuchukuwa ” khatuwa za kuhitajika” za kuzuwiya Muungano na wengine wakapendekeza
84
asubiriwe Babu arudi kutoka safarini, na kufanya mazungumzo namashauriano. Wakati
akiwa njiani, akirudi nyumbani kutoka Indonesia, Babu, huko Pakistan, akapambanishwa
na khabari za waandishi wa magazeti na kuulizwa kama alijuwa kuhusu matayarisho ya
kuunda Muungano huo na kutakiwa kutoa msimao wake,kwamba aliunga mkono khatuwa
hiyo au la; jawabu lake likawa,” ndio, alijuwa nakusema kwamba aliliunga mkono suala
hilo”. Ukweli ulikuwa ni tafauti kabisa nausemi huo na kwamba Babu alikuwa hajajulishwa
kuhusu Muungano, na kwa desturi mtu hawezi kuunga mkono au kupinga kitu asichoki
juwa. Huku nyuma,Tanganyika, kumbe kulikuwa kumekwisha tayarishwa cello maaluum
katika gerezala Simbawanga la kumtilia Babu ndani pindi angelipinga Muungano. Hatimae
ikaonekana kwamba majungu ya Muungano huo yalipikwa na shirika la kijasusi
la Kimarekani la CIA; kumtia chuki, hofu na wasi wasi Karume, kumghilibu na kumlazimisha
mtu huyo kuunda Muungano. Aliyeshirikiana namajasusi hao katika mipango
hiyo ya Muungano, alikuwa ni Nyerere. Wakati huo kulikuwa askari wa Tanganyika walikuja
Zanzibar kusaidia kulinda usalama.Nyerere kwa hivyo alitishia kuondosha askari
polisi wake Zanzibar, pindi Karume angelikataa kujiunga na Muungano. Habari hizo
zinakaririwa kwa urefu katika kitabu cha Amrit Wilson (US Foreing policy and Revolution
– The Creation ofTanzania) kuhusu vipi Zanzibar ililazimishwa kushiriki katika
Muungano huo. Ingelikuwa Umma Party haikusisita, kuchelea na kujiweka nyuma basi
labda Muungano wa Marekani na Nyerere usingeliwezekana. Umma Party kama chama
chengine chochote lazima kujiendeleze kwa mujib wa wakati na hali ya kinchi na kilimwengu
kwa jumla. Kati ya njia moja wapo ya kujiendeleza ni kujikosoa na kukosowana,
na chama chochote cha kisiasa kinachojiheshimu na kutizama, kulinda na kuweka maslahi
ya nchi mbele, kinawajib wa kutumia mtindo wa kujikosoa na kukosowana. Ingawaje,
kuna umuhimuwa kuhadhari na kuweza kujuwa mpaka baina ya siasa ya kinadharia na
85
yautendaji. UmmaParty imetumia muda mwingi sana kwa sera hiyo, yaani kutumia wakati
kujadili siasa ya kinadharia. Hatimae, mijadala hiyo haikuchukuwa muda mwingi tu, bali
imechelewesha utekelezaji wa yale yaliyojadiliwa na hatimae hata kuleta migongano ile
isio yakihasama na ile yakihasama. Babu kiongozi wa Umma Party alikuwa mmoja wapo
wa wale ambao wakitumia siasa nyingi sana, pale ambapo wakati mwengine palihitaji
vitendo. Hasa kwa vile huko Bara baadae kulizuka mkondo wa vijana wenye fikra za
kimaendeleo ambao walikuwa na hamu ya kusaidia urekibishaji wa hali ya mambo Visiwani
(Wengine hata kutaka kuundwa upya kwa Umma Party). Hali hii baadae ikaipa
Umma Party sifa ya kuwa wanasiasa wakinadharia tu, ambao wanakaa wenyewe kwa
wenyewe hata kutokaribisha vijana wengine waliokuwa na hamu ya kujiunga nao, katika
mijadala ya kisiasa. Hali kama hiyo iliwafaidisha wale tu waliyoweza kushiriki katika
baraza hizo na kuwapa nafasi ya kupata elimu bora ya kisiasa. Hali hii ilisababisha hata
kukuweko kwa pengo la kisiasa baina ya mwananchi wa kawaida na Uongozi wa Umma
Party. Ingawaje, Umma Party ilitanabahi baadhi ya makosa yake, kujikosoa baadhi ya
makosa yake na kuweza kusababisha mengi ya mafanikio ya Zanzibar yanayodhihirika
hivi leo, na viongozi na wanachama wake kujiunga na mkondo wa maendeleo wa leo.
Siasa ya Umma Party, kwa ujumla haikuwa yenye kupinga Umoja au Muungano wa nchi
za kiafrika yaliyoamuliwa na kukubaliwa na wananchi wote kwa kupitia kuraya maoni,
mradi Umoja au Muungano wenyewe una maslahi ya umma na kuwafikiwa na umma.
Mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa miaka thelathini iliyopita, si mfumo
wa halali, bali ni wenye sura za kikoloni wa mkubwa kumtawalia mdogo na wa kuigubika
Zanzibar isahaulike na isijulikane, na hatimae kuigeuza jimbo. Wazanzibari wengi zaidi
hawaupenedelei Muunagano wa aina huo, kwa hivyo Muungano huo unafaa uvunjwe na
kama pana haja ya kuunda Muungano wowote basi kufanywe kura ya maoni ya Muungano
86
au Shirikisho, ikiwa kama Muungano au Shirikisho la Afrika ya Mashariki yote au la
Zanzibar na Tanganyika, mradi kila nchi iwe na utawala wake kamili, kuwa na Rais wake
ikiwa Seif Sharif Hamad au Salmin Amour, pamoja na Baraza la Mawaziri na Bunge huru.
Na serikali ya Muungano huo au Shirikisho hilo liwe na mawaziri na wakuu wa maidara
wa Shirikisho au wa Muungano wakishughulikiya mambo ya Muungano/Shirikisho hilo
tu na sio kuingilia kati katika serikali huru za Tanganyika na Zanzibar, ambazo ziwe na
Mabunge yao huru. Nyota ya Muungano imekuwa ikizidi na kuzidi kufifiana kufika hadi
CCM kuuogopa Uzanzibari hasa katika uchaguzi ujao na kutaka kuuondowa Uzanzibari.
Nyerere yumo katika kulazimisha serikali moja, lakini ajuwe kwamba hili ndilo suala
litakalo iuwa CCM moja kwa moja visiwani Zanzibar, na vyovyote Nyerere atakavyo
lazimisha, ikiwa seriakli moja au mbili, hata kufa kabla Zanzibar kuwa huru na kuwa na
serikali yake wenyewe.
5.2 Makosa ya Mapinduzi
Kutekwa nyara kwa mapinduzi kumeathiri kazi muhimu iliyofanywa naWazanzibari katika
kupigania haki zao halali. Udhalimu katika jamii kwa kawaida ndio sababu inayoleta
Mapinduzi, ingawaje mara nyingi jina la Mapinduzi linatumika vibaya, au maana yake
kutumika ovyo, kutumika pale ipasapo na isipopasa, kama vile Kuudi-ACtaa, Puuch, Kuu
ya Ikulu, Kuu ya Kijeshi, mabadiliko yote hayo hali huitwa Mapinduzi, ingawa sifa zake ni
nyengine kabisa na zisizo za Kimapinduzi, mfano mzuri wa Kuu ya Ikulu ni ule wa Jumbe
kuondoshwa madarakani. Mara nyingi watu hudhani kupindua serikali kwa mabavu ndio
Mapinduzi, ilhali ukweli wenyeweni kinyume kabisa. Kwanza hakuna Mapinduzi bila ya
kuwa Mapinduzi ya”kimapinduzi”, kuangusha serikali bila ya misingi ya kimapinduzi si
87
Mapinduzi.Ujana mapinduzi au siasa ya kimapinduzi haina lazima kuambata na kupindua
serikali. Fikra za kimapinduzi ni yale mawazo yanayokusudia kubadilisha maisha ya
wanyonge, yaliyoselelezwa nyuma na ya kudhulumiwa kwa madhumuni ya kuleta maisha
bora, ya haki na usawa, yaani kubadilisha hali iliyoselelea nyuma na kuleta iliyoendelea.
Fikra hizi zinaweza kukuwepo kabla ya mapinduzi ya serikali; bila ya mapinduzi ya serikali
au baada ya mapinduzi ya serikali. Hakuna lazima kuwa baada ya kupinduwa serikali siasa
itakayofuatiya lazima itakuwa ya kimapinduzi.Siasa ya kimapinduzi ni ile inayopigania
mabadiliko ya mfumo wa jamii bora nakuondosha maovu. Hali hii inawezekana kukuwepo
ama kwa kupindua serikali au hata bila ya kutumia mabavu ya kupindua serikali. Serikali
ya Hizbu imepinduliwa kwa kutumia njia za kimapinduzi, lakini kitendo cha mapinduzi
yenyewe mwanzoni hayakuongozwa na wanamapinduzi au na f- ikra za kimapinduzi.
Ni baadae ndipo uongozi na fikra za kimapinduzi zilish- irikishwa.Ingawaje, baada ya
kuonekana hatari ya kuleta mapinduzi ya kimapinduzi katika Afrika Mashariki ilibidi watu
fulani wayasaliti Mapinduzi hayo. Katika muda mfupiwa Mapinduzi ya kimapinduzi ya
Zanzibar, program ya kimapinduzi iliweza kupendekezwa na kutekelezwa kama vile, Matibabu
na siha bora bure; kupendekezwa -Elimu bure kuanzishwa, Mpango wa Uchumi wa
kihalali kupangwa, Ardhi kugawiwa sawa kwa wote,Haki za kimsingi kuhakikishwa, uhuru
wamaandishi na wa fikra kupendekezwa, haki za wafanyakazi kuhakikishwa,kupangwa
uondoshaji wa vibanda na kuhakikisha makaazi bora kwa masikini naupangaji wa mengi
mengineyo ambayo yalitokana na program ya chama cha Umma Party. Hiyo ilikuwa
program ya kimapinduzi iliyokuwa na azma ya kubadilishamfumo wa kijamii kongwe na
kuleta mfumo wa halali. Siku za mwanzo za Mapinduzi, program hiyo ilitekelezwa kwa
kiwango fulani, lakini hatimae, baada ya viongozi walivyo endelea wengi kuhamishwa
kupelekwa Bara na kwengineko, kama itavyokaririwa baadae, program hiyo ilisalitiwa .
