Wazee wetu, Ndugu zetu,

Assalaam Alaaykum,

UMOJA, UHURU, UADILIFU

Qauli ya Umoja wa Wazalendo Kukhusu

Msiba wa Kuzama Meli hapo Bandarini

Malindi, Zanzibar; taarikhi 29.05.09.

Umoja wa Wazalendo, una wingi wa huzni kwa msiba uliotokea usiku wa jana, taarikhi 29 May, 2009; kwa kuzama meli hapo bandarini Malindi na kusababisha vifo, kupotea mali na kusababisha mashaka kwa abiria na kila aliekuwepo wakati huo. Haya ni maqadiri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala, linaloandikwa halizuiliki kutokea; bali lina sababu.

Hapana shaka huu ni msiba wetu sote, msiba wa kila Mzanzibari, ni msiba wa kila Muumini na kila binaadamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala awaghufirie makosa yao marehemu wetu, awalaze mahali pema, awatie Peponi kwa Rehma Zake, wao na jamii ya Waumini; na awazidishie subira na mapenzi wafiwa wote, Aamyn.

Huu ndio mwisho wetu sote, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala atujaalie mwisho mwema, sisi na jamii ya Waumini; Aamyn.

Mkono wetu wa taáazia tunaupeleka kwa Rais wa Zanzibar, Mhishimiwa Rais Aman Abeid Aman, Sirikali ya Zanzibar na wananchi wa Zanzibar kwa jumla.

إنّا لله و إنّا إليه راجعون

Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala awajaalie marehemu wetu hawa ni miongoni mwa Mashahidi, Aamyn.

Wa Billahi Tawfiiq

Umoja wa Wazalendo

Zanzibar

May 30, 2009

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.