Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Pandu Ameir Kificho. Msimamo wake wa kuzuia mjadala wa kuitetea Zanzibar ndani ya Baraza la Wawakilishi umewakera Wazanzibari
Spika Pandu Kificho

“MUWAZA inadai Wazanzibari wapewe haki ya kupiga kura ya maoni juu ya Muungano huu ambao ianze leo kabla ya kesho….inaunga mkono kauli ya Wazanzibari ya kudai kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa….inasisitiza kwamba Wazanzibari wana haki ya kuandamana, kufanya mikutano ya hadhara na kutoa maoni huru… inawanasihi Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge waliochaguliwa na Wazanzibari waungane na kwa pamoja watetee maslahi ya nchi ya Zanzibar.”

Tamko la Jumuiya ya Mustakabali wa Zanzibar (MUWAZA ) kuhusu hatima ya Zanzibar kufuatia mjadala mzito unaondelea sasa nchini kuhusu hadhi na nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano

Kutokana na habari kwamba Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Pandu Kificho kwa mara kadhaa amezuia kutekelezwa kwa mkondo wa kidemokrasia  kwa Wawakilishi waliochaguliwa na Wazanzibari wasilizugumzie katika Baraza suala la kujadiliwa kama Zanzibar ni nchi au la.

Umoja wa Mustabkal wa Zanzibar (MUWAZA) umeshitushwa na kuudhiwa sana na msimamo Mheshimiwa Kificho kwa upungufu wake wa kizalendo na tunawaomba Wazanzibari wote kwa jumla wasimame nasi kidete kulaani khatua hiyo isiyo na maslahi ya nchi ya Zanzibar. Kwa wakati huo huo tunawashajiisha Wazanzibar walio wengi wamuwajibishe Mhe. Kificho na kumwajibisha

MUWAZA inaikemea, inaishutumu vile vile khatua ya Waziri Kiongozi Mhe. Shamsi Vuai ya kuakhirisha kikao cha Baraza la Wawakilishi hadi mwezi wa Oktoba na kwa hali hiyo kuzuia Wawakilishi waliochaguliwa na umma wa Wazanzibari kutetea haki za Zanzibar katika Baraza hilo. Tunashambulia msimamo usio na hisia za Kijananchi  wa Waziri Kiongozi Mhe. Shamsi Vuai na kumnasihi kwamba arejelee msimamo wa kutetea haki za Zanzibar ndani na nje ya Muungano.

MUWAZA inalaani vikali tamko la Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano Mhe. Pinda Mizengo kwa kuidhalilisha Zanzibar na kutaka kulimiminia simenti kaburi la Zanzibar katika njama za kutaka kuifuta Zanzibar katika ramani ya ulimwengu.

MUWAZA inalaani njama zote za serikali ya Muungano kwa njia za kihadaa kutunga Katiba yenye sura za Kikoloni, kama vile Uingereza na Irland, pamoja na kila uchao kizidisha vipengele katika Katiba ya Muungano kwa madhumuni ya kuinyima Zanzibar haki zake za Kidola, Kitaifa, Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni.

MUWAZA inadai uhuru kamili wa Zanzibar

MUWAZA inasisitiza kwa Zanzibar ni nchi kama Tanganyika ilivyo nchi.

MUWAZA inawapongeza, kuwapa hongera na kuwasifu viongozi mashujaa wote  waliosimama kidete kutetea maslahi ya nchi ya Zanzibar

MUWAZA inaunga mkono kuheshimiwa kwa Wazanzibari na siasa zao, mila, utamaduni, utu wao na kuheshimiwa kwa mipaka na rasilmali zao

MUWAZA inadai Wazanzibari wapewe haki ya kupiga kura ya maoni juu ya Muungano huu ambao ianze leo kabla ya kesho

MUWAZA inaunga mkono kauli ya Wazanzibari ya kudai kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa

MUWAZA inasisitiza kwamba Wazanzibari wana haki ya kuandamana, kufanya mikutano ya hadhara na kutoa maoni huru.

MUWAZA inawanasihi Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge waliochaguliwa na Wazanzibari waungane na kwa pamoja watetee maslahi ya nchi ya Zanzibar

MUWAZA inawakumbusha Wabunge wapendao haki wa Tanzania Bara wasimame upande wa haki na kulinda haki za nchi ya Zanzibar

MUWAZA inamkumbusha Rais Kikwete wajibu wake wa kulinda haki za nchi ya Zanzibar kama alivyosimamia haki za G-55 na anavyosimamia maslahi ya nchi tofauti Barani Afrika

Kwa niaba ya Mustakbal Wa Zanzibar (MUWAZA)

Dr. Yussuf S. Salim

Copenhagen

Denmark

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.