88
Matibabu bora yakawekewa Memba wa Baraza la Mapinduzi, kwa kufunguliwa Mapinduzi
Wing, Madaktari, Manasi na Wafanyakazi waliyo kuwa na ujuzi tofauti hospitalini
na sehemu mbali mbali serikalini na katika jamii wakapigwa vita na kukimbiya nchi na
siha, elimu na huduma zote za jamii kurejeshwa khatuwa nying nyuma. Kukiondowa kituo
cha siha cha Umoja wa Mataifa (WHO) na kusababisha utapakaaji upya wa magonjwa na
kurejea kwa malaria, ugonjwa uliyokuwa umeshatoweka Zanzibar ni kati ya usaliti wa hisia
za kimapinduzi. Thamani ya elimu ikashuka kwa kufukuza walimu na wale waliyokuwa
na ujuzi, kuwafanya wakimbie nchi na badala yao kuwaweka watoto wa skuli kusomesha
maskulini. Kuwapa wataalamu waliyorudi masomoni ng’ambo mishahara ya chini kabisa
ya shillingi mia nne (400/ ) wakiwa na shahada za elimu ya juu na ambao wazazi wao
wakiwahitajia wawatizame wakishamaliza kusoma, kuliwafanya wakimbie nchi.Kuleta
ubaguzi baina ya wanafunzi, kuzuwiya wanafunzi kupata elimu ya juu na kutoa elimu kwa
ubaguzi. Kipato kutoka karafuu (shina la uchumi wa nchi)kuhodhiwa na Karume na shirika
la biashara la ZSTC, kutoagizia chakula na watu wakawekwa na njaa. Kutotekelezwa kwa
mpango wa uchumi wa miaka mitatu, na badala yake kubuni uchumi usioku- wa na mbele
wala nyuma. Kuchukuwa kwa eka tatu tatu za ardhi zenye rutba, na zaidi ya moja, na
Memba wa Baraz- a la Mapinduzi. Viongozi wa Baraza la Mapinduzi kujenga majumba
mazuri kwa kuiba mali ya serikali, kama vile vitu vya maonyesho vya Makumbusho na
kuwaibia watu binafsi milango na madirisha yao na kutia katika majumba yao. Pamoja
na kuiba nakunyanganya mali tofauti pamoja na kuozwa kwa watu kwa nguvu na mengi
mengineyo yakina Ali Mzee Mbalia na wengineo, hayakuwa mambo ya kimapinduzi,bali
ya upinduzi. Haki za kimsingi karibu zote kupigwa marufuku, kama vile kutolewa kauli
ya kutofanywa uchaguzi kwa miaka 50, kutoruhusu uandishi na usomaji huru, kuondosha
Mahkama za kisheria na haki ya utetezi huru, kuendeleza sheria yakuweka watu kizuizini
89
na kuuwawa kwa watu kwa sababu ya fikra zao za kisiasa. Kufunga Umoja wa vyama vya
Wafanyakazi na Wanafunzi (The Federation of Revolutionary Trade Unions na Zanzibar
Revolutionary Students Union). Kufuja mipango ya kuwapatiaWazanzibari wote nyumba
nzuri zilizoambatana na mazingara ya Zanzibar, kama zile nyumba za Bambi, ilivurugwa
vur ugwa na hatimaepakajengwa nyumba za mabogi ya gari la moshi pasipo na ujuzi
wowote. Kwenda kinyume huku na program ya kuwatowa Wazanzibari katika mfumo
zorota ulitokana na upungufu wa ufahamivu wa fikra za kimapinduzi ndio ulosababisha
leo kuifanya Zanzibar iko nyuma, masikini na kuwezesha kutawaliwa na Muungano.
5.3 Vuguvugu la Venceremos
Kwa nini kulikuwa na haja ya kuunda Muungano na nani hasa aliyetaka Muungano
huo. Ingawa fununu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa yameshawafikia Wakoloni
pamoja na Mashirika ya Kijasusi, kama ilivyokwisha kaririwa huko nyuma. Watu hao
walishindwa kuamini habari hizo, hasa kwa vile nyendo za Umma Party zilikuwa hazi
kuonyesha harakati zozote zilizokuwa si za kawaida, kwa hivyo habari hizo zikadharauliwa.
Walipokuja kutahamaki, serikali ya Hizbu imekwisha pinduliwa na baada ya
hapo hali ya hewa na mazinga ra ya Zanzibar yalibadilika kwa ghafla na kujaaa hamasa
za kimapinduzi na muamko wa kimaendeleo, kukataa sera kongwe za kijamii na kuleta
mfumo mpya wa kujikombowa. Bila ya muda mrefu kupita upepowa kimapinduzi ukaanza
kupepea Afrika ya Mashariki nzima na kutikisa mizizi ya tawala za kitimba kwiri za nchi
hizo. Wamarekani na Wangereza walipoanza kusikia “Venceremos Patriomuerte “(tutakubali
kufa lakini si kushindwa) wakashituka na kudhani Cuba ya pili imekwisha zaliwa
na wakaona maslahi yao yako hatarini hasa kama wangeliruhusu upepo wa kimapinduzi
90
uliyojaa jazba za kijananchi na nia ya kujitolea uliyokuwa ukipepea Zanzibar na kutambaa
Afrika ya Mashariki na ya Kati. Viongozi wa Afrika ya Mashariki nao, akina
Nyerere, Obote na Kenyatta wakaingiwa na wasi wasi wakupinduliwa na kwa pamoja
na kwa msaada wa Marekani na Mngereza wakawa wanajitayarisha kuivamia Zanzibar
kijeshi. Kenyatta na Obote hatimae wakajitoa katika mipango hiyo na mwishowe akabaki
Nyerere peke yake (soma kitabu cha Amrit Wilson kinachokariri jinsi Nyerere na Ujasusi
wa Kimarekani walivyo shirikiana kuulazimisha Muungano wa Tanzania). Nyerere
akamshawishi naku- mtia uoga Karume na kila mmoja kati yao akiwa na sababu zake,
wakashirikiana kuunda Muungano huo bila ya kuwashauri watu wao. Sababu mojawapo
iliyomfanya Nyerere ashituke na kuogopa mapinduzi ilitokana na hatuwa ya jeshi lake kutaka
kumpinduwa na sababu yake ya pili ilimbidi awatumikie wafadhili na mabwana zake
Marekani na Mngereza (ambaye alimuokoa kijeshi siku za ghasia za Colito Barrackswiki
tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar). Wamarekani na Wangereza walitishwa na mfumo
mpya uliokuwa na program ya ki mapinduzi na kuhatarisha maslahi yao ya kiuchumi na
kisiasa. Karume, kwa upande wake, alikuwa na matatizo yake mbalimbali na yale ya
mstari wa mbele yalikuwa kwa uroho, kujaribu kuhifadhi uongozi wake usichukuliwe na
Othman Sharif na Abdalla Kassim Hanga, watu hawa wakishirikiana na viongozi wengine
waliyosoma na waloendelea katika ASP. Kwa upande wa pili Karume alihisi kwamba siasa
yake ya zamani haikuweza kuwaletea wana Afro tija yoyote, wakati siasa mpya iliyokuwa
na program ya kimapinduzi, ghafla iliibadilisha sura ya Zanzibar na kungwa mkono na
Wazanzibari wengi. Kwa hivyo Nyerere hakuwa na haja ya kutumia ustadi mwingi wa
kumfanya Karume kukubali pendekezo la Muungano, wote wawili walitaka kuhifadhi
khatamu zao za utawala na maslahi yao wenyewe. Kwa kisiri siri na haraka haraka, na kwa
msaada wa wataalam wa sheria wa kikoloni, ikaundwa Katiba ya muda ya Muungano bila
91
yakushirikishwa Wanasheria wa Zanzibar au maoni ya wananchi kuulizwa. Katiba hiyo
ilifuata mfano wa katiba ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini, yaani baina ya mtawala na
mtawaliwa, Tanganyika ya Nyerere ikiwa mtawala. Maandishi mengi yakisheria yamejadili
upungufu wa Uhalali wa Katiba hiyo na Muungano wenyewe kwa jumla. Serikali
ya Tanzania bado haija jibu hoja hizo, isipokuwa kila usiku uchao kuleta mapendekezo
mepya ya kuidhibiti Zanzibar. Utangazaji wa makubaliano hayo baina ya Nyerere na
Karume yalifanywa makusudiwakati A. M. Babu kiongozi wa Umma Party alipokuwa
hayupo nchini. Baada yahapo, karibu viongozi wote waliyokuwa na fikra za kimaendeleo
au waliyokuwa na haki ya kuongoza ASP wa kaondoshwa nchini, ama kupelekwa Bara au
katika Mabalozi mbali mbali. Kati ya waliyoondoshwa nchini kwa sababu ya Muungano
na upingaji wa udikteta na ukoloni mambo leo walikuwa A. M. Babu, A. K. Hanga,Othman
Sharif, Salim Ahmed Salim, Salim Rashid, Mohammed Ali Foum, Hasnu Makame, Idris
Abdulwakil, Ali Mwinyi Gogo, Adam Mwakanjuki, Ali Khamis nawengi wengineo. Wale
viongozi wa ASP waliyobaki Zanzibar na kupinga udikteta na Muungano na kuwa na fikra
za kimaendeleo, karibu wote waliuwawa; hawa ni akina Sa leh Sadalla, Abdulaziz Twala,
Mdungi Usi, Khamis Masoud, Jimmy Ringo,Idrisa Majuya, Jaha Ubwa, Ngwali Usi n.k.
Viongozi wachache waWafanyakazi walibaki Zanzibar na hata hao baada ya muda kupita
na wao wakaombolea gerezani na kuteswa. Karibu makada wote wa Umma waliyo somea
mapambano ya kigorilla huko Cuba pamoja na makada wengine wakasafirishwa kwenda
ama Urusi au Indonesia. Wengi kabisa wa Wazanzibari waliyosoma walilamika kuhama
au kuhamishwa nchi, wengi wao kuifaidisha Bara kwa elimu na ujuzi wao na kuwacha
pengo kubwa la ujuzi Zanzibar. Baada ya vikosi vyote hivyo vya kijananchi kuondoshwa
Zanzibar, Muungano ukazidi kutia mizizi, hatimae kuletewa wataalam wa mabibo kuja
kutibu mikarafuu. Ingawaje Wazanzibari hawaku kubali kukaa kimya bali mapambano
92
na vuguvugu la chini kwa chini yaliendelea. Katika mwaka 1972,mwezi wa Aprili tarehe
saba Karume akapigwa risasi na kuuwawa, na mandhara mpaya ya kisiasa ikachipuka.
Kufuatia tukio hilo maelfu ya watu wakatiwa ndani,kati yao wakiwa wengi wa Viongozi
wa Umma Party pamoja na baadhi ya makada. Baadae pakafanywa kesi, na kesi hiyo
ikaendeshwa katika Mahkama iliyokuwa siya kisheria kwa vile Mahakimu hao walikuwa
hawana ujuzi wa kisheria, waliyokuwa ni watu wenye sura za kimapendeleo kwa vile
walikuwa wafuasi wa chama tawala tuna washtakiwa kutoruhusiwa mawakili wa kisheria
wa kuwatetea. Mkuu wamashtaka hayo ndie wakati huo huo akiwashtaki na wakati huo
huo kupewa wadhifa wa kuwatetea washtakiwa hao hao. Baadhi yao walishtakiwa wakiwa
hawapo, yaani wakiwa Bara na mmoja Salim Ahmed Salim akiwa nchi za nje kama Balozi
waTanzania, mashtaka yake hatimae yakafifirishwa. Wafuatao ndio waliyoshtakiwa:
1. A. M. Babu
2. Khamis A. Ameir
3. A. B. Qullatein
4. Amar Salim Saad
5. Nurbhai Issa
6. Ali Sultan Issa
7. Abdulrazak M. Simai
8. Mussa Shaaban
9. Moh’d A. Baramia
10. Kadiria Mnyeji
11. Miraji Mpatani
12. Ali Mshangama
13. Haroub M. Salim
93
14. Hussein Mbaruk
15. Moh’d S. Mtendeni
16. Cpt.Abdulla Khamis
17. Said Moh’d Said
18. Ali Seif Karkoboi
19. Cpt. Abdull Moh’d
20. R. Moh’d Rashid
21. Lt. M. A. Chululu
22. Lt. Salim A.Rashid
23. Sgt. Humud Ali
24. Yusuf Ramadhan
25. Col. Ali Mahfoudh
26. Cpt. Hassan Makame
27. Moh’d Ali Seif
28. Said Salim Said
29. Naaman Marshed
30. Ali Hemed Humud
31. Ishaq Juma Harakati
32. Rashid M. Ahmed
33. Juma Mussa Juma
34. Ibrahim M. Hussein
35. Khamis Masoud
36. Moh’d A. Ladha
37. Moh’d A. Sahir
94
38. Moh’d Khalef Moh’d 39. Salim Abdalla Saleh
40. Saleh Ali Saleh
41. Moh’d Said Moh’d
42. Khamis Abeid Omar
43. Ibrahim Omar Soud
44. Abdulla Mussa Moh’d
45. Alawi Tahir Moh’d
46. Moh’d Khalfan Salim
47. Ahmada Shafi
48. Hassan Said
49. Tahir Adnan
50. Ali Mzee Mbalia
51. R. M. Rashid
52. Lt.Salum A. Rashid
53. Seif Said Hamadi
54. Lt.Mikidadi Abdulla
55. Lt. Ali Othman
56. Abas Mohammed
57. Lt. Abdulla Juma
58. Lt. Ahmed M. Habib
59. Cpt. Suleiman Moh’d
60. Lt.Hashil S. Hashil
61. Cpt. Hemed Hilal
62. Lt. Shaaban Salim
95
63. Lt. Amour Dg’hesh
64. Maj. Salim S. Salim
65. Lt. Haji Othman
66. Tahir Ali
67. Badru Said Badru
68. Abdulaziz Abdkadir
69. Ali Salim Hafidh
70. Ali M. Ali Nabwa
71. Moh’d A. Ameir
72. Ali Y. Baalawy
73. Saleh Abdulla
Waliyoshtakiwa wote walikuwa 81, wengine waliwachiliwa mapema.
