Umma Usiposema…

Published on :

Wajinga ndio waliwao Waswahili walisema… Sijui kama huo msemo Wanao…maana mimi Siku nyingi duniani nimehama Na yalioko huko sinayo Na ndipo wafanyao Wanapovinjari na jeuri Wengineo wanatizama Wanyonge na wamekosa ari Kwa vitendo na zao kalima Mapuuza…wakifanya Si letu? Wengineo huo wasema Letu sote basi nalitote Umma hausemi Maana kwa […]

Maisha, zama na zamu

Published on :

Nilizaliwa mnyonge Nikakulia unyonge Lakini Nilipambana niishi Niishi waishivyo watu Watu waitwao watu Nami nikajikuta Katika mpambano huo Naingia ulingoni Nikarusha makonde Nami harushiwa pia Kwamba ndivyo maisha yalivyo Maisha zama na zamu

Tupumbazeni kwa Popo Bawa, lakini siku moja itakuwa kweli

Published on :

Kwa kawaida, kuna vitu ambavyo huleta pumbazo la akili. Hivi ni vile vinavyoweza kumpelekea mwanadamu kupumbazika na akaweza kuyasahau baadhi ya mambo ambayo yamemzonga na kuisumbua akili yake. Vipumbazio hivi vinajumuisha michezo, vilevi na hata mikusanyiko ya kawaida au ile ya kisiasa. Ukweli ni kuwa haviliondoshi tatizo husika, lakini humfanya […]

Kuna siku mambo yatabadilika

Published on :

Maisha ya hapa Bongo ni magumu sana, lazima nikiri hivyo. Lakini pia, lazima nikiri kitu kingine: maisha ya hapa yana matumaini makubwa. Siku zangu za kuishi na watu wa hapa zimekuwa zikinipa fundisho moja: kwamba mabadiliko yawezekana. Kila siku napita mitaani na pikipiki langu, naangalia Wabongo wanavyoishi. Napanda daladala nao. […]