RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA
HESABU ZA SERIKALI NA MASHIRIKA (PAC) KWA MWAKA 2008/2009

UTANGULIZI

Mhe. Spika

Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kusimama katika baraza lako tukufu nikiwa naafya njema,pia kukushukuru wewe mhe spika kwa kunipa fursa hii ya kutoa maoni ya Kamati ya Kuchunguza hesabu za Serikali na mashirika ya Umma.

Mhe. Spika

Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa waheshimiwa wajumbe wa Kamati hii kwa imani walionionyesha kwa kunipendekeza na baadae kunichagua kuwa mwenyekiti wa kamati hii, Naahidi kutumia maarifa juhudi ,na uawezo alionijalia Allha katika kutekeleaza majukumu yanayonikabili kwa mashirikiano na wajumbe wote.

Mhe Spika
Kwa mwaka huu wa fedha 2008/2009 tunathamini juhudi za baraza na za Serikali kwa ujumla kwa kutimiza ahadi yake kwa kuiwezesha kamati hii kuweza kutekeleza kazi zake kwa kushughulikia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuanzia mwaka 2004/05/2005/06 na 2007/07 kwa pamoja .

Mhe Spika,

Kazi hii haikuwa nyepesi hasa ukizingatia muda tuliopangiwa kuvifanyia kazi vitabu vyote vya miaka mitatu kwa kipindi kifupi.

Mhe Spika,

Washiriki wa Maendeleo ,Benk ya Dunia Word Bank” waliahidi kuzipa kamati ya PAC na kamati ya fedha na uchumi jumla ya Tsh milioni 200 kwa mwaka wa fedha 2008/2009 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake na pia kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hiyo

Mhe Spika,

Ahadi hiyo haikutekelezwa na badala yake kusababisha kutokuelewana kati ya baraza na Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali. Ni vyema kutambua kuwa uwajibikaji katika matumizi ya mali ni nyenzo muhimun kwa utawala bora na maendeleo, kamati inapendekeza kuwa baraza la Wawakilishi na Serikali zione umuhimu wa kuwaongezea wajumbe wa kamati hii na Sekretariati yake uwezo wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo,bila ya kutegemea wafadhili.

Mhe Spika ,

Taarifa inayokusudia kutoa muhtasari wa ripotio ya PAC kwa mwaka 2008/09 ambapo ufafanuzi zaidi unapatikana katika kitabu cha ripoti za kamati za kudumu za Baraza la wawakilishi ukurasa wa 31 hadi 50 maelezo yaliyomo katika muhtasari huu yanagusia mapiti ya majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa miaka 2004/05,2005./06na 2006/07.

Mhe Spika ,

Mambop muhimu yanayozingatiwa na kamati katika mapitio ya hoja za Mkaguzi,Uchumi na tathmini za hesabu za Serikali za mashirika ya umma ni kutaka kuona kuwa .

Sheria za fedha Nam 8 ya mwaka 2005 na sheria ya manunuzi ya umma nam 9 ya mwaka 2005 pamoja na kanuni zake zinafuatwa kikamilifu.

Uadilifu uaminifu wa taratibu za uwekaji wa kumbukumbu za mahesabu ya fedha unafuatwa..
Katika hayo matumizi yanafuatwa kwa kuzingatia bajet na madhumuni yaliyokubaliwa na Baraza.

Matumizi hayo kuona kwamba thamani inapatikana kwa fedha inayotumika (volue for money) katika huduma zinazotolewa kwa jamii.

Wasiofuata sheria na taratibu za usimamizi wa fedha wanawajibishwa na kwamba hatimae sekta ya umma inatekeleza na kuendeleza uwezo katika usimamizi wa shughuli za kifedha pamoja na maadili ya utawala Bora.

Mhe Spika ,

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na Kamati ya kuchunguza kudhibiti hesabu za Serikali na Mashirika katika Wizara ,Idara Mashirika na taasisi mbali mbali za Serikali yafuatayo yamebainika :-

Kuna baadhi ya hoja hazikuweza kujibika kutokana na kukosekana kwa vielelezo mbali mbali vinavyohusiana na hoja hizo, hoja hizi zinatokana na kutorejeshwa kwa masurufu,kutokupatikana na risiti baada ya kutoa huduma au kufanya malipo .vifaa mbali mbali vilivyonunuliwa ambavyo havikurekodiwa katika madaftari ya kutunzia vifaa vya ghalani, mikataba inayoendelea kutumika huku ikiwa imeshamaliza muda wake, hati za malipo zilizokosekana kwa ukaguzi na madeni ya muda mrefu wanayodai wizara za taasisis mbali mbali kwa watu binafsi . Hali hii inaashiria kwa namna moja au nyengine kuwa ni upotevu wa fedha ulio dhahir kama inavyojionesha katika kitabu cha ripoti yetu .