5.4 Awamu tafauti
Baada ya kuuwawa Karume hali ya mamboikaanza kubadilika Zanzibar. Kwanza kulikuwa
na mchuano mkubwa wa kugombania khatamu za utawala baina ya Aboud Jumbe na Seif
Bakari, ambaye ndie aliyekuwa chini ya Karume. Nyerere akaamua kumuunga mkono
Aboud Jumbe. Jumbe alileta mabadiliko tofauti visiwani, kama vile kuruhusu watu kutoa
maoni yao, kukosoa bila ya kuogopa kutiwa ndani. Aliruhusu waliyoshutumia katika kesi
ya uhaini kupandishwa Mahkamani, ingawa Mahkama yenyewe ilikuwa haijatoa ruhusa
ya utetezi huru au kuwa na Mahakimu waliyosomea sheria. Katika utawala wake Jumbe
aliweza kuondosha khofu, kuheshimu wasomi, kupunguza nguvu za Memba wa Baraza la
96
Mapinduzi, na kuleta nafuu kwa kadri fulani. Alianzisha Baraza laWawakilishi. Ingawaje
kwa sababu yamigongano yake na Baraza la Mapinduzi likiongozwa na Seif Bakari akazidi
kuitia Zanzibar katika kabari ya Muungano. Baadae Jumbe nae akaanza kuwa muamuzi
wapekee. Baada ya muda fulani kupita Jumbe nae kama Karume, akaanza kutan- abahi
uovu wa Muungano na akaanzisha mbinu za kuitoa Zanzibar katika Muungano. Lakini
kwa bahati mbaya makosa aliyokwisha yafanya ya kuizamisha Zanzibar katika matope
ya Muungano yalikuwa ni mengi na kumzamisha mwenyewe kila alipojaribu kujitowa.
Kosa kubwa kabisa alilolifanya Jumbe dhidi ya maslahi ya Zanzibar ilikuwa ni kukifufua
chama cha ASP (viongozi wake halisi kwisha kuteketezwa) na baadae kukiunganisha
na TANU na hatimae ku- zaliwa CCM, MAMA WA BALAA LOTE. Baadae chama
hicho hicho cha CCM alichokuwa mmoja wawakunga wake kikamfukuza kwenye uongozi
kama kitakataka. Baada ya kuondoshwa na kuuzuliwa Jumbe kwa muadhara mkubwa,
akawekwa Ali Mwinyi, ambaye siku za mwanzo alipendeza sana Zanzibar lakini baadae
akababaishwa na Urais wa Muungano na kuusahau Uzanzibari wake. Idris Abdul-wakil
(mmoja kati ya wale viongozi waliyojitowa ASP 1964) baada yakuchukuwa pahala pa Ali
Mwinyi akagonganishwa na Wazanzibari wenzake.Kufuatia tukio hilo kundi la watu Saba
likiongozwa na Seif Sharif Hamadi likafukuzwa Chama na kutolewa madarakani. Idris
Abdulwakil nae nyota yake mwishowe ikafifia katika CCM ya Nyerere, na wakati CCM
inapanga kumuuzulu, Idris akawawahi na kujiuzulu mwenyewe na kujikosha na balaa la
Muungano. Salmin Amour akashika ukanda lakini kabla hajawahi kukaa vizuri katika
Kiti chake Salmin akajiona kwamba alikuwa “Chui wa Karatasi” asiyekuwa na meno
walamakucha. Hali hiyo ilidhihirika wakati alipoiunganisha Zanzibar na Jumuiya wa
Nchi za Kiislaam. Bila ya mapenzi yake akaambiwa aitowe Zanzibar katika Jumuiya hiyo.
Hapo akatanabahi kwamba Urais wake wa Zanzibar ulikuwa ni wa jina tupu, usiyokuwa na
97
nguvu sawa hata za Waziri mdogo wa Bara. Wakati huo alitakiwa Rais Amour aonyeshe
“Ushupavu” wake kama Kiongozi mwenye uzito na ama kuitoa ASP katika CCM au
kuitoa Zanzibar katika Muungano. Wapiiii, kipindi cha kihistoria kimempita Rais Amour
na Wazanzibari itabidi wangojee ushupavu wa Rais mpya atakayekuwa na ukakamavu na
ushupavu wa kutosha unostahiki Rais wa nchi. Amour nyota yake nae imekwishafifia katika
CCM na Nyerere yumo kumtayarisha Dr. Omar au mwengine kama huyo kuchukuwa
madaraka.
5.5 Migogoro ya Nyerere na Karume
Nyerere kwa mara nyingi katika historia ya Zanzibar amekuwa akijaribu kuwaamulia
Wazanzibari nini la kufanya kama vile wao wenyewe hawajajiweza. Kwa ujanja na ulaghai
wake aliweza kufanikiwa kutia fitina baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kama
vile Mngereza alivyofanya siku za nyuma. Wakati wa mwanzoni watu wengi hawakuelewa
nini azma ya Nyerere, na kumdhani kama ni mtu mwema, lakini hatimae ilidhihirika
kwamba alikuwa akitaka kuitawala Zanzibar. Kwa upande mmoja, kati ya baadhi ya njama
zake, baada ya kuundwa Muungano, alisaidia na kuhakikisha kwamba wale Wazanzibari
waliyokuwa wamesoma walihamishwa Zanzibar. Kwa njia kama hiyo sehemu kubwa ya
uongozi uliyobaki Zanzibar ulikuwa ni wa wale wasiosoma, ambao aliweza kuwaendesha
na kuwadanganya kama alivyotaka. Kwa upande wa pili, ingawa suala la usalama lilikuwa
chini ya Muungano na Nyerere ndiye aliyekuwa mkuu wa Muungano, ili kuhifadhi maisha
ya Muungano huo alikataa kuhami maisha ya viongozi wa Kizanzibari waliyouwawa kwa
sababu ya kuwa na fikra tofauti za kisiasa. Kwaupande wa tatu Nyerere aliwatumilia
wale waliyoitwa Wabunge wa Zanzibar, Bungeni Dar es salaam, kuwazuwia Wabunge
98
wa Tanganyika kumshambulia Nyerere na serikali yake. Wabunge hao wa Zanzibar waliogopa
kuwasaidia Wabunge wa Tanganyika kwa vile waliporudi Zanzibar walim’haha
Karume ambaye asingelisita kuwapeleka chuoni kwa Mandera, kwenda kudurusu. Kwa
njia hii Nyerere aliweza kudhibiti utawala wa Tanganyika na wa Zanzibar kwa wakati
mmoja. Ingawaje, kulifika wakati fulani ambapo, maingiliano baina ya Karume na Nyerere
hayakuwa mazuri na Karume alifanya njama na mbinu za kum adhiri Nyerere kila
alipopata nafasi. Katika mwaka wa 1971 Karume alifanya mbinu i li ahakikishe kwamba,
ikiwa kwa sababu yoyote Nyerere atasita kuwa Rais, basi yeye Karume ndiye ahakikishiwe
Urais wa Tanzania. Mipango hiyo aliwahi kuipendekeza hatambele ya mkutano wa Baraza
la Mawaziri. Nyerere akamshitukiya Karume, na akamsail Karume mbele ya mawaziri,
na kumuuliza kama Karume alitarajia kuchukuwa Urais akifa Nyerere. Kama kawaida
ya mgogoro kama huo, Jumbe aliingilia kati na kumhakikishia Nyerere kwamba” Karume
hakuwa na azma mbaya na yeye, bali Karume alieleweka vibaya”. Nyerere bi- la ya kufikiri
na kutanabahi sana, kwa haraka haraka, kama desturi yake akatunga sheria mpya ya
Tanzania Bara, na kuipa serikali uwezo wa kuwa na Waziri Mkuu, ili kama yeye Nyerere
kwa sababu hii au ile angelikutwa na ajali ya kifo cha ghafla, basi Waziri Mkuu huyo
ndiye aliyekuwa achukuwe ukanda wa Urais wa Muungano na sio Makamu wa Kwanza
wa Rais, yaani Karume .Uamuzi huu ulimkasirisha sana Karume kwa vile aliona kwamba
uwezekano wake wa kuwa Rais, pindi Nyerere akifa ulififirishwa na kuondoshwa, na
kwambaWaziri Mkuu huyo atakuwa wa Zanzibar vile vile. Ingawaje, Karume hakukubali
kushindwa, kwani alidai kwamba kitendo hicho cha Nyerere cha kujiamuliya hivyo ilikuwa
ni, kuiruka na kuikuuka Katiba ya Muungano na kujiamulia kuteuwa na kuanzisha Wadhifa
wa Waziri Mkuu kulikuwani kinyume na Katiba ya Tanzania. Kwa hivyo Karume
akaamuwa kumpeleka Nyerere Mahkamani kwa kuikiuka Katiba. (Tutakumbuka baadae
99
hata Jumbe nae alitaka kumpeleka Nyerere katika Mahkama kwa kukiuka makubaliano
ya maandhishi ya Muungano.) Karume tokea mwaka 1970 alikuwa ameanza kampeni
kali sana ya kwenda sehemu mbali mbali kama vile Kariakoo na kwenda kuwahutubia
makabwela na kutia fitna dhidi ya Nyerere na kuwaahidi makabwera kazi na nyumba
bure Zanzibar kama Nyerere angelishindwa kuwapatia vitu hivyo Bara. Karume vile vile
alikuwa akitowa mapesa kuwapa vilabu vya mipira vya Bara ili kuwavutia na siasa yake,
wakati huo huo Wazanzibari wakikaa na njaa. Karume alijaribu kuwashawishi wanajeshi
wa Kizanzibari waliyokuwa Bara, kumpelekea khabari za kijasusi dhidi ya utawala wa Nyerere.
Isitoshe katika sherehe za miaka kumi ya uhuru wa Tanganyika, Karume alipeleka
Dar es salaam majeshi ya Zanzibar na silaha kubwa kubwa, ikiwemo mizinga tofauti.
