<!–[if !mso]> <! st1:*{behavior:url(#ieooui) } –>

Na Mwandishi Wetu

SUALA la kero za Muungano ambalo limekuwa likilitikisa Bunge mara kwa mara katika siku za hivi karibuni na wakati mwingine kuzua mjadala mzito ndani na nje ya Bunge, jana limeibuka tena baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Juma (CUF), kuhoji sababu za kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni kutokana na swali lake la msingi, mbunge huyo aliishangaa kamati ya kushughulikia kero za Muungano, kushughulikia masuala madogomadogo na kuziacha kero kubwa kama suala la kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais, na kero nyingine kubwa zinazoleta matatizo.

Mbunge huyo aliitaka serikali kueleza mambo yaliyosababisha Rais wa Zanzibar kutokuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano na kuhoji sababu ya suala hilo kutozungumzwa na kamati ya kushughulikia kero za Muungano, maana nalo ni kero katika Muungano wa Tanzania.

Pia alihoji kuwapo kwa ukimya wa ahadi iliyotolewa bungeni na serikali ya kuwataka mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mwanasheria wa Serikali ya Muungano wa Tanzania kuiangalia katiba.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib, alisema suala la Rais wa Zanzibar kutokuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano liliamuliwa na Bunge ambalo pia lina wawakilishi kutoka Zanzibar.

Alisema iwapo mbunge huyo anataka Rais wa Zanzibar awe Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano, aandae hoja binafsi na kuiwasilisha bungeni ili maamuzi yatolewe upya na kubainisha kuwa suala hilo si kero ya Muungano.

Kuhusu suala la kukutana kwa mwanasheria wa SMZ na mwanasheria serikali kwa ajili ya kuzungumzia katiba, alisema hajawahi kuzungumzia suala hilo bungeni na kubainisha kwamba mambo ya Muungano hushughulikiwa na kamati maalumu.

“Sijawahi kuzungumzia bungeni hapa kwamba wanasheria wa SMT na SMZ wakutane kujadili katiba, labda kama alizungumza Waziri

<!–[if !mso]> <! st1:*{behavior:url(#ieooui) } –>

<!– /* Style Definitions */ p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal {mso-style-parent:””; margin:0in; margin-bottom:.0001pt; mso-pagination:widow-orphan; font-size:12.0pt; font-family:”Times New Roman”; mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;} @page Section1 {size:8.5in 11.0in; margin:1.0in 1.25in 1.0in 1.25in; mso-header-margin:.5in; mso-footer-margin:.5in; mso-paper-source:0;} div.Section1 {page:Section1;} –>

Mkuu,” alisema Khatib.

Akijibu swali la msingi la mbunge huyo, Khatib alisema hatua mbalimbali zimechukuliwa katika kuimarisha Muungano ikiwamo kuundwa kwa kamati ya pamoja ya kushughulikia kero za Muungano, kutolewa kwa muundo mpya katika kamati hiyo na kuanza kukutana kwa kamati hiyo.

Hadi sasa kamati hiyo imefanya jumla ya vikao vinne na kuzitaja kero zilizopatiwa ufumbuzi kuwa ni mgawanyo wa mapato yanayotokana na misamaha ya mikopo ya fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kero nyingine zilizofanyiwa kazi ni suala la SMZ kukopa katika soko la ndani, sheria ya usimamizi wa uvuvi katika bahari kuu, ushiriki wa SMZ katika masuala mbalimbali ya kimataifa kuanzia hatua za awali.

Waziri alibainisha kuwa kero zinazoshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi zimekuwa zikitangazwa kwa wanachi mara kwa mara na waziri mwenye dhamana ya kuratibu masuala ya Muungano. Kuna baadhi ya kero ambazo kwa sasa zipo katika mchakato wa kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi, ingawa hakuzitaja kero hizo.

Katika siku za hivi karibuni, uliibuka mjadala mzito kuhusu hadhi ya Zanzibar ndani ya Muungano. Mjadala huo ulitokana na majibu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, bungeni kuwa Zanzibar si nchi.

Hoja hiyo ilipingwa vikali na makundi mbalimbali ya jamii hususan visiwani Zanzibar. Hatimaye Rais Jakaya Kikwete aliuzima kwa kutoa ufafanuzi kwamba Zanzibar ni nchi nje ya Muungano, lakini ndani ya Muungano nchi ni Tanzania. Chanzo:

<!– /* Style Definitions */ p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal {mso-style-parent:””; margin:0in; margin-bottom:.0001pt; mso-pagination:widow-orphan; font-size:12.0pt; font-family:”Times New Roman”; mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;} @page Section1 {size:8.5in 11.0in; margin:1.0in 1.25in 1.0in 1.25in; mso-header-margin:.5in; mso-footer-margin:.5in; mso-paper-source:0;} div.Section1 {page:Section1;} –>

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/11/5/habari2.php

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.