Mhe Spika ,

Kamati yangu inaamini kuwa hoja zote zinazohusiana na vifaa ambavyo havikuingizwa ndani ya daftari na hati zilizokosekana kwa ukaguzi sio vitendo vya bahati mbaya ila ni upotevu wa mali za serikali unaotokana na udanganyifu wa baadhi ya watendaji.

Kwa mfano kamati imechunguza hoja ya Mdhibiti inayohusiana na matumizi ya yasiyo na vielelezo vyenye kuthibitisha matumizi hayo ya tsh 151 milioni katika afisi ya mrugenzi wa Vitambulisho vya Mzanzibari ambapo licha ya kutopata mashirikiano juu ya majibu ya hoja hiyo lakini pia kamati imethibitisha upotevu wa mamilioni ya fedha za Wazanzibari,Kamati inapendekeza hatua za kiuwajibikaji zichukuliwe kwa taasisi hiyo .

Mhe Spika ,

Ukaguzi wa kamati umebaini kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa taratibu za na udhibiti wa fedha na mali za Serikali sheria zilizopo hazifuatwi ipasavyo na kupelekea upotaevu mkubwa wa mali na fedha za Serikali rasilimali nyingi za Serikali katika Mawizara na Taasisi za Serikali hazijawekewa kumbukumbu karibu .
Wizara na taasisi zote zilizokaguliwa na kamati ya PAC hazikuwa na madaftari ya kuwekea kumbu kumbu za mali wanazozimiliki yaani “assets register” Vile vile kamati imegundua kuwa kuna idadi kubwa ya thamani ya magari mashamba na majengo ya serikali hayajafanyiwa tathmini na kuelezwa thamani yake ili serikali ifahamu mali zake.

Mhe Spika,

Kamati imesikitishwa sana na kauli ya Wizara ya Kilimo kwamba shamba la Wizara ya Kilimo la Mziwanda Micheweni ambalo lilikuwa ni kituo cha majaribio ya mbegu kwa ajili ya ukulima wa maweni kuhaulishwa kwa mtu binafsi kwa kile kilichoelezwa na Wizara kuwa KUAZIMWA tu.

Mhe spika
Kwa nchi inayoheshimu utawala bora,hili halikubaliki na kamati inaagiza haraka uazimwaji huo wa mali ya Serikali kwa mtu binafsi usitishwe mara moja, ili majaribio ya mbegu kwa ajili ya ukanda wa Micheweni ambao kila mara hukumbwa na njaa uweze kuendelea kuimarishwa.

Mhe Spika,

Kamati pia inahoji uhalali wa uvamizi wa Mashamba ya Serikali unaohalalishwa na Serikali kwa kumilikishwa watu binafsi kinyemela kama ilivyofanywa katika kituo cha kilimo kiliopo Weni, Pemba ambapo eneo la Shamba la Serikali lilikatwa viwanja na kupewa watu binafsi.

Mhe Spika ,

Ili kuepusha mapungufu ya matumizi mabaya ya rasilimali za Umma ,kamati inapendekeza Idara ya Uhakiki Mali kushirikiana na Taasisi za Serikali ili kuhakikisha kwamba juhudi za makusudi na za haraka zinachukuliwa ili mali za Serikali zitambuliwe zithaminiwe na kuekewa kumbu kumbu ili ziweze kudhibitiwa ,kufanikiwa kwa haya pia yatasaidia kuongeza ubora wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.

Mhe Spika ,

Kutokuwepo kwa kumbukumbu muhimu za mali za Serikali (assets ) ni kwenda kinyume na matakwa ya sheria ya Fedha ,Aidha kutokuwepo alama za kutambulisha za thamani na kutokuwepo kwa madaftari ya kuwekea kumbukumbu za mali za afisi ni udhaifu mwengine unaopelekea kukosekana ufanisi wa utumiaji wa mali za Samani za Serikali.

Mhe Spika
Ukaguzi umegundua kuna baadhi ya wizara na Taasisi za Serikali na Mashirika wanachelewa kuwasilisha hesabu zao ktiak Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali. Kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya fedha Nam 8 ya mwaka 2005 kifungu cha 24 (2) kimeeleza wajibu wa taasisi za Seriikali kuwasilisha heasabu za mwisho wa mwaka katika Afisi ya mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu katia kipindi cha miezi mitatu baada ya kumaliza mwaka wa fed.