Majeshi hayo yanasemekana yalikuwa yajiandae sehemu mbili tofauti za Uwanja wa Taifa
ambako sherehe hizo zilikuwa zifanyike. Uwanja huo uliwekwa katikati na makombora
na mafashi fashi yalikuwa yakutanie katika ya anga ya Uwanja huo. Makombora hayo
yalikuwa yatupwe kutoka hizo sehemu mbili tofauti, moja sehemu ya Mgulani na nyengine
sehemu za Mjini. Hapo watu wangelikuwa wakishughulika na kutizama mafashi fashi angani,
na wale askari wa jeshi la Zanzibar waliyoshiriki katika paredi hiyo wangelimtwanga
risasi Nyerere na Karume angelishika ukanda kufuatia kifo cha Nyerere. Kiongozi mmoja
wa jeshi la Zanzibar aliyekuwa aongoze majambo hayo, bahati mbaya amekwishakufa,
nae alikuwa Col. Mussa Maisara, lakini wakuu wengine wengi wa kitendo hicho bado
wahai. Kwa bahati wanajeshi wa Bara walishituka, kutokana na hemkahemka na kwa
sababu ya idadi ya askari wa kushiriki katika sherehe hizo kutoka Zanzibar iliwashitua
Jeshi la Bara na vile vile kushitushwa na wingi wa silaha hasa zikiwa silaha kubwa kubwa.
Vile vile kile kitendo cha wanajeshi wa Zanzibar waliyo omba kutumia nafasi ya zile
sehemu zilizokuwa na ulinzi mkali ili kutekelezea matayarisho ya tafrija zao, zilitia wasi
100
wasi. Baada ya kuchekechwa kwa makini Wanajeshi wa Bara wakanusia harufu ya hatari
na kwa hivyo hizo sherehe zikaaghirishwa na Nyerere kujificha. Baada ya tukio hilo
Col. Ali Mahfoudh akarejeshwa Zanzibar. Karume hakumuwahi Nyerere bali akawahiwa
yeye. Baada ya kuuwawa kwa Karume, Nyerere akaanza kutamba. Katika maziko ya
Karume, Nyerere akatokwa na machozi ya mamba, huku akichekelea ndani kwa ndani na
kuukaribisha wakati mpya. Ingawa wakati Karume alipokuwa hai Nyerere alidai kwamba
Wazanzibari walivyokuwa wakiteswa na kuuliwa yeye hakuwa na uwezo wa kuingilia
kati mambo ya ndani ya serikali ya Zanzibar, lakini mara tu baada ya kuuwawa Karume,
Nyerere mwenyewe hakusita kuchukuwa fursa ya kuwatiya ndani maelfu ya Wazanzibari
waliyokuwa Tanganyika. Wengi ya Wazanzibari hao hawakuwa hata wanasiasa, wangine
walikamatwa kwa kusingiziwa ati wamesherehekea kifo cha Karume kwa kupika pilau ya
kuku, huko Bara; au mtu mmoja, Mzee Salim, alitiwa ndani kutoka kijiji cha Ujamaa, ati
kwa sababu aliweka dhamiri kwamba, ikiwa Karume atak- ufa basi atakula ugari chini,
mchanga ukiwa sahani yake, na mtu huyo akatiwa ndani atikwa sababu alionekana akila
huo ugari chini. Ingawaje kutiwa ndani kwa watu wengine baada ya kufa Karume kulikuwa
na madhumuni maalum ya kuunufaisha utawala wa Nyerere. Shabaha moja muhimu ya
kwa nini mfano Babu alitiwa ndani, ilikuwa na madhumuni maalum kama yale ya 1964
ya kumuondosha Babu, Hanga n.k. wasije kuchafuwa mambo ya Muungano, kwani kwa
mujib wa ngazi za utawala wa Zanzibar Kinara alikuwa Karume, chini yake akawa Hanga
na baada ya Hanga alikuwa Babu. Kwa hivyo maadhali Hanga, kwa wakati huo alikuwa
amekwisha uwawa, kwa hivyo kufuatilia kifo cha Karume aliyekuwa ashike ukanda wa
madaraka ya Utawala wa Zanzibar alikuwa awe Babu (tazama orodha ya Baraza la – Mapinduzi,
1964) na sio Jumbe ambae alikuwa kiongozi wa tano katika orodha hiyo. Muungano
uliundwa kuizuwiya Zanzibar isifuate mwenendo wa kimaendeleo ambao hatimae ungeli-
101
wafanya Watanganyika kudai maendeleo kama hayo na hatimae kumuondosha Nyerere.
Babu na Umma Party, pamoja na mamilitanti wa ASP walionekana kama ni watu waliyoitakia
Zanzibar msimamo madhubuti, uliyokuwa huru na wakimaendeleo, na kuwa dhidi
ya azma na njama za Muungano wa Nyerere.Kwa hivyo kuuwawa kwa viongozi tofauti
Zanzibar na kutiwa ndani kwa Babu kufuatia kifo cha Karume kulikuwa na madhumuni
yale yale kama ya kuunda Muungano, yaani kuimarisha Muungano usiyoamuliwa na watu.
Babu na Umma Party kwa jumla waliwekwa ndani kwa miaka sita, bila ya kufunguliwa
kesi yoyote huko Tanganyika ya wale aliyokuwa wametiwa ndani Tanganyika, na wale
waliyokuwa gerezani Zanzibar kuteswa kikatili, wengine kuuwawa na halafu kufanyiwa
kesi isiyokuwa na Mahakimu wa Kitaalam, wasiopendelea upande wowote, wala kuwa na
uwezo wa kupata mawakili wakuwatetea ambao waliwachaguwa na kuwataka wenyewe.
Kama Nyerere angelikuwa ametaka kesi halali ifanyike, asingelishindwa kufanya hivyo,
kwani kwa wakati huo ule aliyekuwa akimuogopa alikuwa hayuko tena na alikuwa na
nguvu za kutoshaza kuweza kufanya atakacho Zanzibar, kama tulivyoona baadae, alivyo
wasambaza kina Seif Bakari. Nyerere aliogopa kesi kufanyika Tanganyika kwa sababu
aliogopa ufichuliwaji wa mizoga aliyoificha katika makasha na makabati yake na kuogopa,
kama Babu angelimuacha nje Wazanzibari wangelimtaka awaongoze.
5.6 Tanganyika imepiga kamba
Tanganyika kwa kuunganishwa na Zanzibar imeathirika kama Zanzibar ilivyoathirika, na
kugeuzwa kama watu wawili waliyopeyana migongo, kufungwa kamba pamoja na kuambiwa
washindane mbio kila mmoja akielekea kwake, halafu atafutwe mshindi. Sababu
mojawapo ya kuunganishwa kwa nchi mbili hizi ilikuwa nikupunguza kasi za maendeleo
102
ya Zanzibar na kwa njia hiyo kuepusha hamasa kama hizo zisije zikatambaa Tanganyika
na kuwafanya wananchi wa huko kuanza kuzidi kudai haki zao zilizotokana na majasho
yao. Hali hii hatimae ingelileta mgogoro kwa Wakoloni mambo leo, mabeberu na wanyonyaji
kwa jumla. Kuambatana na vuguvugu hilo wananchi wa Tanganyika wangelidai
maendeleo zaidi ambayo hatimae yangeliwafanya kuweza kujitegemea zaidi na kuwa huru
zaidi. Wapata hasara wangelikuwa ni watawala wa Kibeberu waliyomiliki njia na funguo
zote za uzalishaji mali na ambao wanaamua thamani ya jasho la mfanya kazi na
bei za bidhaa ulimwenguni, bidhaa ambazo kwa daima zikimdhalilisha, kunmyonya na
kumkandamiza mnyonge ambae ni Mtanganyika na Mzanzibari wa chini. Wakati huo
huo kumlazimisha alime chai, kahawa na pili pili hoho na asilime chakula chake chakujishibisha
yeye na ukoo wake na kuhakikisha kwamba uchumi umedhibitiwa na wale wale
watawala wetu wa zamani. Kutokana na utawala wa kikatili wa kijerumaniWatanganyika
hata alipokwisha ondoka Mjerumani huko Tnaganyika, walibaki kuwa wananchi watiifu
sana, waliyopenda usalama na waliyokuwa hawapendi vurugu. Suala jengine muhimu- lilo
wasononesha Watanganyika ni lile la mwaka 1964 wakati walipojaribu kuchukuwa silaha
dhidi ya Nyerere, hatimae walimuona Mngereza kaleta majeshi yake kumtetea Nyerere na
kuwakandamiza Watanganyika, kwa hivyo Watanganyika walihisi kwamba kama wangelimu
ondosha Nyerere basi Mngereza angeli rudisha tena kwa kutumia mabavu na ndio
maana baadae walisita sita kumuondowa Nyerere, hasakwa vile wale waliyokuwa na fikra
kama hizo waliambulia kuwekwa vizuizini hadi kuota ukungu. Hii ni sababu mojawapo
ambayo ilimuwezesha Nyerere kuweza kuwatalaWatanganyika bila vuguvugu au mapambano
makali. Kwa vile Tanganyika kulikuwa na makabila mbali mbali,Watanganyika vile
vile walishindwa kuunganana kuweza kumpa Nyerere upinzani wa kutosha ambao hatimae
ungeli waletea maendeleo. Waliyoathirika na kuteseka zaidi katika Muungano huu,
103
walikuwa bila ya shaka yoyote, niWazanzibari, kwani wao walitawaliwa mara mbili, yaani
walitawaliwa na Muungano na wakati huo huo kutawaliwa na utawala wakikatili, wautesaji
na wa kiuwaji. Watanganyika walitawaliwa na Muungano (ambao kwa kweli ukiendeshwa
na serikali ya Tanganyika) wa Nyerere tu, in- gawa baadhi yaWatanganyika walipowekwa
vizuizini walivushwa kwenda Unguja kushuhudia nakuonja mateso ya gerezani kwa Mandera.
Chini ya jina la Muungano, Watanganyika walinyimwa me ngi, hata mambo yale ya
kawaida ya nchi huru, kama vile kuwa na Bunge lao wenyewe, ambamo wangeliweza kukaa
kwa siri au kwa dhahiri na kuamuwa mambo ya maslahi yao wenyewe. Kunyimwa kwa
Watangayika kwa kikao huru kama hiki hakijawanyimaWatanganyika tu ku jitambua kama
Taifa na Nchi huru, bali papo kulileta athara kubwa mno kwa-Wazanzibari. Watanganyika
walikuwa wakijuwa wazi mateso ya kikatili yaliyokuwa yakiwapata Wazanzibari wakati
wa Karume; kinyimwa chakula, kunyimwa masomo, kuozwa kwa nguvu,kufukuzwa nchi
walizozaliwa, kutokuwa na usalama, kunyanganywa wake zao kwa nguvu, kutishwa saa
zote, kupewa mishahara ya chini, kutokuwa na haki za kifanyakazi na kikulima, wanawake
kutoheshimiwa na kutowakilishwa, vijana kulazimishwa kufanya kazi makambi ya kazi
bila manufaa yoyote, kuzuiliwa kusafirikwa wanafunzi, kupigwa risasi watu msikitini,
kutiwa vizuizini kwa mashekhe, kukimbizwa kwa wataalam na kufukuzwa kwa shirika
la siha la Umoja wa Mataifa(WHO), kuhamisha Wazanzibari waliyosoma na waliyokuwa
na fikra za kimaendeleo,kunyang’anywa ovyo kwa mali za watu, kutiwa nd ani kwa ovyo
kwa watu wenye fikra tofauti vizuizini, kuteswa kwa vipigo vya kinyama mbali mbali
kwa waliyotiwa vizuizini, kuuwawa kwa Viongozi wa Kisiasa waliyokuwa na fikra tofauti
na Karume na mengi mengine maovu; ingawa yote haya wakiyajuwa,Watanganyika
waliyanyamazia kimya, maonevu yote haya ya kikatili, kutotetea haki za kibinaadam za
Wazanzibari na badala yake walinong’ona pembeni pembeni tu.Pindi Watanganyika wan-
104
gelikuwa na Bunge lao huru wakati huo, basiWazanzibari wanaamini kwamba mateso hayo
ya Wazanzibari wasingeliyanyamaziya na waasingeliruhusu jeshi la Tanz- ania kumhami
Karume. Kwa hivyoWatanganyika hawana haki tu ya kuwa na Bunge lao huru kama Taifa
na Nchi yeyote huru ulimwenguni, bali wana lazima na wajib wa kupiganiwa haki hiyo.
