KONGAMANO LA MUSTAKBAL WA ZANZIBAR

              DIS. 13-14, 2008, LONDON

           MUWAZA NA MALENGO YAKE           Dr. Yussuf S. Salim

Ni furaha kubwa kwamba leo Wazanzibari wa kila itikadi tumekutana hapa London kwa makusudi ya kutafuta njia za kuinasua nchi yetu baada ya miaka zaidi ya 44 ya Muungano. Kutokana na kuzinduliwa kwamba hatuna nchi wala mafuta Wazanzibari tumeamshwa katoka usingizi wa totoro.

Baadhi yetu tulikuwa tumelala na kukoroma wakati ndugu zetu wapenzi wa Tanganyika wanaimun´gunya mun´gunya Zanzibar kama mchwa. Mwishowe boriti litaanguka na tusiwe nako kwa kwenda.

Ingawaje sio Wazanzibari wote waliokuwa wamelala, wengine walikuwa tokea siku na mwanzo za Muungano hadi leo wamekuwa mstari wa mbele kutetea haki za Zanzibar hasa baada ya kuona muelekeo unazidi kuwa mbaya.

Wazanzibari tofauti, wenye mirengo tofauti, katika nyakati tofauti wamekuwa wakitoa sauti zao kutetea maslahi ya Zanzibar. Wazanzibari wamekuwa kama boya halizami. Wote hao tunawashukuru na kuwaahidi kwamba tutayaendeleza mapambao yao. Majukumu hayo yanatakiwa hasa yanedelezwe na vijana, kwani ni maisha yao ndiyo watakayo kuwa wanayaendeleza.

Kutanabahi kwamba Zanzibar inapelekwa pabaya hakujawazindua wazee tu balia hata na hasa vijana wa siki hizi. Na ndio maana vijana hao wakachukua jukumu la kualika Wazee katika kujaribu kupanga mikakati ya kuikwamua Zanzibar hapa ilipofika. Napo kwa kweli tayari ni pahala pabaya. Kwa bahati nzuri vijana hawa hawana maruirui ya siasa za kizamani na wanamuelekeo wa kutizama mbele na sio kurejearejea nyuma.

Kutokana na hali hiyo, kwa muda sasa wengine tumekuwa tukipigania taifa la Zanzibar kila tulipopata nafasi. Katika jitihada hizo vijana wakasikia sauti zetu kwa mbali na wakatualika kuja kushirikiana nao kulipeleka gurudumu la mabadiliko mbele.

Baada ya kuwasiliana mara kadhaa tukaamua kukutana na hawa vijana hapa London Mwezi wa machi 21-23, 2008, kwa makusudi ya kutafuta njia za kuungana kuiokoa Zanzibar. Wengi wetu tulikuwa na itikadi mbali mbali, wengine tulikuwa hatujuani kabisa si kisiasa si kijamii. Lakini bila ya shaka yoyote tulitambua kwamba tulikuwa na lengo moja nalo ni kuweka kando tofauti zetu zote kwani tulitambua kwamba hali ya Zanzibar inazidi kuwa mbaya kila usiku uchao. Tuliamini kwamba bila ya kuungana hatutafika mbali. Tulijua vile vile kwamba ingawa ushawishi na msukumo mkubwa zaidi uko Zanzibar kwenyewe, lakini nasi tuliwajibika na kuwa na dhamana kamili ya kujitolea kusaidia taifa letu.

Kuambatana na mikutano na majadiliano tofauti umoja wa MUWAZA ukazaliwa.

Kati ya malengo yetu muhimu tuliyojipangia, la mwanzo kabisa lilikuwa ni jukumu la kuwaunganisha Wazanzibari popote walipo katika juhudi ya kuikomboa Zanzibar kama nchi na kuirejeshea mamlaka yake. Katika jukumu hilo, tulikubaliana kwamba Wazanzibari wote lazima tuwe wamoja wakati tunatetea nchi na taifa la Zanzibar. Tujifunze kuheshimu utaifa wetu bila ya kujali itikadi zetu tofauti. Kwanza nchi na baadae ndio ushindani wa kisisiasa.