Hivyo uwasilishaji usizidi tarehe 30 Septemba .hali hiyo husababisha Afisi ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali kushindwa kufanya tathmini ya taasisi hizo na kuwa na mapungufu ndani ya ripoti yao .kamati inapendekeza kwamba sheria zitumike ili kuwabana wale wote wanaochelewesha mahesabu hayo bila ya sababu za msingi.

Mhe Spika ,
Kamati imegundua kumbu kumbu za mrundiko wa madeni ya siku nyingi baina ya Wizara kwa Wizara au Taasisi za Serikali na watu binafsi.Pamopja na marundiko wa madeni Kamati imeshindwa kuona juhusdi zinazofanywa na wahusika kuyadai madeni hayo.
Watendaji hao huweka rekodi za madeni hayo ndani ya makaratasi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kisheria ya kuzidai fedha hizo za Serikali ,baada ya muda Watendaji hupoteza kumbu kumbu za madeni hayo, wanaodaiwa husahaulika na matokeo yake inakuwa ni upotevu wa fedha za Serikali .Baadhi ya Taasisi wanafikia hatua ya kuyafuta madeni hayo kwa kupeleka waraka katika bodi zao au Kamati tendaji za Taasisi na kuyafuta madeni kienyaeji.

Huu ni utaratibu mbovu ambapo kamati yangu haikubaliani na utaratibu huo na tunasisitiza kufuatwa kwa taratibu nasheria ya fedha katika kuyafuta madeni au upotevu wa mali za umma kamati inapaendekeza Wizara ya fedha kuyashughulikia m chombio hiki cha baraaza la wawakilishi kinatetewa kwa kuridhia ufutwaji huo kama sheria ya fedha kifungu Nam 37 (1) (2) kinavyoeleza.

Mhe Spika
Kamati imekerwa na deni la Serikali ZSTC deni hili linaifedhehesha bodi ya Menejment ya Shirika kwa Umma .Pamoja na kudhoofisha ufanisi wa shirika pia huchangia kusitisha kununuliwa kwa zao kwa wakulima na kwa hivyo kuchangia kuaepo kwa magendo ya karafuu.

Mhe Spika
Kutokana na deni hilo Shirika la ZSTC linalazimika kuuza karafuui zetu kwa bei ndogo katikati ya msimu katika soko la dunia,pia linachangia kuawepo kwa bei ndogo kwa wakulima na hatimae kusababisha kutelekezwa kwa mashamba ya mikarafuu, kamati inaitaka Serikali kufanya kila inavyoaweaza kulilipa deni hili.

Mhe Spika
Ukaguzi umebaini kuwa mapato ya ndani yamaekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwa ka lakini bado kuna baadhi ya mambo yanayorudisha nyuma juhudi hizo ambazo kamati inaishauri Serikali kuyatafutia ufumbuzi .

Kuwepo kwa madeni mengi ya baadhi ya wawekezaji ambayo hayajalipwa kwa muda mrefu kwa mfano madeni ya ukodishwaji wa ardhi yalifikia utuaji wa ndege yamaefikia USS 2,023,391.89 na Tsh86,150,635/= kwa mujibu wa Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali 2006/2007. New Folder (2)uile vile kuwepo kwa baadhi ya mahoteli yanayofanya udanganyifu katika kulipa kodi kwa kutolipa ipasavyo .

Mhe Spika
Kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi ya mwaka 2006/2007, Hoteli ya Vera Club ililipa kodi yenye upungufu wa USD 420,205,26 kutokana na upungufuhuo mwekezaji alitakiwa kulipa adhabu ya USD 105,051.31 hadi hadi tunawasilisha ripoti yetu fedha hizo bado hazijalipwa.

Mhe Spika
Kwa kuwa tumeamua kuufanya utalii ndio tagemeo la uchumi wa visiwa hivi hatuna budi kuzidisha mikakati madhubuti ya kuwabana wawekezaji ambao wanakwepa kodo .kamati imeshitushwa na upotevu wa mamiolioni hayo ya shilingi huku Bodi ya mapato Zanziabr ikiwa haina jibu muafaka.

Mhe Spika
Katika mahojiano baina ya bodi ya Mapato na kamati kuhusiana na kadhia hii bodi ilidai kwamba madai hayo yaliyopo ndani ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali si Kweli . hata hivyo Bodi hiyo ilishindwa kuithibitishia kamati ukweli huo kwa kushindwa kuwasilisha vielelezo vya uthibitisho . kamati inapendekeza Serikali kulishughulikia suala hilo mara kwani kama halishughulikiwa harufu ya ufisadi inaweza ikahisiwa kwenye utaratibu mzima wa ukusanyaji mapato ya Serikali.