Kuwepo kwa Bunge huru la Tanganyika kunatarajiwa kuleta haki za kidemokrasia halali
zitazopigania hata haki zaWazanzibari. Na Mzanzibari yeyote yule ambaye atapinga haki
za Watanganyika kuwa na Bunge huru basi si mpinga mandeleo ya Tanganyika peke yake,
bali wakati huo huo mtaka kuwaona Wazanzibari wanateseka milele.
5.7 CCM hazina ya baa na balaa
Kamailivyokwisha kaririwa huko nyuma Mapinduzi ya 1964 hayakupangwa wala kutekelezwa
na ASP, bali na sehemu ya ASYL na hatimae Umoja huo waVijana ukahakikisha kutoweka
kwa karibu viongozi wote wa juu wa ASP, wakiwemo kina Hanga, Othman Sharif, Saleh
Sadalla, Mdungi Usi, Ngwali Usi, Khamis Masoud, Abdulaziz Twala n.k. Chama hasa
kilichokuwa kiki tawala Zanzibar baada ya Mapinduzi, kwa hivyo hakikuwa ASP bali
ilikuwa ASYL ambayo ilishirikiana na Karume kuuwa, kutawala kwa mabavu, na nguvu
za mwisho zikiwa katika Kamati ya Watu 14 wa Baraza la Mapinduzi ambao wote walikuwa
ni ASYL, Karume aliingizwa baada ya Okello kufukuzwa nchi. Aboud Jumbe,
hakuwa- mwana ASYL, wala kuwa mwana kamati wa Kamati ya watu 14, kwa hivyo
Jumbe alipopata khatamu za utawala akiungwa mkono na Nyerere ikambidi ajenge Boma
lake mwenyewe. Kwahivyo akajaribu kuifufua ASP, lakini hichi hakikuwa kile chama
cha ASP kilichotambulika kabla, kwani viongozi wake wote halisia walikwisha toweshwa,
kwa hivyo viongozi wa juu wa chama hicho kipya hatimae wakabaki wale wale wana
105
ASYL. Itakumbukwa, mara tu baada ya kuuwawa Karume jinsi Aboud Jumbe alivyokuwa
akitatanishwa na Seif Bakari, ambae alijihisi kuwa na haki ya Urais wa Zanzibar, baada
ya kufa Karume. Wakati Seif Bakari alipotishia kutumia nguvu za kijeshi, kwa vile jeshi
la Zanzibar lilikuwa chini yake, Nyerere akaingilia kati na kumkanya Seif Bakari awache
njama za kutaka kumpinduwa Jumbe na kama angelijaribu kufanya hivyo basi angelikiona
cha mtema kuni Nyerere; Seif Bakari akaufyata. Kufuatia shida na matatizo ya kila aina
ya Zanzibar wanachama wa zamani wa ASP ndio waliyoteseka zaidi kuliko hata wafuasi
wa vyama vyengine, kwa hivyo wanachama hao wakaamuwa kutokiunga mkono chama
hicho kipya, kwani walijuwa kwamba balaa litakuwa ndilo lile au akhasi ya hivyo. Kwa
vile nguvu za utawala wachama hicho bado zilikuwa chini ya ASYL, Jumbe akaharakiza
kuungana na TANU ili kuvunja nguvu za ASYL. Kile alichokifanya Jumbe ilikuwa sio
kuunganisha TANU na ASP, chama ambacho kilikuwa hakipo tena. Kwa hivyo, bila ya
kutanabahi, kile Jumbe alichokiunganisha ilikuwa ni ASYL na TANU, kwani mwishowe
viongozi hao hao, yaani wa ASYL, ndio waliyowakilisha Zanzibar katika Kamati Kuu ya
CCM, kiini na kinara cha Utawala wa Tanzania. ASYL wakiwa nusuya viongozi katika
Kamati hiyo. Wakiwa pamoja na Nyerere na baadhi ya vibaraka wa Bara, ASYL waliweza
kuhakikisha kwamba siku zote walikuwa wengi katika kuunga mkono baa na balaa la CCM.
Kwa njia hiyo hata waliweza kuibadilisha siasa ya TANU na ya Tanganyika kwa jumla na
kuzidi kuzirejesha nyuma Zanzibar na Tanganyika kwa pamoja. Kabla ya hapo, TANU
haikuonyesha ishara yoyote ya dhahiri ya kuwa na msingi wa siasa ya kikabila, tofauti
na ile siasa iliyofatwa na ASYL. ASLY kwa vile walikuwa hawana sera au siasa yoyote
maalum ya kufuata iliwabidi waung’an’ganiye ukabila. Baada ya hapo uongozi wa juu,
katika Kamati Kuu ya CCM, ukawa unawakilishwa na siasa mbovu ya ukabila ya ASYL
na hatimae CCM ikafilisika na kuanza kutumia siasa dufu ya kudai kwamba Mzanzibari
106
yoyote aliyedai haki za Kizanzibari, haki za kibinaadam na za kidemokrasia alibuniwa
kwamba anataka kurejesha utawala wa Sultani na kutaka utawala waWaarabu urudi. Siasa
hii ilionyesha wazi jinsi CCM ilivyokwisha filisika kisiasa na kutaka kung’an’gania katika
utawala kwa kutumia kila mbinu, nzuri au ovu. ASYL iliimba wimbo h uo kwa sababu
ilikuwa haina mfumo wa kisiasa maalum wa kutatua matatizo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii
na kitamaduni ya Zanzibar. Kwa hivyo siasa za chuki zilikuwa na madhumuni
ya kuwanusisha Wazanzibari kasumba ili walale milele nawasishughulike na ukweli wa
mambo ya leo, na kuacha kutafuta sababu zakuwajulisha kwa nini maisha yao yako chini
na vipi watayabadilisha. CCM ikaingia katika shangwe la kuitikia wimbo huo na kusahau,
kwa makusudi, mambo muhimu sana kuhusu historia ya TANU na historia ya Tanganyika,
makhsusan. CCM ilisahau kwamba katika mapambano ya Watanganyika, palipiganiwa
haki sawa katika midani tofauti baina ya Watanganyika wa kawaida, ukifananisha na yale
matabaka yaliyopendelewa na utawala wa Kiingereza, huko Tanganyika. CCM, mtoto wa
TANU, vile vile inasahau kwamba wakati Zanzibar kulikuwa na tabaka la juu la Ukoo wa
Kisultan, (watu hawa wakiwa wazalia na raia wa Zanzibar), Tanganyika nako kulikuwa
na Koo zilizotukuzwa na kupata manufaa zaidi kupita raia wengine, Koo hizi zilikuwa za
Kifalme wa Bara, yaani za Kichifu. Kila mtu anaweza mwenyewe kukisia kwa nini Koo
za Kichifu hizo hazijatajwa kama ni Koo za tabakali lomuunga mkono, kumtukuza, kumtumikia
na kupendelewa na Mngereza. CCM imesahau vile vile ule ubaguzi uliyofanyika
dhidi ya Waislaam wa Kitanganyika katika kila fani na hata kulazimishwa waislaam
kubadilisha utu wao “identity” yao, na kubadilisha majina yao ili kuweza kupata elimu ya
kwenda maskuli. CCM haijashughulishwa na kubaguliwa kwa Wazanzibari Tanganyika
wala kushughulishwa na ubaguzi wa Baraza la Mapinduzi wa wale Wazanzibari ambao
ama wanafikra tofauti au asili tofauti, wakati wengi wa hao hao Baraza la Mapinduzi
107
wakiwa na asili za kutoka nje ya Zanzibar. CCM imesahau kwamba kwa mujib wa tafsiri
ya kilimwengu ya haki za bidaadam, hata wale walio wengi kuwabaguwa walio wachache
ni haramu. CCM inapoleta ubaguzi wa asili visiwani Zanzibar kwa kutarajia kuungwa
mkono na wananchi, inafaa ikumbuke kwamba wengi wa wake wa viongozi wa Zanzibar,
ni wenye asili za Kiarabu hiyo kuwafanya hata watotowao kuwa wenye asili ya kubaguliwa.
Viongozi hao wa ASYL/ASP walipopata vyeo hawakwenda kumuowa Mwanakheri
wa Ng’ambo, Chwaka, Mkokotoni au Kizimkazi. Kwa kasumba zao za kubabaishwa na
singa na rangi, waliwaona ndugu zao kinyaa na kutafuta masinga, halafu wakitubabaisha
sisi kuhusuWaarabu. Viongozi hao wa leo wanaishi kwa anasa, utukufu na kuwa na nguvu
zaidi ya huo Usultani wa Kibunsaid wanaotubabaishia.
Mwanzoni Wazanzibari wengi walivyosikiya kwamba ASP (yaani ASYL Zanzibar)
itaondoshwa na kuunganishwa na TANU, walipata tamaa na kudhania kwamba hali ya
kisiasa Zanzibar itabadilika na kuona bora chama hicho kikorofi cha ASYL kikiondoshwa.
Haukupita muda mrefu Wazanzibari wakavunjika moyo kuona kwamba CCM badala ya
kufuata siasa njema ya kidemokrasia na iliyoheshimu haki za kibinaadam, ilianza kuongozwa
kwa vitisho na utawala wa mabavu ule ule uliyotumika na ASYL, na wengi wa
viongozi wake wa Kamati Kuu walikuwa ni walewale waliyoiangamiza Zanzibar.
Kuzalishwa kwa CCM katika mwaka 1977 hakumaanishi kwamba TANU imeungana
na chama cha kisiasa Zanzibar, wala kumaanisha kwambahiyo TANU iliunganishwa na lile
tawi lake la Zanzibar la African Association. Kwa hivyo CCM haitokani na muunganisho
wa chama cha kisiasa cha Tanganyika na chama cha kisiasa cha Zanzibar, maana Zanzibar
kulikuwa hakuna chama cha kisiasa tena. Chama cha ASYL kilikuwa ni chama cha vijana
108
na sio chama cha kisiasa kilichotambulika kuwana sifa na ufuasi wa chama cha kisiasa
kilichobainika Zanzibar, kwani hata kabla ya uhuru chama hicho cha vijana kilikuwa na
wafuasi wachache sana. Ingawaje kila Mzanzibari anakumbuka namna Makao yao Makuu
ya Darajani yalivyokuwayakitisha. Kwa hivyo TANU kwa kweli imejibadilisha jina tu na
kujiita CCM bilaya kuwa na sehemu ya chama cha kisiasa kilichowawakilishaWazanzibari.
