MAAZIMIO YA MUWAZA KATIKA MKUTANO WA TAREHE 25.04.2009 JIJINI LONDON INATANGAZA
MGOGORO WA KISIASA WA ZANZIBAR
Na kutamka kwamba ni ukweli usiopingika kwamba Tarehe 12.01.1964 Chama cha ASP kiliipindua Serikali ya ZNP na ZPPP
Na kutamka kwamba Tarehe 26.04.1964 Chama cha TANU kiliipindua Serikali ya ASP Zanzibar
Na kwamba tarehe hiyo hiyo ya 26.06.1964 Serkali ya Tanganyika iliipindua na kuiondoa Nchi ya Zanzibar
KWA HIVYO MUWAZA UNATANGAZA KWAMBA KITAIFA NA KIMATAIFA :
ZANZIBAR NI DOLA, TAIFA NA NCHI HURU SAWA NA NCHI YA TANGANYIKA
Rais wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume ni Rais Sawa na Rais wa Tanganyika Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ni sawa na Waziri Mkuu wa Tanganyika Mhe. Mizegwe Pinda
Serikali ya Zanzibar ina hadhi sawa na serikali ya Tanganyika ijulikanayo kama Serikali ya Muungano
Baraza la Mawaziri la Serikali ya Zanzibar ni sawa na Baraza la Mawaziri la Serikali ya Tanganyika liulikano kama Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano
Baraza la Wawakailishi la Zanzibar ni sawa na Bunge la Tanganyika lijulikano kama ni Bunge la Muungano
Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni sawa na Wabunge wa Bunge la Tanganyika wajulikanao kama Wabunge wa Muungano
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni sawa na Spika wa Bunge la Tanganyika
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ni sawa na Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika
Mahakama Kuu ya Zanzibar ni sawa na Makahama Kuu ya Tangangika
MUWAZA inadai kwamba Baraza la Wawakilishi libadilishe Katiba ya Zanzibar na iwe na nguvu sawa na Katiba ya Tanganyika (Muungano)
MUWAZA inapendekeza kwamba Serikali ya Zanzibar na BLW wapeleke maombi kwenye Umoja wa Mataifa kukidai Kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa
MUWAZA inapendekeza kwamba Zanzibar ijiunge na Mashirika ya Kimataifa kwa maslahi ya Zanzibar
MUWAZA inapendekeza Zanzibar iwe na vyama vyake vya Kisiasa vyenye sifa huru za kitaifa na kimataifa
MUWAZA inapendekeza kwamba Serikali ya Zanzibar na Baraza la Wawakilishi wapitishe sheria ya kulinda mali asili yote ya Zanzibar yakiwemo na Mafuta ya Zanzibar yawe chini ya Zanzibar
MUWAZA inapendekeza kudaiwa kwa Serikali tatu
MUWAZA inapendekeza kwamba Serikali na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar waitishe Kura ya Maoni ya Wazanzibari kuwapa Wazanzibari fursa ya kuyakubali au kuyakataa Mapendekezo ya hapo Juu.
Kwa niaba ya MUWAZA
Dr. Yussuf S. Salim – Mwenyekiti

3 thoughts on “Maazimio ya MUWAZA juu ya hadhi ya Zanzibar”

  1. tatizo kubwa kuwa waunguja ni 2 face, ikiwa mutakua kitu kimoja na kisiwa chapili hakiyenu inshalah kwa uwezo wa mungu mutafanikiwa.

  2. nionavyo mimi na ndivyo ilivyo na ukweli usio pingika kwamba huwezi kuida i zanzibar ndani ya chama tawala ………….maoni yangu.wazanzibari xote kwa ujumla waungane na wapinzani ili kuidai nchi yao.

  3. hiivi tutakua tukijihangaisha kwa kuandika makaratasi na kuitisha makongamano mpaka lini? kwa sababu kwanza viongozi wetu walioko madarakani wao ndio walosababisha sisi kufikishwa hapa tulipo,kwa kuthibitisha haya tangu imetangazwa hadharani kwamba zanzibar sio nchi ni kiongozi gani alofunua domo lake angalau kulalamika? zaidi ya wananchi wa kawaida,mimi naona ipo haja ya kupita njia ya mkato nukta. tumechokaaaa

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.