Mikutano ya MUWAZA ilihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi mbali mbali ulimwenguni na kwa wakati huo huo tukijadiliana kwa njia za simu na mtandao na kuwashirikisha wajumbe tofauti katika mijadala yetu waliokuwa sehemu mbali mbali ulimwenguni

Katika mambo yaliyo tutia mori na kufanya tuvinjari zaidi ni pale tulipoona jinsi mustabal wa Zanzbar unavyodharauliwa na hatimae tuliposikia kauli ya kudai kwamba” Zanzibar si nchi”.

Hapa MUWAZA ilihisi ina wajib wa kutetea hadhi ya Zanzibar kama nchi na

Kudhihirisha kwamba Zanzibar ni nchi na ilikuwa nchi hata kabla ya Tanganyika

MUWAZA ilitetea kwamba Zanzibar ilifikia daraja za maendeleo mbali mbali kabla ya Muungano kama zinavyoorodheshwa hapo chini:

Zanzibar ilikuwa nchi, dola na taifa huru kabla hata jina la nchi ya Tanganyika kujulikana

Zanzibar ilikuwa nchi moja kati ya nchi mbili katika Bara la Afrika kwa kuwa na watalaamu wengi zaidi kufananisha na idadi ya wakaazi wake

Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu Afrika kwa mujib wa kipato cha kichwa

Zanzibar ni nchi ya mwanzo Afrika kuwa na gari la moshi

Zanzibar ilikuwa nchi ya mwanzo Afrika kuwa na simu ya upepo

Zanzibar ilikuwa na taa za umeme mabarabarani kabla London na New York

Zanzibar ilikuwa na lifti kabla ya nchi yeyote Afrika ya Mashariki

Zanzibar katika 1964 ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni kubwa zaidi kushinda karibu nchi nyingi Afrika zikiwemo nchi zote za Afrika ya Mashariki

Ndugu zetu wa Tanganyika hawajui tunatoka wapi ndio maana

MUWAZA inawatanabahisha ndugu zetu kwamba Zanzibar kimaendeleo ilikuwa mbele sana kupita Tanganyika na kusita kwa maendeleo kunatokana na kwama

Zanzibar iko chini ya Muungano na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi vya kila aina

MUWAZA inawatanabahisha Wazanzibari kwamba kutokana na kuporwa kwa mamlaka ya kisiasa na Muungano ndio maana leo

hata Raisi wa Zanzibar amepunguzwa hadhi na kuwekwa kuwa sawa na Waziri mdogo katika Baraza la Mawaziri la Muungano

Baraza la Wakilishi la Zanzibar na maamuzi yake hayatiwi maanani na Serikali ya Muungano

Heshima ya Mawaziri wa Zanzibar iko chini ya Wakuu wa Wilaya wa Muungano

Wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Muungano hawana sauti yoyote

Zanzibar katika Katiba ya Muungano wa nchi mbili haijahakikishiwa Urais wa zamu

Zanzibar chini ya Muungano imepoteza utaifa wake

Zanzibar imepoteza Kiti chake cha Umoja wa Mataifa

Zanzibar imepoteza umashuhuri wake wa kibiashara kwa kuwekewa vizingiti vya kila aina

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo MUWAZA inaona ni lazima yarekibishwe na hayawezi kurekibishika bila ya Wazanzibari kuungana

Tunaona kila usiku uchao jinsi vipengele vya Katiba ya Muungano vinavyozidishwa kuikandamiza Zanzibar Kisiasa, Kiuchumi, Kitamaduni, Kijamii (elimu na siha) na hata Kidini.

Hali hii mbaya ya Zanzibar unaathir zaidi hali za Vijana na Wanawake na kusababisha umasikini wa kutupwa.