Kwa hali hii CCM haina uhalali wowote wa kuwakilisha siasa ya Zanzibar. CCM
kwa hivyo ni chama cha Bara ambacho hakija tekeleza masharti waliyoyaweka wenyewe,
yakwamba “chama lazima kuwakilishwa kote Tanganyika na Zanzibar”, na kwa mujibwa
mantiki za uchaguzi, chama hicho hakina haki ya kuweka mtetezi yoyote wauchaguzi
Zanzibar, na wale wanaojitamba kuwa wana CCM Zanzibar itawabidi amawaende wakasimamie
uchaguzi Tanganyika, au waunde chama chao kipya kabisa, kisicho ASP, kwani
viongozi wa chama hicho wote ni mahtuti, labda ingelikuwa jambo la maana kama wangeliunda
chama kimpya cha ASYL ZANZIBAR. Kutokana na wimbi jipya ulimwenguni
la kutokomeza udikteta na kuleta hishma kwa binaadam na kuthamini maisha ya kawaida
ya binaadam kwa kuondosha uvunjaji wahaki za kibinaadam na kuanzisha demokrasia;
serikali nyingi ulimwenguni zililazimishwa na wafadhila wao kuanzisha siasa ya vyama
vingi. Mojawapo katikahizo ilikuwa Tanzania, ambayo ilikuwa na utawala wa chama
kimoja. Chama hicho hatimae kilikuwa baadala ya kutizama maslahi ya wananchi, kuyatukuza
maisha yabinaadam na kupigania haki sawa za wananchi , kikazidi na kuzidi
kufuata siasa yaufidhuli na utumiaji mabavu. Chama hicho kilisahau msingi wake na
kusahaukwamba kuna tofauti baina ya “Serikali na Chama”, na kwamba chama kwa
kawaida kinashughulikia siasa maalum ya chama hicho na jinsi inavyotumia siasa yake
kuifaidisha nchi nzima na sio viongozi wake tu, bali wananchi wote hata wale ambao si
wanachama wake. Baadala ya kwamba chama hicho kilikuwa kiipe serikali muongozo wa
109
kisiasa, kikaanza kuingilia kati katika kila medani, na chama kujifanya serikali yenyewe,
na mara nyingi viongozi wa chama kuingilia mambo wasiyoyaelewa. Hali hiyo ikawafanya
na wale watumishi wa serikali wajifanye/ au wafanywe wanasiasa, bila hata ya kuwa na
ujuzi au sifa za kisiasa. Kwa njia kama hiyo, ndani ya nchi iliyo filisiwa bila ya kiasi,
ama walipata maslahi bora yaki binafsi katika makazi yao, kupata vyeo pasi na kustahiki
au kuwafanya wale waliyokuwa na vyeo na madaraka serikalini hatimae kugeuzwa kuwa
viongozi wa Chama. Hali hii ilivu- ruga mambo na kuufanya mkono wa kushoto kutojuwa
nini mkono wa kulia unafanya na kinyume cha hivyo. Hapo maamuzi ya kiajabu
ajabu kupitishwa, na mtu kutojuwa nini siasa ya Chama na nini wadhifa wa serikali na
wamtumishi serikalini. Ili mtu aweze kupata- ulwa, hata bila ya kustahiki ilitosha kwa
mfano kujipendekeza na kumtukuza Mwenyekiti wa Chama. Yule aliyepiga makelele
mengi zaidi, ya kumsifu na kumuenzi Mwenyekiti, ndiye aliyezidi kupewa cheo kikubwa
zaidi. Mwenyekiti akalevywa na kutukuzwa huko, na hata kutojali nakutotia maanani
uwezo na ujuzi wa mtu akipewa wadhifa fulani, mradi akimtukuza Mwenyekiti. Kwa
hali hiyo ikawa Mwenyekiti anazungukwa na watu wa “hewallabwana” bila- ya kuthubutu
kumkosoa au kumrekibisha Mwenyekiti. Siasa ya chama chote ikafuata msingi huo huo wa
kutoruhusu wala kustahamili urekibishaji wamawazo au utoaji fikra au makosa. Kasumba
hiyo ikatambaa serikalini hasa kwa vile wakuu wa maidara/jeshi/polisi wote walikuwa
wameshageuzwa wanasiasa. Wakuu hao walijuwa kwamba mradi Chama kilikuwa nyuma
yao, wangeliweza kufanya jambo lolote lililowapendeza bila ya kutarajia kurudiwa au
kuadhibiwa. Hali ya ulanguzi, wizi na unyang’anyi ikawa inapaliliwa serikalini, na kila
kitu kikawa kinahitaji chau chau. Wale waliyoiba na kufanya ulanguzi wakipewauhamisho
au kupewa vyeo vikubwa zaidi sehemu nyengine. Yule aliyekuwa nacho kuzidi kupewa
na masikini ya Mungu kuzidi kunyang’anywa. Wanachama wa CCM walikadiriwa kama
110
millioni mbili, wengi wa hawa kutojiunga na chama hicho kwa hiari zao, bali kwa kutizama
maslahi yao ya kibinafsi , au kwa kulazimishwa, na hakuna mtu anayeweza kuwalaumu,
kwa vile nchi ilikuwa na njaa. Hali kama hii iliwalazimu wanajeshi, polisi na jeshi la
usalama wa siri, pamojana wafanya kazi wengi wa serikali na wale wote waliyotegemea
ama huduma zachama au za serikali. CCM ilikuwa na maofisi na maafisa mbali mbali
bila ya kiasi, wakiwa na vyeo tofauti bila kujulikana hasa kazi na wadhifa wao ni nini.
Hali hii pamoja na utumizi wa vifaa na matumizi tofauti kama vile kusafiri ng’ambo kwa
sababu za “maji kup- wa na maji kujaa” kumekifanya Chama hicho cha CCM, kiwe na
matumizi makubwa mno. Kwa vile CCM ilikuwa haina fedha zake wenyewe, ilibidi fedha
hizo izichote kwenye hazina serikalini, fedha ambazo ni za wananchi wote,yaani hata za
wale millioni ishirini na tano waliyokuwa si wananchama wa CCM. CCM haikuweza wala
kutaka kutafautisha madaraka ya Chama na ya Serikali, kwa hivyo walikuwa wakijitumilia
huduma zote za serikali jinsi walivyotaka wenyewe na kwa vile kulikuwa hakuna chama
cha upinzani, hakuna aliyeweza kulisaili suala hilo. Yule aliyethubutu kuulizia au kuyakemea
mambo kama hayo, ambayo ni hakina halali yake, alijikuta amepumzishwa pahala
maalum, kwa usalama wakemwenyewe. CCM hadi leo, kukiwa na mfumo wa vyama
vingi, imezoweya mtindo huowa kufanya na kujidhani kuwa wao ni Serikali na Dola, na
kufikiri kwamba nchi ni mali ya CCM na hata leo kutoruhusu vyama vya upinzani kutumia
huduma za nchisawa na CCM, mfano kufanya mikutano na matayarisho mengine katika
heka heka za kampeni na kujitayarisha katika uchaguzi ujao. Kuzuwiya uundaji wa NGO
mbalimbali zenye madhumuni ya kukuza maisha ya wananchi wote kwa jumla.
Hali hii ni bayana zaidi Zanzibar hasa kwa vile serikali imeshatambua kwamba haina
uwezo wa kushinda katika uchaguzi ujao, Zanzibar. CCM Zanzibar, bado ina uzoefu wa
kudhani kwambaCCM ndio serikali na ndio yenye uamuzi wa mwisho. Kutoweza kujirek-
111
ibisha na kutambua kwamba sasa kuna mfumo wa vyama vingi, na maana yake ni kwamba
serikali si mali ya chama fulani bali ya vyama vyote na ya nchi nzima. Kwa desturi kile
chama chenye khatamu za utawala kwa muda fulani ni chama chenye dhamana tu ya kuendesha
serikali kwa muda na sio kumiliki serikali kwa milele. Hali ya kuvizuiliya vyama
vya upinzani ruhusa ya kufanya mikutano au kuwachelewechea haki hizo, kuwanyima
kutumia huduma za nchi kama TV na Redio, magazeti huru, ufunguwaji wa matawi n.k.
sio khatuwa zitakazowavunja moyo wananchi bali kuzidi kulipamba moto vugu vugu la
upinzani. Kwani kama vile kila usiku ukizidi giza, asubuhi hupambazuka, ni sawa na kila
ukandamizaji ukizidi, ukombozi kukaribia. Hali ya kukandamiza upinzani hatimae, kwa
desturi, inaleta mapambano makali na kuwapa wananchi muamko wa hali ya juu kabisa.
Viongozi wa CCM wa Zanzibar inafaa waamke na kutambuwa kwamba hakuna njia yoyote
watakayoitumia itakayowafanya washinde katika uchaguzi ujao. Kwa hivyo itakuwa
ni jambo la maana kama wakitafuta njia ya kuungana na Wazanzibari wenzao. Vitisho,
sabotaji, kuvunja haki za kibinaadam, kupinga wimbila demokrasia, kutumia mabavu, kuufumbi
a macho ukweli na kudhani kama haupo, hautawasaidia kitu, bali kuharibu maslahi
ya nchi kwa jumla.
Wakati umefika kwaWazanzibari kwa jumla kukaa pamoja na kutafuta maslahi ya nchi
na sio ya kibinafsi au ya ubinafsi. Zanzibar ina haja kubwa ya kupiga khatuwa mbele na
kuendeleza maisha ya wananchi wake, na haina haja yaNONGWANAUBINAFSI.Wakati
umefika wa Wazanzibari kuunda Baraza jipya la kutunga Sheria mpya na Katiba mpya ya
Zanzibar kwa maslahi ya Wazanzibari wote. Mirengo yote ya kisiasa inafaa iwakilishwe
katika Baraza hilo la muda litakalokuwa namadhumuni ya kuheshimu haki za kibinaadam
na kuje nga misingi mipya yaKidemokrasia.
112
Chapter 6
MFUMO MPYA
6.1 CUF AU ZUF ?
CUF, chama cha wananchi, sehemu ya Zanzibar, ndicho chama kinachotaraji kushinda
kwa kiwango kikubwa Zanzibar katika uchaguzi ujao wa vyama vingi Tanzania. Ingawaje,
CUF si jina halisi la Kizanzibari linalopendeza sana baina ya Wazanzibari wote.
Kukubali kwa CUF na vyama vyengine vya upinzani Zanzibar, kujiunganisha na vyama
vya Tanganyika bila ya kuwa na maslahi ya aina moja na misingi ya kisiasa ipatanayo
na inayoambatana, kumefanya uamuzi huo uonekane kama kuuza heshima ya Uzanzibari.
Kama vyama vya upinzani vya Zanzibar pamoja na wale wanaojiita CCM Zanzibar wangelishikilia
uzi ule ule wa kudai Zanzibar ni nchi huru, taifa huru na dola huru linalostahiki
kuheshimiwa kama taifa, basi bila ya shaka yoyote wangelishinda kuirejeshea Zanzibar
heshima yake . CCM na Nyerere wasingelithubutu kuilazimisha serikali ya Zanzibar kujitoa
katika Jumuiya ya Waislaam na wanasiasa wa Tanganyika wasingeli thubutu kupita
na kutumia lugha ya matusi dhidi yaWazanzibari na viongozi wake. Sababu muhimu mojawapo
ya kufanya Zanzibar kuzidi kutothaminiwa, ni kwa sababu Viongozi wa Serikali
na Viongozi wa Upinzani wa Zanzibar walishindwa kusimama madhubuti na kidete kusisitiza
kwamba walidai vyama vya Kizanzibari, na kama madai yao yasingekubaliwa,
basi wangelidai kwamba vyama vyote vingelikataa kujiandikisha katika uchaguji huo.
Wakosa zaidi, katika suala hili ni CUF, kwani ilikuwa CUF ndiyo iliyotarajiwa kuilazimisha
Serikali ya Zanzibar kuchukuwa khatuwa kama hiyo. Ingawa CUF na Serikali ya
113
Zanzibar zina siasa na malengo tofauti, sehemu zote mbili, bila ya kificho zinataka uhuru
zaidi kutoka Tanganyika. Pindi makundi haya mawili, pamoja na makundi mengine ya
upinzani ya Zanzibar yangelishikilia madai hayo na kutojiandikisha, basi serikali ya CCM
ingelilazimika kuyakubali madai hayo, au kujitayarisha na kulaaniwa ulimwenguni kote.