Mhe Spika
Kamati haikuwaeza kuaelewa utaratibu dhaifu wa ukodishwaji wa ukumbi wa Disco na swimming pool katika hoteli ya Bwawani ambapo mkataba wake wa ukodishwaji umemaliza muda wake tokea Desemba 2005 inaonekana kuna kuachiana ulaji au ufisadi katika ukodishwaji huo kamati inaitaka Serikali kusitishwa mara moja ukodishwaji huo usio na maslahi kwa umma na kwa kuwa menejment ya Hoteli ya Bwawani inayo uwezo wa kuaendesha shughuli hiyo kwa faida basi warejeshewe ili waingiziye Serikali mapato.

Mhe Spika ,
Kuna umuhimu mkubwa kwa Serikali kufanya Tathmini pamoja ya uendeshaji wa mashirika yake ili kuona yanajiendesha kwa faida .Shirika la Meli ni Shirika muhimu kwa mazingira ya Nchi Zanzibar ambayo ni nchi ya visiwa ,Serikali na kutegemea mashirika ya Binafsi ni udhaifu usioaweza kuvumilika .Kwa kuwa shirika lione bodi yenye uwezo pamoja na uongozi mahiri tunaishauri serikalai kuliongaezea mtaji shirik ili liaweze kujiendeleza kibiahsra.

Mhe Spika ,

Shirika la Bandari linaweza kuwa muhimili wa uchumi wa Zanzibar kwenye Sekta ya uchumi na biashara kwa muda mrefu wa matengenezo ya gati ya malindi ilitikisa uchumi na kutia hasara wafanya biashara wengi hata hivyo Kamati imeridhishwa na hatua mbali mbali zinazochukuliwa za kuwarudisha imani wafanya biashara wetu na Wananchi. Kamati inaagiza kutafutwa kwa haraka vifaa vya kupakulia mizigo pia kuharakisha mpango wa kujenga Gati nyengine ili kwenda sambamba na ushindani na nchi za jirani.

Mhe Spika,
Katika kupima ufanisi na mwenendo wa makusudi na hali ya kodi mbali mbali na kuridhisha kwamba hakuna ujanja na uzembe wa makusanyo, kamati uliutaka uongozi wa Shirika kupata manifest ya Meli zilizoleta bidhaa bandarini Zanzibar angalau ya miezi miwili na kuainisha kilichotangazwa Declared na kuainisha malipo ya mapato kwenye ZRB na TRA hata hivyo hadi tunaandika ripoti hiii, Kamati haikupata mashirikiano katika suala hilo ,na hivyo kuiacha kamti na wingu la shaka juu ya usiri wa suala hilo.

Mhe Spika
Kamati inasisitiza kuwa suala hilo ni muhimu kuawekwa wazi na kwamba hadi itakapoaelezwa na vyenginevyo kwa kupewa vielelezo husika bado utashi wa kamati kutaka kujiridhisha utaenadelea kuawepo.

Mhe Spika
Kuhusu hoja za idara ya Uvuvi na Mazao ya Bahari ambazo Afisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali amewahi kuifanyia ukaguzi maalum, Kamati imeamua kujipa muda zaidi kwa kushughulikia hoja hizo baada ya kamati kupatiwa pipoti ya ukaguzi huo maalum.

Aidha kuhusu suala la wafanya kazi hewa ambalo limeripotiwa katika ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2005/2006 na kutokana na kuwa muda tuliopewa ni mdogo sana kuweza kufuatilia suala hilo , tunaliarifu baraza lako tukufu kwamba kamati italifanyia kaazi suala hili na kulitolea ripoti yake katika kipindi kijacho.

Mhe Spika ,
Kamati imerishishwa sana na jitihada zilizofanywa na Bodi ya Shirika la Umeme katiak kusimamia menejmenti ya shirika kuona kwamba hoja zote za mdhibiti zinafutika na kuchukua hatua madhubuiti za kuwezakuzuiya hoja kwa siku za usoni. Hatua hii ya mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya Shirika ni ya kiuwajibikaji na kamati inaagiza Bodi za Taasisi nyengine kufuata mfano huo.