MUWAZA inatambua kwamba hali hii imewezekana kwa sababu Wazanzibari hawajaungana na wameshughulishwa zaidi na kupigana vita wenyewe kwa wenyewe na kusahau mustakbal wa Taifa la Zanzibar.

MUWAZA umeona kuna haja kubwa na muhimu sana ya kuwaunganisha Wazanzibari wote katika mapambano ya kupigania maslahi ya Zanzibar.

MUWAZA inapendekeza kwamba kila mrengo wa kisiasa uweke mustakbal wa Taifa la Zanzibar mbele na siasa binafsi baadae.

Ni pale tu ambapo Wazanzibari wataungana bila ya kujali mirengo ndipo Taifa la Zanzibar litakapo okoka.

Ili kuweza kufanya hivyo imependekezwa kufanyike Mkutano Jijini London baina ya tarehe 13-14.12.08 na kualika Wataalamu wa Kizanzibari ambao watashiriki katika Kongamano la kulijadili suala la Utaifa wa Zanzibar,

Tunawashukuru wataalam Wakizanzibari tuliokuwa nao leo, tunawashukuru na wale waliotuletea makala lakini hawakuweza kuwasili pamoja kuwashukuru na wale ambao wamekuwa wakituunga mkono ki hali umali katika majukumu ya kutayarisha maandishi ya kutetea Utaifa wa Zanzibar katika kila meddani.

Tuna sisitiza kuwa maazimio ya mwanzo ya MUWAZA ni

 1. Kuunganisha Wazanzibari
 2. Kulinda na Kughushisha Taifa la Zanzibar

 3. Kuziunganisha jumuia za Wazanzibari

 4. Kuunda NGO za kusaidia Wazanzibar

 5. Kupigania Haki za kitaifa, kidemokrasia za Wazanzibari na za Wengineo

 6. Kupigania Haki za Wanawake, Watoto, Wazee na Walemavu

 7. Kutetea na kuziendeleza Mila na Utamaduni wa Wazanzibari

Ili kufikia malengo yetu tuliamua kurekibisha harakati zetu ili tuweze

 1. Kuunda na kushirikiana na NGO za kusaidia Wazanzibari na kuepusha kwa vijana kumiminika mijini
 • Kushirikiana na Taasisi zisizo za kiserikali

 • 10.Kupanga mbinu za kutafuta michango hasa ya kifedha na kuendeleza mashirikiano na jumuia zinazosaidia katika maafa na ajali za kimazingira

  11.Kuwa na Jarida letu

  1. Jarida litolewe baada ya Mkutano Mkuu wa Disemba

  13.Tusifikirie kuwa kila mwandishi lazima awe anapendelea Zanzibar

  14.Kutayarisha Kongamano tofauti

  15.Kutafuta njia za kuendeleza Elimu ya Vijana nyumbani na Ughaibuni

  16.Harakati zetu ziwe za kivitendo na faida zake zionekane wazi wazi na jamii

  17.Wazanzibari wa UK wakiamua wanaweza kushiriki katika mapambano na kuweza kusaidiana kwa upeo wa hali ya juu.

  Muafaka na Matokeo yake

  1 Ilikubaliwa kwamba hatukuhusishwa na hatukuwa tunajua udani kuhusu mazungumzo hayo

  2 Suala la Zanzibar ni suala la Wazanzibari wote, tuendelee na harakati zetu bila ya kujali mazungumzo ya muafaka yalipo- au yatakapofika