Kama serikali ya CCM ingeliendelea na kushikilia na njozi za vyama ati vya “kitaifa”
basi ingelikosa misaada ya kiuchumi kutoka kwa wafadhila wao, misaada ambayo Tanzania
Bara isingeliweza kuikosa, wakati Zanzibar kwa miaka na miaka ilikuwa haiitaraji
misaada hiyo iliyokuwa ikiishiya na kumalizikia Tanganyika. CUF, ikiwa Zanzibar na
wafuasi wasiyopunguwa asili mia themanini, iliwajibika nakusisitiza ibaki ZUF, na hata
kama wasingelisajiliwa katika uchaguzi basi nguvuzao hatimae zingezidi kuwa kubwa na
kuifyeka CCM moja kwa moja. Chini ya mwavuli wa ZUF, fikra tofauti za Kizanzibari
zilikuwa zikiwakilishwa, kutetewa, kujadiliwa na kupelekwa mbele. Wazanzibari wengi
hata wale waCCM waliitambuwana kuiheshimu ZUF kwa sababu walijuwa kwamba, ZUF
ikiwakilisha na kutetea Uzanzibari na utaifa wake, wakati huo huo ZUF ikitambulika kama
ni mchanganyikowafikra za kimapambano karibu zaWazanzibari wote, wakiwemo na wale
wanaojiita CCM. Wengi wa Wazanzibari hao wanaojiita CCM, wanafanya hivyo kwa vile
hawanabudi na pindi wangeli kuwa na satwa ya kuchukuwa khatwa zao wenyewe bila
yakuomba ruhusa Dodoma, basi angalau wangelijiita CMZ, yaa- ni Chama Cha Mapinduzi
cha Zanzibar, baadala ya CCM. ZUF kukubali kujiita CUF ilikuwa nimakosa, kwani
sasa CUF inatambulika kama chama cha siasa cha Tanzania wakati,ZUF haikutambulika
kama ni chama kimoja tu bali vyama tofauti vya Kizanzibari vilivyokuwa vikipigania
maslahi ya Zanzibar. Pindi ZUF ingeliendelea kuwa kamaZUF, basi bado ungelikuweko
uwezekano wa vyama vyote na fikra zote za Kizanzibari kuwa chini ya mwavuli mmoja.
Hali hii ingeliiwezesha Zanzibar hatakuweza kuwa na serikali moja ya Taifa ikiwakilisha
114
vyama, fikra na misingi tofautikwa maslahi ya Zanzibar yote kwa jumla na kuepusha
mgogoro wa leo wa kupiganiana kung’ang’ania Kiti cha Urais, kwani katika serikali hiyo
wangelikuwemo Afro-shirazi na CCM Zanzibar vile vile. Viongozi wa ZUF walidhani
kwamba njia pekee na ya urahisi ya kuipatia Zanzibar utaifa wake ni kukamata khatamu za
serikali na kutarajia kwamba mambo yatakaa sawa wenyewe baadae. Kwa bahati mbaya,
hali hii haionekani kuwa inamkinika. ZUF ilikuwa sio chama kimoja tu cha kisiasa, bali
ni muungano wa mikondo ya fikra mbali mbali; fikra ambazo zilitiliwa mkazo na dai la
“Kura ya maoni” . Leo kura ya maoni hatuisikii tena. Mbele kuna khatari fulani inakuja
na hatuna tena ZUF yakutulinda na khatari hiyo; na kama hatujatahadhari mapema, itapita
miaka thelathini mengine bila ya kupata uhuru wetu.
Lengo la baadhi ya Viongozi wa CUF leo ni kukamata khatamu za serikali, na- kwamba
wao pekee ndio wenye haki ya kuiongoza Zanzibar. Baadhi ya viongozi hao wanasahau
vipi wao wameweza kupata nafasi ya kuwa viongozi, wamesahau kwamba roho mbichi
za watu zime toka, wamesahau kwamba watu wameteseka na kuteswa kadri kiasi hata
leo tukafika tulipo fika. Kuna baadhi ya viongozi wa CUF wanahitaji wajisomeshe kisiasa
kabla hawajaanza kutaka kuwafundisha wengine siasa, hasa wanachohitaji ni kukariri
historia ya kisiasa ya Zanzibar ya tokea 1964.Kati ya Viongozi hao wachache katika uongozi
wa CUF wasiote kwamba, CUF ikishashika serikali, wao watakuwa mabwana au
kwamba CUF pekee au viongozi wa CUF pekee ndio watakaokuwa na haki ya uamuzi
wa mwisho wa mambo ya visiwa vyetu. CUF lazima iwaelimishe baadhi ya viongozi
wake tokea hivi sasa kwamba,Wazanzibari hawataki siasa ya chama kimoja kwa sababu
wanapinga CCM tu. Hata sivyo hivyo, kile wanachokipinga Wazanzibari ni mfumo wa
ki- dikteta na wa chama kimoja, na kupinga huko ni kwa kimsingi, yaani hata itapokuwa
CUF ina khatamuza serikali Zanzibar, patatakiwa lazima pawepo vyama vya upinzani
115
na kidemokrasia- kwa jumla. Wadhifa wa kuijenga Zanzibar mpya umo katika viganja
vya mikono vya Wazanzibari wote kwa jumla. Uongozi wa nchi vile vile ni wadhifawa
Wazanzibari wote wenye uwezo na waliyokuwa tayari kuitumikia nchi kwamaslahi ya
nchi na sio maslahi ya ubinafsi. CUF inawajib wa kuhakikisha kwamba wale viongozi
wenye sifa za kudhani ni wao tu wenye haki ya kuongoza Zanzibar,wanachujwa tokea
leo na wasipewe nafasi za hatimae kuleta tena rushwa, ulanguzi,wizi, unyanganyi ubinafsi
na udikteta. CUF inatarajiwa isome kutoka na makosa ya Hizbu ya kusahau kwamba
ASP na- Umma Party vilikuwa ni vyama vya upinzani ambavyo ililazim vitambuliwe navihishimiwe.
Vile vile iepuke makosa ya Hizbu ya kukana kujitayarisha ku- unda serikali
ya Kitaifa na kutokubali kujiandaa kwa siku za mbele pindi chama hicho kingelishindwa
katika uchaguzi na hatimae kuwa chama cha upinzani. CUF vile vile inawajibika kuepuka
makosa ya ASPya kuufyeka upinzani wa ndani na wa nje ya chama, na kuwauwa wanasiasa
wapinzani, wakisahau kwamba na wao wakati fulani walikuwa wapinzani. CUF lazima
iepuke makosa ya UMMA PARTI yakulinyamazia Baraza la Mapinduzi na kutochukuwa
hatuwa mpaka maji yalipomwagika na kujikusanya wao wenyewe tu. CUF lazima ilaani
uuwaji wa Wazanzibari wote na sio Wazanzibari fulani tu. CUF inatakiwa iepuke siasa
ya Baraza la Mapinduzi la kuwafukuza wazalia wa nchi kwa sababu wa likuwa na fikra
tofauti za kisiasa, kuwageuza Wazanzibari hao wakimbizi ilhali nchi yao ikiwahitaji,na
wakati huo huo kuwafukuza kazi na kuwanyanganya mali zao. Hivi ni vitendo vilivyo
dhidi ya haki za kibinaadam na ambavyo lazima vipigwe vita, kwani kila mwananchi ana
haki ya kuwa na fikra huru na kufuata mkondo atakao. CUF ikipata khatamu za serikali
inafaa ipendekeze uanzishaji wa kuruhusu Uraiya wa nchi mbili kwa wale Wazanzibari
waliyolazimika kuchukuwa uraiya wa nchi nyengine. Vile vile CUF inalazimika iepuke
siasa ya CCM ya kukaa Dodoma na kuugubika Umma wa Kizanzibari naWakitanganyika
116
utawala wao bila ya kuwashauri au kuwashirikisha katika kutawala nchi zao na kuwanyima
kila haki ya kushiriki katika ujenzi wa nchi zao. CUF lazima tokea mapema iwaelimishe
wazi wale viongozi dhaifu kwamba madai ya demokrasia na ya kuheshimu haki za kibinaadam
hayatasita baada ya serikali yachama kimoja cha CUF kupatikana, bali kwamba
CUF itahakikisha kutekelezwa kwamfumo wa vyama vingi, kutekelezwa kwa malengo ya
demokrasia na kuheshimiwakwa haki za kibinaadam, na sio kwamba CUF ikipata serikali
basi haya mambo yatasahaulika. Ikiwa CUF itashindwa kuyatekeleza malengo hayo basi
kuna haja muhimu na ya haraka ya kuifufuwa na kuiimarisha ZUF.
6.2 Vyama vya Upinzani vya Tanganyika
Vile vyama vya upinzani vya huko Tanganyika vinatakiwa vipewe haki za kidemokrasia
za kikamilifu bila ya kuwekewa vikwazo vyovyote, vya siri au vya kidhahiri. Kwa vile
misingi ya kisiasa, ya kitamaduni, ya kiuchumi na ya kijamii ya Tanganyika na ya Zanzibar
inatafautiana, lazima mazingara ya vyama vya nchi mbili hizo vitafautiane. Ni kinyume
na muelekeo wowote wa kisiasa kuwatarajiaWatanganyika waweze kuanzisha chama cha
kisiasa Zanzibar, kuweza kujuwa shida za Wazanzibari na kuweza kuzitetea shida hizo
vilivyo. Kwa minttaraf ya mantiki za kisiasa ya kinadharia na ya kitendaji, ni kinyume
kabisa na uzoefu wa kisiasa wa kidemokrasia ambayo ina msingi wa kihalali, kulazimisha
vyama vyenye misingi yao huko Tanganyika kutafuta wafuasi Zanzibar katika dakika za
mwisho za kampeni ya uchaguzi. Ikiwa CCM (pamoja na vyama mama vilivyoizaa)
kwa muda wa miaka thelathini imeshindwa kupata zaidi ya asilimia kumi na tano ya
wapigaji kura wa Zanzibar wa leo, na asilimia kumi ya wa Bara, vipi itatarajia chama
117
kipya cha Tanganyika kuwa na uwezo huo kwa muda mfupi sana. Vyama vya Tanganyika
vinatakiwa vidai kwamba, kama CCM itashikilia msimamo huo, basi Zanzibar iwe na
majimbo na wagombaniaji uchaguzi sawa na wale wa Tanganyika, yaani kama Tanganyika
kuna watetezi 100 na Zanzibar kuwe na watetezi 100, katika Bunge lawajumbe 200 na
chama chochote ambacho kitashinda kwa asili mia kubwa zaidi katika nchi moja wapo ama
pekee au kikiungana na vyama nyengine, kiwe na hakiya kuendesha serikali ya Tanzania
nzima, yaani kama CUF itapata asili mia 80 au zaidi Zanzibar na CCM asili mia 60
Tanganyika, basi CUF ndio itakiwe kuendesha serikali ya Tanzania nzima. Kwa vile CUF
inatarajiwa kushinda Zanzibar zaidi ya asilimia themanini, kwa urahisi inaweza kuongoza
serikali hasa ikiunganisha viti vyake na vile vyama vingine vya Tanganyika. Kwa njia
kama hiyo Bunge na serikali itayofuatia inaweza kubadilisha sheria na kuweza kuanzisha
usajili mpya wa vyama wa kihalali na uondoshaji wa sheria na kanuni potofu za hivi sasa
ambazo zimebuniwa na Nyerere peke yake.
Vyama vya kitaifa vya Kitanganyika na vya kitaifa la Kizanzibari vinatakiwa kuwa na
uwezo wa kujiamualiya wenyewe na kuwa na uhuru wa kusimamisha watetezi wauchaguzi
sehemu zile wazitakazo. Kama vyama vya Tanganyika vitaamua kusimamisha watetezi
wa uchaguzi sehemu ya Tanganyika pekee waweze kufanya hivyo, na kama watapendelea
kusimamisha mjumbe au wajumbe Zanzibar, iwe wenyewe ndio watakao amuwa na sio
kulazimishwa. Vyama vya Zanzibar navyo viwe na haki kama hiyo. Katika nchi za
kidemokrasia vyama vya kisiasa vina haki yakusimamisha au kutosimamisha watetezi
katika jimbo lolote bila ya kulazimishwa na mtu yeyote. Watanganyika kama walivyo
Wazanzibari wana haki kamili za kujiamulimambo yao wenyewe.