Mhe Spika
Ili kuweza kutayarisha ripoti iliyo bora Afisi ya Mdhibiti na mkaguzi wa mahesabu za Serikali inahitaji kupata mashirikiano ya kweli na Taasisis zinazokaguliwa .kamati imaegundua kwamba mashirikiano kati ya wakaguzio na wakaguliwa mara nyingi sio mazuri. Hali hiyo huipaelekea wahusika hao wawili kuonana kama madui na kila mmoja wao kumtuhumu mwenziwe kuwa kuwa hakumpa mashirikiano kamati inapaaendekeza yafuatayo:-

Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali itoe elimu ya kutosha utaratibu wakukaguliwa na wakaguzi ili dhana iliyojaengaeka kwa babadhi yoa kwamba ukaguzi hui kama shughuli za kipolisi iondokae na kila mmoja awe huru kushirikiana na mwengine.

Afisi ya Mdhibiti mkuu wa Hedabu za serikali kuhakiskisha kwa mba utaratibu wa entry meeting unakuwa ni matakwa ya lazima katika utendaji wa shughuli zao.

Kamati pamoja bna kufahamu juu za kuijengea uwezo zinazofanywa na Afisi ya CAG, ikiwa ni pamoja na kujenga mashirikiano ya karibu sana naAfisi ya CAG Bara , inapendekweza kuongeza juhudi katika shughuli zao ili kuhakikisha Ripoti wanayotoa inakidhi haja ya viwango vilivyopo Kitaifa Kikanda na Kimataifa.

Mhe Spika
Kwa Muhtasari huo kamati inaitaka kila wiozara na kila Taasisi za Shirika kujiangalia kwenye ukurasa wa 32/33 wa kitabu cha ripoti za kamati ili ijione hali yake ya uwqajibikaji kifedha na kwamba Serikali kwa ujumla ijuwe kwamba kuna kutowajibika kifedha (unaccounted for) ya karibu Jumla ya Tsh bilioni 6 kwa miaka hiyo mitatu.

Mhe Spika

Kamati inahimiza Serikali kuwasimamia watendaji wake kuzielewa sheria ya fedha na shaeria za manunuzi ya Umma pamoja na kanuni zake na kwamba zinatumiwa kama ni zana muhimu katika kusimamia nidhamu ya matumizi na manunuzi Serikalini.

Mhe Spika

Kamati inaitanabahisha Serikali kuchukua hatua juu ya hoja za mkaguzi za Mdhibiti wa hesabu za Seriakli na mapemdekezio ya ripoti ya kamati ya PAC ni jambo linalokwenda sambamba na utekelezaji wa dhamana ya utawala bora . vyenginevyo ubadhirifu na ufisadi wa rasilimali za umma utamea na kuathiri mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.

Mhe Spika
Kamati inapenda kuwashukuru sana Mdhibioti na mkaguzi mkuu wa Serikali pamoja na warendaji wake kwa masjhirikiano na usaidizi ambao wameipa kamati katika kipindi chote cha utendaji wa shughuli zake kamati inatoa pia shukrani za dhati kwa maafisa wahasibu wotae pamoja na watendaji wao kwamashirikiano katika kufanikisha shughuli za kamati.

Kamati inapenda kutoa shukrani za dhati kwa katibu wa Baraza ndugu Obrahim Mzee na Mkatibu wa kamati hii Ndugu Ali na ndugu Shemsa Maabad kwa kuihudumia kamati hii bila ya kuchoka.
Mwuisho lakini sio kwa umuhimu napenda kuwashukuru wajumbe wote wa kamrti kwa uvumilivu ,umahiri na mashirikiano ya halui yha juu klatiak kutekeleza shughuli za kamati Mhe Spika naomba kuwatambua wajumbe hao ambo ni hawa wafuatao:-

Mhe Fatma Abdulhabib Fereji Mwenyaekiti
Mhe Omar Ali8 Shehe MAkamo Mwenyekiti
Mhe Abasi Juma Muhunzi Mjumbe
Mhe Ali Mohamed Bakari “
‘ Anaclet Thonbias Makungila “
“ Hija Hassan Hija “
“ Said Ali Mbaerouk “
“ Mkongwe Nassor juma “
“ Othman Ali Hija “
“ shemsa Maabad Mohamed “

Mhe Spika
Mwisho nawaomba wajumbe wa Baraza la waichangiae Ripoti hii na watoae mapaendekeazo yao kwa Serikali Nawashukuru wajumbae kwa kunisikiliza M
Mhe Spika Naomba kuwasilisha

FATMA FEREJI
…………………..
Mwenyekiti wa PAC
Baraza la Wawakilishi
Zanzibar

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.