  3 Tunapojadili suala hilo tuwe tunatumia njia za kichambuzi

  4 Mazungumzo yasiwe kwa maslahi ya vyama viwili bali yawe kwa maslahi ya Zanzibar

  5 Tuonane na wahusika na tuwape mawazo yetu itapohitajika

  6 Tutafute njia zetu wenyewe za kutoa msukumo wa kunufaisha Zanzibar

  7 Ilikubalika kwamba kauli za Rais Jakaya Kikwete ni za kuupalilia mpasuko huo na si kinyume cha hivyo

  8 Kati ya harakati zetu tunaweza kwa mfano kufanya maandamano na kuwasilisha risala zetu wenyewe zenye maoni yetu huru

  9 Tunaweza kushirikiana na vyama kwa yale tunayokubaliana na kuweka wazi yale tusiyo kubaliana

  10Katika maandamano ya London tuwashirikishe wale Watanganyika walio na maslahi yanayokubaliana na yetu wakati huo huo tukitia maanani kwamba watu hawawezi kukaa meza moja pasi ya kuaminiana hata kama wote ni Wazanzibari

  11Imedhihirika kwamba sio Rais Amani Karume bali ni Rais Kikwete ndiye anaekwamisha muafaka

  12Muafaka unaonekana kuwa sio wenye mfumo ulio wa kidemokrasia

  13Hatupendelei kuona kwamba ndugu zetu wanapoteza maisha yao bila ya tija yoyote

  Muungano

  1 Kinachotakiwa ni kufanywa haraki na huko Tanganyika vile vile

  2 Kuita mwito wa kukusanya sahihi za kupinga Muungano

  3 Kutayarisha mabango na post-card za kudai kura ya maoni

  4 Ikiwezekana kumleta mjumbe mmoja kati ya wale waliodai Pemba kujitenga

  5 Tuchungue kama tunaweza kuifufua kesi dhidi ya Muungano

  6 Sisi tulio nje tuna uwezo wa kuandika barua na kuzipeleka katika taasisi tofauti nje na ndani ya nchi

  7 Tuchukue jukumu la kila baada ya muda kualika na kuwaandikia Wabunge wa nchi za nje

  8 Katika harakati za media tuungane na tujifunze kutoka kwa kamati za media tofauti

  9 Tutafute wataalamu watakaotupa ushauri wa kisheria

  10Tuwasilishe kilio chetu kama ni Uvamizi wa Kikoloni

  11Tupendekeze yale tunayoweza kuyatimiza bila ya kupin

   dukia mpaka
  

  12Tuliyokubaliana yanatosha lilobaki ni utekelezaji mradi kila mmoja wetu anachukuwa na kutimiza jukumu lake itakikanavyo

  13Ni muhimu tupate watu wenye nia safi wa kutuunga mkono

  14 Tuchukue muda kuutafakari mfumo wa Katiba yetu

  Jarida la MUWAZA

  1 Jarida lilenge kimataifa na kitaifa la Zanzibar

  2 Kupembua makala maalum kila tunapoandika

  3 Kutoa Jarida lenye lugha mbili Kiswahili na Kiingereza na liwe na kurasa 4

  4 Kwa jumla litoke kwa Kiswahili na makala maalum (special column) Kiingereza

  5 Jarida liwaelimishe wasio Wazanzibari vile vile

  6 Lengo la kuandika kwa Kiswahili ni kulipeleka nyumbani ikiwa ni njia ya kuwashajiisha wananchi kupigania nchi yao

  7 Utoaji wa Kiingereza uwe kwa ufupi yaani mfumo wa “Press Release” ili kutowachosha wasomaji wa Kimataifa

  8 Tunahitaji tuwe na msemaji wa kuwasiliana na Press

  9 Tufanye “newsletter” kwa wanachama na wengineo – ikiyumkinika

  10.Kuchuguzwe uwezekano wa redio ya mtandao, jarida la mtandao na website yetu wenyewe kwa kuwasiliana na wataalamu wetu wa mtandao

  11.Kusaidia vitengo vya kisheria viweze kusaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kiuchumi kusimamisha kesi

  12.Kuchangia kwa kununua hisa katika Jarida la Daima

  13.Jamii ya Kizanzibari ielimishwe juu ya historia ya Zanzibar kuwa vitu viwili vimetokea Zanzibar yaani siku ya Uhuru na siku ya Mapinduzi ni mambo ya kihistoria yasioweza kukanika