118
6.3 Matarajio ya Mzanzibari
Matarajio ya Mzanzibari ni kupata ulinzi kamiliwauhuru wake kamili, kupata kuheshimiwa
kwa haki za kibinaadam kama zilivyodaiwa katika Tangazo la Haki za Kibinaadam la
Umoja wa Mataifa la 1949, ambalo linatetea:
uhuru, heshima na haki sawa
kupinga ubaguzi wa kikabila, rangi, uume au uke, lugha, dini, wa fikra tofauti, asili,
kitaifa, kijamii, mali, wa jinsi ya mtu au msimamo mwengine wa kijamii.
linatetea haki ya maisha, uhuru na usalama wa nafsi ya mtu kupinga utumwa wa aina
yoyote
kupinga kuadhibiwa au kufanyiwa mtu ukatili
inatetea kutambuliwa mtu kisheria ulimwenguni kote
watu wote kuwa sawa mbele ya sheria
kutetewa kwa mtu na sheria kwa mujib wa katiba/sheria
mtu asikamatwe bure, kuwekwa kizuizini au kufukuzwa kazi au nchi
kila mtu ana haki kwa kupitia mahkama huru kushughulikiwa kihalali na hadharani
kuhusu shtaka lolote dhidi yake – mshtakiwa hana makosa mpaka kosa lake lithibitishwe
na mahkama halali na ya hadhara akiwa amepewa haki za utetezi kamili mtu hana kosa
kisheria ikiwa kitendo hicho alikifanya kabla ya sheria hiyo kutungwa
mtu alindiwe haki zake za kibinafsi pamoja na maandishi ya barua zake , heshma, staha
na haki zake zilindwe kisheria
mtu ni huru kwenda na kuishi atakako
mtu ana haki ya kuhama na kurejea nchi yoyote
mtu ana haki ya kuomba ukumbizi
119
haki hiyo asiweze kunyang’anywa kwa makosa ambayo si ya kisiasa
watu wote wana haki ya kuwa na uraiya
mtu asinyang’anywe uraiya kwa maonevu au kukataliwa haki ya kubadilisha uraiya
watu wenye umri wa kujitegemea wana haki za ndoa na ya kuanzisha ukoo na kuwa
na haki ya kuingia harusi
jamii inawajibika kulinda ukoo
kila mtu ana haki ya kumiliki rasilmali
mtu asinyang’anywe mali bila ya sababu
mtu ana haki ya kuwa na fikra huru, muamko, dini au imani huru
kila mtu ana haki ya kuwa na uhuru wa fikra na wa kujieleza, kuwa na uhuru wa
haki hizo bila ya kuingiliwa kati, kadhalika kuwa na haki ya kutafuta, kupokea na kutoa
habari/fikra kupitia chombo chochote cha habari bila ya kujali mipaka ya nchi
kila mtu kwa usalama ana haki huru ya kufanya mikutano na kuunda chama
mtu yeyote asilazimishwe kujiunga na chama fulani
mtu ana haki ya kuweza kushiriki katika Serikali ya nchi yake au kwa kupitia njia ya
mtetezi wake aliyechaguliwa katika uchaguzi halali
kila mtu ana haki sawa katika huduma za kiserikali za nchi yake
Matakwa ya umma ndio yawe msingi wa uongozi wa serikali, kwa kupitia uchaguzi wa
halali wa majira, wenye kanuni za kidesturi, pakiwa na haki sawa za kupiga kura; uchaguzi
wenyewe uwe wa siri na huru.
kila mtu ana haki ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni
kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi, kuwa na haki halali za kufanya kazi
na kulindwa na ukosefu wa kazi
kila mtu ana haki ya kupata mshahara sawa kwa kazi sawa
120
mfanya kazi ana haki ya kupata mshahara halali na wakutosha, kuhakiki sha maisha
yake na ya ukoo wake, kwa mujib wa thamani na heshima ya kibinaadam, kupandishiwa
mshahara inapomkinika
kila mtu ana haki ya kuunda na kujiunga na umoja wa wafanya kazi kuhifadhi maslahi
ya kazi yake
kila mtu ana haki ya mapumziko, kujistarehesha, kuwa na kiwango maalum cha saa za
kazi na kupata malipo katika likizo
kila mtu ana haki za lazima kama vile chakula, mavazi, nyumba, matibabu na huduma
nyengine za jamii, kama vile akiwa mgonjwa, kizuka, mzee au kutoweza kujitazama nafsi
yake
Mzazi na mtoto mchanga wachungwe na watizamwe
kila mtu ana haki ya elimu huru tofauti
elimu irekibishwe kuendeleza utu
kila mtu ana haki huru ya kushiriki katika utamaduni wa jamii, kunufaika na sanaa na
sayansi
kila mtu ana haki ya himaya kutokana na maandishi yake yote yakiwemo ya kisayansi
au kisanifu
kila mtu ana haki ya kufaidika na Tangazo hili
kila mtu anawajibika kwa jamii ambayo hatimae itamhakikishiya utu wake
kila mtu ana wajib wa kutekeleza sheria halali yenye msingi wa kidemokrasia uhuru
na haki hizi uepukwe kutumiwa dhidi ya maazimio na msingi wa Umoja wa Mataifa
ni kharamu kwa nchi, kikundi au mtu yoyote kutumilia kifungu chochote katika
Tangazo hili kuvunja haki au uhuru kama ilivyotajwa
121
Katika mkutano wa haki za Kibinaadam wa Umoja wa Mataifa huko Viena, Austria,katika
mwaka 1993 mambo yafuatayo yalisititizwa:
Usawa, heshima na kustahamiliana
kulaani ukabila, ubaguzi wa kikabila, chuki ya wageni na tabia nyengine ya kutostahamiliana
Kuheshimu haki za watu wa mataifa madogo, wenyeji asilia (indegenous – people)
makabila madogo madogo, dini au lugha tofauti
kulinda haki za wafanya kazi wa kigeni
haki za sawa sawa na haki sawa za kibinaadam kwa wanawake
kuhifadhiwa kwa haki za watoto (kutumiliwa kisiasa na kuharibiwa mais- ha yao kwa
sababu ya matumizi ya madawa (unga) ya kulevya)
kuepusha mateso ya utesaji na kuwashitaki wale wanaoshiriki katika uo- vu huo
kukomesha sheria ya kuweka watu vizuizini
kukomesha kupotezwa/kutoweshwa kwa watu (wanasiasa/wapinzani)
Upungufu wa utekelezaji misingi hiyo uchunguzwe na kujulishwa Center ya Haki za
Binaadam, New York, Umoja wa Mataifa.
Ulinzi wa haki za kibinaadam ni jambo la lazima na inatarajiwa wakati CUF itapopata
khatamu za utawala itaanzisha usomeshaji wa haki za kibinaadam hizi maskulini na sehemu
zote zinazotowa huduma ya jamii pamoja na katika Redio na Televisheni.
6.4 Demokrasia
Kukubaliwa kwa uanzishaji wa vyama vingi nchini ni moja tu katika misingi yakutekeleza
demokrasia. Kwa mujib wa hali ilivyo Tanzania, hasa Zanzibar , hata suala hili hali-
122
jatekelezwa kikamilifu, kwani vyama vya upinzani ha- vipewi haki sawana Chama cha
CCM, na CCM bado ina uzoefu wa kujifanya kama ni serikali badalaya kuwa ni chama.
Kwa hivyo vyama vya upinzani si vyama vyenye uhuru wakuendesha kazi zao huru, wala
kuwa na uhuru wa kuamua jina la chama chao auchama hicho kiwakilishe taifa gani.
Mfumo wa vyama vingi wa Tanzania hauheshimu misingi ya Haki za kibinaadam na
Kidemokrasia. Zanzibar panahitajika utekelezaji wa misingi wa vyama huru vya kisiasa
vyen- yemisingi halali ya kidemikrasia.
Upinzani unatakiwa upewe haki zote za kidemokrasia za kuweza kufanya kazi hurbila
ya kuingiliwa kati na wafuasi wake kutopatishwa taabu na kufukuzwa kazi kwa sababu ya
fikra zao. Zanzibar kunatakiwa kuwe na uwezekano wa kufanya mikutano huru nchini kote
, kaskazini, kusini, mashariki na magharibi. Utoaji waruhusa hizo uwe chini ya mikono
ya idara isiyo pendelea na sio vyama hivyo kucheleweshwa cheleweshwa wanapodai haki
zao. Upinzani uwe na uandishi na utangazaji wa habari huru kwa kutumia vyombo vyao
wenyewe pamoja na vyombo vya dola. Upinzani uhakikishiwe kuweko kwa uchaguzi huru
utakaoangaliwa na wachunguzi kutoka Umoja wa Mataifa na upinzani ushirikishwe katika
tume ya kupanga nakutekeleza uchaguzi. Upinzani lazima kushirikishwa katika Baraza la
utungaji wa katiba na utungaji washeria mpya za Zanzibar. Upinzani upewe haki katika
huduma mbali mbali za kitaifa . Upinzani ushirikishwe katika madaraka tofauti serikalini.
Upinzani ushirikishwe katika kuanzisha mipango ya Mahkama huru. Upinzani uwe na
uhuru wa kuunda vyama vyenye utaifa au jina walitakalo. Upinzani ishirikishwe katika
mazungumzo ya kuirejeshea Zanzibar kiti chake katika Umoja wa Mataifa. Upinzani
uruhusiwe kufanya maandamano na kugoma . Upinzani uruhusiwe kuunda vyama vya
wafanyakazi. Upinzani uwe na haki ya kuunda vyama vya wanawake. Upinzani uwe na
haki ya kuunda vyama vya vijana. Upinzani na wananchi wa kawaida wawe na haki ya
123
kuunda NGO tofauti.
Ili kuhakikisha maisha bora ya Mzanzibari, kuishi kwa usalama na amani,kuheshimu
maisha na haki za binaadam za kila Mzanzibari, kumhakikishia kila Mzanzibari haki zote
za kihalali za kidemokrasia, pana wajib mkubwa sana kwa wanasiasa wote wa Kizanzibari
kutizama na kulinda maslahi yaWazanzibari wote kwa jumla bila ya kujali chama wakifuatacho.
Kwa hivyo viongozi wote wa kisiasa lazima wasahau tofauti zao na kuungana na
kutizama maslahi ya nchi nzima. ASP,CCM(ZNZ), Um- ma Parti, ZNP na ZPPP lazima
watambuwe kwamba wanawajib mkubwa sana kwa nchi yao na vizazi vyao, na bila ya
kuungana watu wataendeleakuangamizana na nchi kuselelea nyuma milele. CUF ni chama
pekee kinachowakilisha mirengo yote hiyo tofauti Zanzibar. Kwa hivyo itakuwa jambo
lamaana ikiwa viongozi wa ASP, CCM (ZNZ), Umma Party, ZNP na ZPPP wote wataingia
katika CUF kuendeleza maslahi ya Zanzibar na CUF wenyewe kabla hawajaungwa mkono na vyama hivyo lazima wakubali kujibadilisha jina na kujiita ZUF na wakati huo huo
kuwahakikishia uongozi wa juu wakuu wa vyama vyote hivyo vitakavyojiunga nao.
124

2 thoughts on “Zanzibar: Nchi, Dola na Taifa Huru”

  1. Link exchange is nothing else however it is simply placing the other person’s website link on your page at proper place
    and other person will also do similar in favor of you.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.