  Kuzungumzia Muungano

  MUWAZA inatambua kuwa hali inavyoendelea nyumbani juu ya Muungano imeonekana kuwa hawataki Muungano kwa sababu ya hali ya mfumo ulivyo hivi sasa ni kuwa umejaa matatizo na hasa kuwa haki za Zanzibar zinaporwa kila usiku uchao. Ama – Katiba ya Muungano yenye mfumo wa sasa ibadilishwe kwa kupitia Tume/chombo huru na hatimae wananchi waruhusiwe kuipigia kura kwa kuikubali au kuikataa,

  Kuhakikisha Zanzibar inapata kiti chake cha Umoja wa Mataifa na Tanganyika ipate chake au kama si hivyo Zanzibar ipate uhuru wake kamili.

  Hili la kiti cha Zanzibar linawezekana kutendeka sawa na siku za Umoja wa Ki-Soviet ulivyokuwa na viti vinne katika Umoja wa Mataifa wakati Balarus,Kazakstan, Urusi na Ukrania kila kimoja kikiwa na kiti chake ingawa nchi zote nne hizo zilikuwa chini ya Umoja wa Soviet.

  Hali ilivyo huko Zanzibar hivi sasa ni kwamba Wazanzibari wote wameungana kupigania nchi yao bila ya kujali itikadi zao za kisiasa. Hili limedhihirika wazi kabisa katika Baraza la Wawakilishi na Wazanzibari katika Bunge la Tanzania, hasa baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mazengo Pinda kurejea kauli ya kuwa Zanzibar si nchi na Raisi Kikwete kutamka katika Bunge kwamba Zanzibar si nchi Kimataifa bali ni nchi Kitaifa yaani ndani ya Tanzania.

  Ilibainika kwamba Mwalimu Nyerere amekuwa akiwagonganisha vichwa Wazanzibari ili kuwatawala na ni wajib wa MUWAZA kushajiisha masikilizano baina ya makundi mawili makubwa ya kisiasa Zanzibar yaani CCM na CUF (kuleta suluhi kama ile ya Afrika ya kusini) hasa pakitiwa maanani kwamba viongozi wajuu karibu wote wa CUF wanatoka ama ASP au CCM.

  Vile vile kuwaunganisha wananchi kwa kupitia njia za kuleta Mandeleo ya jumla kwa Wazanzibari wote.
  Kutafuta mbinu za vipi tunaweza kusaidia kukuza Demokrasi Kukuza na kuufufua utamaduni na Utabulisho wa Kizanzibari

  MUWAZA inapendekeza kushirikiana na mashirika ya kimataifa yasiofungamana na upande wowote kama Jumuia ya Madola, AU na kutaka misaada ya kutoka nchi wafadhili kuleta masikilizano Zanzibar.

  Vile vile kuwasiliana na Wabunge wa EU hususan wa Uingereza na wa nchi za Skandinavia.

  Kushajiisha utumiaji wa thuluthi tatu wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wakizanzibari katika kupigania haki za Zanzibar utiliwe mkazo

  Hatimae Kulirudisha suala la Muungano kwa Wananchi kwa uamuzi wa mwisho

  Madhumuni na lengo la Kongamano hili la Disemba 13-14, 2008, London, ni kuwaunganisha Wazanzibari ulimwenguni kote na kwa sauti moja wadai mustakbal wa Zanzibar.

  2 thoughts on “Malengo ya MUWAZA”

  1. nakupongezeni kwanza MUWAZA pia wazanziibari wote kwa ujumla kwanza kwa kuondosha tofauti zetu na kuwa kitu kimoja, pili naunga mkono muliposema kua inabidi suala la muungano lipelekwe kwa wananchi na kutaka ridhaa zao kama watakubali au laa na sio wabunge wala wawakilishi wanaopaswa kuamua hili. insshaallah mungu atatuwezesha kurudisha hadhi ya nchi yetu na kurudi kama zamani

  Leave a Reply

  This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.